• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha apata ajali

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo  amepata ajali  baada ya gari lake kupasuka tairi na kupinduka

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amesema ajali hiyo ilitokea kati ya eneo la Mdori na Minjingu wilayani Babati  jana  Februari 26  saa nane mchana.

Amesema Kamanda Mkumbo ambaye alikuwa anatoka mkoani Singida kurejea Arusha, ameumia kidole cha mkono wa kushoto na michubuko iliyotokana na kukatwa na vioo.

Amesema gari lilipata ajali baada ya kupasuka tairi la nyuma upande wa kushoto.

Ilembo amesema Mkumbo baada ya kufikishwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, aliingizwa chumba cha upasuaji moja kwa moja.

Pia, katika ajali hiyo dereva wa kamanda Mkumbo, Staff Sajent Silvanus aliumia maeneo ya paja.

Mganga mfawidhi wa Mkoa Arusha, Dk Omar Chande amesema  majeruhi wote wanapatiwa matibabu.

Hata hivyo, hakuwa tayari kuelezea hali za majeruhi hasa kwa maelezo kuwa uchunguzi wa kutabibu unaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa pia wamefika  hospitali ya mkoa kumjulia hali Mkumbo na majeruhi wengine.
CHANZO: MPEKUZI
Share:

MTWARA: Waziri mkuu kuzuru MASASI, NANYUMBU, TANDAHIMBA, NANYAMBA, NA NEWALA


Waziri MKuu wa Jamhuri ya Muunganno wa Tanzania MHE KASSIM MAJALIWA anatarajia kufanya ziara ya kikazi Mkoani Mtwara kwa muda wa siku Tatu yaani tarehe 26-28 februari, 2018.
MHE MAJALIWA anatarajia kutembelea wilaya ya MASASI, NANYUMBU, TANDAHIMBA, NANYAMBA, NA NEWALA. Akiwa katika ziara yake anatarajia kupokea taarifa za miradi mbalimbali ya maendeleo, kuzindua jengo la wodi ya akina mama na watoto katika kituo cha afya cha CHIWALE, Ujenzi wa chuo cha ualimu KITANGALI na chanzo vya Maji vya Makonde na Mitema.
Ziara hii ni mwendelezo wa ziara za kikazi ambapo baada ya kuhitimisha katika mkoa wa MTWARA anatarajia kulekea mkoani LINDI



Share:

MASASI: WAUZA MKAA ZINGATIENI SHERIA

Wafanyabiashara wa mazao ya Misitu hasa Mkaa, Kuni na Mbao wilayani MASASI wametakiwa kufuata sheria wakati wa kuvuna  mazao hayo kwa kupata vibali vitakavyowawezesha kufanya biashara hiyo

Akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya kutoa elimu juu ya sheria zinazotakiwa kufuatwa, AFISA MISITU MBWANA MILANZI amesema kuwa idara ya misitu inapita kutoa elimu juu ya sheria na taratibu za kufanya biashara ya misitu kwa mara ya mwisho na baada ya Elimu hii sheria itafuata mkondo wake.

MILLANZI  amefafanua kuwa "Sio mara ya Kwanza kwa wakala wa misitu wilani Masasi kutoa elimu hii kwa wananchi, hivyo watu wanafahamu ndio maana wakikutana na watu wa maliasili wanakimbia. Hivyo kwa anayetaka kuendelea kufanya biashara ya misitu ni lazima afuate sheria ili kulipa kodi ya serikali na kulinda misitu yetu ambayo ina faida kubwa kwa maisha ya binadamu".


Kutokana na changamoto hiyo Wakala wa Misitu Wilayani MASASI inawakumbusha wafanyabiashara wote kutambua sheria na kanuni zilizowekwa na idara hiyo ili waweze kutambulika lakini pia kuzuia uvunaji holela wa mazao Hayo hali inayopelekea uharibifu mkubwa wa misitu.
Share:

DAR ES SALAAM: TRA SASA UNAWEZA KULIPA KODI YA MAJENGO KIELEKTRONIKI

TRWito umetolewa kwa wananchi wote kuanza kulipa Kodi ya Majengo ya mwaka 2017/18 mapema kwa kuwa ulipaji wa kodi hiyo umerahisishwa  ambapo wanaweza kulipa kwa kutumia njia ya kielektroniki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere alisema hakuna muda utakao ongezwa ifikapo Juni 30, mwaka huu na badala yake faini itatozwa kwa kila mmiliki wa jengo atakayechelewa kulipa kodi hiyo.

“Kama mamlaka hatuoni sababu ya kuongeza muda wa kulipa Kodi ya Majengo ifikapo tarehe 30 Juni 2018 kwasababu tumewarahisishia wananchi ulipaji wa Kodi hii ambapo wanaweza kupata ankara ya malipo kwa majengo yaliyosajiliwa kwenye tovuti ya TRA au simu ya mkononi na kufanya malipo katika tawi lolote la Benki ya NMB au CRDB popote nchini au kwa njia ya mitandao ya simu ya Mpesa, Tigopesa au Halopesa”, alisema Kichere.

Kamishna Mkuu Kichere alisema kuwa, wananchi wafuatilie matangazo ya namna ya kulipa Kodi ya Majengo kwa njia ya kielektroniki katika mitandao ya kijamii na kwenye vyombo mbalimbali vya habari au wafike katika ofisi za TRA zilizo karibu na maeneo yao nchi nzima wapate utaratibu wa kulipa kodi hiyo kielektroniki.

Kichere aliongeza kuwa Kodi ya Majengo inalipwa kwa mujibu wa Sheria hivyo, ni muhimu wananchi walipe mapema kodi hiyo ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza mwishoni ikiwa ni pamoja na msongamano wa watu.

“Natoa wito kwa wananchi kwamba, wasisubiri mpaka mwisho ndio waanze kupanga foleni kwenye ofisi za TRA, wanatakiwa kulipa kuanzia sasa hivi katika ofisi zetu na wanaweza kulipa kwa kutumia njia ya kielektroniki kama nilivyoeleza hapo awali, kinyume na hapo itatubidi tutoze faini kwa atakayechelewa kulipa kodi hii ya majengo,” alisisitiza Kichere.

Kodi ya Majengo hulipwa kuanzia mwezi Julai mosi ya mwaka wa fedha husika hadi Juni 30 ya mwaka unaofuatia kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu,  hivyo, muda huu ni muafaka kwa wananchi kuanza kulipia kodi ya majengo mpaka ifikapo tarehe 30 Juni, 2018.


Share:

IRINGA: Wahamiaji Haramu 83 Wakamatwa

Zikiwa zimepita siku tatu tangu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam iwahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela wahamiaji haramu 77 kutoka Ethiopia, wengine 83 wamedakwa mkoani Iringa huku dereva aliyekuwa akiwasafirisha akifanikiwa kutoroka.


Wahamiaji hao walikamatwa wilayani Kilolo mkoani hapa wakiwa safarini kupelekwa Malawi kisha Afrika Kusini.


Hata hivyo katika harakati za kukamatwa kwao, dereva wa lori mali ya mkazi wa Tukuyu mkoani Mbeya alitoroka.


Raia hao wa Ethiopia walikamatiwa katika Kijiji cha Mbigili ambapo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, Hope Kawawa alisema walikamatwa juzi saa kumi na moja jioni karibu na bomba la mafuta la Tazama.


Alisema wahamiaji hao walipelekwa kituo cha polisi cha Lugalo na kwamba, kukamatwa kwao kunatokana na taarifa iliyofikishwa Uhamiaji na wananchi.


Alisema maofisa wa Uhamiaji kwa kushirikiana na polisi walipowakamata baadhi yao waliwakuta hali zao ni mbaya kutokana na kukosa chakula kwa siku tatu na pia kuathiriwa na joto kutokana na bodi la lori walilokuwa wakisafiria kuwa la bati. 

“Wahamiaji hawa walikuwa wanasafiri kwenye lori mali ya mkazi wa Tukuyu mkoani Mbeya, dereva alikimbia na hajapatikana lakini uchunguzi unaendelea,” alisema.


Aliongeza kuwa wahamiaji hao watafikishwa mahakamani kesho kujibu mashtaka yanayowakabili.


“Naomba niwaambie madalali wanaosafirisha hawa wahamiaji kuwa mkoa wa Iringa si mahala salama kuwapitisha kwa kuwa tuko makini saa 24 na tukiwabaini hatua kali zitachukuliwa dhidi yao,” alisema.


Alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa pindi wanapohisi baadhi ya watu si raia wa Tanzania na wanapowaona watu wasiowatambua. Mtanzania aliyekamatwa akihusishwa na usafirishaji wa wahamiaji hao, Hassan Mwalusanjo alisema hana anachofahamu.


Alisema aliomba lifti katika gari hilo kutoka Tukuyu kwenda Dar es Salaam kununua vifaa vya gari wakati gari hilo lilipokuwa likisafirisha ndizi. Mwalusajo alisema baada ya kushusha ndizi eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, dereva aliondoka na aliporeja alipanda kurejea Tukuyu.


Alisema walipofika Ilula alishuka kula ndipo dereva alipoondoka na gari na aliporejea alimuomba amsaidie kusafisha gari.


“Sielewi chochote nilishangaa kuwekwa chini ya ulinzi baada ya dereva kuniambia nimsaidie kusafisha gari ambako nilikuta makopo ya maji na mifuko ya mikate,” alisema akiwa chini ya ulinzi.’’


Share:

MBEYA: Hukumu ya Sugu Kusomwa Kesho February 26

Hatima ya mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu anayeshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli itajulikana kesho.


Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wanakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya ambayo kesho Februari 26,2018 itatoa hukumu.


Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.


Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite anatarajiwa kutoa hukumu baada ya upande wa mashtaka na ule wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari 9,2018.


Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.


Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno wanayoshtakiwa kuyatoa.


Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa na sasa wanawakilishwa na Peter Kibatala.


Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga  walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.


Share:

DAR WS SALAAM: Kakobe akana kukwepa kodi,asema taarifa za TRA ni za Kisiasa

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Followship (FGBF), Zachary Kakobe amekanusha taarifa za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwamba kanisa lake linakwepa kodi.

Akizungumza leo Jumapili Februari 25, 2015 katika kanisa hilo lililopo Mwenge, jijini Dar es Salaam Kakobe amewataka waumini wa kanisa hilo kuzikataa taarifa hizo na kwamba zimejaa siasa,ni za kishilawadu

Kakobe ametoa ufafanuzi huo zikiwa zimepita siku nne tangu TRA kutoa taarifa ya uchunguzi katika kanisa hilo na kubaini mambo saba.
Share:

RUKWA: Polisi wamtia mbaroni Mama anayetuhumiwa kumuua Mwanae na kumzika

Msichana mwenye umri wa miaka 25, Anastazia Elias, mkazi wa Kata ya Kipindu wilayani Nkasi mkoani Rukwa, amenusurika kifo baada ya kuokolewa na polisi akituhumiwa kumuua mtoto wake baada ya kujifungua.

Wananchi wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mawe walianza kumshambulia mwanamke huyo wakimtuhumu kumuua mwanawe wa kiume baada ya kujifungua ambapo alimviringisha na vipande vya khanga na kumuweka kwenye kikapu alichokificha chini ya uvungu wa kitanda chake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa nane mchana katika Kijiji cha Kipundu kilichopo mjini Namanyere.

Kamanda Kyando amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na Polisi wilaya Nkasi na kwamba atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi wa tukio kukamilika. Wakizungumza baadhi ya wanawake  wamedai mtoto huyo alizikwa juzi usiku katika kaburi lililochimbwa ndani ya nyumba ambayo mama yake mzazi anaishi na bibi yake.


Share:

DAR ES SALAAM: NAIBU WAZIRI NISHATI AWAAHIDI UMEME WA UHAKIKA WAKAZI WA MITAA MBALIMBALI KWENYE KATA NNE ZA UKONGA

Naibu waziri wa nishati Mhe. Subira Mgalu amewaahidi umeme wa uhakika wakazi wa mitaa mbalimbali kwenye kata nne zilizopo katika jimbo la Ukonga mkoani Dar es Salaam.
Mhe. Mgalu ametoa ahadi hiyo mapema siku ya jana Jumamosi Februari 24, 2018 alipofanya ziara katika jimbo hilo ambapo alifanya mikutano Zaidi ya sita kwenye maeneo tofauti tofauti ambayo hayana miundombinu ya umeme.
Maeneo ambayo Mhe. Mgalu alitembelea ni pamoja na: mtaa wa Bombambili  kwenye kata ya Kivule, mtaa wa Mbondole, Luhanga na Kiboga kwenye kata ya Msongola, mtaa wa  Zogowale kwenye kata ya Zingiziwa, mtaa wa Yongwe na Virobo kwenye kata ya Chanika, na kata ya Buyuni .
Wananchi wengi wakiongozwa na mbunge wa jimbo hilo Mhe. Mwita Waitara (CHADEMA), madiwani na wenyeviti wa mitaa mbalimbali, walijitokeza katika mikutano hiyo ambapo walimweleza Mhe. Mgalu kilio chao cha kutokuwepo na umeme katika maeneo hayo pamoja na maeneo yenye huduma za jamii mfano, shule za msingi na sekondari, zahanati, na visima vya maji.
Aidha wananchi hao pia walimweleza Mhe. Mgalu kuhusu kuwepo kwa matukio yanayohatarisha hali ya ulinzi na usalama kutokana na maeneo hayo kutawaliwa na giza nyakati za usiku.
Katika kujibu hoja hizo za wananchi pamoja na Mhe. mbunge Waitara, Mhe. Mgalu aliwaeleza kuwa  serikali ya awamu ya tano baada ya kuona changamoto ni kubwa maeneo hayo imepanga  kupeleka  miundombinu ya umeme kupitia wakala wa umeme vijijini REA chini ya mradi wa Peri Urban ambapo tenda ya mradi huu imeshatangazwa na tathimin imeshafanyika na REA ipo katika hatua za mwisho  za kumpata mkandarasi wa kutekeleza mradi huo.
Katika mikutano hiyo Mhe. Mgalu pia amekemea uwepo wa vishoka wanaochangisha wananchi fedha kwa ajili ya kulipia nguzo jambo ambalo amesema ni kinyume kabisa na utaratibu unaotumika katika kuwaunganishia umeme wananchi.
Aidha Mhe. Mgalu aliwaasa wananchi kutorubuniwa na kikundi au mtu binafsi kwa ajili ya kuchangia mradi huo na kwamba gharama ya kuunganisha umeme kupitia miradi ya REA ni Tshs. 27,000 tu na si  vinginevyo.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo hilo Mhe. Waitara akiongea kwa niaba ya wananchi ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kusikia kilio cha wananchi wa maeneo hayo na kubuni mradi utakaowapelekea umeme katika maeneo yao.
Aidha Mhe. Waitara aliwataka wananchi hao kutoa ushirikiano wa kutosha pindi mradi utakapoanza kutekelezwa huku akiwaomba kushirikiana na vyombo vya usalama katika kuwabaini mafundi vishoka ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Katika ziara yake hiyo Mhe. naibu waziri aliambatana na wataalamu kutoka TANESCO mkoa wa Pwani, wilaya ya Ilala na Kisarawe, REA, wizara ya nishati, na wanahabari.


Share:

ARUSHA: PROF. NDALICHAKO ATANGAZA KIAMA KWA WATUMISHI WA UMMA, AKERWA NA UPIKAJI ALAMA VYUO VIKUU

Mapema siku ya leo Jumapili Februari 25, 2018, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.  Joyce Ndalichako amewashukia watumishi wa umma wenye ajira mbili na kuwataka kujiuzulu moja ya ajira kati ya hizo mbili, na kubakia na ajira moja pekee.
Prof. Ndalichako ameyasema hayo leo jijini Arusha alipotembelea katikia Chuo Kikuu cha Mount Meru ili kujionea miundombinu na namna wanavyosimamia suala la utoaji elimu ya juu chuoni hapo.
Akiwa chuoni hapo, Prof. Ndalichako ameonesha kusikitishwa kwake na baadhi ya watumishi wa umma kuwa na ajira mbili kwa wakati mmoja, wakifanya serikalini na kwenye taasisi binafsi kwa mkataba kamili (full time) na hivyo kuwataka kuacha kufanya ivyo mara moja.
Kauli hiyo ya Ndalichako inafuatia kugundua kuwa baadhi ya wafanyakazi katika chuo hicho ni waajiriwa wa serikali na hivyo kupokea mishahara miwili kwa wakati mmoja, yaani ule wa serikali na wa taasisi binafsi.
“Kanuni za utumishi, kifungu cha F cha namba 4 na 7, kinazuia mtumishi wa umma kuwa na ajira mbili, na mtumishi wa umma akiwa na ajira mbili, automatically anapoteza ajira yake kwenye utumishi wa umma” amesema waziri Ndalichako
Katika htua nyingine waziri Ndalichako ameonesha kukerwa na upikaji wa alama unaofanywa na baadhi ya wahadhiri wasiokuwa waaminifu, na wazalendo kwa taifa, na hivyo kuwataka kuacha kufanya vitendo vya namna hiyo mara moja iwezekanavyo.
“Suala la kupika alama za wanafunzi, ni suala ambalo Tanzania hatujafika hapa” amesema Prof. Ndalichako.
Prof. Ndalichako amehitimisha ziara yake chuoni hapo kwa kuutaka uongozi wa chuo kuwaondoa wahadhiri wote wasio na sifa za kufundisha chuoni hapo.


Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>