• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

TANESCO kuongeza uzalishaji wa umeme Mtwara

 

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Ngowele akizungumza na vyombo vya Habari wakati wa upokeaji wa mashine za uzalishaji umeme(Picha na Musa Mtepa)

TANESCO kuongeza uzalishaji wa umeme kwa MW 20 katika kituo cha Hiari, Mtwara, kukabiliana na upungufu wa umeme Lindi na Mtwara. Mashine mpya itakamilika ndani ya mwezi mmoja, ikiongeza uzalishaji hadi MW 70

Na Musa Mtepa

Mtwara, Tanzania – Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatarajia kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa megawati 20 katika kituo cha Hiari, mkoani Mtwara, ikiwa ni juhudi za kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Ngowele, amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme kufikia megawati 70, kutoka megawati 38 zinazohitajika kwa sasa.

Sauti ya , Bi. Irene Ngowele Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO

Ameongeza kuwa ufungaji wa mashine hiyo mpya unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, ambapo baada ya kukamilika, itasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme wa ziada ukilinganisha na matumizi ya kila siku.

Sauti ya 2, Bi. Irene Ngowele Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO

TANESCO imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa maeneo yote ya Tanzania, na hatua hii inatazamiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi na shughuli za kiuchumi za mikoa ya kusini.

Share:

Mtwara yapiga hatua dhidi ya talaka holela

 

Ofisi za Door of Hope Tanzania zilizopo katika mtaa wa Kiyangu Manispaa ya Mtwara Mikindani(Picha na Musa Mtepa)

Door of Hope Tanzania imewasilisha mrejesho wa mradi wa “Pinga Ukatili, Jenga Amani na Kizazi Chenye Usawa” mkoani Mtwara, ukilenga kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa msaada wa kisheria. Viongozi wamesifu mafanikio, ikiwemo kupungua kwa funga nyumba na talaka holela

Na Musa Mtepa

Shirika lisilo la Kiserikali la Door of Hope Tanzania, linalojihusisha na utetezi, uwezeshaji na usaidizi kwa vijana na wanawake nchini kupitia huduma za msaada wa kisheria bila malipo,limewasilisha mrejesho wa utekelezaji wa mradi wake wa “Pinga Ukatili, Jenga Amani na Kizazi Chenye Usawa” kwa wadau mbalimbali mkoani Mtwara.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TCCIA, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mheshimiwa Abdalla Mwaipaya, amesema kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia, hususan vitendo vya “funga nyumba” vinavyofanywa na baadhi ya wanaume, vimepungua ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Sauti ya Abdala Mwaipaya mkuu wa wilaya ya Mtwara

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope Tanzania, Clemence Mwombeki, amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kutoa mrejesho wa shughuli zilizotekelezwa kama sehemu ya mwendelezo wa mradi huo, sambamba na kuishauri serikali kuchukua hatua stahiki juu ya changamoto zilizobainika.

Sauti ya Clemence Mwombeki Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope Tanzania

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Bi. Athmini Mapalilo, amesema serikali imeanza kutoa mafunzo kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya mapato yanayotokana na zao la korosho. Aidha, ametoa rai kwa taasisi za kidini na mashirika ya kiraia kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya talaka holela na vitendo vya funga nyumba.

Sauti ya Bi. Athmini Mapalilo afisa maendelea ya jamii halmashauri ya wilaya ya Mtwara

Akichangia katika kikao hicho, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kata ya Mahurunga, Bi. Asmini Liwowa, pamoja na Bi. Fatuma Shaibu, mkazi wa Chikongola, walisisitiza umuhimu wa wadau kutoa elimu kwa familia kuhusu athari za talaka holela na namna zinavyowaathiri watoto na jamii kwa ujumla.

Sauti ya Asmini Liwowa na Fatuma Shaibu
Share:

CCM Mtwara Mjini yataka mafiga matatu Oktoba 29

 

Rehema Sombi makamu mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) taifa akizungumza na wananchi waliojitokea kwenye uzinduzi wa kampeni wa chama hicho (Picha na Musa Mtepa)

CCM Mtwara Mikindani yazindua kampeni Septemba 14, 2025, kwa wagombea ubunge na udiwani. Rehema Sombi ataka mshikamano na ushindi wa “mafiga matatu” – Diwani, Mbunge, Rais. Joel Nannauka na Arif Primji waahidi maendeleo na huduma bora kwa wananchi kupitia sera za CCM.

Na Musa Mtepa

Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mtwara Mikindani kimezindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, kwa upande wa mgombea ubunge na wagombea udiwani wa Jimbo la Mtwara Mjini.

Akizungumza kama mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Bi. Rehema Sombi, amewataka wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kudumisha mshikamano na kuhakikisha wanaweka “mafiga matatu” kwa kuchagua madiwani, mbunge na rais kutoka Chama cha Mapinduzi.

QUEIN….2 Rehema Sombi makamu mwenyekiti umoja wa vijana taifa

Kwa upande wake, mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CCM, Dkt Joel Nannauka, amesema kuwa ndoto yake ni kuibadilisha taswira ya Mtwara kutoka kuwa ya mwisho hadi kuwa ya mbele katika maendeleo ya kitaifa.

Sauti ya Dkt Joel Nannauka Mgombea ubunge CCM Mtwara mjini
Makamu Mwenyekiti uvccm Rehema Sombi akimkabidhi Mwongozo wa utekelezaji wa ilani Mgombea ubunge Mtwara Mjini Dkt Joel Nannauka(Picha na Musa Mtepa)

Naye mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Arif Primji, amewataka wananchi wa Manispaa ya Mtwara, ambao wanakadiriwa kufikia idadi ya watu 146,772, kuendelea kuiamini CCM kutokana na huduma mbalimbali za kijamii zilizowafikia kupitia serikali ya chama hicho.

Sauti ya Arif Primj Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara vijijini
Share:

Wananchi kijiji cha Nyengedi kuchangia 10,000 ujenzi wa shule

 

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyengedi wakisikiliza kwa umakini maelezo ya viongozi wao wa kata na kijiji katika mkutano (Picha na Musa Mtepa)

Wananchi wa Nyengedi wametakiwa kutekeleza kwa uaminifu makubaliano ya kuchangia shilingi 10,000 kwa kila kaya ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya Msingi Mnyengedi, mradi unaolenga kuboresha elimu na kupunguza adha ya watoto kutembea umbali mrefu

NA MUSA MTEPA

Wananchi wametakiwa kutekeleza kwa uaminifu makubaliano wanayoyafikia kwa hiari kupitia mikutano ya vijiji, ili kufanikisha malengo ya maendeleo ya pamoja.

Akizungumza kuhusu makubaliano ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Mnyengedi, Afisa Tarafa wa Mayanga, Bw. Marco Mapunda amesema wananchi wa kijiji cha Nyengedi wamekubaliana kila kaya ichangie kiasi cha shilingi 10,000.

Aidha Bw Mapunda amesema kwa yeyote ambae atakiuka kutokubali kuchangia atachukuliwa hatua za kisheria kama mwalifu mwingine.

Sauti ya Marco Mapunda afisa tarafa Mayanga

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyengedi, Bi Lukia Mnyachi, amesema kijiji hicho hapo awali kilikuwa kitongoji cha Kijiji cha Kawawa, na hivyo walikuwa wakitegemea huduma muhimu kutoka huko.

Aidha amesema kuwa hivyo kutokana na hali hiyo kupitia mikutano ya kijiji wakakubarina kutoa fedha shilingi 10,000 kwa ajili ya kununua uwanja tayari kwa mchakato wa ujenzi wa shule.

Sauti ya Lukia Mnyachi mwenyekiti wa Kijiji

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamepongeza juhudi za mwenyekiti wao na kuahidi kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa maendeleo.

Sauti ya Wananchi wa Nyengedi

Mradi huu wa ujenzi wa shule unalenga kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kijiji cha Nyengedi na kupunguza changamoto za kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

Share:

13 mbaloni kwa wizi wa pembejeo za korosho

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman akizungumza na Waandishi habari juu ya tukio la kukamatwa kwa watu 13 wanaotuhumiwa kwa wizi wa Pembejeo (Picha na Musa Mtepa)

Jeshi la Polisi Mtwara linawashikilia watuhumiwa 13 kwa tuhuma za wizi wa pembejeo za korosho zilizotolewa kwa wakulima msimu wa 2024/2025, wakiwemo watendaji wa serikali

Na Musa Mtepa

Mtwara, Septemba 10, 2025 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia watu 13 kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa pembejeo za kilimo zilizotolewa kwa wakulima wa korosho katika msimu wa mwaka 2024/2025.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 29, 2025 kufuatia operesheni maalum iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT).

Sauti ya 1 SACP Issa Suleima RPC Mtwara

Kamanda huyo pia ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha vitendo vya kuchepusha au kuiba pembejeo zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya wakulima.

Sauti ya 2 SACP Issa Suleima RPC Mtwara

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bw. Frances Alfred, amepongeza Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wake katika kuhakikisha usalama na uadilifu wakati wa msimu wa ugawaji wa pembejeo.

Sauti ya 1 Frances Alfred mkurugenzi wa CBT

Ameongeza kuwa uchunguzi umeanza katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba na maeneo mengine nayo yatafuata ili kuhakikisha kila mkulima anapata haki yake bila bugudha.

Sauti ya 1 Frances Alfred mkurugenzi wa CBT
Share:

Mwenyekiti atoa shukrani fidia ujenzi wa bandari kisiwa Mgao

 

Mwonekano wa eneo la ujenzi wa Bandari ya bidhaa chafu kabla hapajaanza maandalizi ya ujenzi hapo awali katika eneo la Kisiwa Mgao (Picha na Musa Mtepa)

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao ameishukuru Halmashauri ya Mtwara Vijijini kwa kulipa fidia ya ujenzi wa bandari Kisiwani Mgao, huku akitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari za kiafya kutokana na ongezeko la wageni.

Na Musa Mtepa

 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mgao, kilichopo Kata ya Naumbu, Mzee Shahame, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini kwa hatua ya kuwalipa fidia wakulima waliopisha ujenzi wa Bandari ya bidhaa chafu katika eneo la Kisiwa cha Mgao.

Akizungumza na Jamii FM Radio, Mzee Shahame amesema kuwa baada ya msuguano wa muda mrefu kati ya wananchi wa Kijiji cha Mgao, Kisiwa, na Halmashauri, hatimaye malipo ya fidia yamekamilika kwa wakulima husika. Aidha, amesema kuwa hadi sasa hakuna mwananchi yeyote kutoka kijijini kwake aliyefika kwake kulalamikia malipo hayo.

Sauti ya 1: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao

Aidha, Mzee Shahame amesema kuwa ujio wa bandari hiyo umepokelewa kwa mtazamo chanya kutokana na manufaa yake kwa taifa kwa ujumla. Hata hivyo, ameeleza kuwa bado ana mashaka juu ya wananchi wa kijiji chake kunufaika moja kwa moja kwa kupata ajira za muda (vibarua) katika mradi huo.

Sauti ya 2: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao

Pamoja na hayo, Mzee Shahame amesema kuwa maandalizi ya ujenzi wa bandari hiyo yameanza kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na ongezeko la wageni wanaofika kijijini hapo na kupanga kwenye nyumba za wenyeji, jambo linaloongeza mzunguko wa fedha katika kijiji hicho.

Sauti ya 3: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari za kiafya na kimazingira kutokana na ongezeko la wageni wanaoendelea kufika kijijini hapo.

Sauti ya 4: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao
Share:

Mwenyekiti wa kijiji aongoza ujenzi nyumba ya mwenye ulemavu Mtwara

 

Nyumba mpya aliyojengewa mzee Zomba mlemavu wa macho kwa jitihada za mwenyekiti wa kijiji cha Mnyengedi Bi lukia Mnyachi(Picha na Musa Mtepa)

Familia ya Mzee Salumu Zomba, mwenye ulemavu wa macho, yamekabidhiwa nyumba mpya baada ya kuishi kwenye kibanda kibovu, juhudi zilizowezeshwa na viongozi wa kijiji cha Mnyengedi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.

Na Musa Mtepa

Baada ya kuishi katika mazingira hatarishi kwa muda mrefu, familia ya Mzee Salumu Ismail Zomba, ambaye ni mlemavu wa macho, mkazi wa Kijiji cha Mnyengedi kata ya Mkunwa mkoani Mtwara, hatimaye imekabidhiwa nyumba mpya yenye vyumba viwili na ukumbi, ikiwa ni matokeo ya juhudi za pamoja zilizoongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyengedi, Bi Lukia Mnyachi.

Akitoa taarifa ya ujenzi wa nyumba hiyo, Mtendaji wa Kijiji cha Mnyengedi, Bi Ebby Hamisi, amesema kuwa familia ya Mzee Zomba hapo awali ilikuwa ikiishi katika kibanda kibovu ambacho hakikutoa hifadhi ya kutosha dhidi ya mvua na jua, hali iliyowaathiri hasa watoto waliokuwa wakiishi katika mazingira hayo.

Sauti ya 1 Bi Ebby Hamisi Mtendaji wa Kijiji cha Nyengedi

Aidha, Bi Ebby ameeleza kuwa licha ya mafanikio ya ujenzi huo, familia hiyo bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha. Alitoa shukrani kwa wadau wote waliosaidia kufanikisha ujenzi huo, wakiwemo kituo cha redio cha Jamii FM kilichopo Naliendele, Mtwara.

Sauti ya 2 Bi Ebby Hamisi Mtendaji wa Kijiji cha Nyengedi

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Afisa Tarafa wa Mayanga, Bw. Marco Mapunda, amewapongeza wote waliojitolea katika kusaidia familia hiyo na kusema kuwa kitendo hicho ni mfano bora wa mshikamano wa kijamii na namna viongozi wanavyoweza kuwa chachu ya maendeleo kwa watu wenye uhitaji.

Sauti ya 1 Marco Mapunda afisa tarafa tarafa ya Mayanga
Marco Mapunda akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye kukabidhi nyumba ya Bw Zomba (Picha na Musa Mtepa)

Pia afisa tarafa ameahidi kuzibeba na kuzifanyia kazi changamoto zote zilizowasishwa kupitia risala iliyosomwa na afisa mtendaji wa Kijiji cha Nyengedi Bi Ebby Hamisi kwa kuziwasilisha katika ofisi ya mkuu wa wilaya na kuona namna ya kuisaidia familia hiyo

Sauti ya 2 Marco Mapunda afisa tarafa tarafa ya Mayanga

Kwa upande wake, Bi Lukia Mnyachi, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyengedi, alielezea jinsi alivyoguswa na hali ya maisha ya Mzee Zomba na kuamua kuanzisha juhudi za kutafuta msaada ili kumjengea nyumba.

Sauti ya Bi Lukia Mnyachi Mwenyekiti wa Kijiji cha Mnyengedi
Mwenyekiti wa kijiji cha Nyengedi akielezea jitihada zilizofanyika hadi kukamilika kwa ujenzi wa Nyumba ya Mzee Salumu Zomba mlemavu wa Macho na Mkazi wa kijiji cha Mnyengedi mkoani Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Mzee Salumu Zomba, akizungumza kwa furaha, ameshukuru kwa jitihada kubwa zilizofanywa na viongozi na wadau waliomsaidia kupata makazi bora. Hata hivyo, ametumia nafasi hiyo kuomba msaada zaidi wa vitanda, magodoro, na mahitaji ya watoto wake wanaosoma.

Sauti ya Mzee Salumu Zomba mlemavu wa macho
Mzee Salumu Zomba akiwa na mke wake wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kibanda walichokuwa wanaishi na watoto wao kabla ya Mwenyekiti wa kijiji Bi Lukia Mnyachi kufanikisha ujenzi wa Nyumba Mpya(Picha na Musa Mtepa)

Majirani wa Mzee Zomba pia wameelezea hali ngumu ya maisha anayopitia, wakisisitiza kuwa kwa kuwa ni mlemavu wa macho, anahitaji msaada wa mara kwa mara kutoka kwa jamii na serikali.

Sauti ya majirani wa Mzee Zomba
Mwonekano wa awali wa Nyumba ya Mzee Zomba kabla hajaporomoka na Mvua na kujenga kibanda kidogo cha kuishi (Picha na Musa Mtepa)
Share:

JWTZ yaadhimisha miaka 61 kwa shughuli za kijamii, michezo Mtwara

 

vikosi vya jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ ) wakiwa katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwake katika viwanja vya Nangwanda Sijaona Mjini Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

JWTZ limeadhimisha miaka 61 tangu kuanzishwa kwake kwa kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo uchangiaji damu na mpira wa kirafiki dhidi ya Jeshi la Polisi, katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, Mtwara

Na Musa Mtepa

Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) leo Septemba 1, 2025, limeadhimisha miaka 61 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964, kufuatia kuondoka kwa jeshi la kikoloni.

Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, yakiongozwa na Mkuu wa Vikosi na Vikundi vya JWTZ mkoa wa Mtwara (Base Commander), Kanali James Simon Mwakinyuke.

Kanali Mwakinyuke amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo kuelekea katika maadhimisho hayo huambatana na ufanyaji wa shughuli mbalimbali za kijamii

Sauti ya 1 Kanali James Mwakinyuke mkuu wa vikosi vya JWTZ Mtwara
Kanali James Simon Mwakinyuke akizungumza na Waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa JWTZ yaliyofanyika katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Aidha, Kanali Mwakinyuke amesema katika kilele cha maadhimisho ya mwaka huu, Jeshi la Wananchi mkoani Mtwara limejitoa kushiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu kupitia Mfuko wa Damu Salama – Kanda ya Kusini, pamoja na kucheza mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu kati ya JWTZ na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara.

Sauti ya 2 Kanali James Mwakinyuke mkuu wa vikosi vya JWTZ Mtwara
Miongoni mwaafisa wa Jeshi la Wananchi la Tanzania akiwa katika hatua za mwisho za vipimo tayari kwa kuchangia Damu katika mfuko wa taifa wa Damu Salama (Picha na Musa Mtepa)

Huu ni utaratibu wa kawaida kwa JWTZ mkoani Mtwara ambapo Mwaka jana walifanya usafi katika eneo la Mashujaa na tukachangia damu katika Zahanati ya Jeshi ya 665 Alignment.

Maadhimisho haya ni sehemu ya mwendelezo wa JWTZ kushirikiana na jamii kwa njia za kijamii na kijeshi, ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na mshikamano ndani ya nchi.

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>