Jamii FM logo
90.5Mtwara – Tanzania
Voice to the Voiceless
◉ SIKILIZA LIVE

Jamii FM Radio

Habari | Elimu | Utamaduni | Maendeleo

▶ SIKILIZA LIVE 90.5 FM
Jamii FM
LIVE
๐ŸŽ™ KIPINDI KILICHOPO SASA

Inapakia...

EAT
▣ KIPINDI KINACHOFUATA

Inapakia...

EAT

HABARI MPYA LATEST NEWS

Inapakua habari za Jamii FM...

WAHUDUMU WETU

Jamii FM 90.5 — Sauti ya wasio na sauti, Mtwara.

27/02/2018

DAR ES SALAAM: AWESO AAGIZA WAKANDARASI WANAOTEKELEZA MIRADI YA MAJI VIZURI WALIPWE KWA WAKATI

4Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameagiza wakandarasi wote wanaotekeleza vizuri miradi ya maji nchini walipwe fedha zao kwa wakati, bila kucheleweshwa wanapoleta hati zao za madai, wakati alipokua akikagua utekelezaji wa miradi ya maji katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Aweso alisema pamoja na madai yao kulipwa kwa wakati, pia wakandarasi hao wapewe miradi mingine zaidi kama mfano kwa wakandarasi wengine, kwani nia ya Serikali ni miradi iishe kwa wakati na kufanya kazi na wakandarasi wenye uzalendo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri Aweso alitembelea miradi ya maji ya Hondogo, Kibamba, King’azi A na mradi wa kuchakata majitaka wa DEWAT uliopo Mburahati, unaofadhiliwa na Taasisi ya Kijerumani ya BORDA akiambatana na wataalam kutoka DAWASA na DAWASCO.

Manispaa ya Ubungo imetengewa zaidi milioni 653 kwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, asilimia 60 ya fedha hizo zikiwa ni mapato yake ya ndani.


No comments:

IDADI YA WASOMAJI

Search This Blog

Blog Archive

Powered by Blogger.

Labels

Popular Posts

1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>

Contact Form



Sikiliza jamii FM Radio

๐ŸŽง Jamii FM Live

HABARI ZA HIVI PUNDE

WAENDESHA WEBSITE