• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Malawi Yaonesha Nia Kupata Gesi Kutoka Tanzania



Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na Ujumbe wa Mawaziri wawili kutoka Malawi na kuzungumza kuhusu uwezekano wa Malawi kupata Gesi Asilia kutoka Tanzania na Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji umeme.

Ujumbe wa Malawi uliongozwa na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa ambao waliambatana na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara zao.

Waziri Kalemani alikutana na ujumbe huo Februari 12, 2018 katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam ambapo alielezwa dhumuni la ziara hiyo ya Mawaziri hao wawili kutoka nchini Malawi.

Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Nishati wa Malawi, Aggrey Masi alisema kuwa Malawi inaupungufu mkubwa wa nishati ya umeme na kwamba jitihada mbalimbali zinafanyika kuhakikisha kiwango cha uzalishaji umeme kinaongezeka.

Alisema umeme unaozalishwa nchini humo kwa sasa ni Megawati 140 pekee huku idadi ya watu ikiwa ni milioni 17 kiasi ambacho alisema kimeshindwa kukidhi mahitaji.

“Sasa hivi tumebaki na megawati 140 peke yake, hali siyo shwari; suluhisho la haraka linahitajika ili kuweka mambo sawa. Imani yetu ni kwa Tanzania kutazama namna ya kusaidia katika hili,” alisema.

Alibainisha kwamba chanzo kikuuu cha uzalishaji wa umeme nchini humo ni maporomoko ya maji na kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, chanzo hicho kimeshindwa kuzalisha umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku.

Aliongeza kwamba Serikali ya Malawi imeamua kuwa na vyanzo mbadala vya kuzalishia umeme ikiwemo Gesi Asilia hata hivyo alisema hakuna Gesi Asilia inayozalishwa nchini humo na kwamba matarajio yao ni kupata Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.

“Tumefarijika, tumepokelewa vizuri, lengo la ujio wetu ni kubaini uwezekano wa kupata Gesi Asilia kwa ajili ya kuzalisha umeme,” alisema Masi.

Alisema kwamba baada ya tathmini waliyoifanya wamebaini kwamba chanzo cha haraka kinachoweza kuwasaidia kuvuka kwenye upungufu mkubwa wa umeme uliyoikumba nchi hiyo kwa sasa ni Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.

Aliongeza kuwa tayari mwekezaji amepatikana ambaye atazalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia na kwamba atajenga mitambo yake kwenye eneo la Kalonga mpakani mwa Tanzania na Malawi.

Kwa upande wake Waziri Kalemani alisema suala hilo linaweza kujadiliwa baada ya wataalam wa Tanzania kujiridhisha uwezekano wake.

“Tupo tayari kushirikiana, kinachohitajika hapa ni majadiliano ya kitaalam na wataalam wetu waliopo hapa ili kuelewa mwelekeo,” alisema Waziri Kalemani.

Dkt. Kalemani aliwasisitiza wataalam hao kabla hawajafanya majadiliano wanapaswa kuelewa mambo makuu matatu ambayo wingi wa Gesi Asilia iliyopo kwa sasa, matakwa ya Sera ya Nishati na namna ambavyo Gesi hiyo inaweza kusafirishwa hadi huko Kalonga.

“Je tunayo gesi ya kutosha kugawana ama ni ya kutosha kwa matumizi yetu tu? Je Sera inaruhusu suala hilo? Na kama masuala hayo yanakubalika, Je ni vipi tutaifikisha hiyo Gesi huko mpakani?” alihoji Dkt. Kalemani.

Aliueleza ujumbe huo kuandaa mpango wa ombi lao kimaandishi pamoja na kuandika ombi rasmi na kuwasilisha katika utaratibu maalum wa Kiserikali ili majadiliano yafanyike.

Aidha, suala la Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe, Mawaziri hao kwa pamoja walikubaliana kupitia taarifa ya Tume ya Uendelezaji wa Bonde hilo ambayo inaundwa na nchi hizo mbili ili kubaini hatua za kuchukua kwenye kipengele cha kuzalisha umeme.

Miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika bonde hilo ni pamoja na ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 180 ambazo zitagawanya sawa kwa nchi hizo, kilimo cha umwagiliaji, (hekta 6,200) usambazaji wa maji kwa wananchi, ujenzi wa miundombinu ya jamii (bararabara, shule, na vituo vya afya).

Miradi mingine ni uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati, uvuvi, utalii na uboreshaji wa mazingira, hususan kuimarisha kingo za mto ambao ni mpaka wa Tanzania na Malawi

Share:

REDIO ZATAKIWA KUWA TARISHI WA MAENDELEO

Wafanyakazi wa taasisi za redio wamekumbushwa wajibu wao kama ilivyo chombo chochote cha habari  kuwa matarishi wa amani, upendo, mshikamano na kuhuisha maendeleo.
Aidha wameambiwa kwamba kwa kuwa Redio ina nguvu kuliko chombo chochote kingine duniani kwa kuwafikia watu wengi zaidi hivyo basi wanatakiwa kuwa makini wanapowafikishia wananchi taarifa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Juliana Shonza katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Dodoma ambaye alitaka taarifa kwa wananchi kufikishwa bila ushabiki, chuki au kupiga chuku (kuongeza chumvi).
Alisema tasnia ya uandishi wa Habari ni tasinia adhimu sana, hivyo Waandishi wote wa Habari wanalo jukumu kubwa la kuzingatia misingi ya uandishi ambayo ni mizania (balancing), kutofungamana na upande wowote (impartiality), kutenda haki (fairness), Utu (humanity), na mwisho kabisa kuzingatia ukweli (truthness).
Siku ya Redio Duniani huadhimishwa kila mwaka duniani kote Tarehe 13 mwezi Februari ili kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Redio mahali pote duniani.
 Aliwakumbusha waandishi na wageni historia ngumu na mbaya ya namna redio zilivyotumika vibaya katika baadhi ya nchi duniani na kuleta machafuko hadi umwagaji damu.
“Hivyo niwaase tena kutumia redio hizo na vipaza sauti kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu juu ya masuala ya kilimo na ufugaji, majanga mbalimbali, elimu juu ya sera na sheria mbalimbali za nchi, masuala ya afya kwa jamii na elimu. Na kwa kufanya hivyo tu, ndipo tutakuwa tumeitendea haki tasnia hii.” alisema Dk. Shonza.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani zilizofanyika Mjini Dodoma.
Aidha alipongeza kauli mbiu ya mwaka huu Redio na Michezo na kutoa rai kwa waandishi wote wa habari kudumisha mila na desturi za Kitanzania na kuongea Kiswahili fasaha bila kuchanganya na lugha zingine kama Kiingereza maarufu kama Kiswanglish.
Aidha Waziri Mwakyembe alishukuru Shirika la UNESCO na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) kwa kuwezesha siku ya redio na kusema atatafakari hoja zote zilizowasilsihwa kwake.
Naye Katibu wa Mtadao wa Radio Jamii (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtandao huo, Prosper Kwigize alitaka serikali kuhakikisha kwamba urasimu unaondolewa kwenye utoaji wa taarifa kwa umma ili kuwezesha kufanyika kwa vipindi mbalimbali vya habari.
Katibu wa Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mtandao huo, Prosper Kwigize wakati maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma kwa ufadhili wa UNESCO.
Alitaka Tamisemi kuweka utaratibu wa utoaji habari katika mfumo rahisi ili wananchi wafahamu kinachotekelezwa na serikali yao. Aidha maafisa habari walioajiriwa wapewe mamlaka na wawezeshwe kufahamu kinachofanywa na serikali na wawe na ruhusa ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari katika maeneo yao.
Aidha alisema kutokana kutokuwa na vyanzo vya mapato ya uhakika serikali ingeangalia suala la kodi na ushuru mbalimbali ili kusaidia Redio za Jamii kutolipia huduma za Radio.
Pia amesema sheria zilizopo ukilinganisha na mazingira halisi ya kazi ya mwanahabari, mfano sheria ya Takwimu, sheria ya huduma za habari, sheria ya makosa ya mtandao kumeshabibisha tasnia ya habari na utangazaji kuwa katika mashaka zaidi kuliko kipindi kilichopita.
Pia ameitaka Serikali kutoa Ruzuku ya elimu au mafunzo ya kitaaluma kwa wanahabari ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya kisheria ifikapo 2021
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) nchini, Faith Shayo amewataka waandishi na watangazaji kutumia redio kwa manufaa ya taifa kuleta mshikamano na pia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa pili kushoto) akitoa salamu za UNESCO wakati maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani ambapo huadhimishwa kila mwaka tarehe 13 Februari yaliyofanyika mjini Dodoma na kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini. Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge, Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche (wa kwanza kushoto).
Aidha alikumbusha historia ya redio na kazi iliyofanya duniani na kusema kwamba umuhimu wa radio upo wazi na kutaka wahusika kuzitumia kwa manufaa ya umma unaowazunguka.
Naye Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Dk Moshi Kimizi, alitaka serikali na vyombo vya habari kushirikiana katika kuhimiza michezo kwa kuwa ndicho kinachowaleta wananchi pamoja.
Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo Dk. Moshi Kimizi (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Mjini Dodoma.
Alisema anadhani redio na serikali vitaona njia bora ya kutangaza michezo kwa manufaa ya taifa.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Mh. Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesema Unesco inafanya kazi nzuri sana kwa kuwekeza kwenye vyombo vya Habari na kuvitaka vyombo hivyo kuitangaza Dodoma na fursa zake kwa sababu ndio makao makuu ya nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza, Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche (wa kwanza kushoto).
Aidha aliitaka Redio kutangaza fursa zote ambazo zipo Dodoma ili wafanyakazi na wafanyabiashara wanaohamia Dodoma kujua wanapata wapi mahitaji yao yakiwemo Makazi, Maji, Chakula, Elimu na kadhalika.
Alitaka vyombo hivyo kuvutia wawekezaji ili mji huo uwe kweli katika karne ya 21 na makao makuu ya nchi.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza akiwasili katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma kushiriki sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kulia) pamoja na Katibu wa Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa (kushoto).
Kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge, Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza, Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) nchini, Faith Shayo pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche wakiwa meza kuu wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani mjini Dodoma.
Mratibu wa Mtandao wa Vyombo vya Habari na Jinsia Kusini mwa Afrika (GEMSAT) , Gladness Munuo akitoa mada kuhusu usawa wa jinsia katika kuripoti michezo, changamoto na taratibu zake wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma. Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akisisitiza umuhimu wa maudhui katika vipindi vya redio ambapo aliwaasa kutangaza masuala yanayowahusu wanajamii katika maeneo yanayohusika badala ya kuwalisha wasikilizaji taarifa ambazo ziko nje na mipaka wanayoishi.
Mtaalamu wa Vyombo vya Habari na Mawasiliano, Mariagoreth Charles akiwasilisha kanuni za uandishi wa habari za mtandaoni na mitandao ya kijamii kwa waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini walioshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mtangazaji Mkongwe wa Habari za Michezo nchini, Abdallah Majura amesema pamoja na kwamba waandishi wanatangaza vipindi vya michezo lakini maudhui hayakidhi na kuvutia vile inavyostahili akitoa mfano hai wakati akichangia kwa nini waandishi wengi hawaandiki habari za michezo. Majura amesema yeye mwenyewe amewahi kupata #tuzo mbili kwa ajili ya vipindi vya michezo.
Pichani juu na chini ni sehemu ya waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni  (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa tano kulia) wakicheza wimbo maalum wa ngoma za asili wa Kikundi cha Kaza Roho cha mjini Dodoma ulioongozwa na Msanii Mwinamila wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza  na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
Share:

Wizara ya Maji Yaanza Kutekeleza Agizo la JPM Kwa Kasi.

8
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akionesha namna miundo mbinu ya maji itakavyojengwa kutoka katika mitambo ya maji ya Mailimbili, mjini Dodoma hadi eneo la Ihumwa utakapoojengwa mji wa Serikali

 Wizara ya Maji na Umwagiliaji yaanza kutekeleza Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli la kufikisha huduma ya maji katika eneo linalojengwa mji wa Serikali, Ihumwa Mjini Dodoma kwa kuanza kuchimba visima virefu vyenye uwezo wa kuzalisha mita za ukubwa 600 kwa siku.

Akizungumza wakati wa Ziara yakukagua maendeleo yautekelezaji wa Agizo hilo Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa maji mengine yatachukuliwa kutoka katika matenki ya Maili mbili ambapo maji yanayozalishwa kutoka katika chanzo cha Makutopora ni lita milioni 71 wakati  mahitaji ni lita milioni 46 kwa siku.

Akifafanua Mhandisi Kamwele amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa ziada ya maji katika matenki ya Maili mbili mjini humo wataweka mtandao wa mabomba kutoka katika eneo hilo hadi Ihumwa unakojengwa mji wa Serikali ili kuharakisha shughuli za ujenzi wa mji huo .

“Kiwango cha maji kinachosukumwa ni lita milioni 61 tu kati ya milioni 71 tunazozalisha hali inayopelekea tuwe na maji ya ziada  ambayo yatasaidia upatikanaji wa maji ya uhakika hapa Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya Nchi,” alisisitiza Mhandisi Kamwelwe.

Aliongeza kuwa  moja ya mikakati ya Wizara yake kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dodoma (DUWASA) ni  kuongeza visima virefu katika eneo la Mtumba ambapo visima vingine tayari vimechimbwa tangu mwaka jana ili kukidhi mahitaji ya maji katika Mji  huo ambayo ni takribani lita milioni mbili na laki sita.

Mhandisi Kamwelwe amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi kisichozidi miezi mitatu tangu sasa. Kazi ya uchimbaji wa visima vingine katika eneo la Mtumba nje kidogo ya Mji wa Dodoma inatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia leo, ikitekelezwa na Wakala wa Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA).
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema anaridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo kupitia DUWASA katika kuhakikisha kuwa mji wa Dodoma unakuwa na maji ya uhakika yatakayochochea ujenzi wa uchumi wa viwanda na uwekezaji kwa ujumla.

Mradi wa Kufikisha maji katika mji wa Serikali ni moja ya Maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa hivi karibuni kwa Wizara hiyo, pamoja na Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya umeme inawekwa katika eneo hilo.

CHANZO: Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma


Share:

HALMASHAURI YA LONGIDO YAPEWA GARI LA CHANJO

index


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemkabidhi mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Stephen Kiruswa gari aina Tunland Double cabin kwa ajili ya kuboresha huduma za chanjo na afya katika jimbo hilo.

Amemkabidhi gari hilo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo,  Bw. Jumaa Mhina na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Longido, Bw. Sabore ole Moloimet.

Waziri Mkuu amesema amekabidhi gari hilo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa alipofanya ziara wilayani Longidi, Agosti, 2017. Gari la kutolea huduma za chanjo lilikuwa ni miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinaikabili wilaya hiyo.

Kwa upande wake, Dkt. Kiruswa alitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido. “Gari hili ni zuri sana na linahimili mazingira ya wilaya ya Longido.”

“Naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuboresha huduma mbalimbali wilayani Longido zikiwemo za afya na maji licha ya jimbo hilo kukaa muda mrefu bila ya kuwa na mbunge.”
Amesema atahakikisha gari hilo linatunzwa na linatumika kwa ajili ya matumizi yaliyokusudiwa ambayo ni huduma za chanjo na afya pamoja na huduma za mama na mtoto.


Share:

MAPENZI BILA KUPIMA AFYA YADAIWA KUWA CHANZO KIKUBWA CHA MAAMBUKIZI YA VVU

Dk. Musagasa akizungumza wakati wa mafunzo hayo. Aliwataka watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuzingatia matumizi sahihi ya dawa zinazofubaza makali ya VVU pamoja na kuzingatia lishe bora.

Imeelezwa kuwa watu wengi wanaendelea kupata maambukizi ya Virusi vya #Ukimwi (VVU) kutokana na kuanza mahusiano ya kimapenzi bila kutambua afya zao hali inayosababisha waanze kuishi kama mume na mke bila kujua hali zao za kiafya. 

Hayo yamesemwa leo Februari 14,2018 na wahudumu wa jamii wanaosaidia kazi katika vituo vya tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya VVU vilivyopo katika halmashauri 7 za wilaya mkoani Mwanza yanayofanyika katika ukumbi wa hotel ya Midland jijini Mwanza.

Wahudumu hao wapo katika #mafunzo ya msaada na huduma za kisaikolojia yanayotolewa na Shirika la Ariel Glaser Pediatric #AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa Watu wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC).

Wahudumu walisema kitendo cha kuanza mahusiano ya kimapenzi na kuoana bila kutambua afya ni miongoni mwa tabia hatarishi zinazochangia kwa kiasi kikubwa kuambukizana VVU.

Mmoja wa washiriki hao Chausiku Sitta kutoka halmashauri ya wilaya ya Kwimba alieleza kuwa vijana wanapata maambukizi ya VVU kutokana na kukosa elimu sahihi juu ya VVU na Ukimwi na wengi wao kutawaliwa na tamaa ya ngono isiyo salama na kudhani kuwa kila mtu anayeonekana kuwa na umbo zuri basi hana maambukizi ya VVU.

“Vijana wanakurupuka tu,tena wakiona mwanaume ana mvuto ama mwanamke ana makalio makubwa wao wanaita ‘wowowo’ wanachanganyikiwa kabisa,ndugu zangu huwezi kumtambua mtu mwenye maambukizi ya VVU kwa kumwangalia kwa macho mpaka apimwe”,aliongeza Chausiku.

Naye Musa Ordas kutoka halmashauri ya wilaya ya Buchosa aliitaka jamii kutoendekeza waganga wa jadi kwani baadhi yao wanawadanganya watu wanaoishi na VVU kuwa wamerogwa kwa kuwalaghai kuwa wametupiwa majini mahaba.

Kwa upande wake, Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Dk. Joseph Musagasa aliwataka wanaume kuacha tabia ya kutumia majibu ya wake zao wanapopima VVU kwani majibu yanatofautiana na hutokea wakati mwingine mmoja kati yao kuwa na maambukizi na mwingine kutokuwa nayo.

Dk. Musagasa aliwashauri akina mama #kupima #afya zao kabla ya kubeba ujauzito,na kujifungulia katika vituo vya afya ili kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.
“Siyo watoto wote wanaozaliwa na mama mwenye maambukizi ya VVU wana VVU,hivyo mama unapotaka kubeba mimba pima kwanza afya yako,ukibainika una maambukizi utashauriwa na wataalamu wa afya namna ya kufanya ili usimwambukize mtoto wako”,alieleza Dk. Musagasa.


Share:

SERIKALI YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI

2
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali moja ya mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda

SERIKALI yaendelea kuongeza vituo vya Afya nchini ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali za kuboresha Huduma za afya nchini jambo litakalo saidia kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa kuwa huduma zote zitakuwa zimeishia kwenye ngazi ya Kata.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam.

“Kumekuwa na ongezeko kubwa la vituo vya Afya nchini kutoka vituo vya Afya 6321 kwa mwaka 2010 hadi vituo vya Afya 7680 kwa mwaka 2016, na kazi ya nyongeza inaendelea, kwaiyo tunaamini  vituo hivi vitaweza kupunguza msongamano katika hospitali za Wilaya, pamoja na Hospitali za Mkoa”, alisema Mhe. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametenga kiasi cha Zaidi ya Bilioni 100 ikiwa ni fedha za kuboresha Vituo vya Afya nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi katika maeneo yote nchini.

“Tumeanza kuboresha Vituo vya Afya kwa kujenga Wodi yakinamama wanaojifungua, thieta, wodi za magonjwa yakawaida, maabara, tunaongeza na nyumba za watumishi, ili kila kituo cha Afya kiwe na miundombinu hiyo ili utoaji huduma uwe rahisi” alisema Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mhe. Waziri Mkuu aliendele kusema kwamba Serikali imetumia Zaidi ya Bilioni 161 katika kuendelea kuboresha Huduma za Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa Maisha ya mama na mtoto jambo ambalo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.

Aidha Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Serikali imeendelea kuboresha Huduma za Afya kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 129 kwaajili ya vifaa vya kuwezesha kundesha shughuli za upasuaji katika kila kituo cha Afya ambacho kinaboreshwa.

Wakati akitoa taarifa ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda alisema kwamba wakina mama 126,164 walipata nafasi ya kujifungua katika vituo vya Afya, huku wakinamama 202 ambao ni sawa na Asilimia 0.5 walilazimika kujifungua kwa wakunga, na Asilimia 1.5 zaidi ya akinamama 1976 walijifungua njiani wakielekea kupata huduma, idadi inayoonekana kuwa kubwa sana katika Mkoa wa Dar Es salaam.

Idadi ya 2016 inaonesha Zaidi ya akina mama 85 walikuwa wanapoteza Maisha kati ya kina mama 100,000 waliokuwa wanajifungua lakini kwa sasa tangu maboresho yafanyike ni akina mama 57 kati ya akina mama 100,000 wanaojifungua ndio hupoteza Maisha, huku mikakati thabiti yakupunguza vifo hivyo ikiendelea kuwekwa.

Mhe. Makonda aliendelea kusema kwamba zaidi ya watoto ambao wanafanikiwa kuwa hai na kuwa salamakatika kujifungua ni Zaidi ya watoto 126,712, na watoto 131 huzaliwa wakiwa tayari wameshakufa, idadi hii ikilinganishwa .

Pia Mhe. Makonda alimshukuru AMSONS GROUP ambayo imetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Jengo hilo la Mama na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana huku akiwataka Wadau wengine kuiga mfano huo katika dhana ya kusukuma gurudumu la maendeleo katika jamii zetu.

Nae Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani imeongeza Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 mpaka sasa ni Bilioni 270 likiwa ni ongezeko la Zaidi ya mara 9, huku Wastani wa upatikanaji wa dawa ukiwa Zaidi ya asilimia 80.
“Serikali wakati inaingia madarakani Bajeti ya dawa ilikuwa ni Bilioni 30, mwaka unaofuata ikafikia Bilioni 200, na hivi tunavyoongea Bajeti ya Dawa ni Bilioni 270, likiwa ni ongezeko la mara 9, kama msaidizi wako nasimama kifua mbele


Share:

WAZIRI KALEMANI AMWASHIA MOTO MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME VIJIJI



Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za  Iparamasa pamoja  Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu.

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wananchi wakati alipowasili  kwenye viwanja vya kijiji na kata ya Iparamasa kwaajili ya kuzungumza na wananchi.

Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa.

Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani.

Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu. 

Waziri wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi
shirika la White City  Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea
awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na
kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini  Wilayani Chato
ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana  kwa umeme kwenye  kata yake  na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa
kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.

 Mmoja kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze  kuendesha  biashara
zao.

Aidha kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo kwa Mkandarasi kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.

“Nimesikia kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.

Mradi wa usambazaji wa umeme vijijini  Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi  wa Shirika la White City International ambapo unatarajia kufanyika ndani ya miezi  16 kwenye jumla  vijiji  220 vilivyopo  mkoani humo na jumla ya fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ni  Sh Bilioni 78.56.

Share:

Naibu Waziri aagiza Muhandisi akamatwe



Naibu waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso ameagiza mhandisi wa manispaa ya Temeke Damas Shirima kukamatwa na kuhojiwa na polisi kwa kosa la kutoa maelezo yasiyo ridhisha juu ya utekelezaji wa mradi wa maji wa mwasongo uliopo Kigamboni Dar es salaam.
Akizungumza katika majumuisho ya siku yake ya pili ya ziara yake jijini Dar es salaam Mhe Aweso amesema kuwa serikali haiwezi kunyamaza kimya pale inapooneka miradi ya maji inahujumiwa waziwazi na kwamba watahakikisha wale wote ambao wanagundulika kuhujumu miradi ya maji hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Awali mbunge wa jimbo la Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa jimbo lake bado linachangamoto ya upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo ambapo amehaidi kulisimamia suala hilo ili wananchi waondokane na kero hiyo.

chanzo: eatv


Share:

Waziri Jafo aweka mgomo



Waziri wa Nchi, Ofisi ya rais, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Tamisemi, Seleman Jafo, amegoma kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Itiso wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kutokana na baadhi ya wananchi kuharibu kwa makusudi miundombinu hiyo
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Waziri Jafo, amesema awali mkandarasi wa mradi huo alisuasua na halmashauri ya chamwino na kuamua kumbadilisha mhandisi wa maji ili kuweza kukamilika kwa haraka na kiwango bora.

Amesema wananchi wa kijiji hicho wamekuwa hawana Ushirikiano na viongozi wao na wale wa mradi hadi kusababisha kuharibu miundombinu ya maji, na kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya chamwino kusimamia na wale watakaoharibu miundombinu washughulikiwe.

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Athumani Masasi, amesema serikali ya awamu ya tano imetoa kiasi kikubwa kwa ajili ya mradi wa maji lakini wananchi wamekuwa mstari wa mbele kuharibu miundombinu hiyo.


Share:

Jakaya Kikwete ataka busara kutumika



Rais Mstaafu Kikwete amesema umefika wakati busara kutumika kupunguza changamoto za wakimbizi miongoni mwa nchi za Afrika ikiwa siku chache zimepita tangu Tanzania itangaze msimamo wa kutoendelea kuwapa nafasi ya ajira, ukazi wa kudumu, umiliki ardhi.
Akizungumza kwenye mkutano wa jopo la viongozi mbalimbali duniani lililoundwa kuangalia mfumo wa kuhudumia wakimbizi na jinsi ya kumaliza migogoro iliyopo katika nchi mbalimbali, jijini Dare s Salaam, Dk. Kikwete amesema, jopo hilo pamoja na mambo mengine limekutana kupokea taarifa ya changamoto na kujua jinsi gani nchi zenye uwezo mdogo zinaweza kusaidiwa na Jumuiya ya Kimataifa.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dk. Augustine Mahiga, amesisitiza msimamo wa Tanzania wa kutoendelea  kuwapa nafasi ya ajira, umiliki wa ardhi na ukazi wa kudumu wakimbizi kwa kutumia mkopo wa Benki ya Duniani bila kuzingatia mikataba ya Kimataifa iliyopo na kuitaka Jumuiya ya Kimataifa ingilie kati suala hilo.

Aidha amesema, Serikali imefikia hatua hiyo baada ya kujiridhisha na kuona ukiukwaji wa mikataba ya kimataifa ya kusaidia wakimbizi inakiukwa pamoja na msaada wa Shirika la Kimataifa la Wakimbizi, UNHCR bado halikidhi mahitaji yaliyopo na kukanusha si kweli kwamba Tanzania haitaki kusaidia wakimbizi.


 CHANZO: EATV

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>