Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja
Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao
Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii
Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm
Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo akizungumza na waanishi wa habari mkoani Mtwara (Picha na Musa Mtepa)
Mgombea urais wa CUF, Gombo Samandito Gombo, amewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, akiahidi huduma bora za jamii na maendeleo ya kweli endapo chama chake kitaunda serikali
Na Musa Mtepa
Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Gombo Samandito Gombo, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025, kwa kuchagua viongozi wanaowataka ili kuleta maendeleo ya kweli kwa taifa.
Akizungumza na Waandishi wa habari Oktoba 8, 2025, mjini Mtwara, Gombo amesema kuwa fikra za baadhi ya wananchi kutoshiriki kupiga kura haziwezi kuwasaidia Watanzania kwa namna yoyote ile na kusisitiza kuwa ni muhimu kila mmoja kutumia haki na nguvu yake ya kikatiba kwa kumpigia kura mgombea wa CUF.
Sauti ya 1 Gombo Samandito Gombo Mgombea Urais CUF
Aidha, Gombo ameongeza kuwa chama hicho hakikatishwi tamaa na idadi ya watu wanaojitokeza kwenye mikutano ya kampeni, kwani CUF inaamini kuwa uungwaji mkono kutoka kwa wananchi ni mkubwa na unaendelea kuimarika kila siku.
Sauti ya 2 Gombo Samandito Gombo Mgombea Urais CUF
Akizungumzia sera za chama chake, Gombo amesema kuwa endapo CUF itashinda uchaguzi na kuunda serikali, itahakikisha wananchi wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla wanapata huduma bora za kijamii, ikiwemo matibabu bure na miundombinu ya kisasa.
Sauti ya 3 Gombo Samandito Gombo Mgombea Urais CUF
Chama cha Wananchi (CUF) ni miongoni mwa vyama vinavyowania nafasi ya kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, ambapo wagombea mbalimbali wameendelea na kampeni zao katika maeneo mbalimbali nchini.
Sehemu ya Nyumba ya Bw Roboti iliyoteketea kwa Moto Oktoba 8,2025 (Picha na Grace Khamisi)
Nyumba ya mkazi wa Mangamba Chini, Bw. Roboti, imeteketea kwa moto asubuhi ya Oktoba 8, 2025, kutokana na mkaa uliokuwa bado una moto. Jeshi la Zimamoto lilifika kwa haraka kuzima moto huo, huku viongozi na majirani wakitoa pole na elimu ya tahadhari dhidi ya moto majumbani
Na Grace Khamisi
Mkazi mmoja wa mtaa wa Mangamba Chini, katika Manispaa ya Mtwara Mikindani, anayefahamika kwa jina la Roboti, amejikuta katika wakati mgumu baada ya nyumba yake kuteketea kwa moto. Tukio hilo limetokea majira ya saa tatu asubuhi, Oktoba 8, 2025.
Wakizungumza na Jamii fm redio, majirani wa Bw. Roboti, Bi. Mariamu Yusufu na Mohamedi Moa ,wamesema kuwa wakati moto huo ulipoanza walikuwa nyumba ya jirani, karibu na nyumba ya Roboti, ndipo walipoona moshi na kuwajulisha majirani wengine ili kusaidia kuzima moto huo.
Sauti ya Mariamu Yusufu – Jirani wa Bw. Roboti
Kwa upande wake, Bw. Roboti ambaye ni muathirika wa tukio hilo, amesema kuwa alipata taarifa za kuungua kwa nyumba yake kupitia simu alipokuwa kazini, na alilazimika kukatisha kazi ili kufika nyumbani haraka kwa ajili ya kuokoa mali na kusaidia kuuzima moto huo.
Sauti ya Bw. Roboti – Muathirika wa Moto
Naye Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mtwara, Ambros Ndunguru, amesema chanzo cha moto huo ni kiroba cha mkaa kilichowekwa na Bw. Roboti bila kuchunguza kama mkaa huo ulikuwa bado una moto.
Aidha, Mrakibu Ndunguru ametumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya majiko ya mkaa, huku akitoa onyo dhidi ya tabia ya kuzima mkaa wa moto kwa kutumia majivu, akisema ni hatari kwa usalama wa makazi.
Sauti ya Ambros Ndunguru – Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na UokoajiMrakibu msaidizi wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Ambrosi Ndunguru akizungumza na wakazi wa mtaa wa Mangamba chini jinsi ya matumizi sahihi ya majiko ya mkaa(Picha na Grace Khamisi)
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mangamba Chini, Bw. Abdala Abdala, amempa pole Bw. Roboti kwa tukio hilo, huku akilishukuru Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kufika kwa haraka na kuzuia madhara makubwa zaidi.
Sauti ya Abdala Abdala – Mwenyekiti wa Mtaa wa Mangamba Chini
Afisa mtendaji wa kata ya Mkunwa Bi Rachael Pether wa pili kutokea kulia akiwa katika picha ya pamoja wakati wa kukabidhi msaada wa Godoro kwa familia ya Mzee Salamu Somba (Picha na Musa Mtepa)
Viongozi wa Kata ya Mkunwa wametoa msaada wa godoro, sabuni na taa kwa familia ya Mzee Salumu Somba ili kusaidia kupunguza changamoto za maisha zinazoikabili familia hiyo.
Na Musa Mtepa
Viongozi na watendaji wa vijiji katika Kata ya Mkunwa wametoa msaada wa godoro, sabuni na taa kwa familia ya Mzee Salumu Somba, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi katika kusaidia familia hiyo inayokabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Akizungumza na Jamii FM Radio leo Oktoba 9, 2025 wakati wa kukabidhi msaada huo, Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkunwa, Bi Rechal Bernadater Pether, amesema kuwa uongozi wa Kijiji cha Nyengedi uliwasilisha taarifa juu ya hali ya familia hiyo katika ofisi ya kata, na baada ya kutembelea familia hiyo walijiridhisha kuhusu uhitaji wa msaada.
Aidha, Bi Rechal ametoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kusaidia familia hiyo ambayo inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi.
Sauti ya Bi Rechal Bernadater Pether, Mtendaji wa Kata ya Mkunwa
Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyengedi, Bi Ebby Hamisi, ameushukuru uongozi wa kata kwa kuguswa na changamoto zinazowakabili wananchi wao, akibainisha kuwa msaada huo utasaidia kupunguza kwa kiasi fulani matatizo yanayoikumba familia hiyo.
Hata hivyo, Bi Ebby amesema kuwa pamoja na msaada huo, familia ya Mzee Somba bado inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo watoto wake wa shule ya msingi kukosa mahitaji muhimu ya shule, na hali ya kulala chini kwa kutumia matambala ardhini.
Sauti ya Bi Ebby Hamisi, Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Nyengedi
Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi, Bi Lukia Mnyachi, ameushukuru uongozi wa kata kwa msaada huo, akisema umeleta faraja na kupunguza changamoto kwa familia ya Mzee Somba.
Sauti ya Bi Lukia Mnyachi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mzee Salumu Somba ameushukuru uongozi wa kata pamoja na mwenyekiti wa kijiji kwa jitihada zao za kuwafikia na kuwasaidia, akieleza kuwa hali yao kwa sasa imeimarika ukilinganisha na kipindi cha nyuma.
Sauti ya Mzee Salumu Somba, mlemavu wa macho
Mzee Salumu Somba ni mkazi wa Kijiji cha Nyengedi kilichopo Kata ya Mkunwa, Halmashauri ya Mtwara Vijijini, mkoani Mtwara. Hapo awali alikuwa akiishi katika nyumba chakavu isiyo na paa imara, hali iliyosababisha yeye na watoto wake watatu wenye umri kati ya miaka 5 hadi 8 kulala wakiwa wazi kwa mvua na jua.
Kutokana na hali hiyo, uongozi wa Kijiji cha Nyengedi, kupitia kwa Mwenyekiti wake Bi Lukia Mnyachi, ulijitahidi na kufanikisha ujenzi wa nyumba mpya kwa familia hiyo. Hata hivyo, familia hiyo iliendelea kukosa vitanda na kulazimika kulala chini, hali iliyowalazimu viongozi hao kuandaa msaada wa godoro na mahitaji mengine ya msingi.
Amua Rushita meneja na mtaalamu wa TEHAMA akitoa maelekezo jinsi redio inavyofanya kazi kutokea studio hadi kufikia kwa wasikilizaji(Picha na Musa Mtepa)
Wanafunzi wa Kidato cha Pili wa Dar es Salaam Independent School wametembelea Jamii FM Radio Mtwara kujifunza kuhusu vyombo vya habari na athari za mitandao ya kijamii , ikiwa ni sehemu ya somo la Mtazamo wa Kidunia (Global Perspective).
Na Musa Mtepa
Mtwara —-Wanafunzi wa Kidato cha Pili kutoka Dar es Salaam Independent School (DIS) leo, Oktoba 7, 2025, wametembelea kituo cha kurushia matangazo cha Jamii FM Radio kilichopo Mtwara, kwa lengo la kujifunza kwa vitendo kuhusu vyombo vya habari, hususan redio na mitandao ya kijamii.
Akizungumza kuhusiana na ujio huo, Meneja na Mtaalamu wa Masuala ya TEHAMA kutoka Jamii FM, Amua Rushita, amesema kuwa wanafunzi hao wamefika kituoni hapo ili kujifunza namna mitandao ya kijamii inavyoathiri vyombo vya habari (Traditional Media), pamoja na jinsi jamii inavyoweza kupata taarifa sahihi kupitia vyombo vya habari.
Sauti ya Amua Rushita – Meneja wa Jamii FM
Amua ameongeza kuwa moja ya sababu zilizowavutia wanafunzi kutembelea Jamii FM ni kutokana na namna vipindi vya redio hiyo vinavyogusa makundi yote ya jamii moja kwa moja.
Sauti ya Amua Rushita – Meneja wa Jamii FM
Kwa upande wake, Mwalimu, Donald kutoka Dar es Salaam Independent School, ameishukuru Jamii FM kupitia kwa Amua Rushita kwa kutoa elimu ya kina kuhusu aina mbili za vyombo vya habari faida na changamoto zake kwa jamii .
Pia amesema kuwa moja ya mambo waliokuja kujifunza Mtwara ni somo la Mtazamo wa Kidunia (Global Perspective), ambalo limejikita katika kueleza jinsi mitandao ya kijamii inavyoathiri Jamii hususani kwa upande wa vyombo vya habari.
Sauti ya Mr. Donald – Mwalimu, Dar es Salaam Independent School
Nao wanafunzi wa DIS wamesema kuwa ziara hiyo imewasaidia kuelewa kwa undani namna vyombo vya habari vinavyofanya kazi, na nafasi ya redio kama chanzo cha habari kinachoaminika katika jamii.
Sauti ya Wanafunzi wa Dar es Salaam Independent School
Nabii Nicolous Suguye akizungumza na Wanafunzi baada ya kutoa msaada katika shule ya Msingi Rahaleo (Picha na Musa Mtepa)
Nabii Ncolous Suguye ametoa msaada wa viti mwendo na chakula kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Kituo cha Upendo na Shule ya Msingi Rahaleo, Mtwara, kabla ya kuanza mkutano wa Injili utakaofanyika Oktoba 2, 2025, katika viwanja vya Sabasaba.
Na Musa Mtepa Oktoba 1, 2025 – Nabii Nicolous Suguye ametembelea na kutoa msaada wa viti mwendo pamoja na chakula kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Kituo cha Upendo na kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Msingi Rahaleo, iliyopo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Nabii Suguye amesema kuwa ziara yake Mtwara inalenga kufanikisha mkutano wa Injili, na kwamba ana utaratibu wa kuwatembelea na kuwasaidia watu wenye uhitaji kila anapofika katika maeneo tofauti kwa ajili ya huduma ya kiroho.
Sauti 1: Nabii Ncolous SuguyeNabii Suguye akiwa na Mtoto mwenye ulemavu katika kituo cha upendo kilichopo mtaa wa Mdenga ,Manispaa ya Mtwara Mikindani(Picha na Musa Mtepa)
Aidha, Nabii Suguye ametoa wito kwa jamii kutowatenga watu wenye ulemavu, bali kuendelea kuwaonesha upendo na kuwahudumia kwa moyo wa furaha.
Sauti 2: Nabii Ncolous Suguye
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Rahaleo na mlezi wa kitengo cha wanafunzi viziwi, Bi. Hilda Mapunda, amemshukuru Nabii Suguye kwa mchango wake, akisema kuwa msaada huo umeleta faraja na matumaini kwa watoto hao.
Sauti: Hilda Mapunda, Mwalimu Mkuu Msaidizi
Naye Meneja wa Kituo cha Upendo, Faustini Keha, ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa upendo kwa watoto wenye changamoto ya usonji, huku akimshukuru Nabii Suguye kwa msaada wa viti mwendo vinne na chakula.
Sauti: Fautini Kayeka, Meneja wa Kituo cha Upendo
Nabii Suguye anatarajia kuendesha mkutano mkubwa wa Injili kuanzia Oktoba 2, 2025, katika viwanja vya Sabasaba, Manispaa ya Mtwara Mikindani, ukiwa na ujumbe maalum: ‘Tokomeza Misukule.’
Nabii Suguye akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea kituo cha Upendo cha kulelea watoto wenye usonji na vichwa mfanano kilichopo Mtwara mjini (Picha na Musa Mtepa)
Watanzania wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, kuchagua viongozi watakaosimamia maendeleo ya taifa. Wito umetolewa na Nabii Nicolous Suguye wakati wa ziara yake kwenye vituo vya watoto wenye mahitaji maalum, akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika kulinda amani na kuchochea maendeleo ya jamii.
Na Musa Mtepa
Watanzania wamehimizwa kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29, 2025, kushiriki katika uchaguzi kwa ajili ya kuchagua viongozi watakaosimamia miradi ya maendeleo na maslahi ya wananchi na kuachana na dhana potofu ya kutoshiriki kupiga kura.
Wito huo umetolewa Oktoba 1, 2025, na kiongozi wa kiroho, Nabii Nicolous Suguye, alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Upendo pamoja na kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Msingi Rahaleo.
Amesema kuwa, kama kiongozi wa kiroho na raia Tanzania, ana jukumu la kuhakikisha anachangia kulinda amani ya nchi yake.
Sauti ya 1: Nabii Suguye
Aidha, Nabii Suguye amesema kuwa uchaguzi huu ni Watanzania wote, hivyo kila mwenye sifa ya kupiga kura anapaswa kuwajibika kwa kuchagua viongozi bora watakaoweka vipaumbele kwenye miundombinu na huduma muhimu kwa jamii.
Sauti ya 2: Nabii Suguye
Katika hatua nyingine, Nabii Suguye ameeleza kuwa oparesheni yake iitwayo “Komboa Misukule” inalenga kuwaokoa watu kiakili, kihisia, kiafya na kiroho, kwani wengi wamepoteza dira na fursa muhimu za maisha kutokana na vifungo vya kiakili na kiroho.
Sauti ya 3: Nabii Suguye
Nabii Suguye anatarajia kufanya mkutano mkubwa wa injili kuanzia Oktoba 2 hadi Oktoba 6, 2025, katika viwanja vya Sabasaba, vilivyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara ambapo katika mkutano huo, huduma mbalimbali za kiroho zinatarajiwa kutolewa kwa wananchi.
Wajumbe na wadau wa mamalaka ya usimamizi wa Bandari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika September 29,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa BOT kanda ya Mtwara
Bandari ya Mtwara imeongeza usafirishaji wa mizigo kwa asilimia 49 kati ya 2023/2024, ikihusisha korosho na makaa ya mawe, huku idadi ya makampuni ya meli ikiongezeka
Na Gregory Milanzi
Mtwara-September 29,2025 – Ukusanyaji na usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Mtwara umeongezeka kwa asilimia 49 katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hatua inayodhihirisha ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika ukanda wa kusini.
Akizungumza September 29, 2025 kwenye mkutano wa wadau wa bandari hiyo unaoendelea mkoani Mtwara, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi amesema bandari hiyo imesafirisha tani milioni 2.5 za mizigo kwa mwaka 2024/2025 kutoka tani milioni 1.7 kwa mwaka uliopita wa fedha.
Sauti ya Ferdinand Nyathi Meneja wa Bandari MtwaraFerdinand Nyath meneja wa Bandari ya Mtwara akiwa katika mkutano wa mamala ya usimamizi wa Bandari kuelekea msimu mpya wa zao la korosho
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA), Daniel Mallongo amesema Bandari ya Mtwara ni muhimu sana kwa usafirishaji wa zao la korosho, na kwamba idadi ya makampuni ya usafirishaji wa meli imeongezeka kutoka mawili hadi sita katika misimu mitatu iliyopita.
Sauti ya Daniel Malongo mwenyekiti TASAA
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Emanuel Mrutu amesema Bandari ya Mtwara haifanyi kazi msimu wa korosho pekee, bali imekuwa ikihudumia pia bidhaa nyingine kama makaa ya mawe.
Sauti ya Emanuel Mrutu mwakilishi mkurugenzi TPA
Mkutano huo wa wadau wa bandari unalenga kuangazia fursa na changamoto katika kuendeleza shughuli za usafirishaji kupitia Bandari ya Mtwara.
Wajumbe na wadau wa mamalaka ya usimamizi wa Bandari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika September 29,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa BOT kanda ya Mtwara
Bandari ya Mtwara imeongeza usafirishaji wa mizigo kwa asilimia 49 kati ya 2023/2024, ikihusisha korosho na makaa ya mawe, huku idadi ya makampuni ya meli ikiongezeka
Na Gregory Milanzi
Mtwara-September 29,2025 – Ukusanyaji na usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Mtwara umeongezeka kwa asilimia 49 katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hatua inayodhihirisha ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika ukanda wa kusini.
Akizungumza September 29, 2025 kwenye mkutano wa wadau wa bandari hiyo unaoendelea mkoani Mtwara, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi amesema bandari hiyo imesafirisha tani milioni 2.5 za mizigo kwa mwaka 2024/2025 kutoka tani milioni 1.7 kwa mwaka uliopita wa fedha.
Sauti ya Ferdinand Nyathi Meneja wa Bandari MtwaraFerdinand Nyath meneja wa Bandari ya Mtwara akiwa katika mkutano wa mamala ya usimamizi wa Bandari kuelekea msimu mpya wa zao la korosho
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA), Daniel Mallongo amesema Bandari ya Mtwara ni muhimu sana kwa usafirishaji wa zao la korosho, na kwamba idadi ya makampuni ya usafirishaji wa meli imeongezeka kutoka mawili hadi sita katika misimu mitatu iliyopita.
Sauti ya Daniel Malongo mwenyekiti TASAA
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Emanuel Mrutu amesema Bandari ya Mtwara haifanyi kazi msimu wa korosho pekee, bali imekuwa ikihudumia pia bidhaa nyingine kama makaa ya mawe.
Sauti ya Emanuel Mrutu mwakilishi mkurugenzi TPA
Mkutano huo wa wadau wa bandari unalenga kuangazia fursa na changamoto katika kuendeleza shughuli za usafirishaji kupitia Bandari ya Mtwara.