Mkuu wa mkoa wa MTWARA
MHE GELASIUS BYAKANWA amewahakikishia wananchi wa kata ya NANGOO wilayani MASASI
kuwa watalipwa fidia ya maeneo na Mali zilizoharibiwa wakati wa utekelezaji wa
mradi wa maji wa MBWINJI unaotumiwa na wananchi wa MASASI na NACHINGWEA.
MKuu wa mkoa
ametoa kauli hiyo baaada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata hiyo
yaliyoainishwa katika makundi matatu ikiwemo watu kulipwa pungufu, kulipwa
wasiostahili na wengine kutolipwa kabisa wakati ni wahanga.
Kufuatia hali
hiyo BYAKANWA amewaeleza wananchi wa kata hiyo na Kata jirani kuwa atahakikisha
kila mtu anayestahili kulipwa analipwa ndani ya miezi MIWILI baada ya uchunguzi
wa kutambua waliolipwa wakati hawana sifa kukamilika ambapo ndani ya miezi hiyo
miwili watakuwa wamebainika na hatua zitachukuliwa.
MHE BYAKANWA amesema
"Nipeni hii miezi MIWILI nikipata kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU tutashughulikia ngazi ya Mkoa kwa kuunda kamati itakayo fanya
uchunguzi na kutambua wale wanaostahili na wasiostahili na hatua zitachukuliwa
hapahapa bila kusubiri utaratibu wa TAKUKURU ambazo zina chukua unamlolongo
mrefu"
Wananchi wametoa
malalamiko kuwa kuna watu ambao hawakupitiwa na mradi walilipwa fedha wakati
wanaostahili hawajalipwa litafanyiwa kazi haraka na watarudisha fedha hizo ili
walipwe wanaostahili.
Akijibu hoja ya
kulipa fidia watu hewa Mwakilishi wa ofisi ya TAKUKURU Masasi ameeleza kuwa
uchunguzi unaendelea wa kuwabaini watu hao na kwa kijiji cha Liputu kilichopo
Kata ya ndanda wilayani humo umekamilka na imebainika kweli kuwa wapo watu
ambao walilipwa bila kuwa na maeneo yaliyoathiriwa na mradi.
Aidha MHE.
BYAKANWA amemwagiza Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha anafungua vioski vya
maji vyote vilivyofungwa kwasababu ya wauza maji wamekila hela ili wananchi
waendee kupata huduma ya maji kama serikali ya awamu ya tano inavyoelekeza kuwa
wananchi lazima wapate maji kwani wanaadhibiwa kwa kosa ambalo hawajatenda.
Pia amemsisitiza
Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha wale wauza maji wote waliokula fedha
wakamatwe ili walejeshe fedha hizo haraka na baada ya wiki mbili zoezi hilo
liwe limekamilika.
MHE. BYAKANWA amewataka
wananchi kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya maji kwani jamii ndio yenye
jukumu la kutunza kwa kuto fanya shughuli zozote karibu na vyanzo vya Maji
lakini pia kuilinda miundombinu yake kwani serikali inatumia fedha nyingi
kutekeleza Miradi hiyo.
Mradi wa Mbwiji
ulianza kutekelezwa 2011 mwaka na ulighalimu zaidi ya bilioni 30.
HABARI NA JOINA NZARI- MASASI







No comments:
Post a Comment