
Taharuki yatanda Magomeni Nyasi baada ya kugunduliwa kifaa kisichojulikana chenye hirizi, kinachodhaniwa kuhusika na imani za kishirikina. Wakazi wataka uchunguzi wa kina kufuatia ongezeko la matukio ya aina hiyo kijijini
Na Musa Mtepa
Mtwara –Wakazi wa kijiji cha Magomeni Nyasi, kilichopo kata ya Tangazo, Halmashauri ya Mtwara Vijijini, Oktoba 12,2025 wameamka na taharuki kubwa baada ya kukutwa kwa kifaa kisichojulikana kilichozungushiwa hirizi, tukio linalodhaniwa kuhusishwa na imani za kishirikina.
Wakizungumza na Jamii FM, baadhi ya wananchi wameelezea mshangao wao juu ya tukio hilo, wakikitaja kuwa cha kutisha na kisicho cha kawaida.

Kijana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Alfani amedai kuwa tukio hilo lina uhusiano na ujio wa waganga wa kienyeji waliotembelea kijiji hicho siku za nyuma kwa lengo la kutoa uchawi.
Mzee Abdala Yusuf Nammandila, ambaye ndiye mmiliki wa nyumba iliyokutwa na kifaa hicho chenye hirizi, amesimulia jinsi alivyokigundua na hatua alizochukua mara baada ya kukikuta.
Tukio hili limezua hofu miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho, wengi wao wakitoa wito kwa mamlaka husika kufanya uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya kishirikina ambayo yanaonekana kuongezeka kwa kasi maeneo ya vijijini.






No comments:
Post a Comment