Chama cha CCM kimeitahadharisha Jeshi la Polisi kuhusu vyama ilivyodai kuwa vinataka kulazimisha kuchaguliwa kwenye uchaguzi mdogo wa majimbo mawili ya Siha na Kinondoni unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ijayo ya Februari 17, 2018.
Akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itakadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole, chama hicho kina taarifa za vyama vya upinzani kuwaleta watu kutoka mikoani kwa ajili ya kulinda kura.
“Tunazo taarifa za wenzetu kuwaleta watu toka mikoa mbalimbali kwa kisingizio cha kulinda kura,ziko nyumba zimewahifadhi watu hao. Tumelijulisha jeshi la polisi kuhusu hawa watu walioletwa toka mikoani,tunaomba polisi washughulike nao,” alisema na kuongeza.
“Tunawatahadharisha polisi kuhusu vyama vitakavyolazimisha kuchaguliwa kwenye uchaguzi huu wawadhibiti mapema,wenzetu wamekuwa wakifanya uharifu kila siku na kusingizia watu wasiojulikana.”







No comments:
Post a Comment