• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

WAENDESHA BAISKELI ZA ABIRIA WAPINGA AGIZO LA KUONDOKA MJINI GEITA

Waendesha Baiskeli Maarufu kwa jina la daladala wanaosafirisha abiria kwenye halmashauri ya mji wa Geita, wamepinga agizo la Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo la kuwataka kufikia leo wasitishe shughuli zao kwenye maeneo ya mjini badala yake wafanye kwenye maeneo waliyopangiwa.
 
Hatua hiyo imekuja baada ya kupewa muda wa siku tano kupisha maeneo ya mjini kutokana na wimbi la ajali zinazosababishwa na waendesha Baiskeli kwa kutotumia barabara vizuri wanapokuwa kwenye shughuli zao.
 
Baadhi ya waendesha Baiskeli hao Bw Vistusi Maagani, John Maige na Fredy Maganga wamesema utaratibu uliofanyika sio mzuri kwa kuwa hawajapewa maeneo yatakayowasaidia kufanya kazi zao .
 
“Nasikitishwa sanaa na kitendo cha Mkurugenzi kututoa bila ya kutuandalia maeneo mazuri ya kufanyia kazi zetu kwa mfano mimi hapa hii kazi ndio nategemea kulisha familia pia kutuma pesa kwa mama yangu mzazi kwa kuwa sina ndugu leo natolewa kufanya kazi mjini unategemea nitaishi maisha gani jamani na wale ambao wananitegemea nitawaelezaje mimi naomba haya maamuzi wayaangalie kwa umakini”Alisema Maagini.
 
“Nashindwa hata niseme nini najisikia moyo wangu kutoka  kabisa kutokana na taarifa hii ya kuondolewa mjini maeneo ambayo tunaambiwa kufanya kazi akuna abiria sasa sijui tutaishije sisi waendesha daladala”Alisema  Maganga.
 
Bi,Lucia Paul ambaye mume wake anajishughulisha na kazi hizo alisema  kuondolewa mjini kwa waendasha baiskeli kutaleta athari kwenye familia zao kutokana na wengi wao kutegemea shughuli hiyo kukidhi mahitaji ya familia.
 
“Kwasasa hivi nyumbani hapakaliki kila siku mume wangu anamawazo anashindwa afanye nini na uku anafamilia muda mwingine hadi namuonea huruma  serikali ni vyema ikaangalia maana itatupa wakati mgumu sisi wanawake ambao tunawategemea waume zetu kwenye utafutaji”Alisisitiza Lucia.
 
Kutokana na hali hiyo chama cha ACT wazalendo kupitia kwa katibu wa mkoa huo,Bw Ikolongo Otoo  ameitaka halmashauri ya mji wa Geita kuondoa mara moja zuio hilo  kwa kuwa ni la kibaguzi ambalo alijazingatia wala kuthamini vijana masikini na wanyonge ambao wameamua kujipatia vipato kwa njia halali kabisa.
 
Mkurugenzi wa Halmashari ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly  alisema suala ambalo linafanyika ni la utekelezaji na alilikuwa aliitaji  muda kwani maeneo ambayo wamewapatia kufanya biashara ni makubwa na kwamba hata wangepewa muda  wa kutosha bado wangeombwa kuongezewa.
 
Mbunge wa Jimbo la Geita mjini,Constatine Kanyasu alisema  ahafikiani na makubaliano hayo na kwamba akuna utaratibu wala sheria ambayo inawazuhia waendesha Baiskeli kufanya shughulo zao maeneo ya mjini.
Share:

DKT. KIGWANGALLA ASHTUKIZA BODI YA UTALII (TTB)

#Waziri wa Maliasili na Utaliii, Dkt. #Hamisi #Kigwangalla leo Februari 20, 2018, 
amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Makao makuu ya Bodi ya Utalii 
Tanzania (TTB) Jijini Dar es Salaam na kuitaka kufanya kazi kwa kasi na ubunifu 
zaidi. 

Akizungumza na viongozi wa Bodi hiyo, Dkt. kigwangalla amewataka kuongeza kasi zaidi katika 
kutangaza Utalii wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kimataifa 
ya kutangaza vivutio vya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kutumia lugha 
mbalimbali za Kimataifa. 

Aidha,amewataka kuharakisha zoezi la uwekaji wa mabango yanayotangaza Utalii wa Tanzania katika 
viwanja vya ndege hususani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu #Nyerere Dar 
es Salaam (JNIA). 
Hata hivyo amewataka pia kujikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa 
kuhakikisha inahuishwa mara kwa mara. 
Pamoja na hayo, ameiagiza bodi hiyo, kushirikisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za 
Utalii ikiwemo madereva taxi na Marubani kwa kuwapa elimu ya kutangaza 
utambulisho wa Tanzania kupitia Utalii na vivutio vilivyopo.

Akiwa katika ofisi hizo ndani ya jengo la Utalii House, alikagua ofisi mbalimbali za 
bodi hiyo pamoja na zile za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na 
kupata maelezo machache kutoka wa maafisa wa Shirika hilo.
Share:

MHE BITEKO AWAHAKIKISHIA WANANCHI WALIOWAHI KUWA WAFANYAKAZI WA MGODI WA KIWIRA KULIPWA STAHIKI ZAO

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko amewahakikishia baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe na Wilaya ya Rungwe na Kyela Mkoani Mbeya kuwa serikali inamalizia mchakato wa uhakiki wa madeni yote ya wadai hivyo pindi itakapomaliza mchakato huo wadai wote watalipwa madeni yao.

Naibu Waziri, Mhe #Biteko ametoa kauli hiyo leo 20 Februari 2018 akiwa Kijijini Kapeta, Kata ya Ikinga Wakati akizungumza na wananchi waliowahi kuwa watumishi wa #Mgodi wa #Kiwira waliosimamisha msafara wake wakati akiwa ziarani Mkoani Songwe na Mbeya kukagua shughuli za uchimbaji wa Madini.

Alisema kuwa wananchi hao ndio walioiweka serikali ya awamu ya tano madarakani hivyo serikali haina haiwezi kuwasahau ama kutosimamia haki yao bali wanapaswa kuwa wavumilivu wakati serikali inajiridhisha na madeni hayo kabla ya kuanza kulipa ili kuwa na uhakika na watu wanaostahili malipo hayo.

“Watumishi lazima tukubali kwamba madeni haya tumeyarithi hayakuwa ya serikali bali yalikuwa ya muwekezaji sasa ili serikali iweze kuyalipa ni lazima ijiridhishe isije ikaingia mkenge wa kulipa watu wasiostahili kwani madeni hayo ni makubwa na yanahitaji kujiridhisha” Alisema Mhe Biteko na Kuongeza kuwa

“Sisi serikalini tunalifanyia kazi jambo lenu na tumeshafanya kazi kwa kiasi kikubwa mpaka sasa ya kuona namna ya kuwalipa na ninataka niwahakikishie kuwa kila mwenye haki anayedai lazima atalipwa lakini mtuvumilie tumepita kwenye michakato mingi ya kuibiwa fedha kwa watu kupachika madeni ya watu wasiostahili kulipwa tena wengine walishafariki”

Mhe Biteko aliongeza kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli inatambua kuwa mgodi wa Kiwira na mradi wa uchimbaji makaa ya mawe wa Kabulo ni miradi ya kimkakati katika Wizara ya Madini hivyo inatambua umuhimu wake na tayari ipo mbioni kuanzisha tena uzalishaji katika mgodi huo ambao uzalishaji wake ulisimama tangu mwaka 2009.
Alisema kuwa wananchi wamesubiri kwa muda mrefu malipo yao lakini tatizo kubwa ilikuwa ni serikali kujiridhisha na kuanisha wanufaika wa madeni hayo hivyo serikali italimaliza jambo hilo na itabaki kuwa historia.
Alisisitiza kuwa katika maeneo mengi kulikuwa na changamoto mbalimbali lakini tayari serikali imezipatia ufumbuzi changamoto hizo na wananchi wanaona utofauti.

Akijibu maswali ya wananchi hao waliotaka kufahamu ni lini mradi huo utaanza uzalishaji, Mhe Biteko alisema kuwa ili mradi uweze kuanza zipo taratibu za kisheria ambazo lazima zifuatwe ili yasijejitokeza matatizo ya kisheria baadae hivyo zitakapomalizika haraka mradi huo utaanza uzalishaji na wananchi watajipatia ajira.

Share:

TAKUKURU TANGA: TUNA TAARIFA 204 ZA VITENDO VYA RUSHWA


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Tanga (Takukuru) imepokea taarifa 204 za vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi wakizilalamikia idara mbalimbali za serikali na sekta binafsi.
Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Tanga,Christopher Mariba wakati akitoa taarifa za utendaji wao kwa waandishi wa habari kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2017.
Alisema taarifa hizo ni ongezeko la taarifa 30 sawa na asilimia 17 ukilinganisha na kipindi cha miezi sita iliyopita ambapo taarifa zilizo pokelewa ni 174.
Aidha alisema katika taarifa hizo 52 zilihusu serikali za mitaa, ardhi/ mabaraza ya ardhi 33,vyama vya siasa 28,Polisi 23,Elimu 18,Mahakama 16,Afya 15,Kilimo 8,Tasaf 5,Bandari (TPA) 1,Maji 1,Ushirika 1,Uhamiaji 1,Tanesco 1 na Misitu 1.
Mkuu huyo alisema kati ya taarifa hizo 204 zilizopokelewa taarifa 92 zinaendelea kuchunguzwa wakati nyengine 66 uchunguzi wake ulikamilika na majalada kufungwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi.
Aliongeza kuwa taarifa 46 zilihamishwa kwenye idara nyengine kwa sababu zilikuwa zikihusiana na makosa chini ya kuzuia na kupambana na rushwa.
Hata hivyo alisema katika uendeshaji wa mashitaka takukuru mkoa wa Tanga imefanya uendeshaji wa kesi 18 mahakamani ambapo kati ya kesi hizo 9 zilifunguliwa kipindi cha Julai 2017 hadi Desemba 2017 na kesi 9 ni za kabla ya Julai 2017.
Alieleza pia katika kipindi hicho usikilizwaji wa kesi moja huko wilayani Lushoto kwa mshtakiwa aliyejulikana kwa jina la Ally Mgovi ambaye alikuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Funta ambapo alifikishwa mahakamani kwa makosa ya ubadhirifu wa pembejeo za ruzuku zilizotolewa na serikali kwa ajili ya wakulima.
Alisema mshtakiwa huyo alipatikana na hatia alihukumiwa kifungo cha kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Tsh Milioni 1.9 ambapo alishindwa kulipa faini hivyo alipelekwa gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitatu.
Akizungumzia fedha ambazo zimeokolewa na kazi za uchunguzi na udhibiti ambapo katika utekelezaji wa majukumu yao kwa kipindi cha Julai hadi Desemba 2017 kumekuwa na ongezeko la fedha walizookoa na kuzirejesha serikalini kutoka milioni 6,450,000 kwa miezi sita ya mwanzo hadi Milioni 52,508,260.
Alieleza fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya malipo ya wanafunzi hewa ndani ya mpango wa elimu bila malipo katika shule za sekondari,mishahara hewa na gharama kwa ajili ya semina hewa.
CHANZO: Habari na Blog ya Tanga Raha.
Share:

DKT. NDUGULILE: WATOTO WA KIKE PAMBANENI DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA


Watoto wa kike nchini wameaswa kujitambua, kujiamini na kujilinda dhidi ya vishawishi vinavyosababisha matukio maovu ya Ukatili wa Kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni na kusababisha kukatisha ndoto zao za kupata haki ya kuendelezwa na elimu bora kwa manufaa yao, family na Taifa.
Rai hiyo imetolewa na  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wakati wa uzinduzi wa klabu za wasichana katika shule ya Sekondari ya Mwendakulima.
Dkt. Ndugulile amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia vinazidi kushamiri katika jamii zetu hususan katika meneo ambayo bado wanafuata mila na desturi ambazo zinamkandamiza mtoto wa kike na mwanamke.
Ameongeza kuwa namna bora ya kupambana na ukatili wa kijinsia ni kwa watoto wa kike kutonyamaza pale ambapo wanafanyiwa vitendo vya ukatili hasa kuozeshwa na kushawishiwa kuingia kwenye mahusiano ya kingono katika umri mdogo: mambo yanayosababisha mimba na ndoa za utotoni.
“Kila mtu aunge mkono juhudi zetu za pamoja za kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa kuacha usiri na kushirikiana kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia  kwa mamlaka zilizopo,” alisiistiza Dkt. Ndugulile.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkulu amesema kuwa Wilaya yake inaendelea kushirikiana na jamii na wadau wa maendeleo katika kuendeleza juhudi za Serikali za Kupambana na Vitendo vya Ukatili wa Kijinsia zikiwemo mimba na ndoa za utotoni ili kuwapatia watoto wa kike haki yao ya kuendelezwa na kuwaandaa kuwa nguvu kazi bora ya Taifa la uchumi wa kati na wa viwanda.
Naye mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Mwajuma Salum amesema klabu za wasichana zinawasaidia sana watoto wa kike kujitambua kwa kupata elimu zinazowawezesha kupamabana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa mimba na ndoa za utotoni. 
Aidha, ameeleza kuwa mbinu wanazopata zinawasaidia kuishi na wanafunzi wenzao wa kiume kama kaka na dada wakiwa na jukumu la kuwalinda na kuwapa kuwashauri kuzingatia wajibu wao katika masomo.
Share:

#CCM YAITAHADHARISHA #JESHI LA POLISI


Chama cha CCM kimeitahadharisha Jeshi la Polisi kuhusu vyama ilivyodai kuwa vinataka kulazimisha kuchaguliwa kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo mawili ya Siha na Kinondoni unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo ya Februari 17, 2018.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itakadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole, chama hicho kina taarifa za vyama vya upinzani kuwaleta watu kutoka mikoani kwa ajili ya kulinda kura.
“Tunazo taarifa za wenzetu kuwaleta watu toka mikoa mbalimbali kwa kisingizio cha kulinda kura,ziko nyumba zimewahifadhi watu hao. Tumelijulisha  jeshi la polisi kuhusu hawa watu walioletwa toka mikoani,tunaomba polisi washughulike nao,” alisema na kuongeza.
“Tunawatahadharisha polisi kuhusu vyama vitakavyolazimisha kuchaguliwa kwenye uchaguzi huu wawadhibiti mapema,wenzetu wamekuwa wakifanya uharifu kila siku na kusingizia watu wasiojulikana.”
Share:

ZFDA YAPEWA CHETI CHA #UBORA WA HUDUMA CHA #ISO


Wakala wa #Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umekabidhiwa rasmi Cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015.
Cheti hicho cha ubora ni kielelezo cha taasisi ya #ZFDA juu ya kusimamia misingi imara ya kuhakiki ubora wa huduma katika kiwango cha kimataifa.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Cheti hicho Waziri wa Afya wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa vitendo wa azma ya serikali inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya hususan upatikanaji chakula, dawa na Vifaa tiba.
Amesema kunahitajika ubunifu na jitihada za makusudi za kila mfanyakazi wa ZFDA kuhakikisha Chakula, Dawa, Vipodozi na Vifaa tiba ni bora na salama kwa afya za wananchi.Amefahamisha kuwa mafanikio hayo yaliyopatikana yawe chachu ya kuongeza ufanisi kiutendaji ili kufikia dira iliyowekwa.
“Mkifikia dira dira hiyo itakuwa mmetekeleza kikamilifu jukumu mllopewa na Serikali la kulinda afya ya jamii.Serikali inaaamini mnao uwezo wa kuwa taasisi bora ya udhibiti Afrika na Duniani kwani hakuna kizuizi cha kufikia dira hiyo,” alisema Waziri Kombo.
Aliitaka menejimenti ya ZFDA kuimarisha udhibiti wa uingizaji wa Chakula, Dawa na Vipodozi nchini kiholela ili kulinda afya za Wazanzibari.

CHANZO: Faki Mjaka – Maelezo, Zanzibar
Share:

DKT. #SLAA: "NITAFANYA KAZI KWA MOYO WANGU WOTE”


Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Muhidin Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria na Dkt. Wilbrod Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Baada ya kuapishwa, Dkt. Slaa amemshukuru Rais Magufuli kwa uteuzi huo na kuahidi kutumia nafasi hiyo vyema ili kuisaidia nchi kuingia katika uchumi wa kati.
“Nikushuru wewe Mhe. Rais kwa imani uliyonayo kwangu, bila shaka una vigezo vyako ulivyotazama, umeona kwamba ninastahili katika nafasi hii, na kama nilivyoapa ninaomba kusema kwamba sitakuangusha. Hakuna heshima kubwa Taifa linaweza kukupatia kama kulitumia,” alisema Dkt. Slaa na kuongeza.
“Katika ulimwengu wa sasa diplomasia kubwa ni ya kiuchumi, ninakushuru kwamba umenipeleka mahali ninaweza kutoa mchango wangu, nifanye kazi kwa moyo wangu wote, kwa uwezo wangu wote, kwa akili yangu yote na Mwenyezi Mungu akinisaidia niweze kutoa mchango katika safari hii ya kujenga uchumi wa Tanzania, hasa Tanzania ya viwanda, Tanzania inayolenga kuingia kwenye uchumi wa kati.”
Share:

MPINA AAGIZA KUHARAKISHWA KWA MCHAKATO WA KUTAIFISHA MELI YA BUAH NAGA ONE


Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga amemuagiza Katibu Mkuu Uvuvi, Dk. Yohana Budeba kuharakisha mchakato wa kuomba kibali cha Mahakama ili kutaifisha meli ya Kampuni ya Buah Naga One ya nchini Malaysia baada ya mmiliki wa meli hiyo kukaidi amri halali ya Serikali iliyomtaka kulipa faini ya Dola za Kimarekani 350,000 sawa na sh milioni 770 ndani ya siku saba baada ya kubainika kukiuka Kanuni ya 66 ya Kanuni za Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha 18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.
Mpina amesema, Januari 25 mwaka huu meli hiyo ilikutwa na makosa mawili ambayo ni kukutwa na mapezi na mikia ya samaki aina ya papa 30 bila kuwepo miili yake na Kapteni wa meli hiyo Han Ming Chuan raia wa Malaysia kukutwa na bastola aina ya Bereta na risasi kumi ambayo alikuwa anaimiliki kinyume cha sheria.
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kukagua Meli ya Uvuvi ya Kampuni ya XISHIJI 37 ya nchini China kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa ajili ya ukaguzi ambapo aliipongeza kwa kufuata taratibu za kimataifa za ukaguzi, Waziri Mpina aliagiza vyombo vya dola kuisaka na kuichukulia hatua kali za kisheria meli ya Kampuni ya Tai Hong No. 1 ambayo pia ilikaguliwa na
kukutwa na mikia ya papa 44 bila kuwa na miili yake kinyume cha sheria za uvuvi.
Waziri Mpina alisema meli hiyo ilitoweka katika mazingira ya kutatanisha na kuagiza vyombo vya dola kufuatilia ili ikamatwe na hatimaye ifikishwe katika vyombo vya sheria.
“Tutahakikisha meli hii tunaikamata ili sheria ichukue mkondo wake kwa kuwa bahari ya Tanzania siyo shamba la bibi,” alisisitiza Mpina
Katika hatua nyingine Waziri Mpina amevitaka vyombo vya dola kuzisaka hadi kuzipata meli nyingine 16 zilizopewa leseni ya kuvua katika bahari ya Tanzania ambazo zilitoroshwa na wenye meli kwa kushirikiana na watumishi wasio waaminifu mara baada ya kuanza kwa operesheni Jodari aliyoiunda hivi karibuni iliyojumuisha vyombo mbalimbali vya Serikali kudhibiti uvuvi haramu.
Waziri Mpina alisema doria hiyo pia inalenga kudhibiti utoroshaji wa samaki na mazao yake, kudhibiti biashara haramu ya madawa ya kulevya, biashara ya binadamu, usafirishaji wa silaha na magendo, utupaji wa taka hatarishi kutoka katika meli na uhalifu wowote unaoweza kujitokeza katika maji ya nchi yetu.
Aidha Mpina alisema jumla ya meli 24 zilipewa leseni ya uvuvi wa bahari kuu ambapo hadi sasa ni meli 8 tu ndizo zilizokaguliwa huku 16 zikitoroshwa.
Waziri Mpina aliyataja baadhi ya maeneo manne ambayo Serikali imeyafanyia maboresho katika marekebisho ya Kanuni za uvuvi za mwaka 2009 na kuweka vifungu vipya ambavyo vitasaidia Serikali kudhibiti uvuvi haramu na biashara haramu ya mazao ya uvuvi kuwa ni pamoja na;
Kufanya ukaguzi wa meli zote zinazokuja kuvua nchini kabla ya kuanza kuvua na baada ya kumaliza kuvua ili kubaini idadi halisi ya kiasi cha raslimali za uvuvi inayovunwa na kutozwa kodi halisi ili kuinua pato la taifa.
Kupakia asilimia 10 ya mabaharia wazawa katika kila meli inayokuja kuvua katika maji ya Tanzania ili kuwajengea uwezo na na kuwapatia ajira.
Kushusha samaki waliovuliwa bila kutarajiwa na kukabidhi katika kwa Serikali kwa vile ni mali ya serikali ili wauziwe wananchi kwa taratibu za kisheria ikiwa ni pamoja na kupigwa mnada.
Pia kutoza mrabaha wa dola za kimarekani 0.4 kwa kila kilo ya samaki walengwa (targeted species) kuongeza pato la nchi.
Wakala wa meli ya XISHIJI 37 nchini Abdulkarim Karia Maina kutoka kampuni ya Scaforth Gereral Agencies ya jijini Dar es Salaam amesifu juhudi zinazofanywa na Waziri Mpina katika kudhibiti meli zilizokuwa zinalihujumu taifa kwa kutofuata taratibu na kusema kuwa zinapashwa kuigwa na watumishi wote katika Wizara yake.
“Mageuzi yanaofanywa na Mheshimiwa Mpina katika kudhibiti uvuvi haramu nchini yataleta mapinduzi makubwa katika sekta katika siku za hivi karibuni na kuliingizia taifa mapato makubwa,” alisisitiza Maina
Naye Katibu Mkuu Uvuvi, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Yohana Budeba alisifu miongozo inayotolewa na Waziri Mpina kuendeleza Sekta ya Uvuvi na kuahidi kusimamia kikamilifu maelekezo yote ili sekta iweze kuchangia inavyositahili kwenye uchumi wa nchi yetu.
Kwa upande wake, Bw. Wankyo Simon ambaye ni Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkuu wa Dawati linalohusiana na Makosa ya Mazingira, amesisitiza kuwa Tanzania imejizatiti kuhakikisha kwamba Sheria zinachukua mkondo wake ili kudhibiti uhalifu wowote unaotokea katika bahari ya Tanzania.
CHANZO: John Mapepele
Share:

MAUAJI YA KIONGOZI WA #CHADEMA KUCHUNGUZWA

Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro na timu yake kufanya uchunguzi wa kina juu ya mauaji ya Daniel John ambaye alikiwa ni Katibu wa kata ya Hananasifu (Chadema) yaliyotokea Kinondoni Jijini Dar es salaam.
Waziri Mwigulu amelitaka Jeshi la Polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kujua undani wake nini na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.
“Mataifa mengine mtu akiuwawa shighuli zote zinasimama, tusiweke haya mazoea ya watu wanapotepotea kama mtu kapuliza dawa ya mbu kama jambo la kawaida tu, wafanye uchunguzi kwa kina kujua nani amehusika na tukio hili,” alisema Waziri Mwigulu.
Ameongeza kusema kuwa maswala ya demkrasia huamukiwa kwa peni na karatasi na si kwa panga,lungu wala mkuki.
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>