
DAR ES SALAAM: TFDA Yasitisha utoaji wa vibali vya uingizaji wa bidhaa za nyama kutoka Afrika Kusini kuazia leo Machi 7, 2018
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imezuia uingizaji wa soseji kutoka Afrika Kusini zilizobainika kuwa na bakteria aina ya listeria.
Uamuzi wa TFDA unatokana na soseji hizo aina ya Polony kubainika kuwa na aina hiyo ya bakteria wanaosababisha ugonjwa wa listeriosis uliosababisha vifo vya watu 180 nchini Afrika Kusini.
Soseji hizo kwa mujibu wa habari zilizochapishwa na vyombo kadhaa vya kimataifa zinatengenezwa na kiwanda cha tiger brands unit enterprises na cha RCL foods vyote vya Afrika Kusini.
Waziri wa Afya wa Afrika Kusini, Aaron Motsoaledi alikaririwa na mitandao ya kijamii akisema ameagiza kuondolewa sokoni soseji hizo, huku akiwashauri wananchi kuacha kula.
Motsoaledi alisema ingawa kiwanda cha RCL hakijatajwa kama chanzo cha ugonjwa huo, kitengo chake kinafanyiwa uchunguzi.
Ugonjwa wa listeriosis uliibuka Desemba mwaka jana na umeshasababisha vifo vya watu 180.

MTWARA: WANANCHI KULIPWA FIDIA NDANI YA WIKI MBILI
Mkuu wa mkoa wa MTWARA
MHE GELASIUS BYAKANWA amewahakikishia wananchi wa kata ya NANGOO wilayani MASASI
kuwa watalipwa fidia ya maeneo na Mali zilizoharibiwa wakati wa utekelezaji wa
mradi wa maji wa MBWINJI unaotumiwa na wananchi wa MASASI na NACHINGWEA.
MKuu wa mkoa
ametoa kauli hiyo baaada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa kata hiyo
yaliyoainishwa katika makundi matatu ikiwemo watu kulipwa pungufu, kulipwa
wasiostahili na wengine kutolipwa kabisa wakati ni wahanga.
Kufuatia hali
hiyo BYAKANWA amewaeleza wananchi wa kata hiyo na Kata jirani kuwa atahakikisha
kila mtu anayestahili kulipwa analipwa ndani ya miezi MIWILI baada ya uchunguzi
wa kutambua waliolipwa wakati hawana sifa kukamilika ambapo ndani ya miezi hiyo
miwili watakuwa wamebainika na hatua zitachukuliwa.
MHE BYAKANWA amesema
"Nipeni hii miezi MIWILI nikipata kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa
TAKUKURU tutashughulikia ngazi ya Mkoa kwa kuunda kamati itakayo fanya
uchunguzi na kutambua wale wanaostahili na wasiostahili na hatua zitachukuliwa
hapahapa bila kusubiri utaratibu wa TAKUKURU ambazo zina chukua unamlolongo
mrefu"
Wananchi wametoa
malalamiko kuwa kuna watu ambao hawakupitiwa na mradi walilipwa fedha wakati
wanaostahili hawajalipwa litafanyiwa kazi haraka na watarudisha fedha hizo ili
walipwe wanaostahili.
Akijibu hoja ya
kulipa fidia watu hewa Mwakilishi wa ofisi ya TAKUKURU Masasi ameeleza kuwa
uchunguzi unaendelea wa kuwabaini watu hao na kwa kijiji cha Liputu kilichopo
Kata ya ndanda wilayani humo umekamilka na imebainika kweli kuwa wapo watu
ambao walilipwa bila kuwa na maeneo yaliyoathiriwa na mradi.
Aidha MHE.
BYAKANWA amemwagiza Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha anafungua vioski vya
maji vyote vilivyofungwa kwasababu ya wauza maji wamekila hela ili wananchi
waendee kupata huduma ya maji kama serikali ya awamu ya tano inavyoelekeza kuwa
wananchi lazima wapate maji kwani wanaadhibiwa kwa kosa ambalo hawajatenda.
Pia amemsisitiza
Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha wale wauza maji wote waliokula fedha
wakamatwe ili walejeshe fedha hizo haraka na baada ya wiki mbili zoezi hilo
liwe limekamilika.
MHE. BYAKANWA amewataka
wananchi kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya maji kwani jamii ndio yenye
jukumu la kutunza kwa kuto fanya shughuli zozote karibu na vyanzo vya Maji
lakini pia kuilinda miundombinu yake kwani serikali inatumia fedha nyingi
kutekeleza Miradi hiyo.
Mradi wa Mbwiji
ulianza kutekelezwa 2011 mwaka na ulighalimu zaidi ya bilioni 30.
HABARI NA JOINA NZARI- MASASI
KIGOMA: ACT YATOA KILIO CHA WAKULIMA WA MAHARAGE KWA SERIKALI
Kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa leo Kiongozi wa ACT, Zitto Kabwe, amesema wakulima hao hulaliwa na wanunuzi wa zao hilo na kulazimika kuuza kilo moja ya maharage kwa bei ya Sh. 700 hadi 800, wakati yakisafirishwa mjini huuzwa Sh. 1800 hadi 2000 kwa kilo.
Amesema kufuatia changamoto hiyo, chama hicho kupitia Diwani wake wa Kata ya Biturana, Barnabas Baranzila wamehamasisha wananchi kuchonga barabara kutoka kwenye vijiji vya kata hiyo hadi makao makuu ya Kata, ili kurahaisha usafirishaji wa mazao na hivyo kupunguza unyonyaji kwenye soko.
Hata hivyo, Zitto amesema ACT itawasaidia wakulima hao kuunda ushirika imara ili kuhakikish ahawanyonywi katika soko la mazao yao.
CHANZO: DEWJBLOG
SINGIDA: WAZIRI NCHEMBA ACHANGIA UJENZI WA ZAHANATI NA MABWENI YA SHULE
Waziri Nchemba amesema anakwelwa na jengo kukaa mda mrefu bila kumaliziwa hivyo ameamua kutoa bati 210 na kuchangia shilingi milioni moja na nusu kwa ajili ya ununuzi wa mbao ili ujenzi uanze mala moja na kikamilike ndani ya mwaka huu kianze kutoa huduma.
Dr Nchemba amesema hayo akiwa ziarani katika kata ya Mtoa kijiji cha Masiga kitongoji cha kisaki jimboni kwake iramba Magharibi mkoa wa Singida kutekeleza ahadi alizozitoa wakati anagombea mwaka 2015.
Aliongeza kusema kuwa wakati wa masika kama huu baadhi ya maeneo ni ngumu sana hata magari kufika kutokana mito kujaa maji na barabara kuwa na utelezi na kufanya gari au watu kushindwa kupita kufata huduma hivyo ameamua kutoa mifuko 100 yaa cement ili ujenzi wa bweni la shule ya sekondari mtoa likamalike kuwasaidia wanafunzi ambao wanaishi mbali wawwze kujisomea vizuri kuliko sasa hadha wanayopata kuvuka mito ambapo ni hatari.
“Mimi nakelwa na jengo kukaa mda mrefu hivi,hatulali hata sekunde tunaendelea kutafuta mbao na bati nyingi zikafunike baadhi ya vituo kwahiyo ninapoona jengo lipo hivi wala mtu asidhanie nafurahie jengo libaki vilee”alisema Dr Mwigulu
Nao wananchi wa kata ya mto awamemshukuru mbunge wao kwa kuwaletea mabati na cement kwa ajili ya kumalizia zahanati yao ya mtoa kwani ni jambo ambalo walikuwa wanalilia kupata zahanati hiyo.
DAR ES SALAAM: WATANZANIA WAHIMIZWA KUJIUNGA NA MTANDAO WA MITAJI
Profesa Kamuzora alisema hayo wakati akizindua Mtandao wa Mitaji ya Ubia Tanzania – Tanzania Venture Capital Network jijini Dar es salaam jana.
Aidha Katibu Mkuu huyo amesema uzinduzi wa mtandao huo umefanyika wakati mwafaka ambapo serikali ya awamu ya tano ipo katika mikakati ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda,
Aliwataka wananchi kuacha uoga katika ushiriki wa kuwawezesha kuwepo kwa mitaji ya kutosha kwa ajili ya uimarishaji wa uwekezaji nchini Tanzania.
Alisema serikali kwa sasa inafanya kila linalowezekana kuhakikisha mazingira ya biashara na uwekezaji yanakuwa bora, ndio maana wameanzisha mchakato wa kutengeneza sera ya maendeleo ya viwanda hasa katika sekta binafsi.
Alisema ni vyema wenye viwanda na wananchi wengine kushiriki katika mchakato huo ili kufanikisha nia ya kuipeleka Tanzania katika nchi ya viwanda. Alisema kwa kuwa na sera sheria nyingi zitabadilika na hivyo kupunguza urasimu na pia vikwazo vya kuwezesha kazi katika masuala ya viwanda na biashara.
Pia alitaka wamiliki wa Ubia huo kushirikiana na Costech katika kuhakikisha kwamba viwanda vinaanzishwa na kuendelezwa.
Alitaka kuwepo na elimu ya fedha na mitaji ili wananchi waweze kuthubutu na kufanikisha mitaji.
Mapema Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini- TPSF Dr. Reginald Mengi amewataka wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa uwazi, kwa kuzingatia sheria za nchi, na kuwa tayari kujifunza maarifa mapya kila fursa inapojitokeza.
Akisitikishwa na mahudhurio duni ya wafanyabiashara katika hafla hiyo alisema kutofahamu undani wa soko la mitaji na fursa zake kunatokana na kutokuwa wazi na kufanya biashara kwa kufuata kanuni.
Akizungumzia kuhusu madai ya kuwapo kwa hali kuwa ngumu nchini Dr. Mengi pia amewataka Watanzania kuichukulia hali hiyo kama fursa ya kubuni biashara itakayowawezesha kupata faida kubwa.
Akiutambulisha Mtandao wa Tanzania Venture Capital kwa wadau, Muasisi wake Bw. Salum Awadh amesema Mtandao huo ni fursa kwa wawekezaji nchini kujipatia mitaji ya kuanzisha ama kuendeleza biashara zao kwa ubia kwa masharti rahisi.
Alisema kwamba wakati umefika kwa Tanzania kusonga mbele kutumia fursa zilizopo duniani za mitaji na kusema jirani zetu wa Kenya wamesonga mbele katika hilo.
Alisema kwamba kutokana na kutojua umuhimu na ushiriki katika mitaji yenye ubia, wananchi wengi wanakimbilia katika mabenki ya biashara ambako pia wanapambana na vikwazo vingine.
Alisema kwa kuwa na kampuni ya mitaji inayoweza kutafuta pia mtaji inayomilikiwa na wananchi wenyewe kupitia mitaji yao kutawezesha kuwapo na uimara wa viwanda na kuongeza idadi zake kwa kuwa mfumo wa fedha wa mitaji ni tofauti na kwenda benki.
Tanzania kwa sasa ina zaidi ya mabenki 50 ambayo yanajishughulisha na mambo mbalimbali yanayogusa biashara na hifadhi ya kawiada.
Alisema mazingira ya sasa yanahitaji mfumo mwingine wa ziada kusaidia upatikanaji wa mitaji nje ya mabenki na kuzinduliwa kwa mtandao wa ubia wa mitaji kutasaidia kuziba pengo lililopo.
Kwa sasa Tanzania kwa rekodi zilizopo inapata asilimia 17 ya mitaji ya ubia ya dola bilioni 2.4 iliyopo duniani huku Kenya ikiwa na nfasi nzuri zaidi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya sekta Binafsi nchini-TPSF Bw. Godfrey Simbeye, baadhi ya viongozi wa taasisi za serikali na wafanyabiashara mbalimbali.
DODOMA: SHILINGI TRILIONI 1 ZATENGWA KULIPA MADENI MBALIMBALI MWAKA WA FEDHA 2017/2018
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi ameeleza hayo leo Mjini Dodoma alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa miradi na ahadi mbalimbali za Serikali.
“Kati ya shilingi Trilioni 1 zilizotengwa kulipia madeni kwa mwaka huu wa fedha, shilingi Bilioni 896.3 zimeshalipwa kwa watoa huduma, wazabuni na watumishi wa Serikali,” alisema Dkt. Abbasi.
Amesema hesabu hiyo inajumuisha shilingi Bilioni 43 ambazo zimelipwa Februari, 2018 ikiwa ni malimbikizo ya wafanyakazi wa sekta ya Umma.
“Madeni mengine uhakiki unaendelea na yataendelea kulipwa siku zijazo na tutawajulisha,” alifafanua Dkt. Abbasi.
Vile vile amesema, Serikali katika kuwaondolea adha ya usafiri kwa wananchi wa maziwa makuu likiwemo Ziwa Nyasa, Tanganyika na Victoria. Kwa upande wa Ziwa Victoria, mkandarasi amepatikana na majadiliano ya mwisho na kusaini mkataba na kampuni ya STX ya Jamhuri ya Korea vitafanyika mwezi huu kwa ajili utengenezaji wa meli mpya itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na mizigo tani 400.
Kwa upande wa Ziwa Tanganyika zabuni kwa ajili ya utengenezaji wa meli mpya ya abiria na mizigo itatangazwa mwezi huu. Meli hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 600 na tani 400 za mizigo na italeta mapinduzi makubwa katika usafiri ziwani hilo.
Aidha Dkt. Abbasi amesema Julai mwaka huu nchi itapokea ndege kadhaa mpya ikiwemo Boeing Dreamliner na ukarabati wa viwanja vya ndege vya Kitaifa, Kimataifa na Kimkoa unaendelea kwa kasi kote nchini.
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
DODOMA: BASHE Akabidhi hoja binafsi kwa katibu wa BUNGE "kuchunguza matukio ya Mauaji na Utekaji Nchini"
Mbunge wa Nzega (CCM), Hussein Bashe ameshindwa kuvumilia matukio mbalimbali yanayojitokeza katika ardhi ya Tanzania na mwisho ameamua kuandika barua yenye hoja binafsi kwa Katibu wa Bunge ili kuundwe kamati ya teule ya uchunguzi.
"Leo asubuhi (jana) nimewasilisha kwa Katibu wa Bunge barua ya kusudio la kuwasilisha hoja binafsi ya kuunda Kamati teule ya Bunge kuchunguza matukio mbalimbali yanayoonesha kutishia umoja, usalama na mshikamano wa Taifa letu", amesema Bashe.
CHANZO: MPEKUZI HURU

MBEYA: Saba Watiwa Mbaroni Mbeya Kwa Mauaji ya Mlinzi Wa SUMA-JKT
#Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linawashikilia watu saba kwa matukio mbalimbali ya uhalifu, wakiwamo vijana watano wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya mlinzi wa SUMA-JKT.
Wanadaiwa kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumpora bunduki na kutokomea nayo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa #Mbeya, Mohammed Mpinga, alisema Februari 26, mwaka huu ya saa 1:30 jioni, vijana hao wakiwa na mapanga, walimvamia na kumshambulia mlinzi huyo, Chewe Wilson (34), akilinda kituo cha mafuta cha Manyanya kilichopo Uyole.
Aliwataja vijana hao ni Hamis Shaban (19) na Ibrahim Mbilinyi (22) wote wakazi wa Itezi, Stan Wema (21) mkazi wa Uyole, Bahati Laulend (22) mkazi wa Iduda na Sambaa Samson (32) mkazi wa Isyeseye.
Alisema vijana hao baada ya kumjeruhi wakidhani amekufa walimpora bunduki aina ya Shortgun, mali ya SUMA-JKT aliyokuwa anaitumia na kutokomea nayo.
Hata hivyo, alisema mlinzi huyo alikutwa na wasamaria wema akiwa hai na kukimbizwa katika Hospitali ya Kanda ya Rufani ya Mbeya, lakini akafariki kesho yake kutokana na kuvuja damu nyingi.
“Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata vijana hao na baada ya kupekuliwa walikutwa na bunduki hiyo waliyopora yenye namba za usajili 009009906-MP-18EM-M wakiwa wameificha nyumbani,” alisema Mpinga na kuongeza:
“Vilevile vijana hao wanaojiita ‘Doshaz’ walikutwa na mapanga matatu ambayo mojawapo lilitumika kumjeruhi Chewe na maganda matatu matupu ya risasi, tulipowahoji walikiri kuhusika na tukio hilo na tunatarajia kuwafikisha mahakamani upelelezi ukikamilika.”
Aliongeza kuwa vijana hao walieleza kuna mtu aliwatuma ili wakaibe bunduki hiyo kwa ahadi ya kupewa zawadi ya Sh. milioni tatu.
Katika tukio lingine, watu wawili akiwamo mzee wa miaka 60, wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kutengeneza bunduki ya kienyeji aina ya Shortgun pamoja na kukutwa na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengenezea silaha hiyo.
Mpinga aliwataja ni Mzee Fadhili Mayenga (60) na Mashaka Samuel (38), wote wakazi wa Kijiji cha Kambikatoto Wilaya ya Chunya.
Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Machi Jumamosi mchana kufuatia msako mkali uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
Kwa mujibu wa Mpinga, baada ya kukamatwa walipekuliwa na kukutwa na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutengeneza silaha hiyo pamoja na risasi 25 za kienyeji ambazo hutumika kwenye silaha hiyo.
Alisema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani muda wowote upelelezi utakapokuwa umekamilika.
CHANZO: MPEKUZI HURU
Zaidi ya Vibanda 600 vimeungua katika Ajali ya moto Mbagala
Soko la Kampochea lililopo Mbagala Rangi Tatu jijini Dar es Salaam limeteketea kwa moto alfajiri ya leo Jumanne Machi 6, 2018 na kusababisha hasara kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.Imeelezwa moto huo ulianza kuteketeza mabanda ya soko hilo saa 12 alfajiri huku uongozi ukitaja kuwa chanzo ni hitilafu ya umeme.
Mwenyekiti wa soko hilo, Mohamedy Njiwa amesema limekuwa likikumbwa na hitilafu za mara kwa mara licha ya kuripoti kwa mamlaka husika.
"Wiki mbili zilizopita hapa kulikuwa na hitilafu ya umeme, ulikuwa unakuja na kukata. Tanesco walikuja kufanya ukaguzi wakaeleza kuwa kuna hitilafu kwenye transfoma,"amesema.
Amesema mabanda yote 673 yaliyokuwapo eneo hilo yameungua kwa moto na kwamba, hasara ni kubwa.
Mmoja wa wafanyabiashara sokoni hapo, Chacha Mwang'wene amesema hajafanikiwa kuokoa chochote zaidi ya taarifa zake za biashara.
Msemaji wa Zimamoto Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Peter Mwambene amesema jeshi hilo lilijitahidi kudhibiti moto huo, lakini tatizo kubwa ni aina ya bidhaa zilizokuwamo.
"Soko hili lina mali ambazo zinachangia kusambaza moto kwa kasi sana kama mitumba ambayo ni rahisi kuteketea kwa moto,"amesema.
Pia, amesisitiza kuwapo kwa vifaa vya awali vya kuzimia moto ili kunusuru mali kwenye masoko mengine jijini hapa.
Hatahivyo, wafanyabiashara hao wameeleza nia yao ya kuendelea kulitumia soko hilo licha ya agizo la mkuu wa Wilaya ya Temeke kuwataka kuhamia masoko mengine.
CHANZO: MPEKUZI HURU
MTWARA: BIASHARA KATI YA INDIA NA MTWARA KUENDELEA KUIMARIKA
Ushirikiano
wa Kibiashara kati ya Tanzania na India umeendelea kuimarika kutokana na
kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zinazouzwa na kununuliwa baina ya nchi hizo
mbili. Hayo yalisemwa na Mheshimiwa Sandeep Arya, Balozi wa India nchini
Tanzania wakati wa Kongamano la Kukuza Biashara kati ya India na Mtwara
lililofanyika jana Jumamosi tarehe 3 Machi, 2018 katika Ukumbi wa NAF Hotel
Apartment, Mjini Mtwara.
Balozi Sandeep alisema asilimia
24 ya mauzo ya bidhaa za Tanzania nchi za nje kwa mwaka 2017 ziliuzwa nchini
India. Mwaka 2017 Tanzania iliuza nchini India bidhaa zenye thamani ya Dola za
Kimarekani 977.5 ambapo ilinunua bidhaa mbalimbali kutoka nchini India zenye
thamani ya Dola za Kimarekani 1,165.
Alisema mauzo ya bidhaa za Tanzania zilizouzwa India mwaka 2017
yaliongezeka kwa wastani wa asilimia 38 ikinganishwa na mauzo ya mwaka 2016.
Hii ilitokana na
ongezeko la bidhaa zilizozalishwa nchini ambazo zilihitajika kwa wingi huko
India zikiwemo dhahabu, korosho n.k. Aidha, Balozi huyo alisema ili kuimarisha
biashara kati ya Tanzania na India, Serikali ya India imeondoa tozo za ushuru
kwa baadhi ya bidhaa zinazosafirishwa kutoka Tanzania kwenda India zikiwemo
korosho, mchele n.k na pia imefuta gharama za kibali cha kuingia India (Visa)
kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania na kubaki 7,000 tu.
Kongamano hilo liliandaliwa kwa ushirikiano baina ya Chama cha
Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Mtwara na Ubalozi wa India
nchini Tanzania.
Karim Faida – JAMII FM.











