• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

MASASI: WAALIMU WAPIGANA "JEKI" MASOMO YA HESABATI NA KIINGEREZA


Image may contain: 1 person, sitting, table and indoorWalimu za shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya MASASI Mkoani MTWARA wameamua kutumia muda wao wa likizo fupi kujengeana uwezo wa mada ngumu kwa masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza lengo ikiwa ni kuongeza ufanisi wa ufundishaji wa masomo hayo na hivyo kuinua ufaulu katika Mitihani ya Kitaifa.

Akiongea wakati wa mafunzo hayo katika Tarafa ya LULINDI wilayani humo, AFISA ELIMU Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya MASASI Ndugu ELIZABETH MLAPONI amesema kuwa mafunzo hayo ni kati mikakati ya kuongeza ufaulu kwa matokeo ya darasa la NNE na la SABA kwa mwaka 2018.

Walimu wamefikia hatua hiyo baada ya kuona baadhi ya walimu hawana uwezo wa kufundisha baadhi ya mada kutokana kutokuzielewa vizuri hivyo mafunzo hayo yatawasaidia walimu hao kuwa na uwezo wa kufundisha masomo hayo kwa ufanisi na hivyo kuongeza ufaulu wa masomo hayo.

MLAPONI amesema kuwa kwa matokeo ya mwaka 2017 masomo ya Kiswahili na Maarifa ya Jamii ufaulu ulikuwa asilimia 50  wakati Masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiingereza ufaulu ulikuwa chini ya asilimia 40 ambapo somo la Kiingereza ufaulu ulikuwa chini ikifuatiwa na Hisabati.
Na Joina Nzali
Share:

Kamati ya Fedha yajiridhisha Ujenzi wa OPD ya Milioni 750 Kituo cha Afya Nanguruwe

Mapema mwezi huu, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya Mtwara imefanya ziara katika Kata ya Nanguruwe yenye lengo la kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Jengo la kupokelea wagonjwa (OPD) katika Kituo cha Afya ambacho kipo katika hatua nzuri ya kupandishwa hadhi na kuwa Hospitali ya Mtwara Vijijini.
Ujenzi huo unaotekelezwa na Mkandarasi Mzalendo Kutoka Jeshi la Kujenga Taifa yaani Kampuni ya Suma JKT unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa robo hii ya pili kulingana na Mkataba, hapo awali kulikuwa na hali ya kusuasua katika utekelezaji hadi pale timu ya wataalamu walipofanya ufuatiliaji wa kina kwa kushirikiana na Waheshimiwa Madiwani kisha wakaomba wakutane na Mkandarasi ili kujadiliana baadhi ya mambo.
Kabla ya ziara hiyo Kamati ya fedha ilifanya mazungumzo ya kina na Uongozi wa Jeshi hilo katika ukumbi wa Halmashauri kwa lengo la kutathmini maendeleo ya mradi husika na kuainisha changamoto zinazoukabili mradi huo, uongozi wa JKT na Halmashauri ulifikia muafaka wa kuhakikisha kuwa kazi inafanyika kwa Haraka na Usahihi kwakuwa fedha yote ya Mradi ipo.
 Kutokana na Mtwara Vijijini kukosa Hospitali yao Viongozi wake wakiongozwa na Mhe. Hawa A. Ghasia (Mb) wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanaisemea kero hiyo kila wapatapo nafasi hali iliyosikika na upande wa Serikali wakaamua kuwa Kituo cha Afya Nanguruwe kifanyiwe upanuzi kwa kujenga majengo mapya, kuboresha yaliyopo kulingana na mahitaji yanayotakiwa katika Hospitali.
Kutokana na hali hiyo kilianza kufanya kazi chache zinazoshabihiana na hospitali ikiwepo kulaza wagonjwa, kufanya upasuaji wa kawaida na Uzazi, kupokea wagonjwa wa sehemu mbalimbali, Ujenzi wa Duka la Dawa la Serikali katika eneo la Kituo na kuongeza Vifaa na Wataalamu wa kutoa huduma za Afya.
Inaaminika kuwa Jengo la Kupokelea wagonjwa linalojengwa likikamilika litakuwa na muonekano wa Kisasa zaidi lenye kupokea wagonjwa wengi sana na kutoa huduma nyingi kwa wakati mmoja, kwa mujibu wa msimamizi wa Ujenzi huo ambaye ni Mhandisi wa Halmashauri Ndg. Frank Kiunga, ameeleza kuwa kwa hali ya sasa mradi unaenda kama ilivyopangwa na inategemewa kasi hii itafanikisha ujenzi kumalizika kwa wakati.
“Kusema ukweli mradi huu kwa sasa unaenda vizuri na kasi ambayo tuliitegemea ingaa hapo awali kulikuwa na kusuasua lakini hii hali ikienda hadi mwisho basi huu mradi utakamailika kwa wakati kabisa kwa kuwa kila kinachohitajika kipo hususani fedha yake yote” alimalizia Mhandisi Kiunga.
Wajumbe wa kamati ya fedha walilidhishwa na hali ya mradi, wamemuagiza Mkurugenzi kuendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mradi huo ili umalizike kwa wakati, pia kamati hiyo ilimtaka Mganga Mkuu wa Wilaya kufanya usimamizi wa karibu wa Zahanati na Vituo vya Afya ili huduma zinazotolewa ziwe muarobaini sahihi wa kutatua kero za afya kwa wananchi.
Juuu ya hapo waliitaka kusimamia kwa umakini matumizi ya fedha yote 750 Milioni iliyoletwa kwaajili ya ujenzi wa Jengo hilo kwasababu kufanikiwa kwake kutaleta matumaini ya kuletewa kiasi kingine cha fedha kwa wakati ilikumalizia Hospitali hiyo na miradi mingine.
chanzo: manispaa
Share:

Jeshi la Polisi lawadaka watekaji Morogoro

Image result for Ulrich MateiJeshi la polisi Morogoro limewakamata watu wawili ambao wanadaiwa kuwa ni watekaji wa watu na kujihusisha na matukio ya ubakaji kisha kuwapiga picha za utupu waliowafanyia vitendo hivyo kwa lengo la kuwatisha kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa watu hao wawili na kusema kuwa wapo watu wengine watatu pia wamekamatwa kwa kufanya wizi kupitia njia ya mitandao ya kijamii.

"Ni kweli tumemkamata mtuhumiwa mmoja akiwa na mwenzake wanaojihusisha na utekaji wa watu, kuwabaka kisha kuwapiga picha za utupu na kuwatishia kuzisambaza picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kama hawata toa fedha lakini mbali na hao wawili tunawashikilia watu wengine watatu ambao wao wamekuwa wakifanya wizi na utapeli kwa njia za mitandao ya kijamii" alisema Kamanda Matei

Aidha Kamanda Matei amesema kuwa uchunguzi utakapokamilika watu hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao kutokana na makosa hayo.
Share:

"Nimesikitishwa sana taarifa ya vifo" - Magufuli


Rais Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani kufuatia vifo vya watu 26 ambao wamepoteza maisha katika jali ya basi dogo (Hiace) iliyogongana na Lori katika kijiji cha Mparange Mkuranga mkoani Pwani. 
Rais Magufuli ametuma salamu hizo kwa  Mhandisi Evarist Ndikilo na kumtaka amfikishe pole hizo kwa familia za watu ambao wamepoteza maisha katika ajali hiyo mbaya iliyotokea jana tarehe 24 Machi mwaka huu. 

“Nimesikitishwa sana na taarifa ya vifo vya watu 26 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea huko Mkuranga Mkoani Pwani, tumepoteza idadi kubwa ya Watanzania wenzetu na nguvu kazi ya Taifa. Naungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao na watu waliowategemea”

Aidha Rais Magufuli amevitaka vyombo vinavyohusika na usalama wa barabarani kuchunguza chanzo cha ajali hiyo na kuchukua hatua zinazostahili lakini pia Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema na majeruhi 9 wa ajali hiyo wapone haraka ili waungane na familia na jamaa zao kuendelea na shughuli za kila siku.
CHANZO: EATV

Share:

Mrisho Gambo awapigia magoti


Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo amefunguka na kuwaomba viongozi wa CHADEMA jijini humo akiwepo Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Meya wa Jiji la hilo, Calist Lazaro kushirikiana na serikali.
Mrisho Gambo amesema hayo baada ya jana Machi 24, 2018 viongozi hao wa CHADEMA ambao anadai walikuwa wamealikwa kushiriki katika zoezi la utoaji wa mikopo kwa kina mama kutotokea kwa kuwa zoezi hilo lilikuwa likisimamiwa na serikali. 

"Nipenda kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wenzangu bila kujali itikadi ya vyama vyao maana leo tulimualika hapa mbunge, Meya na madiwani lakini wakasema tu sisi hatuendi sababu lile jambo linasimamiwa na serikali, mimi nataka tu niwaombe viongozi wenzangu kwamba masuala ya maendeleo hayana vyama kwa sababu na sisi pia tungeangalia vyama pengine tungewaambia watu wa CCM wawape tu mikopo hiyo wanachama wao lakini tukasema sisi wenye serikali watu wetu ni wote bila kujali itikadi ya vyama vyao hivyo niwaombe wakubali kwamba Rais wa Tanzania ni Dkt. John Pombe Magufuli" 

Aidha Mkuu huyo wa mkoa amezungumzia suala la maandamano ya April 26, 2018 kwa namna na kusema kuwa wapo watu wanafanya kazi ya kushawishi watu kuandamana lakini wao kama viongozi wanatoa njia za watu kupambana na maisha. 

"Wakati wao wanahamasisha watu waandamane sisi tunawapa mbinu za kupambana na maisha, wakati wao wanahamasisha waandamane sisi tunawagea mitaji ili waweze kupata ridhiki na familia zao, wakati wao wanahamasisha waandamane Dkt John Pombe Magufuli anatoa elimu bure kwa shule zote nchi nzima" alisema Gambo. 
Mwanadada Mange Kimambi ni kati ya watu ambao wapo mstari wa mbele kushawishi Watanzania kote nchini kupitia mitandao ya kijamii kuandamana April 26, 2018 ili kudai haki zao.
CHANZO: EATV
Share:

Rais Magufuli atoa pongezi kwa Bohari ya dawa Tanzania MSD

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametoa pongezi kwa Bohari ya dawa Tanzania (MSD), baada ya kufanikisha ununuzi wa dawa kwa pamoja na moja kwa moja bila kutumia 'middle men'.

Pongezi hizo amezitoa leo jijini Dar es salaam wakati akizindua magari 181 ya Bohari ya dawa, ambayo yatakuwa yanasambaza madawa na vifaa tiba nchini na kurahisisha upatikanaji wa dawa na vifaa hivyo katika hospitali zote nchini.

''Nawapongeza sana MSD nyinyi mnatekeleza uzalendo vizuri, nasema kwa dhati mmeanza vizuri, mimi ni mgumu kupongeza kwahiyo kama nawapongeza mjue ukweli mnafanya kazi, nakumbuka Mkurugenzi wa MSD na Waziri wa Afya waliniomba fedha ili wawe wananunua dawa wenyewe bila 'Middle men' na wamefanikisha hilo'', amesema.

Aidha Rais Magufuli ametoa ruhusa kwa MSD kufungua maduka yao ya dawa sehemu mbalimbali nchini, lakini wasiyakabidhi kwa halmashauri bali wayasimamie wenyewe hata kama wataongeza wafanyakazi ni sawa tu.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amewalilia wafanyabiashara nchini kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuokoa kiasi cha zaidi ya bilioni 500 ambazo zinatumika kununua dawa nje ya nchi kila mwaka.
Share:

Kampeni safari ya 'HIJA' yazinduliwa

Baraza la waislamu nchini, BAKWATA leo limezindua rasmi kampeni ya maandalizi ya safari ya hijja kwa mwaka 1439 ambapo ni sawa na mwaka 2018.

Akizundua kampeni hiyo Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh Abubakar Zubeir amewashukuru watu wote ambao wanaofanikisha maandalizi ya safari ya kwenda kwenye ibada hiyo maalum ingawa kuna changamoto mbalimbali ambazo zinajitokeza.

Pia amesihi taasisi na vyombo vyote  ambavyo vinasimamia kushikamana ili kuboresha mahitaji yote ya Mahujaji ambao wataenda kutekeleza ibada hiyo.


"Kazi hii haitakiwi kulala, inahitaji ukweli, kuwafundishwa, kuwaelimisha Mahujaji pia kufanya kwa ajili ya radhi za mwenyezimungu ili mambo yote yaende sawa" amesema Shekh Zubeir.

Aidha ametoa rai kwa wale wote ambao wataenda kuhijji kuwa wapole, wenyenyekevu, wasikivu na kufuata taratibu zote kutoka kwa wasimamizi pindi wanapoenda kuhijji ili  kuepuka usumbufu unaojitokeza mara kwa mara.

Kwa upande wako Kamishina wa Uraia na pasipoti, Gerad Kihinga amesema kama serikali watahakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha safari hiyo.
Share:

Mwigulu: Wapo wanaotamani tuvurugane

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Mwigulu Nchemba amesema kuwa Serikali inazuia kuwepo kwa maandamano ili kutoruhusu watu wachache wanaotamani Tanzania wavurugane kuharibu taswira ya nchi.

Akizungumza katika harambee iliyoandaliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Masaka dayosisi ya Pare, wilayani Same, Mh. Nchemba amesema kuwa katika maandamano hayo wapo watu watakaofanya vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na hata kufyatua risasi ili ionekane kwamba nchi inaua watu.

"Wapo wanaotamani tuvurugane na tunapowaeleza wananchi wanaweza kujiuliza kwanini tunazuia maandamano wakati wapo watu wanaofanya mazoezi na ni kwa sababu hatutaki kuruhusu watu watuvuruge,’’ Dk Nchemba

Ameongeza kuwa wapo watu wenye mitazamo mibaya zaidi ambao wataiba na pia wataandaliwa watu watakaofyatua risasi ili ionekane watu wameuawa katika maandamano.

Amesisitiza kuwa lengo la kuzuia maandamano ni baada ya kuangalia kwa jicho la tatu maandamano hayo hivyo raia na vyama vya siasa wawaelewe kwani hawana nia ya kuminya uhuru wao ambao upo kwa mujibu wa katiba.

‘’Tunaangalia sura ambayo adui anaweza kupitia, wasione majira haya ni ya kawaida kuna mahali tumegusa hivyo hawafurahi na ndio sababu haya mambo yanatokea hivyo tunaomba msichukulie kuwa ni vitu vyepesi vyepesi bali mpanue mitazamo yenu mnapoona masuala haya yanapojitokeza,’’ ameongeza.
Share:

DC Mjema azindua zoezi la upandaji miti Ilala

ZIKIWA zmebaki siku saba kufikia siku ya upandaji miti duniani, Wilaya ya Ilala imeanza rasmi zoezi ilo ikiwa ni uungwaji wake mkono kwa Makamu wa rais, Samia Suluhu ambaye amekuwa akisisitiza kuwa na Tanzania ya kijani.

Zoezi hilo la upandaji miti kwa manispaa ya Ilala limezinduliwa leo katika kata ya Chanika na Mkuu wa Wilaya hiyo, Sophia Mjema ambaye aliambatana na Diwani wa kata hiyo Ojambi Masaburi.

Akizungumza na umati wa wananchi waliojitokeza katika uzinduzi huo, DC Mjema amesema utunzaji wa mazingira nchini unapaswa kuendana na kasi ya upandaji miti ambayo inasaidia kuleta mvua na kusaidia upatikanaji wa hali safi ya hewa.

DC Mjema amewataka wananchi wa Ilala kutunza mazingira yao kwa kuhamasishana kupanda miti kuanzia ngazi ya familia huku akiwaimiza kuwaripoti Serikali za mtaa wale wote ambao wamekuwa wakiharibu mazingira.

" Wananchi kila mmoja kwa nafasi yenu mnapaswa kutunza mazingira, kuhakikisha mnapanda miti kwa wingi hasa katika maeneo yenu na pia kwenye shule za msingi na sekondari, lengo la zoezi hili ni kujenga mazingira yaliyo bora na salama.

" Tumuunge mkono Rais wetu John Magufuli na Mama Samia ambao wamekuwa wakisisitiza kuwa na Tanzania ya kijani. Lakini kingine kwa wakina mama wenzangu wale mnaofanya biashara ya chakula nafahamu umuhimu wa biashara yenu lakini niwatake sasa mpikie majumbani kisha mbebe chakula hicho na kuja kuuza na siyo kupikia barabarani," amesema Sofia.

Sophia amesema upikaji wa chakula kando ya barabara una athari nyingi za kiafya ikiwemo ugonjwa wa kifua kikuu, huku pia akipiga marufuku utemaji holela wa mate.

Kwa upande wake, diwani wa kata hiyo, Ojambi Masaburi alimshukuru DC Mjema kwa kuja kuzindua zoezi hilo katika kata yake huku akimuahidi kushirikiana na wananchi wake katika kuunga mkono upandaji miti.

" Mheshimiwa DC kwanza nikushukuru sana kwa kuja kwenye kata yetu lakini nikuahidi kuwa sisi tupo kamili kuunga mkono juhudi zote zinazofanywa na serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo ikiwemo suala la mazingira bora, afya na usalama wake," amesema Masaburi
CHANZO: MUUNGWANA
Share:

Kamanda Sabasi asisitiza Oparesheni endelevu


Mkuu wa Oparesheni maalum za Kipolisi Liberatus Sabas amesema jeshi la polisi litaendelea na ya kukabiliana na mtandao wa dawa za kulevya Zanzibar itaendelea sambamba na kuwadhibiti wahalifu wanaofanya vitendo vya kuwaibia na kuwadhuru watalii.

Kamanda Sabas amesema wataendeleza operation hizo mpaka wahalifu watakaposema wamesalimu amri katika kufanya vitendo hivyo.

Aidha amesema kwa upande wa dawa za kulevya wamegundua wapo wafanyabiashara Zanzibar wanaoshirikiana na wale wa Tanzania bara na kuhakikisha kwamba watawashughulikia na kisha kuwafikisha katika mikono ya sheria na kusisitiza kuwa hakuna atakayechomoka.

Aidha imedaiwa kwatika Oparesheni hizo wamekamatwa wahalifu wapatao 21 pamoja na kete za dawa za kulevya kete 695 zenye ujazo takribani 31.3 gram.

CHANZO: EATV

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>