
CCM Mtwara Mikindani yazindua kampeni Septemba 14, 2025, kwa wagombea ubunge na udiwani. Rehema Sombi ataka mshikamano na ushindi wa “mafiga matatu” – Diwani, Mbunge, Rais. Joel Nannauka na Arif Primji waahidi maendeleo na huduma bora kwa wananchi kupitia sera za CCM.
Na Musa Mtepa
Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mtwara Mikindani kimezindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, kwa upande wa mgombea ubunge na wagombea udiwani wa Jimbo la Mtwara Mjini.
Akizungumza kama mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Bi. Rehema Sombi, amewataka wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kudumisha mshikamano na kuhakikisha wanaweka “mafiga matatu” kwa kuchagua madiwani, mbunge na rais kutoka Chama cha Mapinduzi.
Kwa upande wake, mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CCM, Dkt Joel Nannauka, amesema kuwa ndoto yake ni kuibadilisha taswira ya Mtwara kutoka kuwa ya mwisho hadi kuwa ya mbele katika maendeleo ya kitaifa.

Naye mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Arif Primji, amewataka wananchi wa Manispaa ya Mtwara, ambao wanakadiriwa kufikia idadi ya watu 146,772, kuendelea kuiamini CCM kutokana na huduma mbalimbali za kijamii zilizowafikia kupitia serikali ya chama hicho.







No comments:
Post a Comment