amefanya ziara ya kushtukiza katika ofisi za Makao makuu ya Bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) Jijini Dar es Salaam na kuitaka kufanya kazi kwa kasi na ubunifu
zaidi.
Akizungumza na viongozi wa Bodi hiyo, Dkt. kigwangalla amewataka kuongeza kasi zaidi katika
kutangaza Utalii wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuanzisha studio ya kimataifa
ya kutangaza vivutio vya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kutumia lugha
mbalimbali za Kimataifa.
Aidha,amewataka kuharakisha zoezi la uwekaji wa mabango yanayotangaza Utalii wa Tanzania katika
viwanja vya ndege hususani uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu #Nyerere Dar
es Salaam (JNIA).
Hata hivyo amewataka pia kujikita zaidi katika matumizi ya mitandao ya kijamii kwa
kuhakikisha inahuishwa mara kwa mara.
Pamoja na hayo, ameiagiza bodi hiyo, kushirikisha wadau mbalimbali wanaotoa huduma za
Utalii ikiwemo madereva taxi na Marubani kwa kuwapa elimu ya kutangaza
utambulisho wa Tanzania kupitia Utalii na vivutio vilivyopo.
Akiwa katika ofisi hizo ndani ya jengo la Utalii House, alikagua ofisi mbalimbali za
bodi hiyo pamoja na zile za Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na
kupata maelezo machache kutoka wa maafisa wa Shirika hilo.






No comments:
Post a Comment