• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Nabii Suguye atoa msaada kwa watoto maalum Mtwara

 

Nabii Nicolous Suguye akizungumza na Wanafunzi baada ya kutoa msaada katika shule ya Msingi Rahaleo (Picha na Musa Mtepa)

Nabii Ncolous Suguye ametoa msaada wa viti mwendo na chakula kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Kituo cha Upendo na Shule ya Msingi Rahaleo, Mtwara, kabla ya kuanza mkutano wa Injili utakaofanyika Oktoba 2, 2025, katika viwanja vya Sabasaba.

Na Musa Mtepa
Oktoba 1, 2025 – Nabii Nicolous Suguye ametembelea na kutoa msaada wa viti mwendo pamoja na chakula kwa watoto wenye mahitaji maalum katika Kituo cha Upendo na kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Msingi Rahaleo, iliyopo katika Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Akizungumza baada ya kutoa msaada huo, Nabii Suguye amesema kuwa ziara yake Mtwara inalenga kufanikisha mkutano wa Injili, na kwamba ana utaratibu wa kuwatembelea na kuwasaidia watu wenye uhitaji kila anapofika katika maeneo tofauti kwa ajili ya huduma ya kiroho.

Sauti 1: Nabii Ncolous Suguye
Nabii Suguye akiwa na Mtoto mwenye ulemavu katika kituo cha upendo kilichopo mtaa wa Mdenga ,Manispaa ya Mtwara Mikindani(Picha na Musa Mtepa)

Aidha, Nabii Suguye ametoa wito kwa jamii kutowatenga watu wenye ulemavu, bali kuendelea kuwaonesha upendo na kuwahudumia kwa moyo wa furaha.

Sauti 2: Nabii Ncolous Suguye

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Rahaleo na mlezi wa kitengo cha wanafunzi viziwi, Bi. Hilda Mapunda, amemshukuru Nabii Suguye kwa mchango wake, akisema kuwa msaada huo umeleta faraja na matumaini kwa watoto hao.

Sauti: Hilda Mapunda, Mwalimu Mkuu Msaidizi

Naye Meneja wa Kituo cha Upendo,   Faustini Keha, ametoa wito kwa jamii kuwa na moyo wa upendo kwa watoto wenye changamoto ya usonji, huku akimshukuru Nabii Suguye kwa msaada wa viti mwendo vinne na chakula.

Sauti: Fautini Kayeka, Meneja wa Kituo cha Upendo

Nabii Suguye anatarajia kuendesha mkutano mkubwa wa Injili kuanzia Oktoba 2, 2025, katika viwanja vya Sabasaba, Manispaa ya Mtwara Mikindani, ukiwa na ujumbe maalum: ‘Tokomeza Misukule.’

Share:

Wananchi wahimizwa kujitokeza kupiga kura Oktoba 29, 2025

 

Nabii Suguye akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kutembelea kituo cha Upendo cha kulelea watoto wenye usonji na vichwa mfanano kilichopo Mtwara mjini (Picha na Musa Mtepa)

Watanzania wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, 2025, kuchagua viongozi watakaosimamia maendeleo ya taifa. Wito umetolewa na Nabii Nicolous Suguye wakati wa ziara yake kwenye vituo vya watoto wenye mahitaji maalum, akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika kulinda amani na kuchochea maendeleo ya jamii.

Na Musa Mtepa

Watanzania wamehimizwa kujitokeza kwa wingi ifikapo Oktoba 29, 2025, kushiriki katika uchaguzi kwa ajili ya kuchagua viongozi watakaosimamia miradi ya maendeleo na maslahi ya wananchi na kuachana na dhana potofu ya kutoshiriki kupiga kura.

Wito huo umetolewa Oktoba 1, 2025, na kiongozi wa kiroho, Nabii Nicolous Suguye, alipotembelea kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum cha Upendo pamoja na kitengo cha wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia katika Shule ya Msingi Rahaleo.

Amesema kuwa, kama kiongozi wa kiroho na raia Tanzania, ana jukumu la kuhakikisha anachangia kulinda amani ya nchi yake.

Sauti ya 1: Nabii Suguye

Aidha, Nabii Suguye amesema kuwa uchaguzi huu ni Watanzania wote, hivyo kila mwenye sifa ya kupiga kura anapaswa kuwajibika kwa kuchagua viongozi bora watakaoweka vipaumbele kwenye miundombinu na huduma muhimu kwa jamii.

Sauti ya 2: Nabii Suguye

Katika hatua nyingine, Nabii Suguye ameeleza kuwa oparesheni yake iitwayo “Komboa Misukule” inalenga kuwaokoa watu kiakili, kihisia, kiafya na kiroho, kwani wengi wamepoteza dira na fursa muhimu za maisha kutokana na vifungo vya kiakili na kiroho.

Sauti ya 3: Nabii Suguye

Nabii Suguye anatarajia kufanya mkutano mkubwa wa injili kuanzia Oktoba 2 hadi Oktoba 6, 2025, katika viwanja vya Sabasaba, vilivyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara ambapo katika mkutano huo, huduma mbalimbali za kiroho zinatarajiwa kutolewa kwa wananchi.

Share:

TPA Mtwara yaongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo

 

Wajumbe na wadau wa mamalaka ya usimamizi wa Bandari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika September 29,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa BOT kanda ya Mtwara

Bandari ya Mtwara imeongeza usafirishaji wa mizigo kwa asilimia 49 kati ya 2023/2024, ikihusisha korosho na makaa ya mawe, huku idadi ya makampuni ya meli ikiongezeka

Na Gregory Milanzi

Mtwara-September 29,2025 – Ukusanyaji na usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Mtwara umeongezeka kwa asilimia 49 katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hatua inayodhihirisha ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika ukanda wa kusini.

Akizungumza September 29, 2025 kwenye mkutano wa wadau wa bandari hiyo unaoendelea mkoani Mtwara, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi amesema bandari hiyo imesafirisha tani milioni 2.5 za mizigo kwa mwaka 2024/2025 kutoka tani milioni 1.7 kwa mwaka uliopita wa fedha.

Sauti ya Ferdinand Nyathi Meneja wa Bandari Mtwara
Ferdinand Nyath meneja wa Bandari ya Mtwara akiwa katika mkutano wa mamala ya usimamizi wa Bandari kuelekea msimu mpya wa zao la korosho

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA), Daniel Mallongo amesema Bandari ya Mtwara ni muhimu sana kwa usafirishaji wa zao la korosho, na kwamba idadi ya makampuni ya usafirishaji wa meli imeongezeka kutoka mawili hadi sita katika misimu mitatu iliyopita.

Sauti ya Daniel Malongo mwenyekiti TASAA

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Emanuel Mrutu amesema Bandari ya Mtwara haifanyi kazi msimu wa korosho pekee, bali imekuwa ikihudumia pia bidhaa nyingine kama makaa ya mawe.

Sauti ya Emanuel Mrutu mwakilishi mkurugenzi TPA

Mkutano huo wa wadau wa bandari unalenga kuangazia fursa na changamoto katika kuendeleza shughuli za usafirishaji kupitia Bandari ya Mtwara.

Share:

TPA Mtwara yaongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo

 

Wajumbe na wadau wa mamalaka ya usimamizi wa Bandari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika September 29,2025 kwenye ukumbi wa mikutano wa BOT kanda ya Mtwara

Bandari ya Mtwara imeongeza usafirishaji wa mizigo kwa asilimia 49 kati ya 2023/2024, ikihusisha korosho na makaa ya mawe, huku idadi ya makampuni ya meli ikiongezeka

Na Gregory Milanzi

Mtwara-September 29,2025 – Ukusanyaji na usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Mtwara umeongezeka kwa asilimia 49 katika mwaka wa fedha 2023/2024 ikilinganishwa na miaka ya nyuma, hatua inayodhihirisha ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika ukanda wa kusini.

Akizungumza September 29, 2025 kwenye mkutano wa wadau wa bandari hiyo unaoendelea mkoani Mtwara, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Ferdinand Nyathi amesema bandari hiyo imesafirisha tani milioni 2.5 za mizigo kwa mwaka 2024/2025 kutoka tani milioni 1.7 kwa mwaka uliopita wa fedha.

Sauti ya Ferdinand Nyathi Meneja wa Bandari Mtwara
Ferdinand Nyath meneja wa Bandari ya Mtwara akiwa katika mkutano wa mamala ya usimamizi wa Bandari kuelekea msimu mpya wa zao la korosho

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Meli Tanzania (TASAA), Daniel Mallongo amesema Bandari ya Mtwara ni muhimu sana kwa usafirishaji wa zao la korosho, na kwamba idadi ya makampuni ya usafirishaji wa meli imeongezeka kutoka mawili hadi sita katika misimu mitatu iliyopita.

Sauti ya Daniel Malongo mwenyekiti TASAA

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Emanuel Mrutu amesema Bandari ya Mtwara haifanyi kazi msimu wa korosho pekee, bali imekuwa ikihudumia pia bidhaa nyingine kama makaa ya mawe.

Sauti ya Emanuel Mrutu mwakilishi mkurugenzi TPA

Mkutano huo wa wadau wa bandari unalenga kuangazia fursa na changamoto katika kuendeleza shughuli za usafirishaji kupitia Bandari ya Mtwara.

Share:

Umuhimu wa wanandoa kushiriki elimu ya uzazi wa mpango

 

Picha hii ni kwa msaada wa Mtandao

Karibu usikilize makala maalum ya dakika 13 inayoangazia Umuhimu wa wanandoa kushiriki elimu ya uzazi wa mpango.
Makala hii imeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na shirika la WELLSPRING, linalotekeleza mradi wa kutoa elimu kuhusu afya ya mama na mtoto, uzazi wa mpango, na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Muandaaji na msimuliaji wa makala hii ni Mwanaidi Kopakopa.

Karibu usikilize makala maalum ya Umuhimu wa wanandoa kushiriki elimu ya uzazi wa mpango.
Share:

Mgombea udiwani Chuno ataka ushirikiano wa wanawake katika siasa

 

Bi Mariamu Chimbwahi akiwa katika studio za jamii fm Redio akizungumza na Wananchi juu ya ushiriki wa wanawake katika Siasa na Changamoto wanazokutananazo (Picha na Musa Mtepa)

Mgombea udiwani Kata ya Chuno kupitia CCM, Mariamu Chimbwahi, amewataka wanawake kuanza uongozi ngazi za chini ili kujijengea uzoefu, huku akihimiza ushirikiano baina yao na kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kujitegemea

Na Musa Mtepa

Wanawake wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi za chini, ili kujijengea uzoefu na kujiamini kabla ya kuwania nafasi za juu katika uongozi wa kisiasa na kijamii.

Kauli hiyo imetolewa leo, Septemba 29, 2025, na mgombea udiwani wa Kata ya Chuno, Manispaa ya Mtwara Mikindani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mariamu Chimbwahi, wakati akizungumza katika kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio.

Bi. Chimbwahi amesema licha ya kuwepo kwa jitihada za kuwawezesha wanawake kisiasa, bado ni muhimu kwao kuanza uongozi kutoka ngazi ya chini ili kupata uzoefu wa kusimama jukwaani, kujibu hoja, na kushiriki mijadala ya kisiasa kwa ufanisi.

Sauti ya 1: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno
Mgombea udiwani kata ya Chuno Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi Mariamu Chimbwahi akiwa katika Studio za jamii fm Redio(Picha na Musa Mtepa)

Aidha, Mariamu Chimbwahi ametoa wito kwa wanawake kutoa ushirikiano wa dhati kwa wanawake wenzao pindi wanapoamua kugombea nafasi mbalimbali za uongozi, huku akitaka jamii kuachana na dhana potofu kwamba “adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake”.

Sauti ya 2: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno

Katika hatua nyingine, Bi. Chimbwahi amesema endapo atafanikiwa kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Chuno, atahakikisha anawahamasisha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi zitakazowawezesha kujitegemea, kulea familia zao kwa ufanisi, na kuwawezesha watoto kupata elimu bora.

Sauti ya 3: Mariamu Chimbwahi, Mgombea Udiwani Kata ya Chuno
Share:

Watoto kuacha shule chanzo viashiria vya uvunjifu wa amani

 

Maafisa kutokashirika la TASA Tanzania wakiwa katika studio za Jamii fm redio zizopo Mtwara Mjini mtaa wa Naliende (Picha na Musa Mtepa)

Mdondoko wa wanafunzi na ukatili wa kijinsia vyatajwa kuchangia ongezeko la vitendo vinavyohatarisha amani katika jamii , huku wazazi wakilaumiwa kwa kulegeza majukumu ya malezi na ufuatiliaji wa watoto wao

Na Musa Mtepa

Mtwara, Septemba 24, 2025 – Ukatili wa kijinsia pamoja na mdondoko wa wanafunzi mashuleni vimetajwa kuwa miongoni mwa sababu zinazochochea viashiria vya uvunjifu wa amani katika jamii.

Akizungumza katika kipindi Dira ya Asubuhi kinachorushwa na  Jamii FM radio tarehe 24 Septemba, 2025, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Safety Alliance (TASA), Bw. Hamisi Mwinshekhe, amesema wanafunzi wanaokumbwa na changamoto ya kuacha shule hukosa mwelekeo wa maisha, hali inayowafanya kuwa rahisi kushawishika kujiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.

Sauti ya Hamisi Mwinshekhe, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji – TASA

Bw. Mwinshekhe ameongeza kuwa chanzo kikuu cha mdondoko wa wanafunzi ni kulegalega kwa wazazi katika jukumu la malezi. Ameeleza kuwa baadhi ya wazazi huacha watoto wao kulelewa na mazingira ya mitaani, jambo linalowapelekea vijana hao kujiunga na makundi hatarishi.

Sauti ya Hamisi Mwinshekhe, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji – TASA

Kwa upande wake, Mratibu wa Miradi kutoka shirika la TASA, Bi. Betty Chenge, amesema wazazi wengi wamekuwa wakiwaachia walimu jukumu la malezi na ufuatiliaji wa watoto wao, badala ya kushirikiana nao kikamilifu. Hali hiyo, amesema, imekuwa chanzo cha ongezeko la utoro na mdondoko mashuleni.

Sauti ya 1 Betty Chenge, Afisa Miradi – TASA

Aidha, Bi. Chenge ameisisitiza jamii kutambua kuwa malezi ya mtoto si jukumu la mtu mmoja pekee, bali ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha mtoto anapata mahitaji yake ya msingi. Ameongeza kuwa jamii inapaswa kuwasaidia watoto wanaoonesha viashiria vya mienendo hatarishi kwa kuwaelimisha na kuwaongoza katika njia sahihi.

Sauti ya 2 Betty Chenge, Afisa Miradi – TASA

Katika mjadala huo, baadhi ya wasikilizaji waliopiga simu kushiriki kipindi wamelishukuru shirika la TASA kwa elimu waliyopatiwa, huku wakikiri kuwa uzembe wa malezi kutoka kwa baadhi ya wazazi umekuwa chanzo kikuu cha mdondoko wa wanafunzi na kushiriki kwao katika vitendo vinavyohatarisha amani ya jamii.

Sauti za wasikilizaji wakichangia kwa njia ya simu

Shirika la Tanzania Safety Alliance (TASA) kwa sasa linatekeleza mradi wa “Amani Yetu Kesho Yetu” , unaotekelezwa katika kata tano za Halmashauri ya Mtwara Vijijini ambazo ni MadimbaTangazoNalinguMsimbati, na Mahurunga.

Share:

TANESCO kuongeza uzalishaji wa umeme Mtwara

 

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Ngowele akizungumza na vyombo vya Habari wakati wa upokeaji wa mashine za uzalishaji umeme(Picha na Musa Mtepa)

TANESCO kuongeza uzalishaji wa umeme kwa MW 20 katika kituo cha Hiari, Mtwara, kukabiliana na upungufu wa umeme Lindi na Mtwara. Mashine mpya itakamilika ndani ya mwezi mmoja, ikiongeza uzalishaji hadi MW 70

Na Musa Mtepa

Mtwara, Tanzania – Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linatarajia kuongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa megawati 20 katika kituo cha Hiari, mkoani Mtwara, ikiwa ni juhudi za kukabiliana na changamoto ya upungufu wa umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara, Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Ngowele, amesema kuwa hatua hiyo inalenga kuongeza nguvu ya uzalishaji wa umeme kufikia megawati 70, kutoka megawati 38 zinazohitajika kwa sasa.

Sauti ya , Bi. Irene Ngowele Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO

Ameongeza kuwa ufungaji wa mashine hiyo mpya unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, ambapo baada ya kukamilika, itasaidia kuongeza uzalishaji wa umeme wa ziada ukilinganisha na matumizi ya kila siku.

Sauti ya 2, Bi. Irene Ngowele Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO

TANESCO imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa maeneo yote ya Tanzania, na hatua hii inatazamiwa kuwa mkombozi mkubwa kwa wakazi na shughuli za kiuchumi za mikoa ya kusini.

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>