Prof. Ndalichako ameyasema
hayo leo jijini Arusha alipotembelea katikia Chuo Kikuu cha Mount Meru ili
kujionea miundombinu na namna wanavyosimamia suala la utoaji elimu ya juu
chuoni hapo.
Akiwa chuoni hapo, Prof.
Ndalichako ameonesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watumishi wa umma kuwa na
ajira mbili kwa wakati mmoja, wakifanya serikalini na kwenye taasisi binafsi
kwa mkataba kamili (full time) na hivyo kuwataka kuacha kufanya ivyo mara moja.
Kauli hiyo ya Ndalichako
inafuatia kugundua kuwa baadhi ya wafanyakazi katika chuo hicho ni waajiriwa wa
serikali na hivyo kupokea mishahara miwili kwa wakati mmoja, yaani ule wa
serikali na wa taasisi binafsi.
“Kanuni za utumishi, kifungu cha F cha
namba 4 na 7, kinazuia mtumishi wa umma kuwa na ajira mbili, na mtumishi wa
umma akiwa na ajira mbili, automatically anapoteza ajira yake kwenye utumishi
wa umma” amesema
waziri Ndalichako
Katika htua nyingine waziri Ndalichako
ameonesha kukerwa na upikaji wa alama unaofanywa na baadhi ya wahadhiri
wasiokuwa waaminifu, na wazalendo kwa taifa, na hivyo kuwataka kuacha kufanya
vitendo vya namna hiyo mara moja iwezekanavyo.
“Suala la kupika alama za wanafunzi, ni
suala ambalo Tanzania hatujafika hapa” amesema Prof. Ndalichako.
Prof. Ndalichako amehitimisha
ziara yake chuoni hapo kwa kuutaka uongozi wa chuo kuwaondoa wahadhiri wote
wasio na sifa za kufundisha chuoni hapo.






No comments:
Post a Comment