Jamii FM logo
90.5Mtwara – Tanzania
Voice to the Voiceless
◉ SIKILIZA LIVE

Jamii FM Radio

Habari | Elimu | Utamaduni | Maendeleo

▶ SIKILIZA LIVE 90.5 FM
Jamii FM
LIVE
๐ŸŽ™ KIPINDI KILICHOPO SASA

Inapakia...

EAT
▣ KIPINDI KINACHOFUATA

Inapakia...

EAT

HABARI MPYA LATEST NEWS

Inapakua habari za Jamii FM...

WAHUDUMU WETU

Jamii FM 90.5 — Sauti ya wasio na sauti, Mtwara.

27/02/2018

DAR ES SALAAM: Wanasheria zaidi ya 100 wameanza kupitia na kuchambua malalamiko mbalimbali ya wananchi

IMG_1871WANASHERIA zaidi ya 100 wameanza kupitia na kuchambua  malalamiko mbalimbali ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa  lengo la kuhakikisha yanapatiwa majibu.

Hatua hiyo inatokana na wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kufika  kwa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda na kisha kutoa malalamiko  kuhusu mambo mbalimbali.

Kutokana na malalamiko hayo Makonda aliaahidi kuyashughulikia  na sasa timu hiyo ya wataalamu wa masuala ya sheria wameanza jukumu la kupitia malalamiko ya wananchi hao na kisha kutafuta ufumbuzi wake wa kisheria.

Akizungumza leo, Mwanasheria wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Fabiola Mwingira amesema wanasheria hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko hayo na baada ya hapo wataanza  kuyasikiliza kwa kukutanisha pande zote mbili kwa maana ya mtoa malalamiko na anayelalamikiwa.

“Wanasheria hao wameanza kufanya uchambuzi wa malalamiko ya  wananchi kuanzia leo hadi Machi 9 mwaka huu na lengo  kila mwananchi aliyepeleka malalamiko yake basi yapate  ufumbuzi.

“Malalamiko wanayoyashughulikia ni yale ambayo hayako  mahakamani na yaliyo mahakamani basi yatabaki  huko huko yapatiwe ufumbuzi na tayari wamewaandikia barua wahusika,’amesema Mwingira.

Amefafanua baada ya wanashera hao kumaliza kusikiliza  malalamiko hayo, watatoa ushauri wa kisheria ambao utamuwezesha  sasa Mkuu wa Mkoa kutoa uamuzi.

Pia amesema utoaji majibu ya kero za wananchi hao awamu ya pili ,majina yatabandika kwenye geti la ofisi ya Mkuu wa Mkoa ,hivyo wananchi watatangaziwa siku na saa.


No comments:

IDADI YA WASOMAJI

Search This Blog

Blog Archive

Powered by Blogger.

Labels

Popular Posts

1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>

Contact Form



Sikiliza jamii FM Radio

๐ŸŽง Jamii FM Live

HABARI ZA HIVI PUNDE

WAENDESHA WEBSITE