Mwili wakutwa ukining’inia kwenye mkorosho Lindi

Omari Bakari Hidobelele (35), mkazi wa Madangwa, Lindi, amekutwa amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali. Polisi wamesema marehemu alikuwa na msongo wa mawazo. Familia imeshangazwa na tukio hilo, ikieleza kuwa hakuwa na matatizo yoyote. Polisi wamehimiza jamii kusaidia wenye changamoto za afya ya akili

Na Musa Mtepa

Mtu mmoja aliefahamika kwa jina Omari Bakari Hidobelele(35) mkazi wa Kijiji Cha madangwa kata ya Sudi halmashauri ya Mtama mkoani Lindi amekutwa amejinyonga hadi kufa kwa kutumia mkanda wa suruali yake.

Akitihibitisha tukio hilo Daktari wa Zahanati ya kijiji cha Mtegu Jackine Joseph Sita amesema kwa mujibu wa vipimo vilivyofanyika inonekana kuwa na alama zinazo thibitisha kujinyonga kupitia kifo chake .

Sauti ya Jackline Joseph Sita Daktari wa Zahanati ya Mtegu

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Bw. Salumu Hassani Kuku, kijana huyo alitoweka tangu saa tatu asubuhi ya Julai 21, 2025. Jitihada za kumtafuta zilianza mara moja bila mafanikio hadi siku iliyofuata, Jumanne ya Julai 22, ambapo alikutwa akiwa amejinyonga kwenye mti wa mkorosho majira ya saa mbili asubuhi.

Sauti ya Salumu Hassani Kuku Mwenyekiti wa kijiji cha Madangwa

Bibi wa marehemu, Bi. Fatuma Ahmadi Liyai, amesema familia imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hiyo, lakini wamelazimika kuikubali kama sehemu ya maisha.

Aidha, Bi. Fatuma amesema tangu Omari aliporejea kutoka Kilwa, hakuwa na matatizo yoyote wala migogoro na mtu yeyote, jambo linaloendelea kuwashangaza.

Sauti ya Bi Fatuma Liyai Bibi wa Marehemu

Kwa upande wake, Jeshi la Polisi mkoa wa Lindi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anapitia hali ya msongo wa mawazo kwa kipindi cha muda mrefu, jambo linalodhaniwa kuwa chanzo cha uamuzi huo wa kujiua.

Jeshi la Polisi pia limetoa wito kwa jamii kuhakikisha wanaimarisha usaidizi wa kisaikolojia kwa watu wanaoonesha dalili za msongo wa mawazo au matatizo ya afya ya akili, na kutoa taarifa mapema kwa wataalamu husika ili kusaidia kuzuia matukio ya aina hii.

Share:

No comments:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>