Jamii FM logo
90.5Mtwara – Tanzania
Voice to the Voiceless
◉ SIKILIZA LIVE

Jamii FM Radio

Habari | Elimu | Utamaduni | Maendeleo

▶ SIKILIZA LIVE 90.5 FM
Jamii FM
LIVE
๐ŸŽ™ KIPINDI KILICHOPO SASA

Inapakia...

EAT
▣ KIPINDI KINACHOFUATA

Inapakia...

EAT

HABARI MPYA LATEST NEWS

Inapakua habari za Jamii FM...

WAHUDUMU WETU

Jamii FM 90.5 — Sauti ya wasio na sauti, Mtwara.

27/02/2018

DAR ES SALAAM: KAMANDA MAMBOSASA "OLE WAO WATAKAOFANYA MAANDAMANO"

BOKAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema ni marufuku kwa mwanachi yoyote kushiriki kwenye maandamano kwani hawapo tayari kuona watu wakiandamana na kusababisa uvunjifu wa amani iliyopo.

Mambosasa ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mambo mbalimbali na ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wananchi kutojihusisha na maandamano.

Amefafanua kwenye mitandao ya kijamii kuna baadhi ya watu wanaitumia vibaya na sasa wameanza kuhamasisha maandamano kwa kupanga tarehe ambayo itakuwa Aprili 26 mwaka huu.

“Kwenye mitandao ya kijamii tumeona watu wanahamasisha maandamano.Tunawaambia Polisi hatutakaa kimya na wale ambao wataandamana kitakachotokea wasitulaumu.

“Polisi tumejipanga kwa ajili ya kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na wanafurahia hali ya ulitulivu iliyopo.Wale ambao wanataka kufanya maandano wahesabu hawana bahati na ndio maana tunaomba wananchi wasishiriki kwenye maandamano ambayo yameanza kuhamasishwa kupitia mitandao ya kijamii,”amesema Mambosasa.

Amefafanua Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linataka kuona wananchi wakiendelea na shughuli zao za kimaendeleo na wachache wenye kutaka kuvuruga amani iliyopo haitawavumilia.
CHANZO: FULL SHANGWE

No comments:

IDADI YA WASOMAJI

Search This Blog

Blog Archive

Powered by Blogger.

Labels

Popular Posts

1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>

Contact Form



Sikiliza jamii FM Radio

๐ŸŽง Jamii FM Live

HABARI ZA HIVI PUNDE

WAENDESHA WEBSITE