
TANESCO kuongeza uzalishaji wa umeme kwa MW 20 katika kituo cha Hiari, Mtwara, kukabiliana na upungufu wa umeme Lindi na Mtwara. Mashine mpya itakamilika ndani ya mwezi mmoja, ikiongeza uzalishaji hadi MW 70
Na Musa Mtepa
Mtwara, Tanzania – Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatarajia kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa megawati 20 katika kituo cha Hiari, mkoani Mtwara, ikiwa ni juhudi za kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Ngowele, amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme kufikia megawati 70, kutoka megawati 38 zinazohitajika kwa sasa.

Ameongeza kuwa ufungaji wa mashine hiyo mpya unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, ambapo baada ya kukamilika, itasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme wa ziada ukilinganisha na matumizi ya kila siku.

TANESCO imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa maeneo yote ya Tanzania, na hatua hii inatazamiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi na shughuli za kiuchumi za mikoa ya kusini.






No comments:
Post a Comment