• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Mgombea udiwani Chuno ataka ushirikiano wa wanawake katika siasa

 

Bi Mariamu Chimbwahi akiwa katika studio za jamii fm Redio akizungumza na Wananchi juu ya ushiriki wa wanawake katika Siasa na Changamoto wanazokutananazo (Picha na Musa Mtepa)

Mgombea udiwani Kata ya Chuno kupitia CCM, Mariamu Chimbwahi, amewataka wanawake kuanza uongozi ngazi za chini ili kujijengea uzoefu, huku akihimiza ushirikiano baina yao na kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kujitegemea

Na Musa Mtepa

Wanawake wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za chini, ili kujijengea uzoefu na kujiamini kabla ya kuwania nafasi za juu katika uongozi wa kisiasa na kijamii.

Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 29, 2025, na mgombea udiwani wa Kata ya Chuno, Manispaa ya Mtwara Mikindani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariamu Chimbwahi, wakati akizungumza katika kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio.

Bi. Chimbwahi amesema licha ya kuwepo kwa jitihada za kuwawezesha wanawake kisiasa, bado ni muhimu kwao kuanza uongozi kutoka ngazi ya chini ili kupata uzoefu wa kusimama jukwaani, kujibu hoja, na kushiriki mijadala ya kisiasa kwa ufanisi.

Sauti ya 1: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno
Mgombea udiwani kata ya Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi Mariamu Chimbwahi akiwa katika Studio za jamii fm Redio(Picha na Musa Mtepa)

Aidha, Mariamu Chimbwahi ametoa wito kwa wanawake kutoa ushirikiano wa dhati kwa wanawake wenzao pindi wanapoamua kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, huku akitaka jamii kuachana na dhana potofu kwamba “adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake”.

Sauti ya 2: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno

Katika hatua nyingine, Bi. Chimbwahi amesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Chuno, atahakikisha anawahamasisha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi zitakazowawezesha kujitegemea, kulea familia zao kwa ufanisi, na kuwawezesha watoto kupata elimu bora.

Sauti ya 3: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno
Share:

Watoto kuacha shule chanzo viashiria vya uvunjifu wa amani

 

Maafisa kutokashirika la TASA Tanzania wakiwa katika studio za Jamii fm redio zizopo Mtwara Mjini mtaa wa Naliende (Picha na Musa Mtepa)

Mdondoko wa wanafunzi na ukatili wa kijinsia vyatajwa kuchangia ongezeko la vitendo vinavyohatarisha amani katika jamii , huku wazazi wakilaumiwa kwa kulegeza majukumu ya malezi na ufuatiliaji wa watoto wao

Na Musa Mtepa

Mtwara, Septemba 24, 2025 – Ukatili wa kijinsia pamoja na mdondoko wa wanafunzi mashuleni vimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochochea viashiria vya uvunjifu wa amani katika jamii.

Akizungumza katika kipindi Dira ya Asubuhi kinachorushwa na  Jamii FM radio tarehe 24 Septemba, 2025, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Safety Alliance (TASA), Bw. Hamisi Mwinshekhe, amesema wanafunzi wanaokumbwa na changamoto ya kuacha shule hukosa mwelekeo wa maisha, hali inayowafanya kuwa rahisi kushawishika kujiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.

Sauti ya Hamisi Mwinshekhe, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji – TASA

Bw. Mwinshekhe ameongeza kuwa chanzo kikuu cha mdondoko wa wanafunzi ni kulegalega kwa wazazi katika jukumu la malezi. Ameeleza kuwa baadhi ya wazazi huacha watoto wao kulelewa na mazingira ya mitaani, jambo linalowapelekea vijana hao kujiunga na makundi hatarishi.

Sauti ya Hamisi Mwinshekhe, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji – TASA

Kwa upande wake, Mratibu wa Miradi kutoka shirika la TASA, Bi. Betty Chenge, amesema wazazi wengi wamekuwa wakiwaachia walimu jukumu la malezi na ufuatiliaji wa watoto wao, badala ya kushirikiana nao kikamilifu. Hali hiyo, amesema, imekuwa chanzo cha ongezeko la utoro na mdondoko mashuleni.

Sauti ya 1 Betty Chenge, Afisa Miradi – TASA

Aidha, Bi. Chenge ameisisitiza jamii kutambua kuwa malezi ya mtoto si jukumu la mtu mmoja pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha mtoto anapata mahitaji yake ya msingi. Ameongeza kuwa jamii inapaswa kuwasaidia watoto wanaoonesha viashiria vya mienendo hatarishi kwa kuwaelimisha na kuwaongoza katika njia sahihi.

Sauti ya 2 Betty Chenge, Afisa Miradi – TASA

Katika mjadala huo, baadhi ya wasikilizaji waliopiga simu kushiriki kipindi wamelishukuru shirika la TASA kwa elimu waliyopatiwa, huku wakikiri kuwa uzembe wa malezi kutoka kwa baadhi ya wazazi umekuwa chanzo kikuu cha mdondoko wa wanafunzi na kushiriki kwao katika vitendo vinavyohatarisha amani ya jamii.

Sauti za wasikilizaji wakichangia kwa njia ya simu

Shirika la Tanzania Safety Alliance (TASA) kwa sasa linatekeleza mradi wa “Amani Yetu Kesho Yetu” , unaotekelezwa katika kata tano za Halmashauri ya Mtwara Vijijini ambazo ni MadimbaTangazoNalinguMsimbati, na Mahurunga.

Share:

TANESCO kuongeza uzalishaji wa umeme Mtwara

 

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Ngowele akizungumza na vyombo vya Habari wakati wa upokeaji wa mashine za uzalishaji umeme(Picha na Musa Mtepa)

TANESCO kuongeza uzalishaji wa umeme kwa MW 20 katika kituo cha Hiari, Mtwara, kukabiliana na upungufu wa umeme Lindi na Mtwara. Mashine mpya itakamilika ndani ya mwezi mmoja, ikiongeza uzalishaji hadi MW 70

Na Musa Mtepa

Mtwara, Tanzania – Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatarajia kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa megawati 20 katika kituo cha Hiari, mkoani Mtwara, ikiwa ni juhudi za kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Ngowele, amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme kufikia megawati 70, kutoka megawati 38 zinazohitajika kwa sasa.

Sauti ya , Bi. Irene Ngowele Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO

Ameongeza kuwa ufungaji wa mashine hiyo mpya unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, ambapo baada ya kukamilika, itasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme wa ziada ukilinganisha na matumizi ya kila siku.

Sauti ya 2, Bi. Irene Ngowele Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO

TANESCO imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa maeneo yote ya Tanzania, na hatua hii inatazamiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi na shughuli za kiuchumi za mikoa ya kusini.

Share:

Mtwara yapiga hatua dhidi ya talaka holela

 

Ofisi za Door of Hope Tanzania zilizopo katika mtaa wa Kiyangu Manispaa ya Mtwara Mikindani(Picha na Musa Mtepa)

Door of Hope Tanzania imewasilisha mrejesho wa mradi wa “Pinga Ukatili, Jenga Amani na Kizazi Chenye Usawa” mkoani Mtwara, ukilenga kupinga ukatili wa kijinsia na kutoa msaada wa kisheria. Viongozi wamesifu mafanikio, ikiwemo kupungua kwa funga nyumba na talaka holela

Na Musa Mtepa

Shirika lisilo la Kiserikali la Door of Hope Tanzania, linalojihusisha na utetezi, uwezeshaji na usaidizi kwa vijana na wanawake nchini kupitia huduma za msaada wa kisheria bila malipo,limewasilisha mrejesho wa utekelezaji wa mradi wake wa “Pinga Ukatili, Jenga Amani na Kizazi Chenye Usawa” kwa wadau mbalimbali mkoani Mtwara.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa TCCIA, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mheshimiwa Abdalla Mwaipaya, amesema kuwa matukio ya ukatili wa kijinsia, hususan vitendo vya “funga nyumba” vinavyofanywa na baadhi ya wanaume, vimepungua ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Sauti ya Abdala Mwaipaya mkuu wa wilaya ya Mtwara

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope Tanzania, Clemence Mwombeki, amesema kuwa lengo la kikao hicho ni kutoa mrejesho wa shughuli zilizotekelezwa kama sehemu ya mwendelezo wa mradi huo, sambamba na kuishauri serikali kuchukua hatua stahiki juu ya changamoto zilizobainika.

Sauti ya Clemence Mwombeki Mkurugenzi Mtendaji wa Door of Hope Tanzania

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, Bi. Athmini Mapalilo, amesema serikali imeanza kutoa mafunzo kwa jamii juu ya matumizi sahihi ya mapato yanayotokana na zao la korosho. Aidha, ametoa rai kwa taasisi za kidini na mashirika ya kiraia kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara ya talaka holela na vitendo vya funga nyumba.

Sauti ya Bi. Athmini Mapalilo afisa maendelea ya jamii halmashauri ya wilaya ya Mtwara

Akichangia katika kikao hicho, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Kata ya Mahurunga, Bi. Asmini Liwowa, pamoja na Bi. Fatuma Shaibu, mkazi wa Chikongola, walisisitiza umuhimu wa wadau kutoa elimu kwa familia kuhusu athari za talaka holela na namna zinavyowaathiri watoto na jamii kwa ujumla.

Sauti ya Asmini Liwowa na Fatuma Shaibu
Share:

CCM Mtwara Mjini yataka mafiga matatu Oktoba 29

 

Rehema Sombi makamu mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) taifa akizungumza na wananchi waliojitokea kwenye uzinduzi wa kampeni wa chama hicho (Picha na Musa Mtepa)

CCM Mtwara Mikindani yazindua kampeni Septemba 14, 2025, kwa wagombea ubunge na udiwani. Rehema Sombi ataka mshikamano na ushindi wa “mafiga matatu” – Diwani, Mbunge, Rais. Joel Nannauka na Arif Primji waahidi maendeleo na huduma bora kwa wananchi kupitia sera za CCM.

Na Musa Mtepa

Chama cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mtwara Mikindani kimezindua rasmi kampeni zake kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, kwa upande wa mgombea ubunge na wagombea udiwani wa Jimbo la Mtwara Mjini.

Akizungumza kama mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Bi. Rehema Sombi, amewataka wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla kudumisha mshikamano na kuhakikisha wanaweka “mafiga matatu” kwa kuchagua madiwani, mbunge na rais kutoka Chama cha Mapinduzi.

QUEIN….2 Rehema Sombi makamu mwenyekiti umoja wa vijana taifa

Kwa upande wake, mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CCM, Dkt Joel Nannauka, amesema kuwa ndoto yake ni kuibadilisha taswira ya Mtwara kutoka kuwa ya mwisho hadi kuwa ya mbele katika maendeleo ya kitaifa.

Sauti ya Dkt Joel Nannauka Mgombea ubunge CCM Mtwara mjini
Makamu Mwenyekiti uvccm Rehema Sombi akimkabidhi Mwongozo wa utekelezaji wa ilani Mgombea ubunge Mtwara Mjini Dkt Joel Nannauka(Picha na Musa Mtepa)

Naye mgombea ubunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Arif Primji, amewataka wananchi wa Manispaa ya Mtwara, ambao wanakadiriwa kufikia idadi ya watu 146,772, kuendelea kuiamini CCM kutokana na huduma mbalimbali za kijamii zilizowafikia kupitia serikali ya chama hicho.

Sauti ya Arif Primj Mgombea Ubunge jimbo la Mtwara vijijini
Share:

Wananchi kijiji cha Nyengedi kuchangia 10,000 ujenzi wa shule

 

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Nyengedi wakisikiliza kwa umakini maelezo ya viongozi wao wa kata na kijiji katika mkutano (Picha na Musa Mtepa)

Wananchi wa Nyengedi wametakiwa kutekeleza kwa uaminifu makubaliano ya kuchangia shilingi 10,000 kwa kila kaya ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya Msingi Mnyengedi, mradi unaolenga kuboresha elimu na kupunguza adha ya watoto kutembea umbali mrefu

NA MUSA MTEPA

Wananchi wametakiwa kutekeleza kwa uaminifu makubaliano wanayoyafikia kwa hiari kupitia mikutano ya vijiji, ili kufanikisha malengo ya maendeleo ya pamoja.

Akizungumza kuhusu makubaliano ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Msingi Mnyengedi, Afisa Tarafa wa Mayanga, Bw. Marco Mapunda amesema wananchi wa kijiji cha Nyengedi wamekubaliana kila kaya ichangie kiasi cha shilingi 10,000.

Aidha Bw Mapunda amesema kwa yeyote ambae atakiuka kutokubali kuchangia atachukuliwa hatua za kisheria kama mwalifu mwingine.

Sauti ya Marco Mapunda afisa tarafa Mayanga

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyengedi, Bi Lukia Mnyachi, amesema kijiji hicho hapo awali kilikuwa kitongoji cha Kijiji cha Kawawa, na hivyo walikuwa wakitegemea huduma muhimu kutoka huko.

Aidha amesema kuwa hivyo kutokana na hali hiyo kupitia mikutano ya kijiji wakakubarina kutoa fedha shilingi 10,000 kwa ajili ya kununua uwanja tayari kwa mchakato wa ujenzi wa shule.

Sauti ya Lukia Mnyachi mwenyekiti wa Kijiji

Baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamepongeza juhudi za mwenyekiti wao na kuahidi kushiriki kikamilifu kwenye mchakato wa maendeleo.

Sauti ya Wananchi wa Nyengedi

Mradi huu wa ujenzi wa shule unalenga kuboresha upatikanaji wa elimu kwa watoto wa kijiji cha Nyengedi na kupunguza changamoto za kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

Share:

13 mbaloni kwa wizi wa pembejeo za korosho

 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman akizungumza na Waandishi habari juu ya tukio la kukamatwa kwa watu 13 wanaotuhumiwa kwa wizi wa Pembejeo (Picha na Musa Mtepa)

Jeshi la Polisi Mtwara linawashikilia watuhumiwa 13 kwa tuhuma za wizi wa pembejeo za korosho zilizotolewa kwa wakulima msimu wa 2024/2025, wakiwemo watendaji wa serikali

Na Musa Mtepa

Mtwara, Septemba 10, 2025 – Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia watu 13 kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa pembejeo za kilimo zilizotolewa kwa wakulima wa korosho katika msimu wa mwaka 2024/2025.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, SACP Issa Suleiman, amesema watuhumiwa hao walikamatwa Agosti 29, 2025 kufuatia operesheni maalum iliyoendeshwa kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na usalama na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT).

Sauti ya 1 SACP Issa Suleima RPC Mtwara

Kamanda huyo pia ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya ushirika pamoja na wananchi kwa ujumla kuacha vitendo vya kuchepusha au kuiba pembejeo zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya wakulima.

Sauti ya 2 SACP Issa Suleima RPC Mtwara

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Bw. Frances Alfred, amepongeza Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wake katika kuhakikisha usalama na uadilifu wakati wa msimu wa ugawaji wa pembejeo.

Sauti ya 1 Frances Alfred mkurugenzi wa CBT

Ameongeza kuwa uchunguzi umeanza katika Halmashauri ya Mji wa Nanyamba na maeneo mengine nayo yatafuata ili kuhakikisha kila mkulima anapata haki yake bila bugudha.

Sauti ya 1 Frances Alfred mkurugenzi wa CBT
Share:

Mwenyekiti atoa shukrani fidia ujenzi wa bandari kisiwa Mgao

 

Mwonekano wa eneo la ujenzi wa Bandari ya bidhaa chafu kabla hapajaanza maandalizi ya ujenzi hapo awali katika eneo la Kisiwa Mgao (Picha na Musa Mtepa)

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao ameishukuru Halmashauri ya Mtwara Vijijini kwa kulipa fidia ya ujenzi wa bandari Kisiwani Mgao, huku akitoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari za kiafya kutokana na ongezeko la wageni.

Na Musa Mtepa

 Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Mgao, kilichopo Kata ya Naumbu, Mzee Shahame, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Vijijini kwa hatua ya kuwalipa fidia wakulima waliopisha ujenzi wa Bandari ya bidhaa chafu katika eneo la Kisiwa cha Mgao.

Akizungumza na Jamii FM Radio, Mzee Shahame amesema kuwa baada ya msuguano wa muda mrefu kati ya wananchi wa Kijiji cha Mgao, Kisiwa, na Halmashauri, hatimaye malipo ya fidia yamekamilika kwa wakulima husika. Aidha, amesema kuwa hadi sasa hakuna mwananchi yeyote kutoka kijijini kwake aliyefika kwake kulalamikia malipo hayo.

Sauti ya 1: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao

Aidha, Mzee Shahame amesema kuwa ujio wa bandari hiyo umepokelewa kwa mtazamo chanya kutokana na manufaa yake kwa taifa kwa ujumla. Hata hivyo, ameeleza kuwa bado ana mashaka juu ya wananchi wa kijiji chake kunufaika moja kwa moja kwa kupata ajira za muda (vibarua) katika mradi huo.

Sauti ya 2: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao

Pamoja na hayo, Mzee Shahame amesema kuwa maandalizi ya ujenzi wa bandari hiyo yameanza kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na ongezeko la wageni wanaofika kijijini hapo na kupanga kwenye nyumba za wenyeji, jambo linaloongeza mzunguko wa fedha katika kijiji hicho.

Sauti ya 3: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari za kiafya na kimazingira kutokana na ongezeko la wageni wanaoendelea kufika kijijini hapo.

Sauti ya 4: Mzee Shahame – Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgao
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>