JAMII FM 90.5
SIKILIZA LIVE
● LIVE
Bonyeza PLAY kusikiliza
JAMII FM 90.5 | RATIBA YA VIPINDI (Q4 2026)
KIPINDI KILICHOPANGWA SASA
Ratiba inathibitishwa
Taarifa zitawekwa hivi karibuni
KIPINDI KINACHOFUATA
Ratiba inathibitishwa
Saa za Afrika Mashariki (EAT)

Matumizi ya mkaa-Makala

 

Mmoja wa wajasiliamali akindaa jiko kwaajili ya kuchoma mahindi ili kupata kipato. Picha na Gregory Millanzi

Ongezeko la watu pamoja na kupanda kwa gharama za nishati mbadala kama gesi na umeme kumeongeza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa mkaa.

Na Gregory Millanzi

Kwa miongo mingi, mkaa umekuwa chanzo kikuu cha nishati kwa kaya nyingi, hususani katika maeneo ya mijini na vijijini. Hapo awali matumizi ya mkaa yalionekana kuwa suluhisho rahisi na la gharama nafuu kwa shughuli za kupikia na matumizi mengine ya kila siku. Wananchi waliutumia kwa kiasi na kwa uangalifu, wakitegemea misitu iliyokuwepo kwa wingi wakati huo.

Kadri miaka ilivyopita, ongezeko la watu pamoja na kupanda kwa gharama za nishati mbadala kama gesi na umeme kumeongeza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa mkaa. Hali hii imesababisha ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa, jambo ambalo limeathiri vibaya misitu na mazingira kwa ujumla.

Athari za matumizi makubwa ya mkaa sasa zimeanza kujidhihirisha waziwazi. Miongoni mwa athari hizo ni uharibifu wa misitu, mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa joto duniani, pamoja na changamoto za kiafya zitokanazo na moshi unaozalishwa wakati wa matumizi ya mkaa majumbani.

Makala haya yanalenga kuelimisha jamii kuhusu madhara ya matumizi ya mkaa na kuhamasisha matumizi ya nishati safi, salama na endelevu ili kulinda mazingira pamoja na afya ya binadamu.

Bonyeza hapa kusikiliza kwa undani zaidi

Share:

No comments:

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

Sikiliza jamii FM Radio

JAMII FM 90.5● LIVE
SIKILIZA LIVE • SAUTI YA JAMII
Tayari kusikiliza

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form