Makampuni 88 yajisajili kununua korosho nchini msimu wa 2025/2026

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania Brigadia Mstaafu Aloyce Mwanjile akizungumza na Waandishi wa Habari (Picha na Musa Mtepa)

Zaidi ya makampuni 88 yamejisajili kununua korosho msimu wa 2025/2026. Bodi ya Korosho Tanzania yatoa onyo kwa wanunuzi wasio rasmi na kusisitiza matumizi ya mfumo wa TMX kuhakikisha wakulima wanapata bei bora

Na Musa Mtepa

Wakati wakulima wa korosho wakiendelea na shughuli za upaliliaji na uvunaji, imeelezwa kuwa zaidi ya makampuni 80 tayari yamejisajili kununua zao hilo kwa msimu wa mwaka 2025/2026, huku makampuni 48 yakionyesha nia ya kununua korosho karanga.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Korosho Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Brigedia Mstaafu Aloyce Mwanjile, amesema hadi kufikia Oktoba 18, 2025 jumla ya makampuni 88 yalikuwa yamejisajili kwa ajili ya kununua korosho, ambapo kati ya makampuni hayo, 24 yamejisajili kwa ajili ya soko la awali, 48 kwa ajili ya kununua korosho karanga, na 16 kwa ajili ya kununua korosho ghafi.


Sauti ya 1: Brigedia Mstaafu Aloyce Mwanjile, Mwenyekiti CBT

Aidha, Brigedia Mwanjile ametoa wito kwa makampuni mengine yanayokusudia kununua korosho kuendelea kujisajili, huku akihimiza waje na bei nzuri zitakazowanufaisha wakulima pindi msimu wa mauzo utakapoanza.

Sauti ya 2: Brigedia Mstaafu Aloyce Mwanjile, Mwenyekiti CBT

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Frances Alfred, ameeleza kuwa kumekuwepo na taarifa za baadhi ya watu kuanza kusambaza mizani kwa ajili ya ununuzi wa korosho nje ya mfumo rasmi (maarufu kama “kangomba”) na kubainisha kuwa Bodi hiyo tayari imepeleka timu maalum inayozunguka maeneo mbalimbali kubaini vitendo hivyo na kuchukua hatua kwa wale watakaobainika kwenda kinyume na utaratibu wa kisheria.

Sauti ya 1: Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania

Frances Alfred amesema kuwa kuelekea msimu wa 2025/2026, Bodi ya Korosho imeimarisha mfumo wa usimamizi kwa lengo la kudhibiti kwa ufanisi zaidi biashara ya korosho na kuhakikisha mnunuzi anapata korosho bora.

Sauti ya 2: Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania
Frances Alfred mkurugenzi mkuu wa Bodi ya korosho Tanzania akizungumza na Waandishi wa habari (Picha na Musa Mtepa)

Kwa mujibu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), minada ya korosho itaendelea kufanyika kupitia Soko la Bidhaa Mtandao (TMX) kama ilivyokuwa msimu uliopita, ili kuhakikisha wakulima wanapata bei kulingana na hali halisi ya soko.

Share:

No comments:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>