• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Wanawake waliovunja ukimya, safari ya Coletha, Zaituni kisiasa

2 August 2025, 15:18 pm

Coletha Chiponde na Zaituni Selemani Namkola wakizungumza na Mwanaidi Kopakopa (hayupo pichani) Picha na mwandishi wetu

Na Mwanaidi Kopakopa

Walizunguka kwa miguu, walikutana na wananchi, wakahamasisha, na walipambana kwa hali na mali kuhakikisha sauti ya mwanamke inasikika katika uongozi wa ngazi ya chini

Na Mwanaidi Kopakopa

Katika miaka ya karibuni, Tanzania imeanza kushuhudia mwamko mpya wa wanawake kushiriki kikamilifu katika uongozi, hasa kwenye siasa za mitaa. Katika mazingira ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakitawaliwa na wanaume, wanawake sasa wanasimama kidete kudai nafasi zao za uongozi si kwa maneno tu, bali kwa vitendo.

Katika kona ya kusini mwa Tanzania, mabadiliko haya yanaanza kuchipua, si kwa baraka za kisiasa, bali kwa sauti zenye uthubutu na dhamira ya kweli kutoka kwa wanawake. Katika kata za Mkunwa na Libobe, wanawake wawili jasiri Coletha Chiponde na Zaituni Selemani Namkola waliamua kuvunja ukimya. Walichukua fomu na kujitokeza kuwania nafasi za udiwani katika kata zao. Walizunguka kwa miguu, walikutana na wananchi, wakahamasisha, na walipambana kwa hali na mali kuhakikisha sauti ya mwanamke inasikika katika uongozi wa ngazi ya chini.

Hata hivyo, licha ya jitihada kubwa walizofanya, majina yao hayakufanikiwa kupenya katika hatua ya kura za maoni. Lakini huu si mwisho wa safari. Ushiriki wao umeacha alama, umeleta majadiliano, umeibua matumaini mapya kwa wanawake na wasichana wengine katika jamii zao. Ni ushahidi wa wazi kuwa demokrasia ya kweli huanza kwa ujasiri wa mtu mmoja au wawili kusimama na kusema: “Naweza.”

Coletha na Zaituni wametoa mfano wa kuigwa. Safari yao ni mwanga kwa kizazi kijacho cha viongozi wanawake walioshikilia imani kuwa uongozi bora huanzia mtaani, kijijini, na katika vikao vya kata. Ni wajibu wa jamii sasa kuenzi jitihada hizi, kuunga mkono usawa wa kijinsia, na kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa ya kushiriki katika maamuzi yanayoathiri maisha yao ya kila siku.

Bonyeza hapa kusikiliza makala haya

Share:

Wanachama CCM Msimbati watishia kujiondoa uanachama

 

Wanachama wa CCM wakiwa katika ofisi ya chama wakipinga kuondolewa kwa jina la Rashidi Linkoni aliyeshinda kwenye kura za maoni(Picha na Musa Mtepa)

Wanachama zaidi ya 150 wa CCM Msimbati wamelalamikia kuondolewa kwa jina la Rashidi Linkoni aliyeshinda kura za maoni, wakitishia kurudisha kadi zao, huku viongozi wa wilaya wakisisitiza maamuzi ya kamati ya siasa

Na Musa Mtepa

Zaidi ya wanachama 150 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Msimbati, wilayani Mtwara Vijijini, wameonesha kutoridhishwa na kitendo cha kuondolewa jina la Rashidi Omari Linkoni, aliyeshinda kura za maoni kwa kura 116, na kurejeshwa jina la Abrehemani Hamisi aliyeshika nafasi ya pili kwa kura 101.

Wanachama hao, wakizungumza na Jamii FM Agosti 17, 2025, wamesema hatua hiyo ni dharau kwa maamuzi ya wajumbe na kutishia kurudisha kadi za chama.

Sauti ya Wanachama wa CCM Kata ya Msimbati
Baadhi ya kadi za Wanachama wa CCM wa kata ya Msimbati zilizo rejeshwa na kutupwa baada ya wanachama kutoridhishwa na kitendo cha kuenguliwa mgombea aliyepitishwa na wajumbe Kwenye kura za maoni

Mzee Musa Ali maarufu kama Mzee Chituka, muasisi wa CCM kata ya Msimbati, amesema kitendo hicho kimekwenda kinyume na maamuzi ya wajumbe na akashauri uongozi wa wilaya kufika Msimbati kufanya mazungumzo na wanachama waliomchagua Linkoni.

Sauti ya Mzee Musa Ali muasisi wa CCM kata ya Msimbati
Mzee Musa Ali muasisi wa CCM kata ya Msimbati (Picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake, Salumu Uchumi, mwenyekiti wa CCM tawi la Liumo, alithibitisha kuwa hadi kufikia Agosti 17, zaidi ya wanachama 150 walikuwa tayari wamerudisha kadi zao za uanachama kutokana na uamuzi huo.

Sauti ya Salumu Uchumi Mwenyekiti CCM tawi la Liumo

Rashidi Omari Linkoni, diwani mstaafu aliyeenguliwa licha ya kuongoza kura za maoni, amesema amepokea kwa namna yake maamuzi ya viongozi wa wilaya, lakini hana budi kuyakubali.

Sauti ya Rashidi Linkoni Diwani mstaafu
Rashidi Linkon aliyekuwa Diwani wa kata ya Msimbati akizungumza baada ya wanachama kuandamana wakihitaji kurejeshwa kwa jina lake lililochaguliwa kwenye kura za maoni(Picha na Musa )

Naye Shahame Masudi Ahmadi, katibu wa CCM kata ya Msimbati, amekiri jina la Abrehemani Hamisi kurudi badala ya Linkoni na kueleza kuwa ni maamuzi ya Kamati ya Siasa ya Wilaya, huku akiwataka wanachama kuwa watulivu na kufuata maelekezo ya viongozi wa juu.

Sauti ya Shame Masudi Ahmadi Katibu wa CCM kata ya Msimabti

Akizungumzia hali hiyo, Hamisi Wanyama, katibu wa siasa na uenezi CCM Mtwara Vijijini, amesema wajumbe walimteua Linkoni kwenye kura za maoni, lakini kamati ya siasa wilaya ina mamlaka ya kubadili jina endapo itaona inafaa. Aidha, ameongeza kuwa malalamiko ya wanachama ni ishara ya utovu wa nidhamu na kutoifuata itikadi ya chama.

Sauti ya 1 Hamisi Wanyama katibu wa Siasa na uenezi wilaya

Wanyama amebainisha kuwa taarifa za wanachama kurudisha kadi ameziona mitandaoni na hajapokea rasmi, lakini endapo zitafikishwa watazipokea, huku akiahidi kufika Msimbati kuzungumza na wanachama husika.

Sauti ya 2 Hamisi Wanyama katibu wa Siasa na uenezi wilaya
Katibu wa Siasa na uenezi CCM Mtwara Vijijini Hamisi Wanyama akitolea ufafanuzi juu ya malalamiko ya wanachama wa CCM kata ya Msimbati
Share:

Waandishi wa habari watahadharishwa kuzingatia weledi uchaguzi mkuu

Amua Rushita akiendelea na mafunzo na Waandishi wa habari wa kituo cha Jamii fm redio yaliyofanyika leo August 15,2025 katika kituoni hapo (Picha na Musa Mtepa)

 Mafunzo kwa waandishi wa Jamii FM Redio yamewahimiza kuzingatia weledi, usalama kazini na kujikinga na uhalifu mtandaoni kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025

Na Musa Mtepa

Waandishi wa habari wametakiwa kuwa makini na kuzingatia weledi wa taaluma yao, hususan kuelekea katika kipindi cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025 nchini.

Wito huo umetolewa leo, Agosti 15, 2025, na mkufunzi Amua Rushita wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa kituo cha Jamii FM Redio kuhusu ulinzi na usalama katika kipindi cha uchaguzi. Amesema kuwa waandishi wanapaswa kuchukua tahadhari wanapokuwa kazini ili kuepuka hatari zinazoweza kujitokeza.

Sauti ya 1 Amua rushita mkufunzi wa mafunzo

Akifafanua, Amua amesema mafunzo hayo yamejikita katika maeneo matatu makuu: kuzingatia taratibu wakati wa kuhudhuria mikutano ya vyama vya siasa, kujikinga na uhalifu mtandaoni kupitia vifaa vya kidijitali, na kuimarisha ustawi wa kisaikolojia kwa waandishi wa habari wakiwa kazini.

Sauti ya 2 Amua rushita mkufunzi wa mafunzo

Waandishi wa habari wa Jamii FM Redio, Shaibu Omari na Msafiri Kipila, wameeleza kufurahia mafunzo hayo, wakisema yamegusa moja kwa moja namna ya kuboresha usalama wao na kufuata taratibu sahihi wakati wa mchakato wa uchaguzi.

Sauti ya msafiri kipila na Shaibu Omari

Kwa upande wake, Mwanahamisi Chikambu, mwandishi wa habari wa kituo hicho, amesema ameongeza uelewa kuhusu umuhimu wa kuvaa mavazi yanayomtambulisha mwandishi wa habari, pamoja na kujitambulisha kwa viongozi wa usalama kwenye eneo la tukio ili kurahisisha utambuzi endapo changamoto itatokea

Sauti ya Mwanahamisi Chikambu Mwandishi

Mafunzo haya ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ni sehemu ya mradi wa usalama wa mwandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025 nchini ambayo yanasimamiwa na umoja wa Klabu za waandishi wa habari nchini (UTPC).

Share:

Jamii inachangiaje kuwalinda, kuwatunza watu wenye ulemavu?

Hamisi Mshamu Bakari akiwa na biadhaa zake za mtumba. Picha na Msafiri Kipila

“Hamisi Bakari anakiri kuwa changamoto kubwa anayokumbana nayo ni ukosefu wa eneo maalum la kufanyia biashara, kama angepata sehemu hiyo rasmi basi angeweza kupiga hatua zaidi za kimaendeleo kwa kuwa angeendesha biashara yake kwa utulivu na kujiimarisha zaidi kiuchumi”

Na Msafiri Kipila

Katika harakati za kujikwamua na umasikini, watu wenye ulemavu wameendelea kuonyesha juhudi na uthubutu mkubwa wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kama walivyo watu wengine katika jamii. Licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili, bado wengi wao wamejiajiri na kufanya biashara ndogondogo ili kujitegemea kiuchumi na kuondoa dhana potofu kuwa ulemavu ni mwisho wa uwezo wa mtu.

Hamisi Mshamu Bakari ni miongoni mwa watu hao. Ni mlemavu wa mguu ambaye amejikita katika biashara ya kuuza viatu na nguo za mtumba kwa zaidi ya miaka 20. Akiwa na azma ya kubadili maisha yake, Hamisi hutembea umbali mrefu kila siku kutoka Mtawanya Juu hadi Magomeni, ambako huchukua bidhaa zake kabla ya kuzitembeza mitaani kwa ajili ya kuziuza. Safari hizo ndefu, licha ya hali yake ya ulemavu, zinadhihirisha kiwango kikubwa cha uvumilivu, bidii na kujituma alichonacho.

Hamisi Mshamu Bakari akiwa kwenye makazi yake. picha na Msafiri Kipila

Hata hivyo, Hamisi anakiri kuwa changamoto kubwa anayokumbana nayo ni ukosefu wa eneo maalumu la kufanyia biashara. Anasema kama angepata sehemu hiyo rasmi, basi angeweza kupiga hatua zaidi za kimaendeleo kwa kuwa angeendesha biashara yake kwa utulivu na kujiimarisha zaidi kiuchumi. Anaeleza kuwa msaada wa aina hiyo ungekuwa chachu kubwa ya mafanikio kwa watu wenye ulemavu, ambao mara nyingi hukosa fursa za msingi zinazoweza kuwainua kiuchumi.

Kupitia simulizi hii, jamii inapaswa kutambua kuwa watu wenye ulemavu hawahitaji huruma, bali wanahitaji fursa, mazingira rafiki na msaada wa kweli utakaowawezesha kujitegemea. Kama jamii itawekeza kwao, kwa kuwapatia maeneo ya biashara, mikopo au mafunzo ya ujasiriamali, basi watakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya taifa letu. Kisa cha Hamisi kinatoa somo la matumaini, lakini pia changamoto inayohitaji hatua za haraka.

 Bonyeza hapa kusikiliza makala haya

Share:

Mtamba aibuka kidedea kura za maoni CUF Mtwara Vijijini

Mh.Shamsia Azizi Mtamba mshindi wa kura za maoni CUF Mtwara Vijijini(Picha na Musa Mtepa)

Mh. Shamsia Mtamba ashinda kura za maoni CUF Mtwara Vijijini kwa kura 334 kati ya 374, akimuacha Abdull Mahupa nyuma kwa kura 39

Na Musa Mtepa

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mtwara Vijijini, Mh. Shamsia Azizi Mtamba, ameibuka mshindi katika uchaguzi wa kura za maoni wa Chama Cha Wananchi (CUF), uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Paris, mjini Mtwara.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo, Msimamizi wa uchaguzi Bw. Masudi Muhina amesema jumla ya kura 374 zilipigwa ambapo Mh. Shamsia Mtamba alipata kura 334, huku mpinzani wake Abdull Bakari Mahupa akijizolea kura 39. Kura moja iliharibika.

Sauti ya Bw Masud Muhina msimamizi wa uchaguzi wa CUF

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo, Abdull Mahupa alikubali kushindwa na kumpongeza Mh. Shamsia kwa ushindi huo. Aidha, aliwaomba wanachama wa CUF kuvunja makundi na kuungana kwa pamoja kumpa ushirikiano Shamsia katika harakati za kulirudisha jimbo hilo mikononi mwa chama katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Sauti ya Abdull Mahupa mshindi wa pili wa kura za maoni CUF
Diwani mstaafu wa kata ya Ndumbwe ambae alikuwa mgombea ubunge kupitia CUF Mtwara vijini katika uchaguzi wa kura ya maoni kwa ujumbe Mh. Abdull Mahupa(Picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake, Mh. Shamsia Mtamba amewashukuru wajumbe wa mkutano kwa kuendelea kumuamini na kumchagua tena kuwa mgombea wa jimbo hilo, huku akiwaomba kuendelea kushirikiana naye katika kampeni zijazo.

Sauti ya Shamsia Azizi Mtamba mshindi wa kura za maoni

Kabla ya uchaguzi, wagombea walipata fursa ya kunadi sera zao mbele ya wajumbe wa mkutano huo, sambamba na kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wanachama – hatua iliyowapa nafasi ya kueleza kwa kina mikakati yao ya kuimarisha maendeleo ya jimbo la Mtwara Vijijini.

Sauti ya wagombea wakinadi sera zao mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya CUF
Share:

Wenye ulemavu wanapojikomboa kupitia biashara

 

Hamisi Mshamu Bakari akifanya mahojiano na Msafiri kipila (mwenye kinasa sauti). Picha na Musa Mtepa

“Hamisi Bakari anakiri kuwa changamoto kubwa anayokumbana nayo ni ukosefu wa eneo maalumu la kufanyia biashara, kama angepata sehemu hiyo rasmi basi angeweza kupiga hatua zaidi za kimaendeleo kwa kuwa angeendesha biashara yake kwa utulivu na kujiimarisha zaidi kiuchumi”

Na Msafiri Kipila

Katika harakati za kujikwamua na umasikini, watu wenye ulemavu wameendelea kuonyesha juhudi na uthubutu mkubwa wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kama walivyo watu wengine katika jamii. Licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili, bado wengi wao wamejiajiri na kufanya biashara ndogo ndogo ili kujitegemea kiuchumi na kuondoa dhana potofu kuwa ulemavu ni mwisho wa uwezo wa mtu.

Hamisi Mshamu Bakari ni miongoni mwa watu hao. Ni mlemavu wa mguu ambaye amejikita katika biashara ya kuuza viatu na nguo za mtumba kwa zaidi ya miaka 20. Akiwa na azma ya kubadili maisha yake, Hamisi hutembea umbali mrefu kila siku kutoka Mtawanya Juu hadi Mangomeni, ambako huchukua bidhaa zake kabla ya kuzitembeza mitaani kwa ajili ya kuziuza. Safari hizo ndefu, licha ya hali yake ya ulemavu, zinadhihirisha kiwango kikubwa cha uvumilivu, bidii na kujituma alichonacho.

Mke wa Hamisi Mshamu Bakari akizungumza na mwandishi wa makala haya. picha na Musa Mtepa

Hata hivyo, Hamisi anakiri kuwa changamoto kubwa anayokumbana nayo ni ukosefu wa eneo maalumu la kufanyia biashara. Anasema kama angepata sehemu hiyo rasmi, basi angeweza kupiga hatua zaidi za kimaendeleo kwa kuwa angeendesha biashara yake kwa utulivu na kujiimarisha zaidi kiuchumi. Anaeleza kuwa msaada wa aina hiyo ungekuwa chachu kubwa ya mafanikio kwa watu wenye ulemavu, ambao mara nyingi hukosa fursa za msingi zinazoweza kuwainua kiuchumi.

Kupitia simulizi hii, jamii inapaswa kutambua kuwa watu wenye ulemavu hawahitaji huruma, bali wanahitaji fursa, mazingira rafiki na msaada wa kweli utakaowawezesha kujitegemea. Kama jamii itawekeza kwao, kwa kuwapatia maeneo ya biashara, mikopo au mafunzo ya ujasiriamali, basi watakuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya taifa letu. Kisa cha Hamisi kinatoa somo la matumaini, lakini pia changamoto inayohitaji hatua za haraka.

 Bonyeza hapa kusikiliza makala haya

Share:

Kuruthumu apatiwa msaada wa kununua kiatu maalum

Bi. Kuruthumu Seifu Mohamed akiwa ameketi na kiatu maalumu. Picha na Msafiri Kipila

“Kuruthumu amepatiwa msaada wa shilingi 300,000 kwa ajili ya gharama za ununuzi wa kiatu hicho maalumu. Huu ni mwanzo mpya kwa maisha yake, kwani sasa ataweza kushiriki ipasavyo katika shughuli za kila siku bila kikwazo kikubwa cha utembeaji”

Na Msafiri Kipila

Katika jamii yenye changamoto mbalimbali, watu wenye ulemavu mara nyingi hukumbwa na hali ngumu ya maisha, hususan kwa wale wanaohitaji vifaa maalumu ili kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku. Hali hiyo imekuwa ikiwakwamisha katika kushiriki kikamilifu kwenye shughuli za kijamii na kiuchumi. Hata hivyo, kuna nuru ya matumaini kupitia moyo wa huruma kutoka kwa wadau na viongozi wa jamii.

Miongoni mwa walionufaika na msaada huo ni Bi. Kuruthumu Seifu Mohamed, mama mwenye ulemavu wa mguu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akihitaji kiatu maalumu ili aweze kutembea kwa urahisi. Kupitia juhudi za wadau wa haki na maendeleo ya watu wenye ulemavu, Kuruthumu amepatiwa msaada wa shilingi 300,000 kwa ajili ya gharama za ununuzi wa kiatu hicho maalumu. Huu ni mwanzo mpya kwa maisha yake, kwani sasa ataweza kushiriki ipasavyo katika shughuli za kila siku bila kikwazo kikubwa cha utembeaji.

Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake na Wasichana Wenye Ulemavu Mtwara Mikindani, amethibitisha kuwa fedha hizo zimepokelewa rasmi na kumfikia mhusika. Aidha, ametumia fursa hiyo kuhamasisha jamii iendelee kujitokeza kusaidia watu wenye ulemavu, kwani bado kuna changamoto nyingi zinazowakabili.

Bi. Kuruthumu Seifu Mohamed akipokea kiasi cha shilingi laki tatu. Picha na Musa Mtepa

Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mtwara, Mhe. Anastazia Wambura, ameeleza kuguswa na hali wanayopitia watu wenye ulemavu. Amesema kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha watu hao wanapata usaidizi unaowasaidia kujikwamua kimaisha. “Nimekuwa nikifanya hivi mara kwa mara, lengo ni kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashiriki katika shughuli za maendeleo kama watu wengine,” alisema Mhe. Wambura.

Msaada huu kwa Bi. Kuruthumu ni mfano hai wa jinsi mshikamano wa kijamii na uongozi wenye maono unavyoweza kuleta mabadiliko katika maisha ya watu wanaohitaji msaada. Ni wito kwa jamii nzima kuendelea kuwathamini, kuwaunga mkono na kuwajumuisha watu wenye ulemavu katika nyanja zote za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kusikiliza makala haya, Bonyeza Hapa

Share:

Wananchi wa mtaa wa Mkunja Nguo waomba barabara rasmi

 

Sehemu ya Barabara ya Mkunjanguo kuelekea mtaa wa Namdohola ilivyo haribika (Picha na Musa Mtepa)

Uchongaji wa Barabara hiyo itarahisisha huduma kwa wakazi, hususan nyakati za dharura, Mwenyekiti wa mtaa, Bw. Kuladaku, ameunga mkono wazo hilo, akisisitiza mchango wake kwa maendeleo ya vijiji jirani

Na Musa Mtepa

Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya njia ya kutoka Mkunja Nguo kuelekea Namdohola, mdau wa maendeleo Bw. Ahmadi Issa Chihipu ameiomba Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani kuiangalia kwa “jicho la tatu” na kuichonga rasmi kuwa barabara inayopitika kwa urahisi na usalama kwa wananchi.

Akizungumza na Jamii fm Redio, Bw. Chihipu amesema kuwa njia hiyo imekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Namdohola, pamoja na vijiji vya jirani vya Litumbo na Mnyengedi vya halmashauri ya Mtwara vijijini , na tayari ameanza kuchukua hatua binafsi kwa kujitolea kufanya usafi na kufyeka ili kuiandaa kwa ajili ya uchongaji, mara tu Halmashauri itakaporidhia.

Ahmadi Chihipu – Mdau wa Maendeleo

Mbali na mchango wake binafsi, Bw. Chihipu ameeleza kuwa moja ya sababu kubwa zilizomsukuma kuibua umuhimu wa barabara hiyo ni changamoto za usafiri nyakati za dharura, hususan wakati wanawake wajawazito wanapopatwa na uchungu wa kujifungua usiku.

2: Ahmadi Chihipu – Mdau wa Maendeleo

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkunja Nguo, Bw. Musa Ali maarufu kama Kuladaku, ameunga mkono hoja hiyo na kubainisha kuwa barabara hiyo itakuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi wa maeneo mbalimbali ya jirani.

Musa Kuladaku – Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkunja Nguo

Mwenyekiti Kuladaku ametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka kuifanyia kazi ombi hilo, akisisitiza kuwa barabara hiyo ni hitaji la muda mrefu linalogusa maisha ya watu moja kwa moja.

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>