
JWTZ limeadhimisha miaka 61 tangu kuanzishwa kwake kwa kushiriki shughuli za kijamii ikiwemo uchangiaji damu na mpira wa kirafiki dhidi ya Jeshi la Polisi, katika viwanja vya Nangwanda Sijaona, Mtwara
Na Musa Mtepa
Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) leo Septemba 1, 2025, limeadhimisha miaka 61 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964, kufuatia kuondoka kwa jeshi la kikoloni.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, yakiongozwa na Mkuu wa Vikosi na Vikundi vya JWTZ mkoa wa Mtwara (Base Commander), Kanali James Simon Mwakinyuke.
Kanali Mwakinyuke amesema kuwa maadhimisho hayo ni kumbukizi ya kuzaliwa kwake ambapo kuelekea katika maadhimisho hayo huambatana na ufanyaji wa shughuli mbalimbali za kijamii

Aidha, Kanali Mwakinyuke amesema katika kilele cha maadhimisho ya mwaka huu, Jeshi la Wananchi mkoani Mtwara limejitoa kushiriki katika zoezi la uchangiaji wa damu kupitia Mfuko wa Damu Salama – Kanda ya Kusini, pamoja na kucheza mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu kati ya JWTZ na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara.

Huu ni utaratibu wa kawaida kwa JWTZ mkoani Mtwara ambapo Mwaka jana walifanya usafi katika eneo la Mashujaa na tukachangia damu katika Zahanati ya Jeshi ya 665 Alignment.
Maadhimisho haya ni sehemu ya mwendelezo wa JWTZ kushirikiana na jamii kwa njia za kijamii na kijeshi, ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na mshikamano ndani ya nchi.







No comments:
Post a Comment