• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

DAR ES SALAAM: Rais Magufuli atoa neno kifo cha Dkt. Kabourou

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dkt. Walid Amani Kaburu na kusisitiza kuwa amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Dkt. Magufuli ametoa salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga baada ya kupokea taarifa za kifo cha Dkt. Kabourou aliyekuwa anatibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbuili Jijini Dar es Salaam kilichotokea usiku wa kuamkia leo Machi  07, 2018.
"Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Dkt. Walid Amani Kabourou kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Dkt. Walid Amani Kabourou atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu",amesema Rais Dkt. Magufuli.
Pamoja na salamu hizo Dkt. Magufuli ameiombea familia ya marehemu na wote walioguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
NA ISMAEL MOHAMED - EATV
Share:

DAR ES SALAAM: Huyu ndio paka anayeharibu mimba

Daktari wa wanyama nchini Tanzania, Dkt. Obed Kiariro amedai kuna uwezekano mkubwa wa Paka anayefugwa majumbani hupelekea kuharibu ujauzito kwa binadamu endapo mnyama huyo hatopewa matunzo mazuri yanayostahili kwa wakati.

Dkt. Kiariro ameeleza hayo kupitia kipindi cha Supamix kinachorushwa na East Afrika Radio baada ya kuwepo matatizo mengi wanayoyapata jamii ya kike (wanawake) hasa hasa pale wanapokuwa wamebahatika kushika ujauzito na kwa bahati mbaya hutokea kuharibika bila ya kujua sababu za msingi kilichopelekea kupoteza ujauzito wake.
"Kuna ugonjwa tunaita 'toxoplasmosis' kitaalamu ugonjwa huu unatoka kwa Paka ambao unapelekea kutoka kwa mimba 'abortion', kama Paka hawatibiwi vizuri wala kuwepo na matunzo ya aina yeyote basi wanakuwa na ugonjwa huo na matokeo yake wanaambukia wanadamu. Unaweza ukawa na paka nyumbani unamtunza vizuri lakini huwezi kumzuia kwa namna yeyote ile kutokutana na paka wengine wanaozurura mtaani maana wakikutana tu wanaambukizana ugonjwa huo", amesema Dkt. Kiariro.
Mtazame hapa chini Dkt. Kiariro akielezea vizuri namna ya paka anayesababisha kuharibika kwa ujauzito (mimba).
NA ISMAEL MOHAMED - EATV
Share:

DODOMA: Watumishi wa umma walioondolewa kazini kimakosa kurejeshwa

Share:

LHRC wafafanua hoja za NEC dhidi ya tamko la asasi za Kiraia

TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI WA HOJA ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) DHIDI YA TAMKO LA ASASI ZA KIRAIA


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepokea barua Kumb. Na. BA.71/75/01/124 ya tarehe 22 February 2018 kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani na kupitia kwa umakini mkubwa hoja za Tume Ya Uchaguzi dhidi ya tamko lililotolewa na umoja wa Asasi Za Kiraia, chini ya Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI, Februari 21, 2018 kuzungumzia hali ya usalama wa raia, haki za binadamu na utawala wa sheria hapa nchini.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kama moja ya asasi zinazounda umoja wa AZAKI hizo kimelazimika kujibu hoja hizo kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika tamko lake lililotolewa Ijumaa Februari 23, 2018 imekituhumu moja kwa moja Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kupitia kwa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi, Bw. Paul Mikongoti, kwa kutoa tamko lenye tuhuma za kupotosha baadhi ya mambo kupitia tamko hilo la umoja wa AZAKI.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kutanguliza pongezi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kupitia hoja pamoja na mapendekezo yaliyotolewa na asasi za kiraia nchini na hata kutoa kasoro za uwasilishaji wa baadhi ya hoja hizo. 

Hata hivyo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kuikumbusha Tume kwamba, tamko husika halikutolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu bali tamko hilo lilitolewa na Umoja wa AZAKI chini ya Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilishiriki kwenye tamko hilo kama mwanachama wa AZAKI kwa kutambua wazi kuwa lengo la tamko hilo ni kuimarisha hali ya haki za binadamu na demokrasia nchini na si vinginevyo. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kuitoa wasiwasi Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa hakuna maslahi tofauti wala upotoshaji wa makusudi katika utoaji wa tamko hili.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinakiri kufahamu kwa kina sheria na kanuni zinazoratibu chaguzi na kinatambua kwamba lengo la AZAKI haikuwa kubeza wala kuvunja kanuni hizo bali kutoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho ya chaguzi na hatimaye kuimarisha demokrasia nchini Tanzania.

Hata hivyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimesikitishwa na kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumshambulia moja kwa moja Bw. Paul Mikongoti licha ya ukweli kwamba, Bw. Paul Mikongoti alikiwakilisha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kama mwanachama wa umoja huo wa AZAKI. 

Kituo kinapenda kuifahamisha Tume kuwa tamko hili la AZAKI lilisomwa na wakurugenzi tofauti maeneo tofauti nchi nzima na hivyo haikuwa busara kwa Tume kumshambulia moja kwa moja Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wala Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa ubinafsi wake.

Ingawa Tume ya Taifa ya Uchaguzi haikuwa sahihi kukituhumu Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Paul Mikongoti, bado Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeonelea ni busara kufafanua hoja zilizotolewa na umoja wa AZAKI kama ifuatavyo:

1. Kuhusu kituo cha televisheni cha ITV kuadhibiwa na kutakiwa kuomba radhi kwa kurusha habari za kuibwa kwa sanduku la kura

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kuijuza Tume ya Uchaguzi kuwa kilikubaliana na hoja hii iliyotolewa na umoja wa AZAKI kwa kuzingatia misingi ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba Tanzania inayotoa haki kwa kila Mtanzania pamoja na vyombo vya habari kutafuta na kupokea habari mahali popote pale bila kujali mipaka ya nchi.
 
Hata hivyo baada ya kupitia hoja hii kama ilivyofafanuliwa na Tume ya Uchaguzi, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaishauri Tume kuboresha kanuni za usimamizi wa uchaguzi ili kutokuweka mipaka kwa vyombo vya habari kwa kuzingatia kwamba vyombo vya habari vinatoa taarifa kwa maslahi ya umma.

2. Kuhusu mashirika mbalimbali kunyimwa kibali cha uangalizi wa uchaguzi

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilikubaliana na hoja hii kwa kuzingatia malalamiko yaliyotokana na AZAKI ya PACUSO ambao walikiri kupata majibu kutoka Tume kuwa tayari nafasi zimejaa.
Hata hivyo baada ya kupitia hoja hii ya Tume, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaishauri Tume ya Uchaguzi kuboresha utaratibu wa maandalizi kuelekea uchaguzi ili kutoa nafasi kwa asasi zenye lengo la kufanya uangalizi kufurahia haki hiyo bila kuhisi uwepo wa kuzuiliwa. Moja ya maboresho hayo ni kuweka muda wa kutosha wa kutuma maombi na kuweka nguvu katika kufikisha taarifa kwa mashirika na wadau wengine. Kufuatia ukweli kwamba Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ndio asasi pekee iliyopata kibali kutazama uchaguzi huu, hili lilipelekea butwaa kwa umoja wa AZAKI kwa kulinganisha na chaguzi zilizopita.

3. Tume kuweka utaratibu mpya unaowataka watazamaji kuwasilisha taarifa hizo ili zikaguliwe, kuangalia yaliyomo na kuridhiwa na Tume ikiipendeza.

Katika hoja hii, Kituo kinaungana na AZAKI kuhoji umuhimu wa utaratibu ulioanzishwa na Tume mwaka 2015 wa AZAKI kusubiri hadi Ripoti ya awali ya uangalizi iwasilishwe kwa Tume, na Tume kukiri kupokea ripoti hiyo ndipo AZAKI zinazoangalia uchaguzi kuweza kutoa kwa umma taarifa za uangalizi. AZAKI zimeonelea kwamba utaratibu huu unafifisha misingi ya uhuru wa asasi za kiraia katika uangalizi wa uchaguzi.

Utaratibu huu pia umelalamikiwa kwa kuzingatia kuwa Tume haijaweka muda maalumu ambao itatumia kabla ya kukiri kupokea ripoti ya uchaguzi.
 
Utaratibu huu umelalamikiwa na AZAKI kuwa kwa upande mwingine unaondoa dhana ya AZAKI kuwa vyombo huru vya uangalizi wa uchaguzi.

Mwisho Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaishauri Tume ya Uchaguzi kuzishirikisha asasi za kiraia na wadau wengine muhimu katika maboresho ya sheria, kanuni na taratibu zinazoratibu utendaji wa Tume na usimamizi wa chaguzi kwa lengo la kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini Tanzania. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaisihi Tume ya Uchaguzi bila kujali madhaifu katika uwasilishaji, kufanyia kazi changamoto zinazoibuliwa na wadau kwa lengo la kujenga Jamii yenye Haki na Usawa.

Imetolewa na;

Naemy Sillayo (Wakili)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

Share:

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) adaiwa kutoweka Katika mazingira Ya Kutatanisha

Taarifa zilizoenea mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana saa sita usiku.

Marafiki za Nondo wamedai alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa TSNP kuwa yuko katika hatari na baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea chochote, na baada ya muda alianza kujiondoa kwenye magroup ya WhatsApp.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa TSNP kuhusu Nondo inasema hajulikani alipo wakiwemo wazazi wake.   

Viongozi wa TSNP wamefika Kituo cha Polisi kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na  kutoa taarifa za kupotea kwake.

February 18, 2018, Nondo alijitokeza na kuikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya Ndani, na mara ya mwisho kuongea na wanahabari, alishinikiza Waziri  Mwigulu Nchemba ajiuzulu. 

Akizungumza na wanahabari jana March 6 2018, Nondo aliwataka TAHLISO waache kuwa wasemaji wa wizara na serikali na kuwataka wakumbuke majukumu yao mazito ya kusemea wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sababu wanalipishwa ada vyuo vikuu.

“TAHLISO ambayo kila chuo kikuu nchini kinatoa ada isiyopungua shillingi laki tano kwa mwaka ili TAHLISO iweze kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, imeacha kutimiza wajibu wake wa msingi na badala yake imegeuka kuwa taasisi yenye kusema kwa niaba ya serikali pamoja na kushambulia taasisi ambazo zinatetea maslahi ya wanafunzi nchini ikiwemo TSNP.

“Akwiline alikuwa ni mwanafunzi pia, TSNP ni mtandao wa kutetea wanafunzi, tunayo hayo mamlaka kusemea, kukemea, kushauri na hata kutoa mapendekezo yetu juu ya tukio lolote linaloashiria upotevu wa haki kwa wanafunzi.  TAHLISO wanatoa wapi ujasiri, mamlaka ya kutuzuia TSNP tusitimize wajibu wetu?” alisema Nondo.
Share:

DAR ES SALAAM: TFDA Yasitisha utoaji wa vibali vya uingizaji wa bidhaa za nyama kutoka Afrika Kusini kuazia leo Machi 7, 2018

Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imezuia uingizaji wa soseji kutoka Afrika Kusini zilizobainika kuwa na bakteria aina ya listeria.

Uamuzi wa TFDA unatokana na soseji hizo aina ya Polony kubainika kuwa na aina hiyo ya bakteria wanaosababisha ugonjwa wa listeriosis uliosababisha vifo vya watu 180 nchini Afrika Kusini.

Soseji hizo kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na vyombo kadhaa vya kimataifa zinatengenezwa na kiwanda cha tiger brands unit enterprises na cha RCL foods vyote vya Afrika Kusini.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi alikaririwa na mitandao ya kijamii akisema ameagiza kuondolewa sokoni soseji hizo, huku akiwashauri wananchi kuacha kula.

Motsoaledi alisema ingawa kiwanda cha RCL hakijatajwa kama chanzo cha ugonjwa huo, kitengo chake kinafanyiwa uchunguzi.

Ugonjwa wa listeriosis uliibuka Desemba mwaka jana na umeshasababisha vifo vya watu 180.
Share:

MTWARA: WANANCHI KULIPWA FIDIA NDANI YA WIKI MBILI

Image may contain: 32 people, people smiling, crowd and outdoor
Mkuu wa mkoa wa MTWARA MHE GELASIUS BYAKANWA amewahakikishia wananchi wa kata ya NANGOO wilayani MASASI kuwa watalipwa fidia ya maeneo na Mali zilizoharibiwa wakati wa utekelezaji wa mradi wa maji wa MBWINJI unaotumiwa na wananchi wa MASASI na NACHINGWEA.

MKuu wa mkoa ametoa kauli hiyo baaada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata hiyo yaliyoainishwa katika makundi matatu ikiwemo watu kulipwa pungufu, kulipwa wasiostahili na wengine kutolipwa kabisa wakati ni wahanga.

Kufuatia hali hiyo BYAKANWA amewaeleza wananchi wa kata hiyo na Kata jirani kuwa atahakikisha kila mtu anayestahili kulipwa analipwa ndani ya miezi MIWILI baada ya uchunguzi wa kutambua waliolipwa wakati hawana sifa kukamilika ambapo ndani ya miezi hiyo miwili watakuwa wamebainika na hatua zitachukuliwa.

MHE BYAKANWA amesema "Nipeni hii miezi MIWILI nikipata kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tutashughulikia ngazi ya Mkoa kwa kuunda kamati itakayo fanya uchunguzi na kutambua wale wanaostahili na wasiostahili na hatua zitachukuliwa hapahapa bila kusubiri utaratibu wa TAKUKURU ambazo zina chukua unamlolongo mrefu"

Wananchi wametoa malalamiko kuwa kuna watu ambao hawakupitiwa na mradi walilipwa fedha wakati wanaostahili hawajalipwa litafanyiwa kazi haraka na watarudisha fedha hizo ili walipwe wanaostahili.

Akijibu hoja ya kulipa fidia watu hewa Mwakilishi wa ofisi ya TAKUKURU Masasi ameeleza kuwa uchunguzi unaendelea wa kuwabaini watu hao na kwa kijiji cha Liputu kilichopo Kata ya ndanda wilayani humo umekamilka na imebainika kweli kuwa wapo watu ambao walilipwa bila kuwa na maeneo yaliyoathiriwa na mradi.

Aidha MHE. BYAKANWA amemwagiza Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha anafungua vioski vya maji vyote vilivyofungwa kwasababu ya wauza maji wamekila hela ili wananchi waendee kupata huduma ya maji kama serikali ya awamu ya tano inavyoelekeza kuwa wananchi lazima wapate maji kwani wanaadhibiwa kwa kosa ambalo hawajatenda.

Pia amemsisitiza Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha wale wauza maji wote waliokula fedha wakamatwe ili walejeshe fedha hizo haraka na baada ya wiki mbili zoezi hilo liwe limekamilika.

Image may contain: 10 people, people smiling, outdoorMHE. BYAKANWA amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya maji kwani jamii ndio yenye jukumu la kutunza kwa kuto fanya shughuli zozote karibu na vyanzo vya Maji lakini pia kuilinda miundombinu yake kwani serikali inatumia fedha nyingi kutekeleza Miradi hiyo.

Mradi wa Mbwiji ulianza kutekelezwa 2011 mwaka na ulighalimu zaidi ya bilioni 30.

HABARI NA JOINA NZARI- MASASI

Share:

KIGOMA: ACT YATOA KILIO CHA WAKULIMA WA MAHARAGE KWA SERIKALI

Chama cha ACT-Wazalendo kimepaza sauti ya wakulima wa zao la maharage katika Kata ya Biturana iliyoko Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, ambao wanauza zao hilo kwa bei isiyo na faida kutokana na ukosefu wa miundombinu hasa barabara. 
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe, amesema wakulima hao hulaliwa na wanunuzi wa zao hilo na kulazimika kuuza kilo moja ya maharage kwa bei ya Sh. 700 hadi 800, wakati yakisafirishwa mjini huuzwa Sh. 1800 hadi 2000 kwa kilo.
Amesema kufuatia changamoto hiyo, chama hicho kupitia Diwani wake wa Kata ya Biturana, Barnabas Baranzila wamehamasisha wananchi kuchonga barabara kutoka kwenye vijiji vya kata hiyo hadi makao makuu ya Kata, ili kurahaisha usafirishaji wa mazao  na hivyo kupunguza unyonyaji kwenye soko. 
Hata hivyo, Zitto amesema ACT itawasaidia wakulima hao kuunda ushirika imara ili kuhakikish ahawanyonywi katika soko la mazao yao.

CHANZO: DEWJBLOG
Share:

SINGIDA: WAZIRI NCHEMBA ACHANGIA UJENZI WA ZAHANATI NA MABWENI YA SHULE

Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa mabati 210 na mifuko ya saruji 100 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na mabweni ya wanafunzi katika kata ya Mtoa kusaidia kupunguza hadha wanayopata wananchi ambao inawalazimu kuvuka mto mkubwa kufata huduma ya afya umbali wa zaidi ya kilimota 10.
Waziri Nchemba amesema anakwelwa na jengo kukaa mda mrefu bila kumaliziwa hivyo ameamua kutoa bati 210 na kuchangia shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya ununuzi wa mbao ili ujenzi uanze mala moja na kikamilike ndani ya mwaka huu kianze kutoa huduma.
Dr Nchemba amesema hayo akiwa ziarani katika kata ya Mtoa kijiji cha Masiga kitongoji cha kisaki jimboni kwake iramba Magharibi mkoa wa Singida kutekeleza ahadi alizozitoa wakati anagombea mwaka 2015.
Aliongeza kusema kuwa wakati wa masika kama huu baadhi ya maeneo ni ngumu sana hata magari kufika kutokana mito kujaa maji na barabara kuwa na utelezi na kufanya gari au watu kushindwa kupita kufata huduma hivyo ameamua kutoa mifuko 100 yaa cement ili ujenzi wa bweni la shule ya sekondari mtoa likamalike kuwasaidia wanafunzi ambao wanaishi mbali wawwze kujisomea vizuri kuliko sasa hadha wanayopata kuvuka mito ambapo ni hatari.
“Mimi nakelwa na jengo kukaa mda mrefu hivi,hatulali hata sekunde tunaendelea kutafuta mbao na bati nyingi zikafunike baadhi ya vituo kwahiyo ninapoona jengo lipo hivi wala mtu asidhanie nafurahie jengo libaki vilee”alisema Dr Mwigulu
Nao wananchi wa kata ya mto awamemshukuru mbunge wao kwa kuwaletea mabati na cement kwa ajili ya kumalizia zahanati yao ya mtoa kwani ni jambo ambalo walikuwa wanalilia kupata zahanati hiyo.
Share:

DAR ES SALAAM: WATANZANIA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MTANDAO WA MITAJI

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Prof. Faustine Kamuzora amewataka wafanyabiashara nchini kuhamasika kujiunga na mtandao wa mitaji ya ubia ili kuimarisha vitega uchumi vyao na pia kusaidia kuanzisha viwanda hapa nchini.
Profesa Kamuzora alisema hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
Aliwataka wananchi kuacha uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji ya kutosha kwa ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.
Alisema serikali kwa sasa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya biashara na uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa kutengeneza sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.
Alisema ni vyema wenye viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato huo ili kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda. Alisema kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza urasimu na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na biashara.
Pia alitaka wamiliki wa Ubia huo kushirikiana na Costech katika kuhakikisha kwamba viwanda vinaanzishwa na kuendelezwa.
Alitaka kuwepo na elimu ya fedha na mitaji ili wananchi waweze kuthubutu na kufanikisha mitaji.
Mapema Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa uwazi, kwa kuzingatia sheria za nchi, na kuwa tayari kujifunza maarifa mapya kila fursa inapojitokeza.
Akisitikishwa na mahudhurio duni ya wafanyabiashara katika hafla hiyo alisema kutofahamu undani wa  soko la mitaji na fursa zake kunatokana na kutokuwa wazi na kufanya biashara kwa kufuata kanuni.
Akizungumzia kuhusu madai ya kuwapo kwa hali kuwa ngumu nchini Dr. Mengi pia amewataka Watanzania kuichukulia hali hiyo kama fursa ya kubuni biashara itakayowawezesha kupata faida kubwa.
Akiutambulisha Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa wadau, Muasisi wake Bw.  Salum Awadh amesema Mtandao huo ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti rahisi.
Alisema kwamba wakati umefika kwa Tanzania kusonga mbele kutumia fursa zilizopo duniani za mitaji na kusema jirani zetu wa Kenya wamesonga mbele katika hilo.
Alisema kwamba kutokana na kutojua umuhimu na ushiriki katika mitaji yenye ubia, wananchi wengi wanakimbilia katika mabenki ya biashara ambako pia wanapambana na vikwazo vingine.
Alisema kwa kuwa na kampuni ya mitaji inayoweza kutafuta pia mtaji inayomilikiwa na wananchi wenyewe kupitia mitaji yao kutawezesha kuwapo na uimara wa viwanda na kuongeza idadi zake kwa kuwa mfumo wa fedha wa mitaji ni tofauti na kwenda benki.
Tanzania kwa sasa ina zaidi ya mabenki 50 ambayo yanajishughulisha na mambo mbalimbali yanayogusa biashara na hifadhi ya kawiada.
Alisema mazingira ya sasa yanahitaji mfumo mwingine wa ziada kusaidia upatikanaji wa mitaji nje ya mabenki na kuzinduliwa kwa mtandao wa ubia wa mitaji kutasaidia kuziba pengo lililopo.
Kwa sasa Tanzania kwa rekodi zilizopo inapata asilimia 17 ya mitaji ya ubia ya dola bilioni 2.4 iliyopo duniani huku Kenya ikiwa na nfasi nzuri zaidi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye, baadhi ya viongozi wa taasisi za serikali na wafanyabiashara mbalimbali.
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>