Mgombea udiwani Chuno ataka ushirikiano wa wanawake katika siasa

 

Bi Mariamu Chimbwahi akiwa katika studio za jamii fm Redio akizungumza na Wananchi juu ya ushiriki wa wanawake katika Siasa na Changamoto wanazokutananazo (Picha na Musa Mtepa)

Mgombea udiwani Kata ya Chuno kupitia CCM, Mariamu Chimbwahi, amewataka wanawake kuanza uongozi ngazi za chini ili kujijengea uzoefu, huku akihimiza ushirikiano baina yao na kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kujitegemea

Na Musa Mtepa

Wanawake wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za chini, ili kujijengea uzoefu na kujiamini kabla ya kuwania nafasi za juu katika uongozi wa kisiasa na kijamii.

Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 29, 2025, na mgombea udiwani wa Kata ya Chuno, Manispaa ya Mtwara Mikindani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariamu Chimbwahi, wakati akizungumza katika kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio.

Bi. Chimbwahi amesema licha ya kuwepo kwa jitihada za kuwawezesha wanawake kisiasa, bado ni muhimu kwao kuanza uongozi kutoka ngazi ya chini ili kupata uzoefu wa kusimama jukwaani, kujibu hoja, na kushiriki mijadala ya kisiasa kwa ufanisi.

Sauti ya 1: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno
Mgombea udiwani kata ya Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi Mariamu Chimbwahi akiwa katika Studio za jamii fm Redio(Picha na Musa Mtepa)

Aidha, Mariamu Chimbwahi ametoa wito kwa wanawake kutoa ushirikiano wa dhati kwa wanawake wenzao pindi wanapoamua kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, huku akitaka jamii kuachana na dhana potofu kwamba “adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake”.

Sauti ya 2: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno

Katika hatua nyingine, Bi. Chimbwahi amesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Chuno, atahakikisha anawahamasisha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi zitakazowawezesha kujitegemea, kulea familia zao kwa ufanisi, na kuwawezesha watoto kupata elimu bora.

Sauti ya 3: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno
Share:

No comments:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>