 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo  amepata ajali  baada ya gari lake kupasuka tairi na kupinduka
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo  amepata ajali  baada ya gari lake kupasuka tairi na kupindukaKamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha apata ajali
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo  amepata ajali  baada ya gari lake kupasuka tairi na kupinduka
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo  amepata ajali  baada ya gari lake kupasuka tairi na kupinduka
Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema ajali hiyo ilitokea kati ya eneo la Mdori na Minjingu wilayani Babati  jana  Februari 26  saa nane mchana.
Amesema Kamanda Mkumbo ambaye alikuwa anatoka mkoani Singida kurejea Arusha, ameumia kidole cha mkono wa kushoto na michubuko iliyotokana na kukatwa na vioo.
Amesema gari lilipata ajali baada ya kupasuka tairi la nyuma upande wa kushoto.
Ilembo amesema Mkumbo baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, aliingizwa chumba cha upasuaji moja kwa moja.
Pia, katika ajali hiyo dereva wa kamanda Mkumbo, Staff Sajent Silvanus aliumia maeneo ya paja.
Mganga mfawidhi wa Mkoa Arusha, Dk Omar Chande amesema  majeruhi wote wanapatiwa matibabu.
Hata hivyo, hakuwa tayari kuelezea hali za majeruhi hasa kwa maelezo kuwa uchunguzi wa kutabibu unaendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa pia wamefika  hospitali ya mkoa kumjulia hali Mkumbo na majeruhi wengine.
CHANZO: MPEKUZI
MTWARA: Waziri mkuu kuzuru MASASI, NANYUMBU, TANDAHIMBA, NANYAMBA, NA NEWALA
 Waziri MKuu wa Jamhuri ya
Muunganno wa Tanzania MHE KASSIM MAJALIWA anatarajia kufanya ziara ya kikazi Mkoani
Mtwara kwa muda wa siku Tatu yaani tarehe 26-28 februari, 2018.
Waziri MKuu wa Jamhuri ya
Muunganno wa Tanzania MHE KASSIM MAJALIWA anatarajia kufanya ziara ya kikazi Mkoani
Mtwara kwa muda wa siku Tatu yaani tarehe 26-28 februari, 2018.
MHE
MAJALIWA anatarajia kutembelea wilaya ya MASASI, NANYUMBU, TANDAHIMBA, NANYAMBA, NA
NEWALA. Akiwa katika ziara yake anatarajia kupokea taarifa za miradi mbalimbali
ya maendeleo, kuzindua jengo la wodi ya akina mama na watoto katika kituo cha
afya cha CHIWALE, Ujenzi wa chuo cha ualimu KITANGALI na chanzo vya Maji vya Makonde
na Mitema.
Ziara
hii ni mwendelezo wa ziara za kikazi ambapo baada ya kuhitimisha katika mkoa wa
MTWARA anatarajia kulekea mkoani LINDI
MASASI: WAUZA MKAA ZINGATIENI SHERIA
 Wafanyabiashara
wa mazao ya Misitu hasa Mkaa, Kuni na Mbao wilayani MASASI wametakiwa kufuata sheria
wakati wa kuvuna  mazao hayo kwa kupata
vibali vitakavyowawezesha kufanya biashara hiyo
Wafanyabiashara
wa mazao ya Misitu hasa Mkaa, Kuni na Mbao wilayani MASASI wametakiwa kufuata sheria
wakati wa kuvuna  mazao hayo kwa kupata
vibali vitakavyowawezesha kufanya biashara hiyo
Akizungumza na wananchi
wakati wa ziara ya kutoa elimu juu ya sheria zinazotakiwa kufuatwa, AFISA
MISITU MBWANA MILANZI amesema kuwa idara ya misitu inapita kutoa elimu juu ya
sheria na taratibu za kufanya biashara ya misitu kwa mara ya mwisho na baada ya
Elimu hii sheria itafuata mkondo wake.
MILLANZI  amefafanua kuwa "Sio
mara ya Kwanza kwa wakala wa misitu wilani Masasi kutoa elimu hii kwa wananchi,
hivyo watu wanafahamu ndio maana wakikutana na watu wa maliasili wanakimbia.
Hivyo kwa anayetaka kuendelea kufanya biashara ya misitu ni lazima afuate
sheria ili kulipa kodi ya serikali na kulinda misitu yetu ambayo ina faida kubwa
kwa maisha ya binadamu".
Kutokana na
changamoto hiyo Wakala wa Misitu Wilayani MASASI inawakumbusha wafanyabiashara
wote kutambua sheria na kanuni zilizowekwa na idara hiyo ili waweze kutambulika
lakini pia kuzuia uvunaji holela wa mazao Hayo hali inayopelekea uharibifu
mkubwa wa
misitu.
DAR ES SALAAM: TRA SASA UNAWEZA KULIPA KODI YA MAJENGO KIELEKTRONIKI
Akizungumza jijini
Dar es Salaam hivi karibuni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Charles Kichere alisema hakuna muda utakao ongezwa ifikapo Juni 30, mwaka huu
na badala yake faini itatozwa kwa kila mmiliki wa jengo atakayechelewa kulipa
kodi hiyo.
“Kama mamlaka hatuoni
sababu ya kuongeza muda wa kulipa Kodi ya Majengo ifikapo tarehe 30 Juni 2018
kwasababu tumewarahisishia wananchi ulipaji wa Kodi hii ambapo wanaweza kupata
ankara ya malipo kwa majengo yaliyosajiliwa kwenye tovuti ya TRA au simu ya
mkononi na kufanya malipo katika tawi lolote la Benki ya NMB au CRDB popote
nchini au kwa njia ya mitandao ya simu ya Mpesa, Tigopesa au Halopesa”, alisema
Kichere.
Kamishna Mkuu Kichere
alisema kuwa, wananchi wafuatilie matangazo ya namna ya kulipa Kodi ya Majengo
kwa njia ya kielektroniki katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo
mbalimbali vya habari au wafike katika ofisi za TRA zilizo karibu na maeneo yao
nchi nzima wapate utaratibu wa kulipa kodi hiyo kielektroniki.
Kichere aliongeza kuwa
Kodi ya Majengo inalipwa kwa mujibu wa Sheria hivyo, ni muhimu wananchi walipe
mapema kodi hiyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza mwishoni ikiwa ni
pamoja na msongamano wa watu.
“Natoa wito kwa
wananchi kwamba, wasisubiri mpaka mwisho ndio waanze kupanga foleni kwenye
ofisi za TRA, wanatakiwa kulipa kuanzia sasa hivi katika ofisi zetu na wanaweza
kulipa kwa kutumia njia ya kielektroniki kama nilivyoeleza hapo awali, kinyume
na hapo itatubidi tutoze faini kwa atakayechelewa kulipa kodi hii ya majengo,”
alisisitiza Kichere.
Kodi ya Majengo
hulipwa kuanzia mwezi Julai mosi ya mwaka wa fedha husika hadi Juni 30 ya mwaka
unaofuatia kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu,  hivyo, muda huu ni
muafaka kwa wananchi kuanza kulipia kodi ya majengo mpaka ifikapo tarehe 30
Juni, 2018.
IRINGA: Wahamiaji Haramu 83 Wakamatwa
 Zikiwa zimepita siku tatu tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam iwahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela wahamiaji haramu 77
kutoka Ethiopia, wengine 83 wamedakwa mkoani Iringa huku dereva aliyekuwa
akiwasafirisha akifanikiwa kutoroka.
Zikiwa zimepita siku tatu tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
jijini Dar es Salaam iwahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela wahamiaji haramu 77
kutoka Ethiopia, wengine 83 wamedakwa mkoani Iringa huku dereva aliyekuwa
akiwasafirisha akifanikiwa kutoroka.Wahamiaji hao walikamatwa wilayani Kilolo mkoani hapa wakiwa safarini kupelekwa Malawi kisha Afrika Kusini.
Hata hivyo katika harakati za kukamatwa kwao, dereva wa lori
mali ya mkazi wa Tukuyu mkoani Mbeya alitoroka.
Raia hao wa Ethiopia walikamatiwa katika Kijiji cha Mbigili
ambapo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Hope Kawawa
alisema walikamatwa juzi saa kumi na moja jioni karibu na bomba la mafuta la
Tazama.
Alisema wahamiaji hao walipelekwa kituo cha polisi cha Lugalo na
kwamba, kukamatwa kwao kunatokana na taarifa iliyofikishwa Uhamiaji na
wananchi.
Alisema maofisa wa Uhamiaji kwa kushirikiana na polisi
walipowakamata baadhi yao waliwakuta hali zao ni mbaya kutokana na kukosa
chakula kwa siku tatu na pia kuathiriwa na joto kutokana na bodi la lori
walilokuwa wakisafiria kuwa la bati. 
“Wahamiaji hawa walikuwa wanasafiri kwenye lori mali ya mkazi wa
Tukuyu mkoani Mbeya, dereva alikimbia na hajapatikana lakini uchunguzi
unaendelea,” alisema.
Aliongeza kuwa wahamiaji hao watafikishwa mahakamani kesho
kujibu mashtaka yanayowakabili.
“Naomba niwaambie madalali wanaosafirisha hawa wahamiaji kuwa
mkoa wa Iringa si mahala salama kuwapitisha kwa kuwa tuko makini saa 24 na
tukiwabaini hatua kali zitachukuliwa dhidi yao,” alisema.
Alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapohisi baadhi
ya watu si raia wa Tanzania na wanapowaona watu wasiowatambua. Mtanzania
aliyekamatwa akihusishwa na usafirishaji wa wahamiaji hao, Hassan Mwalusanjo
alisema hana anachofahamu.
Alisema aliomba lifti katika gari hilo kutoka Tukuyu kwenda Dar
es Salaam kununua vifaa vya gari wakati gari hilo lilipokuwa likisafirisha
ndizi. Mwalusajo alisema baada ya kushusha ndizi eneo la Mabibo jijini Dar es
Salaam, dereva aliondoka na aliporeja alipanda kurejea Tukuyu.
Alisema walipofika Ilula alishuka kula ndipo dereva alipoondoka
na gari na aliporejea alimuomba amsaidie kusafisha gari.
“Sielewi chochote nilishangaa kuwekwa chini ya ulinzi baada ya
dereva kuniambia nimsaidie kusafisha gari ambako nilikuta makopo ya maji na
mifuko ya mikate,” alisema akiwa chini ya ulinzi.’’
MBEYA: Hukumu ya Sugu Kusomwa Kesho February 26
Hatima ya mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi
maarufu Sugu anayeshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais
John Magufuli itajulikana kesho.
Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,
Emmanuel Masonga wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Mbeya ambayo kesho Februari 26,2018 itatoa hukumu.
Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini
Mbeya.
 Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite anatarajiwa kutoa hukumu
baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari
9,2018.
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite anatarajiwa kutoa hukumu
baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari
9,2018.
Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha
sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.
Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na
Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.
Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface
Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa na sasa wanawakilishwa na Peter
Kibatala.
Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga  walifikishwa
mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph
Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na
usikilizaji.
DAR WS SALAAM: Kakobe akana kukwepa kodi,asema taarifa za TRA ni za Kisiasa
 Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Followship (FGBF), Zachary Kakobe amekanusha taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba kanisa lake linakwepa kodi.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Followship (FGBF), Zachary Kakobe amekanusha taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba kanisa lake linakwepa kodi.
Akizungumza leo Jumapili Februari 25, 2015 katika kanisa hilo lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam Kakobe amewataka waumini wa kanisa hilo kuzikataa taarifa hizo na kwamba zimejaa siasa,ni za kishilawadu
Kakobe ametoa ufafanuzi huo zikiwa zimepita siku nne tangu TRA kutoa taarifa ya uchunguzi katika kanisa hilo na kubaini mambo saba.
RUKWA: Polisi wamtia mbaroni Mama anayetuhumiwa kumuua Mwanae na kumzika
 Msichana mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata
ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na
polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.
Msichana mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata
ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na
polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.
Wananchi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza
kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya
kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kumuweka kwenye
kikapu alichokificha chini ya uvungu wa kitanda chake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha
kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha
Kipundu kilichopo mjini Namanyere.
Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi
wilaya Nkasi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio
kukamilika. Wakizungumza baadhi ya wanawake  wamedai mtoto huyo alizikwa
juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi
anaishi na bibi yake.
DAR ES SALAAM: NAIBU WAZIRI NISHATI AWAAHIDI UMEME WA UHAKIKA WAKAZI WA MITAA MBALIMBALI KWENYE KATA NNE ZA UKONGA
Mhe. Mgalu ametoa ahadi hiyo
mapema siku ya jana Jumamosi Februari 24, 2018 alipofanya ziara katika jimbo
hilo ambapo alifanya mikutano Zaidi ya sita kwenye maeneo tofauti tofauti
ambayo hayana miundombinu ya umeme.
Maeneo ambayo Mhe. Mgalu
alitembelea ni pamoja na: mtaa wa Bombambili  kwenye kata ya Kivule, mtaa
wa Mbondole, Luhanga na Kiboga kwenye kata ya Msongola, mtaa wa  Zogowale
kwenye kata ya Zingiziwa, mtaa wa Yongwe na Virobo kwenye kata ya Chanika, na
kata ya Buyuni .
Wananchi wengi wakiongozwa na
mbunge wa jimbo hilo Mhe. Mwita Waitara (CHADEMA), madiwani na wenyeviti wa
mitaa mbalimbali, walijitokeza katika mikutano hiyo ambapo walimweleza Mhe.
Mgalu kilio chao cha kutokuwepo na umeme katika maeneo hayo pamoja na maeneo
yenye huduma za jamii mfano, shule za msingi na sekondari, zahanati, na visima
vya maji.
Aidha wananchi hao pia
walimweleza Mhe. Mgalu kuhusu kuwepo kwa matukio yanayohatarisha hali ya ulinzi
na usalama kutokana na maeneo hayo kutawaliwa na giza nyakati za usiku.
Katika kujibu hoja hizo za
wananchi pamoja na Mhe. mbunge Waitara, Mhe. Mgalu aliwaeleza kuwa 
serikali ya awamu ya tano baada ya kuona changamoto ni kubwa maeneo hayo
imepanga  kupeleka  miundombinu ya umeme kupitia wakala wa umeme
vijijini REA chini ya mradi wa Peri Urban ambapo tenda ya mradi huu
imeshatangazwa na tathimin imeshafanyika na REA ipo katika hatua za
mwisho  za kumpata mkandarasi wa kutekeleza mradi huo.
Katika mikutano hiyo Mhe.
Mgalu pia amekemea uwepo wa vishoka wanaochangisha wananchi fedha kwa ajili ya
kulipia nguzo jambo ambalo amesema ni kinyume kabisa na utaratibu unaotumika
katika kuwaunganishia umeme wananchi.
Aidha Mhe. Mgalu aliwaasa wananchi
kutorubuniwa na kikundi au mtu binafsi kwa ajili ya kuchangia mradi huo na
kwamba gharama ya kuunganisha umeme kupitia miradi ya REA ni Tshs. 27,000 tu na
si  vinginevyo.
Kwa upande wake mbunge wa
jimbo hilo Mhe. Waitara akiongea kwa niaba ya wananchi ameishukuru serikali ya
awamu ya tano kwa kusikia kilio cha wananchi wa maeneo hayo na kubuni mradi
utakaowapelekea umeme katika maeneo yao.
Aidha Mhe. Waitara aliwataka
wananchi hao kutoa ushirikiano wa kutosha pindi mradi utakapoanza kutekelezwa
huku akiwaomba kushirikiana na vyombo vya usalama katika kuwabaini mafundi
vishoka ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Katika ziara yake hiyo Mhe.
naibu waziri aliambatana na wataalamu kutoka TANESCO mkoa wa Pwani, wilaya ya
Ilala na Kisarawe, REA, wizara ya nishati, na wanahabari.
ARUSHA: PROF. NDALICHAKO ATANGAZA KIAMA KWA WATUMISHI WA UMMA, AKERWA NA UPIKAJI ALAMA VYUO VIKUU
Prof. Ndalichako ameyasema
hayo leo jijini Arusha alipotembelea katikia Chuo Kikuu cha Mount Meru ili
kujionea miundombinu na namna wanavyosimamia suala la utoaji elimu ya juu
chuoni hapo.
Akiwa chuoni hapo, Prof.
Ndalichako ameonesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watumishi wa umma kuwa na
ajira mbili kwa wakati mmoja, wakifanya serikalini na kwenye taasisi binafsi
kwa mkataba kamili (full time) na hivyo kuwataka kuacha kufanya ivyo mara moja.
Kauli hiyo ya Ndalichako
inafuatia kugundua kuwa baadhi ya wafanyakazi katika chuo hicho ni waajiriwa wa
serikali na hivyo kupokea mishahara miwili kwa wakati mmoja, yaani ule wa
serikali na wa taasisi binafsi.
“Kanuni za utumishi, kifungu cha F cha
namba 4 na 7, kinazuia mtumishi wa umma kuwa na ajira mbili, na mtumishi wa
umma akiwa na ajira mbili, automatically anapoteza ajira yake kwenye utumishi
wa umma” amesema
waziri Ndalichako
Katika htua nyingine waziri Ndalichako
ameonesha kukerwa na upikaji wa alama unaofanywa na baadhi ya wahadhiri
wasiokuwa waaminifu, na wazalendo kwa taifa, na hivyo kuwataka kuacha kufanya
vitendo vya namna hiyo mara moja iwezekanavyo.
“Suala la kupika alama za wanafunzi, ni
suala ambalo Tanzania hatujafika hapa” amesema Prof. Ndalichako.
Prof. Ndalichako amehitimisha
ziara yake chuoni hapo kwa kuutaka uongozi wa chuo kuwaondoa wahadhiri wote
wasio na sifa za kufundisha chuoni hapo.










