• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Orodha ya Vyuo/Taasisi Zinazoruhusiwa Kufanya Udahili wa Wanafunzi Wapya 2018

Na Jina la Chuo/Taasisi

1 Agency for Development of Education Management (ADEM) – Mbeya Campus
2 AMO Training Centre - Bugando
3 Arafah Teachers' College - Tanga
4 Archbishop John Ramadhan School of Nursing - Korogwe
5 Ardhi Institute - Tabora
6 Ardhi Institute Morogoro - Morogoro
7 Arusha Institute of Business Studies - Arusha
8 Arusha Lutheran Medical Centre School of Nursing - Arusha
9 Arusha Technical College - Arusha
10 Assistant Medical Officers Training College -Mbeya
11 Bagamoyo College of Arts (TaSUBa) - Bagamoyo)
12 Bagamoyo School of Nursing - Bagamoyo
13 Bariadi Teachers College - Bariadi
14 Berega School of Nursing - Kilosa
15 Besha Health Training Institute - Tanga
16 Bishop Nicodemus Hando College of Health Sciences - Babati
17 Borigaram Agriculture Technical College - Dar es Salaam
18 Bugando School of Nursing - Nyamagana
19 Bulongwa Health Sciences Institute - Makete
20 Bulongwa Training Institute - Makete
21 Bustani Teachers’ College - Kondoa
22 Butimba Teachers College - Nyamagana
23 Capital Teachers’ College - Dodoma
24 Centre for Educational Development in Health Arusha
25 Centre for Foreign Relations - Dar-es-Salaam
26 Coast Teachers College - Kibaha
27 College of Business and Management - Dar es Salaam
28 College of Business Education - Dar-es-Salaam
29 College of Business Education - Dodoma
30 College of Business Education – Mwanza Campus
31 Dabaga Institute of Agriculture - Kilolo
32 Dar es Salaam School of Journalism - Dar es Salaam
33 Dar-es-Salaam Institute of Technology - Dar-es-Salaam
34 Dar-es-Salaam Maritime Institute - Dar-es-Salaam
35 Dodoma Institute of Development and Entrepreneurship – Dodoma
36 Eastern Africa Statistical Training Centre - Dar-es-Salaam
37 Eastern and Southern African Management Institute - Arusha
38 Ebonite Institute of Education - Dar es Salaam
39 Eckernforde Teachers' College - Tanga
40 Elijerry Training Centre - Muheza
41 Faraja Health Training Institute - Moshi
42 Fisheries Education and Training Agency (FETA) Mbegani - Bagamoyo
43 Fisheries Education Training Agency (FETA) - Nyegezi
44 Forest Industries Training Institute (FITI) - Moshi
45 Forestry Training Institute (FTI) Olmotonyi - Arusha
46 Future World Business College - Dar es Salaam
47 Geita School of Nursing - Geita
48 Habari Maalum College - Arusha
49 Heri Nursing School - Kigoma
50 Horticultural Research and Training Institute – Tengeru Arusha
51 Huruma Health Training Institute - Rombo
52 Igabiro Training Institute of Agriculture - Muleba
53 Ilasi Training Institute - Mbozi
54 Ilembula Institute of Health and Allied Sciences - Njombe
55 Ilonga Teachers’ College - Kilosa
56 Ilula Nursing School - Kilolo
57 Institute of Accountancy Arusha - Arusha
58 Institute of Adult Education - Dar-es-Salaam
59 Institute of Adult Education – Mwanza
60 Institute of Finance Management - Dar-es-Salaam
61 Institute of Finance Management - Mwanza Campus
62 Institute of Judicial Administration - Lushoto
63 Institute of Procurement and Supply - Dar-es-Salaam
64 Institute of Rural Development and Planning - Dodoma
65 Institute of Rural Development and Planning – Mwanza Campus
66 Institute of Social Work - Dar-es-Salaam
67 Institute of Tax Administration - Dar-es-Salaam
68 Institution of Construction Technology – Morogoro
69 International Film Angels Training School – Dar-es-Salaam
70 Isimila Nursing School - Iringa
71 Kabanga School of Nursing - Kasulu
72 Kahama College of Health Sciences - Kahama
73 Kairuki School of Nursing - Dar es Salaam
74 Kaliua Institute of Community Development -Tabora
75 KAM college of Health Sciences - Dar es Salaam
76 KAPS Community Development Institute - Mufindi
77 Karagwe Institute of Allied Health Sciences - Karagwe
78 Karatu Health Training Institute - Karatu
79 Karume Institute of Science and Technology - Zanzibar
80 Kasulu Teachers College - Kasulu
81 Katoke Teachers College - Muleba
82 Katoro Teachers College - Bukoba
83 KCMC AMO General School Moshi - Moshi
84 KCMC AMO Ophthalmology School - Moshi
85 KCMC School of Physiotherapy - Moshi
86 Kibaha College of Health and Allied Sciences - Kibaha
87 Kidugala Teachers College - Njombe
88 Kilacha Agriculture and Livestock Training Institute - Moshi
89 Kilema College of Health Sciences - Moshi
90 Kilimanjaro Agricultural Training Centre - Moshi
91 Kilimanjaro Institute of Technology and Management - Dar es Salaam
92 Kilimanjaro International Institute for Telecommunications, Electronics and Computers (KIITEC) - Arusha
93 Kilimanjaro Modern Teachers' College - Moshi
94 Kilimanjaro School of Pharmacy - Moshi
95 Kilombero Agricultural Training and Research Institute (KATRIN) - Kilombero
96 King’ori Teachers’ College - Arusha
97 Kirinjiko Islamic Teachers' College - Same
98 Kisanga Teacher’s College - Dar es Salaam
99 Kisongo Teachers' College - Arusha
100 Kiuma Nursing School -Tunduru
101 Kiuma Teachers College - Tunduru
102 Kizimbani Agricultural Training Institute - Zanzibar
103 Kolandoto College of Health Sciences - Shinyanga
104 Korogwe Teachers College - Korogwe
105 Landmark Institute of Education Sciences and Technology – Geita
106 Livestock Training Agency - Mpwapwa
107 Livestock Training Agency (LITA) - Dar es Salaam
108 Livestock Training Agency (LITA) - Morogoro
109 Livestock Training Agency (LITA) Mabuki - Misungwi
110 Livestock Training Agency Buhuri Campus - Tanga
111 Livestock Training Agency Kikulula - Karagwe
112 Livestock Training Agency Tengeru Campus –Arusha
113 LUA Teacher’s College - Dar es Salaam
114 Lugala School of Nursing - Ulanga
115 Lugalo Military College of Medical Sciences - Dar es Salaam
116 Lugarawa Health Training Institute - Ludewa
117 Mabughai Community Development Technical Training Institute - Lushoto
118 Machame Health Training Institute - Moshi
119 Makambako Institute of Health Sciences - Makambako
120 Malya College of Sports Development - Kwimba
121 Mamire Teachers' College - Babati
122 Mamre Agriculture and Livestock College - Wanging’ombe
123 Mandaka Teachers’ College - Moshi
124 Mary Queen Technology College - Morogoro
125 Mbalizi Polytechnic College - Mbeya
126 Meteorological Training Cntre - Kigoma
127 Military Aviation School – Ngerengere
128 Mineral Resources Institute - Dodoma
129 Ministry of Agriculture Training Institute - Mbeya
130 Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Ilonga - Kilosa
131 Ministry of Agriculture Training Institute (MATI) Mtwara - Mtwara
132 Ministry of Agriculture Training Institute Igurusi -Mbeya
133 Mirembe School of Nursing - Dodoma
134 MISO Teachers College - Mufindi
135 Mkolani School of Nursing and Midwifery - Mwanza
136 Monduli Teachers' College - Monduli
137 Montessori Teacher Training College - Mtwara
138 Montessori Teachers' Training Centre - Lushoto
139 Montessori Training Centre - Mwanza
140 Moravian Teachers Training College - Mbeya
141 Morogoro Teachers College - Morogoro
142 Moshi Teachers’ College - Moshi
143 Mpuguso Teacher Training College - Tukuyu
144 Ms Training Centre for Development Cooperation - Arusha
145 Mt. Maria Goretti Agriculture Training Institute - Kilolo
146 Mtwara (K) Teachers College - Mtwara
147 Mtwara (U) Teachers College - Mtwara
148 Mtwara Clinical officers training Centre - Mtwara
149 Mtwara Nursing Training College (MNTC) - Mtwara
150 Mufindi Teachers College - Mufindi
151 MusomaUtalii College - Tabora
152 Muyoge Health Science and Management College - Mafinga
153 Mvumi Institute of Health Sciences - Dodoma
154 Mwambani School of Nursing - Songwe
155 Mweka College of African Wildlife Management - Moshi
156 Nachingwea Teachers College -Nachingwea
157 National College of Tourism (NCT), Temeke Campus - Dar es Salaam
158 National College of Tourism, Bustani Campus - Dar es Salaam
159 National Institute of Transport - Dar-es-Salaam
160 Nazareth College of Education - Mbinga
161 Ndala Teachers’ College - Nzega
162 Ndolage School of Nursing - Bukoba
163 New Mafinga Health and Allied Institute - Mafinga
164 Newala School of Nursing - Mtwara
165 Njombe Health Training Institute - Njombe
166 Njombe School of Nursing - Njombe
167 Njuweni Institute of Hotel, Catering and Tourism Management - Kibaha
168 Nkinga Institute of Health Sciences - Igunga
169 Northern Highlands Teachers’ College - Moshi
170 Operating Theatre Management School - Mbeya
171 Paradigms College of Health Sciences - Dar es Salaam
172 Paradise Business College - Sumbawanga
173 Peramiho School of Nursing - Songea
174 Primary Health Care Institute - Iringa
175 Richrice Teachers College - Geita
176 Rubya Health Training Institute - Muleba
177 Rungemba Teacher College - Iringa
178 Rungwe International College of Business and Entrepreneurship Development - Rungwe
179 School of Optometry – KCMC - Moshi
180 Sengerema Clinical Officers Training Institute - Sengerema
181 Shaalika Institute of Science and Technology - Same
182 Shinyanga Teachers College - Shinyanga
183 Shirati College of Health Scinces - Rorya
184 Shiwanda Teachers College - Mbozi
185 Singachini Teachers' College - Moshi
186 Singida Health Laboratory Assistants School - Singida
187 Songe Teachers’ College - Kilindi
188 Songea Teachers College - Songea
189 Sr. Dr. Thekla Nyangao School of Nursing - Mtwara
190 St Aggrey College of Health Science - Mbeya
191 St. Alberto Teachers College - Musoma
192 St. Bakhita Health Training Institute - Nkasi
193 St. Bernard Teachers’ College - Singida
194 St. Francis Technical College – Dar es Salaam
195 St. Gaspar School of Nursing - Itigi
196 St. John College of Health Science - Mbeya
197 St. Magdalene School of Nursing - Misenyi
198 St. Mary’s Teachers College - Dar es Salaam
199 St. Monica Teachers College - Iringa
200 St. Rock College of Early Education - Korogwe
201 Sumve School of Nursing - Kwimba
202 Sunrise Teachers College - Mbozi
203 Suye Health Institute – Arusha
204 Tanzania Correctional Training Academy - Dar es Salaam
205 Tanzania Geommological Centre – Arusha
206 Tanzania Institute of Accountancy - Dar-es-Salaam
207 Tanzania Institute of Accountancy – Mbeya Campus
208 Tanzania Institute of Accountancy - Mwanza Campus
209 Tanzania Institute of Accountancy – Singida Campus
210 Tanzania Peoples Defence Force ICT Centre - Dar es Salaam
211 Tanzania Police School - Moshi
212 Tanzania Police Staff College - Kidatu
213 Tanzania Regional Immigration Training Academy - Moshi
214 Tanzania Training Center for International Health (TTCIH) - Ifakara
215 Tengeru Community Development Training Institute - Arusha
216 The Mwalimu Nyerere Memorial Academy - Dar-es-Salaam
217 The Mwalimu Nyerere Memorial Academy - Zanzibar
218 Triple J Institute of Social Studies – Arusha
219 Tumaini Jipya Medical Training School - Mafinga
220 Tusaale Business and Planning College – Mafinga
221 Tusaale Teachers College - Mufindi
222 Unique Academy - Dar-es-Salaam
223 University Computing Centre - Dodoma
224 University of Dar es Salaam Computing Centre - Arusha
225 University of Dar es salaam Computing Centre - Mbeya Campus
226 University of Dar es Salaam Computing Centre - Mwanza
227 Ununio Institute of Professionals - Dar es Salaam
228 Vector Control Training Centre - Muheza
229 VETA Kipawa ICT Centre - Dar es Salaam
230 Vikindu Teachers College - Mkuranga
231 Visele Live-Crop Skills Training Centre - Mpwapwa
232 Waama Lutheran Teachers’ College - Mbulu
233 Wami International College of Business Management - Morogoro
234 Water Development and Management Institute - Dar-es-Salaam
235 Wesley College – Mwanza
236 Yohana Wavenza Health Institute - Songwe
237 Zanzibar College of Business Education - Zanzibar
238 Zanzibar Law Resource Centre - Zanzibar
239 Zanzibar Police College - Zanzibar
240 Zanzibar School of Journalism and Media Studies - Zanzibar

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
TAREHE : 20 Machi, 2018
Share:

Tamko La Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu Kuelekea Maadhimisho Ya Siku Ya Kifua Kikuu Duniani Machi 24 – Leo Mjini Dodoma

Na WAMJW-Dodoma.
# Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.

# Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.

# Tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini mwao.

# Kauli mbiu ya mwaka huu inasema *” Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB.”*

#Nchini Tanzania kila mwaka jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.

# Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele.

# Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma na Binafsi.

# Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kikuu nchini ikiwemo kuimarisha uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu katika Vituo vya Afya.

# Serikali na wadau mbalimbali tunaendelea na utekelezaji wa kampeni za uhamasishaji na upimaji wa Wananchi katika maeneo ya migodi, makazi duni kwenye miji mikubwa, magereza na shule za bweni.

# Pia Serikali imezindua dawa mpya za TB za watoto ili kuhakikisha zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani ( WHO), dawa hizo mpya ni za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na  tayari zimeshawasili nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na Halmashauri zote nchini.

# Nawaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya  kuanza masomo.

#Ni marufuku kwa Madaktari  kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima wanafunzi husika. Kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa  kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.

# Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.

#Mpaka sasa takribani watoa huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.

Share:

Anna Makinda ataka viongozi wanawake kupewa elimu

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania mstaafu, Mama Anna Makinda ametoa elimu wa uongozi wa Kijinsia kwa madiwani wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo madiwani hao.

Akizungumza katika warsha hiyo, Bi. Makinda alisema suala la kuwajengea uwezo wanawake linapaswa kuanza mapema mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi ili kupata muda zaidi wa viongozi hao kupata elimu stahiki, kwani mara nyingi elimu hiyo hucheleweshwa kutolewa.

“…Kimsingi muda huu tumechelewa mikakati ya kuanza kumuwezesha kiongozi mwanamke hupaswa kuanza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi hii itatusaidia hata kujipanga mapema uongozini…,” alisema Mama Makinda akizungumza na madiwani hao.

Aliwataka wanawake wote viongozi kuwa pamoja hasa wanapopigania masuala ya wanawake ili kwani umoja mara zote ni nguvu na utengano ni udhaifu. Changamoto za wanawake hazitofautiani kiitikadi za chama, rangi wala imani hivyo kuna kila sababu ya kuungana pale wanapogombea ajenda za wanawake.

Pamoja na hayo aliwataka madiwani wanawake kujipanga kimikakati na kutokubali kuondolewa katika nafasi za uongozi kizembe, kwani uwezo wa kuwatumikia wananchi wanao tena wa kiwango kikubwa kama watajipanga vizuri.

“…Hivi unakubalije mtu aliye nje kuja kukutoa katika nafasi yako kirahisi rahisi ilhali wewe upo karibu na wananchi, usikubali tuwaoneshe kwa vitendo tulioingia tusitoke kirahisi bila kupenda labda tupande ngazi lakini sio kushuka,” alisisitiza Mama Makinda.

Aidha aliwaomba kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano na viongozi wa kiume kwani idadi yao ni kubwa hivyo ushawishi pekee ndio unaweza kuongezea nguvu ajenda zao. 

Alibainisha idadi ya madiwani na wabunge wa kiume ni kubwa ukilinganisha na wao hivyo njia pekee ya wao kufanikiwa ni kujenga urafiki, ukaribu na ushawishi kwa agenda anuai zinazobebwa na wanawake.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Bi. Suzan Lyimo akizungumza na madiwani hao aliwaomba kuwa kitu kimoja haswa wanapopigania masuala ya msingi kumuwezesha mwanamke.

Alisema kama wanawake hawatakuwa kitu kimoja hawawezi kufanikiwa katika agenda zao. Hata hivyo aliongeza kuwa usawa wa kijinsia unapaswa kuanzia ndani ya vyama vya siasa kwani ndipo mipango mingi ya chama upangwa kwa utekelezaji zaidi.
Share:

DODOMA: Polisi Wamtia Mbaroni aliyejifanya JWTZ na Usalama wa Taifa

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 14 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu wakiwemo matapeli waliojifanya kuwa ni maofisa ununuzi kutoka Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na maofisa usalama wa Taifa.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakifanya vitendo vya uhalifu baada ya kumtapeli mfanyabishara mmoja kiasi cha sh. Million 8.

Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shaaban Kwiyela (58) Mkazi wa Kijiji cha Igunga Mkoani Tabora, ambaye alifukuzwa kazi kwa  utovu wa nidhamu tangu mwaka 1995 akiwa kikosi cha 36KJ Msangani Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha sajenti lakini amekamatwa akiwa na mavazi ya cheo cha Kaptein.

Wengine ni Emmanuel Michael (45) mkazi wa Iringa, Juma Pesambili (33) Mkazi wa Sai Mbeya na Emmanuel Mwagonela (50) Mkazi wa Mtaa wa Ghana mkoani Mbeya.

Share:

DODOMA: Serikali kuwatumia waganga wa kienyeji Kuwasaka Wagonjwa wa TB

Katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) nchini, serikali imesema kuwa itawatumia waganga wa kienyeji katika kuwagundua wagonjwa hao ili waweze kufikishwa kwenye vituo vya afya na kupata tiba sahihi.

Kauli hiyo imetolewa jana (Machi 23, 2018) mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yanayofanyika leo (Machi 24, 2018).

Waziri Mwalimu alisema kuwa waganga wa kienyeji ni wadau muhimu katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa wagonjwa wengi hukimbilia kwao kwa kudhani kuwa wamerogwa.

Aidha, Ummy amesema kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO inakadiriwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua kifua kikuu kila mwaka duniani huku milioni moja kati yao wakiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 15 na hapa nchini kila mwaka jumla ya watu 60,000 wanaambukizwa ugonjwa huo wakati mwaka 2016 watu 65,908 waliogundulika kuugua na kuanza matibabu.
Share:

DODOMA: Mbarawa "Serikali itaendelea kuiwezesha TMA"

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa ya hali ya hewa ili kuwezesha huduma bora za utabiri kutolewa kwa wakati na usahihi kwa manufaa ya taifa.

Profesa Mbarawa amesema hayo jana mjini Dodoma  wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Hali ya hewa, na kusisitiza kuwa kwa sasa TMA imeongeza imani kwa wananchi kwani imekuwa ikitoa utabiri wa kuaminika kwa  sababu ya kuwa  vifaa vingi na vya kisasa vya utoaji taarifa.

“Nipende kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwezesha TMA na kuhakikisha kuwa inatoa utabiri ambao ni sahihi na wa uhakika kwani kuwepo kwa utabiri sahihi kutawezesha vyombo husika kuchukua hatua mapema kabla ya madhara makubwa kutokea” alisema Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji na kuepuka kuchafua maeneo ya bahari ili kuepusha athari zinazoepukika zikiwemo uharibifu wa miundombinu ya  uchukuzi.

 “Niwaombe wananchi wote watunze mazingira kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu kutokana na shughuli zinazofanywa na binadamu katika maeneo mbalimbali yasiyotakiwa kulimwa au kujengwa, alisisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ameishukuru Serikali kwa jitihada inazozifanya kuwekeza kwenye miundombinu ya hali ya hewa kwa kutoa fedha kununua vifaa mbalimbali ambavyo vimewezesha mamlaka hiyo kutoa utabiri uliosahihi kwa zaidi ya asilimia 70.

Dkt Kijazi ameongeza kuwa kwa sasa taarifa za hali ya hewa hasa kwenye usafiri wa anga zimeimarika ambapo hutolewa kila baada ya nusu saa na kuwawezesha watumiaji wa usafiri huo kupata taarifa kabla ya kuanza safari zao.

“Kwa sasa utabiri wa usafiri wa anga ni wa  uhakika mpaka asilimia 90 na hutolewa kila baada ya nusu saa na marubani hupata taarifa hizo kwa wakati kabla ya kuanza safari zao, alisema Dkt. Kijazi.

Siku ya Hali ya Hewa duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 23 Machi ambapo mwaka huu yanaongozwa na kauli mbinu isemayo“JIWEKE TAYARI NA ZINGATIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA”.
Share:

DAR ES SALAAM: Majaji watatu kusikiliza kesi ya ACT Wazalendo dhidhi ya Jeshi la Polisi

Mahakama  kuu ya Dar es salaam Aprili 5, 2018 itaanza kusikiliza kesi ya madai ya chama cha ACT Wazalendo dhidi ya jeshi la polisi

Tarifa iiliyotolewa jana  na Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamisi  ilisema kuwa kesi hiyo itasikilizwa chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.

"Machi 18 tulizungumza na umma juu ya hali mbaya ya nchi Kiuchumi, na tukaeleza hatua ambazo kama chama tutachukua katika kutatua masuala kadhaa ya kinchi. 

"Kwenye eneo la DEMOKRASIA tulieleza kuwa tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza.

"Leo Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba."- Ilisema taarifa hiyo
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>