• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Paka wa ajabu aibua taharuki Mtwara vijijini

 

Paka wa ajabu aliyekutwa amekufa baada ya kudhaniwa kujipiga kwenye nyumba ya Bi Maimuna Abilahi mkazai wa kijiji cha Nangumi(Picha na Musa Mtepa)

Wananchi wa kitongoji cha Shangani, Nangumi, wamekumbwa na taharuki baada ya paka kupatikana amekufa na kuvalishwa hirizi katika nyumba ya mkazi mmoja. Tukio hilo limeibua hofu na maswali, huku viongozi wa kijiji wakieleza kusikitishwa na hali hiyo isiyo ya kawaida

Na Musa Mtepa

Wananchi wa kitongoji cha Shangani, kijiji cha Nangumi, kata ya Mayanga wilayani Mtwara Vijijini, wamekumbwa na taharuki baada ya kuonekana kwa paka aliyekufa huku mwilini mwake akiwa amevalishwa hirizi.

Tukio hilo limetokea alfajiri ya leo, Februari 17, 2026, katika nyumba ya Maimuna Abilahi, mchuuzi wa samaki na mkazi wa kijiji hicho.

Wakizungumza na Jamii FM Radio, baadhi ya wananchi wa Nangumi wameeleza kushangazwa na tukio hilo, huku wakilihusisha na imani za kishirikina. Wamedai kuwa paka huyo alionekana akiwa amejitupa katika eneo la nyumba hiyo, na baada ya kuchunguzwa alikutwa na hirizi shingoni na kiunoni.

Sauti ya wananchi wa Nangumi

Akizungumzia tukio hilo, Maimuna Abilahi, mmiliki wa nyumba hiyo, amesema alipata taarifa za tukio hilo kupitia simu alipokuwa feri kununua samaki kwa ajili ya biashara yake. Ameeleza kuwa aliondoka nyumbani mapema asubuhi akitumia mlango wa nyuma, ambao ni tofauti na eneo alikokutwa paka huyo.

Sauti ya Maimuna Abilahi, mmiliki wa nyumba

Kwa upande wake, baba mzazi wa Maimuna, mzee Abilahi Issa Mohamedi, amesema baada ya kupata taarifa hizo alifika eneo la tukio na kisha kumpigia simu mwanawe kumjulisha. Ameeleza kuwa walikubaliana kumchoma moto paka huyo majira ya saa kumi jioni.

Alipoulizwa sababu ya kusubiri hadi saa kumi jioni, mzee Abilahi amesema ni maagizo ya wataalamu, akidai kuwa paka huyo ni wa aina ya kipekee.

Sauti ya mzee Abilahi Issa Mohamedi

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Nangumi, Musa Salumu Nassoro, ameeleza kusikitishwa na tukio hilo, akisema linaweza kujenga taswira mbaya kwa kijiji hicho. Ameongeza kuwa katika kipindi chote cha uongozi wake hajawahi kushuhudia wala kusikia tukio la aina hiyo katika kijiji cha Nangumi.

Sauti ya Musa Salumu Nassoro, mwenyekiti wa kijiji cha Nangumi
Share:

CBT yasisitiza wakulima upogoleaji na utibuaji wa Mashamba ya Mikorosho

 

Mwonekano wa shamba la mikorosho lilotibuliwa ili kurahisisha maji kupenya ardhini na kuifikia mizizi ya Mikorosho(Picha na Musa Mtepa)

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Frances Alfred, amewataka wakulima kuzingatia upogoleaji na utibuliaji wa mashamba kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Amesema ruzuku za pembejeo zimeongeza uzalishaji, huku akisisitiza umuhimu wa kudumisha ubora wa korosho ili kupata bei nzuri sokoni

Na Musa Mtepa

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Frances Alfred, amewataka wakulima kuendelea na zoezi la upogoleaji wa matawi ya mikorosho pamoja na utibuliaji wa mashamba yao ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi yanayosababisha upungufu wa maji katika mikorosho.

Ameyasema hayo Februari 11, 2026, alipokuwa akizungumza katika kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio, kilichopo Naliendele, Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara. Amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, moja ya changamoto kubwa iliyoikabili zao la korosho ni mabadiliko ya tabianchi, yakiwemo mvua zisizotabirika na hali ya baridi isiyotarajiwa.

Sauti ya Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)

Aidha, amesema mmea wa mkorosho unahitaji maji ya kutosha ili uweze kufyonza virutubisho kutoka kwenye udongo kwa ufanisi. Kutokana na taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zinazoonesha uwepo wa mvua za chini ya wastani, amewasisitiza wakulima kupogoa na kutibua mashamba yao ili kukabiliana na changamoto hiyo.

Sauti ya Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)

Hata hivyo, amesema pamoja na changamoto za mabadiliko ya tabianchi, uwepo wa pembejeo za ruzuku zinazotolewa na Serikali umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la uzalishaji wa zao hilo. Ameeleza kuwa uzalishaji umeongezeka kutoka tani 300,010 mwaka 2023/2024 hadi tani 528,000 mwaka 2024/2025, hatua inayochangiwa na ruzuku hizo.

Sauti ya Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)

Katika hatua nyingine, amewataka wakulima wanaokabiliwa na bei ndogo kuendelea kusimamia ubora wa zao la korosho kuanzia ngazi ya vyama vya msingi hadi kwa mkulima mmoja mmoja, ili waweze kupata bei nzuri na kuongeza manufaa yatokanayo na zao hilo.

Sauti ya Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)
Share:

“Kwanini uzito wa korosho utofautiane na malipo yake ?’’

 

Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Ndugu Frances Alfred akiwa katika studio za Jamii FM Radio akishiriki Mubashara kipindi cha Dira ya Asubuhi akizungumzia hali na mwenendo wa zao la korosho katika msimu uliopita na mwelekeo katika msimu ujao (Picha na Grace Hamisi)

Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania, Frances Alfred, ametaka wakulima walipwe kulingana na uzito uliopokelewa na wahusika wa upungufu wawajibike baada ya wakulima kulalamikia tofauti ya uzito wa mazao kati ya Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) na ghala kuu, hali inayosababisha upungufu wa malipo

Na Musa Mtepa

Wakulima wa zao la korosho wamehoji kitendo cha baadhi ya Vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS) kupunguza kiwango cha uzito wa korosho kilichopimwa ghalani, hali inayosababisha tofauti ya malipo baada ya korosho hizo kuuzwa katika ghala kuu.

Wakichangia katika kipindi cha Dira ya Asubuhi kinachorushwa na Jamii FM Radio Februari 11, 2026, wakulima hao wamesema uzito unaopimwa wanapowasilisha mzigo kwenye vyama vya msingi huwa tofauti na uzito unaokuja kuzingatiwa baadaye wakati wa malipo. Wamedai kuwa wanapohoji  hali hiyo kwa makatibu wa vyama wanaambiwa inatokana na tofauti ya mizani inayotumika kupimia kwenye vyama vya msingi na ile ya ghala kuu.

Sauti ya Wakulima wa Korosho

Akijibu hoja hiyo mubashara katika kipindi hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Ndugu Frances Alfred, amesema mkulima anapaswa kulipwa kulingana na uzito wa korosho zilizopokelewa katika chama cha msingi, na hapaswi kupunguziwa malipo kwa sababu yoyote.

Sauti ya Frances Alfred Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho

Aidha, amesisitiza kuwa iwapo kutatokea upungufu wa uzito wakati wa usafirishaji kutoka chama cha msingi kwenda ghala kuu, mhusika aliyesimamia mzigo huo anapaswa kuwajibika na kufidia tofauti hiyo, badala ya mzigo huo kuhamishiwa kwa mkulima. Ameeleza kuwa vitendo vya namna hiyo ni sawa na wizi.

Sauti ya 2 Frances Alfred Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho

Pia ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa wakulima kuripoti changamoto zozote wanazokutana nazo kwa Bodi ya Korosho, pamoja na kuendelea kushirikiana na maafisa kilimo katika maeneo yao ili kuhakikisha wanazalisha korosho zenye ubora na zinazoweza kupata soko lenye tija zaidi.

Sauti ya 3 Frances Alfred Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Korosho
Share:

97% ya watanzania wanafanya kazi sekta ya madini

 

Washiriki wakiwa katika warsha. Picha na Gregory Millanzi

Mabadiliko makubwa ya sheria ya madini yaliyofanyika mwaka 2017 yameleta mafanikio makubwa kwa Watanzania katika sekta ya madini, ambapo katika migodi mikubwa ya madini iliyopo nchini asilimia 97 ya wafanyakazi ni Watanzania na zaidi ya asilimia tisini ya uongozi na utawala pia unashikiliwa na Watanzania.

Na Gregory Millanzi

Mabadiliko makubwa ya sheria ya madini yaliyofanyika mwaka 2017 yamewezesha watanzania wengi kufanya kazi katika sekta ya madini, ambapo katika migodi migubwa ya madini iliyopo nchini asilimia 97 ya wafanyakazi ni watazania huku asilimia zaidi ya tisini ya uongozi na utawala katika migodi hiyo ni watanzania.

Kabla ya mabadiliko ya sheria ya madini mwaka 2017, idadi ya watanzania waliokuwa wanafanya kazi katika migodi mikubwa ya madini, shughuli za utafutaji na uchakataji wa gesi asilia ilikuwa ni ndogo.

Lakini baada ya kufanyika kwa mabadiliko watanzania wengi wanafanya kazi na kusimamia migodi hiyo.

Kamishina wa madini nchini Terence Ngole akiwa mkoani Mtwara katika warsha ya kuelimisha umma kuhusu shughuli za uwazi na uwajibikaji katika sekta ya madini, mafuta na gesi asilia iliyoandaliwa na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) anafafanua zaidi.

Sauti ya Terence Ngole -Kamishina wa Madini

Sheria hiyo inawataka wawekeza kutumia huduma zinazopatikana nchini, na zisizopatikana nchini zihusishe makampuni ya ndani ya nchi, hatua hii imesaidia kuongezeka kwa manunuzi yanayofanywa na watazania.

Sauti ya Terence Ngole – Kamishina wa Madini

Wazawa wanaofanya kazi katika sekta hiyo wanaonesha ufanisi mkubwa na halmashauri zikinufaika zaidi na matokeo ya sheria hiyo.

Sauti ya Hidaya Gariatano – Mfanyakazi kampuni ya Gesi Asilia MNP
Share:

Watanzania wanufaika na mageuzi ya sheria ya madini

 

Mabadiliko ya sheria ya Madini, zaidi ya Asilimia 97 ya watanzania wajitokeza kufanya kazi kwenye sekta ya madini

Na Gregory Milanzi

Mabadiliko makubwa ya sheria ya madini yaliyofanyika mwaka 2017 yamewezesha watanzania wengi kufanya kazi katika sekta ya madini, ambapo katika migodi migubwa ya madini iliyopo nchini asilimia 97 ya wafanyakazi ni watazania huku asilimia zaidi ya tisini ya uongozi na utawala katika migodi hiyo ni watanzania.

Kabla ya mabadiliko ya sheria ya madini mwaka 2017, idadi ya watanzania waliokuwa wanafanya kazi katika migodi mikubwa ya madini, shughuli za utafutaji na uchakataji wa gesi asilia ilikuwa ni ndogo.

Lakini baada ya kufanyika kwa mabadiliko watanzania wengi wanafanya kazi na kusimamia migodi hiyo.

Kamishina wa madini nchini Terence Ngole akiwa mkoani Mtwara katika warsha ya kuelimisha umma kuhusu shughuli za uwazi na uwajibikaji katika sekta ya madini, mafuta na gesi asilia iliyoandaliwa na Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji Katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) anafafanua zaidi.

Sauti ya 1 TERENCE NGOLE-Kamishina wa Madini

Sheria hiyo inawataka wawekeza kutumia huduma zinazopatikana nchini, na zisizopatikana nchini zihusishe makampuni ya ndani ya nchi, hatua hii imesaidia kuongezeka kwa manunuzi yanayofanywa na watazania.

Sauti ya 2 TERENCE NGOLE-Kamishina wa Madini

Wazawa wanaofanya kazi katika sekta hiyo wanaonesha ufanisi mkubwa na halmashauri zikinufaika zaidi na matokeo ya sheria hiyo.

Sauti ya HIDAYA GARIATANO-Mfanyakazi kampuni ya Gesi Asilia MNP na

Share:

Mahakama yaendelea kuimarisha utoaji wa haki Mtwara

 

Mhe.Edwin Kakolaki Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara akihutubia katika maadhimisho ya siku ya sheria nchini iliyofanyika viwanja vya Mahakama kanda ya Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara imesema inaendelea kuimarisha uwezo wake ili kuhakikisha utoaji wa haki kwa wakati kama sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050. Kauli hiyo imetolewa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika Mtwara.

Na Musa Mtepa

Katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, Mahakama kwa kushirikiana na Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha uwezo wake ili kusimamia utoaji wa haki kwa wakati kwa taasisi, mashirika na wananchi nchini.

Hayo yameelezwa Februari 2, 2026 na Mheshimiwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Edwin Kakolaki, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara.

Sauti ya 1: Edwin Kakolaki – Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara

Mheshimiwa Jaji Kakolaki amesema kuwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, muhimili wa Mahakama una nafasi muhimu katika kujenga taifa lenye haki, amani, usalama na utulivu kwa kujenga mazingira salama ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.

Sauti ya 2: Edwin Kakolaki – Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara
Watumishi wa Mahakama wakiwa katika viwanja Mahakama kuu kanda ya Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Aidha, Jaji Kakolaki amesema Mahakama imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika matumizi ya teknolojia, hatua inayochangia kuongeza ufanisi na kasi ya utendaji kazi ikilinganishwa na miaka ya nyuma, jambo linalosaidia wananchi kupata haki kwa wakati.

Sauti ya 3: Edwin Kakolaki – Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara
Mkuu wa wilaya ya Mtwara Abdala Mwaipaya akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Mtwara tayari kwa kutoa salamu za mkoa katika maadhimisho hayo(Picha Musa Mtepa)

Akitoa salamu za maadhimisho hayo, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mkoa wa Mtwara, Lightness Kikao, amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo imebeba uzito mkubwa kwa kuwa inaakisi ukweli kwamba hakuna maendeleo ya kweli bila uwepo wa haki, utawala wa sheria na misingi ya utawala bora.

Sauti: Lightness Kikao – Makamu Mwenyekiti, TLS Mkoa wa Mtwara
Makamu Mwenyekiti, TLS Mkoa wa Mtwara Lightness Kikao akitoa akitoa salamu za TLS (picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrik Sawala, ambaye alikuwa mgeni maalumu katika maadhimisho hayo, amesema utoaji wa haki kwa wakati kwa wananchi utadumisha amani na utulivu katika mkoa wa Mtwara na taifa kwa ujumla, hali itakayowapa wananchi fursa ya kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo kwa amani.

Sauti: Kanali Patrik Sawala – Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Kanal Patrik Sawala akitoa salamu za mkoa katika maadhimisho ya siku sheria nchini (Picha na Musa Mtepa)
Share:

Matumizi ya mkaa-Makala

 

Mmoja wa wajasiliamali akindaa jiko kwaajili ya kuchoma mahindi ili kupata kipato. Picha na Gregory Millanzi

Ongezeko la watu pamoja na kupanda kwa gharama za nishati mbadala kama gesi na umeme kumeongeza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa mkaa.

Na Gregory Millanzi

Kwa miongo mingi, mkaa umekuwa chanzo kikuu cha nishati kwa kaya nyingi, hususani katika maeneo ya mijini na vijijini. Hapo awali matumizi ya mkaa yalionekana kuwa suluhisho rahisi na la gharama nafuu kwa shughuli za kupikia na matumizi mengine ya kila siku. Wananchi waliutumia kwa kiasi na kwa uangalifu, wakitegemea misitu iliyokuwepo kwa wingi wakati huo.

Kadri miaka ilivyopita, ongezeko la watu pamoja na kupanda kwa gharama za nishati mbadala kama gesi na umeme kumeongeza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa mkaa. Hali hii imesababisha ukataji mkubwa wa miti kwa ajili ya uzalishaji wa mkaa, jambo ambalo limeathiri vibaya misitu na mazingira kwa ujumla.

Athari za matumizi makubwa ya mkaa sasa zimeanza kujidhihirisha waziwazi. Miongoni mwa athari hizo ni uharibifu wa misitu, mabadiliko ya tabianchi, kuongezeka kwa joto duniani, pamoja na changamoto za kiafya zitokanazo na moshi unaozalishwa wakati wa matumizi ya mkaa majumbani.

Makala haya yanalenga kuelimisha jamii kuhusu madhara ya matumizi ya mkaa na kuhamasisha matumizi ya nishati safi, salama na endelevu ili kulinda mazingira pamoja na afya ya binadamu.

Bonyeza hapa kusikiliza kwa undani zaidi

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>