
Jeshi la Polisi Mtwara linawashikilia watuhumiwa 13 kwa tuhuma za wizi wa pembejeo za korosho zilizotolewa kwa wakulima msimu wa 2024/2025, wakiwemo watendaji wa serikali
Na Musa Mtepa
Mtwara, Septemba 10, 2025 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia watu 13 kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa pembejeo za kilimo zilizotolewa kwa wakulima wa korosho katika msimu wa mwaka 2024/2025.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 29, 2025 kufuatia operesheni maalum iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT).
Kamanda huyo pia ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha vitendo vya kuchepusha au kuiba pembejeo zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya wakulima.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bw. Frances Alfred, amepongeza Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wake katika kuhakikisha usalama na uadilifu wakati wa msimu wa ugawaji wa pembejeo.
Ameongeza kuwa uchunguzi umeanza katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba na maeneo mengine nayo yatafuata ili kuhakikisha kila mkulima anapata haki yake bila bugudha.






No comments:
Post a Comment