• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

WATOTO WOTE WAPEWE ELIMU SAWA


Na Habiba Mpimbita

Wananchi wa Mkoa wa Mtwara na wilaya zake wametakiwa kuachana na mawazo mgando ya kuwabagua watoto kijinsia katika suala la utoaji wa elimu ili kuwajengea misingi bora watoto wao.

Hayo yamesemwa na Afisa elimu, vifaa na takwimu wa Wilaya ya Mtwara vijijini Bw. Kitonka Manase na kuwahasa wazazi kutowanyima haki ya msingi ya kupata elimu watoto wa kike kwa sababu za kimila na desturi.


Aidha Bw.Manase amewaomba Wasichana waliofanikiwa katika elimu kuwasaidia wasichana ambao bado wapo kwenye adha hii na jamii kwa ujumla kwa kuwapa elimu ili waeze kubadilika kifikra,na kuongeza kuwa sheria haibagui jinsia,dili ,wala kabila.
  
Na kwa upande wake Lenfrida Mwagama Mwanafunzi wa chuo cha kilimo mkoani Mtwara,amewashauri wasichana ambao wamepata nafasi ya kupata elimu waitumie vizuri ili iwasaidie kujiajiri wenyewe katika maisha yao na si kuajiriwa.

Hata hivyo nchini Tanzania takwimu zinaonyesha tatizo la ubaguzi wa kijinsia katika utoaji wa elimu kwenye miaka ya hivi karibuni kutokana na jitahada zinazofanywa na serikali pamoja  na taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo elimu zinazoendelea kutolewa kwa wananchi,ikiwa kwa Mwaka 2012 takwimu zinaonyesha uwiano sawa kati ya wasichana na wavulana katika elimu ya msingi,katika elimu ya sekondari ya kawaida uwiano ni 0.6% na sekondari ya juu ni 0.5%,hali inayoashiria kupungua kwa uwiano huo ukilinganisha na mwaka 2017  ambapo uandikishaji katika elimu msingi wavulana  milioni 4,629,027 sawa na 49.7% wasichana milioni 4,688,383 sawa 50.3% katika jumla ya wanafunzi milioni 9,317,410 na kwa upande wa sekondari jumla ya wanafunzi 199,019 wameandikishwa ikiwa wavulana 947,486 sawa 49.6% na  wasichana 961,531 sawa 50.4%.

Share:

SDA YAWANOA WATOTO WA KIKE

Na Ramla Massali



Shirika lisilo la kiserikali ya Sports Development Aid ambalo limejikita katika michezo na kutoa Elimu kwa watoto wa kike, wameendelee kuwaelimisha watoto wa kike hasa wale waliopo sekondari katika kata ya mayanga.



lengo kuu ni mtoto wa kike kutambua haki zake na kuza sauti pale anapohitaji msaada. sikiliza upate kujua kile kilichijiri










Share:

Amuua Mkewe, aenda polisi na kuwaambia “Nimemmaliza nendeni mumchukue

Na Mwandishi Wetu, Kenya.
Anthony Karanja mwenye umri wa miaka 25 anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumuua mkewe kwa kumkata na shoka na kumchoma visu kufuatia ugomvi uliozuka baada ya kupokea ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake (ya Karanja).
Kwa mujibu wa Polisi wa eneo la Trans Nzoia nchini Kenya, Karanja alipokea ujumbe huo kwenye simu yake ambao mkewe aliouna na kuanzisha ugomvi kutokana na wivu wa mapenzi, lakini alijibiwa kwa kushambuliwa kwa visu na kumkata na shoka.
Polisi wameeleza kuwa mtuhumiwa ambaye alijisalimisha mwenyewe polisi baada ya kutekeleza mauaji hayo alieleza kuwa alimchoma mkewe Esther Wangui kisu kwenye paja, kwenye miguu na kifuani.
Imeelezwa kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo Jumapili iliyopita, alijaribu kujiua bila mafanikio na ndipo alipofika katika kituo cha polisi akipiga kelele, “Nimemmaliza endeni mumchukue.”
Majirani wameeleza kuwa walisikia ugomvi kati ya wawili hao majira ya saa moja na nusu asubuhi. Wameeleza kuwa baada ya kutekeleza mauaji, mtuhumiwa alikunywa sumu ili ajiue lakini hakufanikiwa ndipo alipoamua kujinyonga kwa kamba lakini pia hakufanikiwa.
“Mtuhumiwa aliwapeleka maafisa wetu nyumbani kwake na akawapa funguo kuwawezesha kuuchukua mwili wa marehemu,” Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Jackson Mwenga anakaririwa.
Mwenga alisema kuwa wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa na wameanza kufanya upelelezi.
Share:

FAMILIA YA BABU SEYA YAPATA PIGO

 


Ikiwa ni siku chache zimepita mara baada ya msanii mkongwe Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha kuachiwa huru kutokana na kupewa msamaha wa rais Magufuli katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika Desemba 9, mwaka huu mjini Dodoma familia hiyo imepata pigo baada ya mdogo wa Babu Seya aitwaye Crizo Chimbukizi kufariki dunia.


Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, King Kikii, Crizo alifariki dunia jana kutokana na mshtuko wa moyo baada ya kupewa taarifa ya kuachiliwa huru kwa wawili hao na kwamba taratibu za mazishi zinafanywa.


Marehemu anatarajiwa kuzikwa mkoa wa Katanga Kongo nyumbani kwa familia ya Nguza.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli alitoa msamaha kwa mwanamuziki maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza maarufu kama Papii Kocha wasanii waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.

Share:

MSAADA WA KISHERIA

Na Mwandishi wetu

Naibu katibu mkuu wa wizara na sheria Amon Mpanju
ameongoza wadau mbalimbali wanaojihusisha na masula ya utoaji wa msaada wa
kisheria katika maadhimisho ya wiki ya wasaidizi wa sheria nchini, katika kanda
ya kusini





Share:

SHERIA ZA BARABARANI ZATEKELEZWA


Image result for MABASI YA MIKOANI
Madereva nchini wamepongezwa   kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji usiozingatia sheria za barabarani.
Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania  Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) amezungumzo pindi akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani  unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali
Kamanda Mselemu amesema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote  ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi  wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili  na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike  na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri na
Hata hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salanma na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekeklezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50 kama
“Serikali ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali inatengeneza uchumi wa kati  na viwanda kwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda  miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda Mselemu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na nmapenzi ya Mungu “hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za barabarani.


Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 2 ilikua 639,vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376,vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.
Naye  Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia  Mery Kessy alisema zaidi ya asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni asilimia 10 tu nchi hizo  zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni  vijana kati ya miaka miaka 15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya afya.
CHANZO: MJENGWA
Share:

KUANGUKA KWA TAKATAKA BARABARANI KUELEKEA DAMPO KUU LA MTWARA


Na Msafiri kipira


Wananchi wanaoishi jirani na dampo la mangamba wamelalamika kutokana na hali ya dampo, pia udondokaji wa takataka barabarani kutokana na uendeshaji wa mwendo na kusababisha udondokaji wa takataka barabarni kitendo kinachosababisha kuonekana wananchi ndio watupaji wa takataka.

Kauli ya mkazi mmoja anaefahamika kwa jina la shungi mkazi wa mangamba amewaomba wafanyakazi wa magari yanayobeba takataka kufunika vizuri pindi wanapobeba takataka ili kuepuka kudondoka kwa takataka barabarani. Sikiliza ripoti hii inahusu mazingira na kero hii katika barabara kuu inayoelekea dampo kuu la mkoa wa mtwara.

Je Diwani wa kata hii analizungumziaje jambo hili?


Share:

ATHARI ZA UKATAJI WA MITI - MTWARA


Na Karimu Faida

Kwa mujibu wa tafiti ya sera ya taifa ya misitu ya mwaka 1998, theruthi mbili ya misitu iko hatarini kuvamiwa huku Tanzania ikiathirika kwa matumizi ya mkaa. Kijiji cha Moma ni sehemu ya maeneo yaliyoathirika kutokana na matumizi mabovu ya ardhi.

Wananchi wengi hasa maeneo ya vijijini huvamia na kukata miti hovyo, pamoja na kuwepo kwa hali hiyo kumesababisha kuhama kwa wanyama pamoja na upotevu wa Mvu. Fuatilia makala haya kujua nini jitihada zinazofanyika ili kuhakikisha misitu inahifadhiwa.




Share:

IFAHAMU JAMII FM

Utangulizi
Jamii FM Radio, ilianza matangazo yake rasmi mwezi Septemba mwaka 2016. Madhumuni ya Radio hii ni kupasha Habari na kutoa fursa ya Mawasiliano kwa Jamii, hasa Jamii ya vijijini. Vipindi vyake vinaandaliwa kwa namna inayogusa na kulenga maisha ya jamii ya vijijini, ikiwa ni pamoja na watu wenye mahitaji maalum kama Walemavu na watu wasiojiweza.


Radio Jamii FM hutangaza habari zinazoelimisha na kuwa Jukwaa la kubadilishana habari za maendeleo ya jamii, hivyo kutengeneza fursa huru kwa jamii kupaaza sauti. Ushirikishwaji jamii unasisitizwa katika kuandaa vipindi. Hivyo,Radio Jamii hutoa fursa kwa wasio na sauti katika Jamii kupaza sauti.

Introduction

JAMII FM is a Community Radio that was launched in September 2016 for the purpose of giving community members particularly from rural areas access to information and means of communication. The programmes are basically focused on issues that directly or indirectly reflects community livelihood including people with special needs. Through Jamii FM Radio, educational and developmental information is disseminated and exchanged; important local issues are aired; a free market place of ideas and opinions is opened up and people are given the opportunity to express themselves. Broad participation by community members is always encouraged in Program production. JAMII FM RADIO gives voice to the voiceless.

Jamii fm On-Air

Dira

Kuona kwamba kupitia Radio Jamii FM, Jamii ya Mikoa ya Mtwara na Lindi hasa inayoishi vijijini, inapata habari na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazohusu maendeleo yao.


Vision
The VISION of Jamii FM is to see the community of Lindi and Mtwara Regions particularly from rural areas have access to information and increased capacity to play a meaningful role for their own development through media..

Production control room                                                                      Production room     


Dhima

Kuwezesha Jamii kutumia Vyombo vya habari katika kukuza mawasiliano shirikishi ili kujiletea maendeleo endelevu

Dhima

Kuwezesha Jamii kutumia Vyombo vya habari katika kukuza mawasiliano shirikishi ili kujiletea maendeleo endelevu


Eneo
Kituo cha Radio Jamii kipo Kitongoji cha Naliendele, kilichopo umbali wa kilometa 9 kutoka Mtwara Mjini katika barabara inayoelekea Newala. Kituo hiki kipo mkabala na Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo, Naliendele, Mtwara

Location

JAMII FM Radio Station is located at Naliendele area 9km from Mtwara Town along Mtwara-Newala road. The station is opposite to Naliendele Agriculture Research Institute.



Located at mtwara

News Room


Eneo la Huduma
Radio Jamii inamiliki Mnara wenye urefu wa Mita 60 unaowezesha Kituo kurusha matangazo na kufikia idadi kubwa ya wakazi wa eneo hili kuanzia Manispaa ya Mtwara na kusambaa hadi kufikia Nanyamba, Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea, Lindi na baadhi ya maeneo yanayoambaa kwenye mpaka wetu na Nchi jirani ya Msumbuji

Coverage:
JAMII FM RADIO owns its 60 meters transmission tower that enables to reach the huge population from both Mtwara and Lindi regions, from Mtwara Municipal up to Nanyamba, Tandahimba, Newala, Nachingwea, Lindi and some parts along the boarder with neighbouring country-Mozambique.

 
Adminstration

Ratiba ya Vipindi
0600 – 1000hrs – Dira ya Asubuhi
1000 – 1300hrs – Kapu la Jamii
1300 – 1300hrs – Habari kwa ufupi
1300 – 1600hrs – Mchakamchaka
1600 – 1610hrs – Habari (News Bulletin)
1610 – 1800hrs – Sauti ya Jamii
1800 – 1900hrs – Radio France International (RFI)
1900 – 1910hrs – Habari (News Bulletin)
1910 – 2000hrs – Dimba la Michezo (Sports)
2000 – 2100hrs – Makala Maalum
2100 – 2200hrs – Usiku Mwema
2200 – 0000hrs – Love Boat

0000 – 0600hrs – Music Mix

Programme Schedule
0600 – 1000hrs – Dira ya Asubuhi
1000 – 1300hrs – Kapu la Jamii
1300 – 1300hrs – Habari kwa ufupi
1300 – 1600hrs – Mchakamchaka
1600 – 1610hrs – Habari (News Bulletin)
1610 – 1800hrs – Sauti ya Jamii
1800 – 1900hrs – Radio France International (RFI)
1900 – 1910hrs – Habari (News Bulletin)
1910 – 2000hrs – Dimba la Michezo (Sports)
2000 – 2100hrs – Makala Maalum
2100 – 2200hrs – Usiku Mwema
2200 – 0000hrs – Love Boat

0000 – 0600hrs – Music Mix

Share:

Ahadi ya Rais Magufuli kwa waandishi wa Habari

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>