
Malawi Yaonesha Nia Kupata Gesi Kutoka Tanzania

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na Ujumbe wa Mawaziri wawili kutoka Malawi na kuzungumza kuhusu uwezekano wa Malawi kupata Gesi Asilia kutoka Tanzania na Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji umeme.
Ujumbe wa Malawi uliongozwa na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa ambao waliambatana na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara zao.
Waziri Kalemani alikutana na ujumbe huo Februari 12, 2018 katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam ambapo alielezwa dhumuni la ziara hiyo ya Mawaziri hao wawili kutoka nchini Malawi.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Nishati wa Malawi, Aggrey Masi alisema kuwa Malawi inaupungufu mkubwa wa nishati ya umeme na kwamba jitihada mbalimbali zinafanyika kuhakikisha kiwango cha uzalishaji umeme kinaongezeka.
Alisema umeme unaozalishwa nchini humo kwa sasa ni Megawati 140 pekee huku idadi ya watu ikiwa ni milioni 17 kiasi ambacho alisema kimeshindwa kukidhi mahitaji.
“Sasa hivi tumebaki na megawati 140 peke yake, hali siyo shwari; suluhisho la haraka linahitajika ili kuweka mambo sawa. Imani yetu ni kwa Tanzania kutazama namna ya kusaidia katika hili,” alisema.
Alibainisha kwamba chanzo kikuuu cha uzalishaji wa umeme nchini humo ni maporomoko ya maji na kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi, chanzo hicho kimeshindwa kuzalisha umeme wa kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku.
Aliongeza kwamba Serikali ya Malawi imeamua kuwa na vyanzo mbadala vya kuzalishia umeme ikiwemo Gesi Asilia hata hivyo alisema hakuna Gesi Asilia inayozalishwa nchini humo na kwamba matarajio yao ni kupata Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.
“Tumefarijika, tumepokelewa vizuri, lengo la ujio wetu ni kubaini uwezekano wa kupata Gesi Asilia kwa ajili ya kuzalisha umeme,” alisema Masi.
Alisema kwamba baada ya tathmini waliyoifanya wamebaini kwamba chanzo cha haraka kinachoweza kuwasaidia kuvuka kwenye upungufu mkubwa wa umeme uliyoikumba nchi hiyo kwa sasa ni Gesi Asilia kutoka nchini Tanzania.
Aliongeza kuwa tayari mwekezaji amepatikana ambaye atazalisha umeme kwa kutumia Gesi Asilia na kwamba atajenga mitambo yake kwenye eneo la Kalonga mpakani mwa Tanzania na Malawi.
Kwa upande wake Waziri Kalemani alisema suala hilo linaweza kujadiliwa baada ya wataalam wa Tanzania kujiridhisha uwezekano wake.
“Tupo tayari kushirikiana, kinachohitajika hapa ni majadiliano ya kitaalam na wataalam wetu waliopo hapa ili kuelewa mwelekeo,” alisema Waziri Kalemani.
Dkt. Kalemani aliwasisitiza wataalam hao kabla hawajafanya majadiliano wanapaswa kuelewa mambo makuu matatu ambayo wingi wa Gesi Asilia iliyopo kwa sasa, matakwa ya Sera ya Nishati na namna ambavyo Gesi hiyo inaweza kusafirishwa hadi huko Kalonga.
“Je tunayo gesi ya kutosha kugawana ama ni ya kutosha kwa matumizi yetu tu? Je Sera inaruhusu suala hilo? Na kama masuala hayo yanakubalika, Je ni vipi tutaifikisha hiyo Gesi huko mpakani?” alihoji Dkt. Kalemani.
Aliueleza ujumbe huo kuandaa mpango wa ombi lao kimaandishi pamoja na kuandika ombi rasmi na kuwasilisha katika utaratibu maalum wa Kiserikali ili majadiliano yafanyike.
Aidha, suala la Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe, Mawaziri hao kwa pamoja walikubaliana kupitia taarifa ya Tume ya Uendelezaji wa Bonde hilo ambayo inaundwa na nchi hizo mbili ili kubaini hatua za kuchukua kwenye kipengele cha kuzalisha umeme.
Miradi inayotarajiwa kutekelezwa katika bonde hilo ni pamoja na ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 180 ambazo zitagawanya sawa kwa nchi hizo, kilimo cha umwagiliaji, (hekta 6,200) usambazaji wa maji kwa wananchi, ujenzi wa miundombinu ya jamii (bararabara, shule, na vituo vya afya).
Miradi mingine ni uanzishaji wa viwanda vidogo na vya kati, uvuvi, utalii na uboreshaji wa mazingira, hususan kuimarisha kingo za mto ambao ni mpaka wa Tanzania na Malawi
REDIO ZATAKIWA KUWA TARISHI WA MAENDELEO
Wafanyakazi wa taasisi za redio wamekumbushwa wajibu wao kama ilivyo chombo chochote cha habari kuwa matarishi wa amani, upendo, mshikamano na kuhuisha maendeleo.
Aidha wameambiwa kwamba kwa kuwa Redio ina nguvu kuliko chombo chochote kingine duniani kwa kuwafikia watu wengi zaidi hivyo basi wanatakiwa kuwa makini wanapowafikishia wananchi taarifa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Juliana Shonza katika maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika Dodoma ambaye alitaka taarifa kwa wananchi kufikishwa bila ushabiki, chuki au kupiga chuku (kuongeza chumvi).
Alisema tasnia ya uandishi wa Habari ni tasinia adhimu sana, hivyo Waandishi wote wa Habari wanalo jukumu kubwa la kuzingatia misingi ya uandishi ambayo ni mizania (balancing), kutofungamana na upande wowote (impartiality), kutenda haki (fairness), Utu (humanity), na mwisho kabisa kuzingatia ukweli (truthness).
Siku ya Redio Duniani huadhimishwa kila mwaka duniani kote Tarehe 13 mwezi Februari ili kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Redio mahali pote duniani.
Aliwakumbusha waandishi na wageni historia ngumu na mbaya ya namna redio zilivyotumika vibaya katika baadhi ya nchi duniani na kuleta machafuko hadi umwagaji damu.
“Hivyo niwaase tena kutumia redio hizo na vipaza sauti kwa ajili ya kutoa taarifa muhimu juu ya masuala ya kilimo na ufugaji, majanga mbalimbali, elimu juu ya sera na sheria mbalimbali za nchi, masuala ya afya kwa jamii na elimu. Na kwa kufanya hivyo tu, ndipo tutakuwa tumeitendea haki tasnia hii.” alisema Dk. Shonza.
Aidha alipongeza kauli mbiu ya mwaka huu Redio na Michezo na kutoa rai kwa waandishi wote wa habari kudumisha mila na desturi za Kitanzania na kuongea Kiswahili fasaha bila kuchanganya na lugha zingine kama Kiingereza maarufu kama Kiswanglish.
Aidha Waziri Mwakyembe alishukuru Shirika la UNESCO na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) kwa kuwezesha siku ya redio na kusema atatafakari hoja zote zilizowasilsihwa kwake.
Naye Katibu wa Mtadao wa Radio Jamii (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa niaba ya Mwenyekiti wa mtandao huo, Prosper Kwigize alitaka serikali kuhakikisha kwamba urasimu unaondolewa kwenye utoaji wa taarifa kwa umma ili kuwezesha kufanyika kwa vipindi mbalimbali vya habari.
Alitaka Tamisemi kuweka utaratibu wa utoaji habari katika mfumo rahisi ili wananchi wafahamu kinachotekelezwa na serikali yao. Aidha maafisa habari walioajiriwa wapewe mamlaka na wawezeshwe kufahamu kinachofanywa na serikali na wawe na ruhusa ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari katika maeneo yao.
Aidha alisema kutokana kutokuwa na vyanzo vya mapato ya uhakika serikali ingeangalia suala la kodi na ushuru mbalimbali ili kusaidia Redio za Jamii kutolipia huduma za Radio.
Pia amesema sheria zilizopo ukilinganisha na mazingira halisi ya kazi ya mwanahabari, mfano sheria ya Takwimu, sheria ya huduma za habari, sheria ya makosa ya mtandao kumeshabibisha tasnia ya habari na utangazaji kuwa katika mashaka zaidi kuliko kipindi kilichopita.
Pia ameitaka Serikali kutoa Ruzuku ya elimu au mafunzo ya kitaaluma kwa wanahabari ili kuwawezesha kukidhi vigezo vya kisheria ifikapo 2021
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo amewataka waandishi na watangazaji kutumia redio kwa manufaa ya taifa kuleta mshikamano na pia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Aidha alikumbusha historia ya redio na kazi iliyofanya duniani na kusema kwamba umuhimu wa radio upo wazi na kutaka wahusika kuzitumia kwa manufaa ya umma unaowazunguka.
Naye Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Dk Moshi Kimizi, alitaka serikali na vyombo vya habari kushirikiana katika kuhimiza michezo kwa kuwa ndicho kinachowaleta wananchi pamoja.
Alisema anadhani redio na serikali vitaona njia bora ya kutangaza michezo kwa manufaa ya taifa.
Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Mh. Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesema Unesco inafanya kazi nzuri sana kwa kuwekeza kwenye vyombo vya Habari na kuvitaka vyombo hivyo kuitangaza Dodoma na fursa zake kwa sababu ndio makao makuu ya nchi.
Aidha aliitaka Redio kutangaza fursa zote ambazo zipo Dodoma ili wafanyakazi na wafanyabiashara wanaohamia Dodoma kujua wanapata wapi mahitaji yao yakiwemo Makazi, Maji, Chakula, Elimu na kadhalika.
Alitaka vyombo hivyo kuvutia wawekezaji ili mji huo uwe kweli katika karne ya 21 na makao makuu ya nchi.
Mtangazaji Mkongwe wa Habari za Michezo nchini, Abdallah Majura amesema pamoja na kwamba waandishi wanatangaza vipindi vya michezo lakini maudhui hayakidhi na kuvutia vile inavyostahili akitoa mfano hai wakati akichangia kwa nini waandishi wengi hawaandiki habari za michezo. Majura amesema yeye mwenyewe amewahi kupata #tuzo mbili kwa ajili ya vipindi vya michezo.
Wizara ya Maji Yaanza Kutekeleza Agizo la JPM Kwa Kasi.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe akionesha namna miundo mbinu ya maji itakavyojengwa kutoka katika mitambo ya maji ya Mailimbili, mjini Dodoma hadi eneo la Ihumwa utakapoojengwa mji wa Serikali
Wizara
ya Maji na Umwagiliaji yaanza kutekeleza Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli
la kufikisha huduma ya maji katika eneo linalojengwa mji wa Serikali, Ihumwa
Mjini Dodoma kwa kuanza kuchimba visima virefu vyenye uwezo wa kuzalisha mita
za ukubwa 600 kwa siku.
Akizungumza
wakati wa Ziara yakukagua maendeleo yautekelezaji wa Agizo hilo Waziri wa Maji
na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa maji mengine yatachukuliwa
kutoka katika matenki ya Maili mbili ambapo maji yanayozalishwa kutoka katika
chanzo cha Makutopora ni lita milioni 71 wakati mahitaji ni lita milioni
46 kwa siku.
Akifafanua
Mhandisi Kamwele amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa ziada ya maji katika
matenki ya Maili mbili mjini humo wataweka mtandao wa mabomba kutoka katika
eneo hilo hadi Ihumwa unakojengwa mji wa Serikali ili kuharakisha shughuli za
ujenzi wa mji huo .
“Kiwango
cha maji kinachosukumwa ni lita milioni 61 tu kati ya milioni 71 tunazozalisha
hali inayopelekea tuwe na maji ya ziada ambayo yatasaidia upatikanaji wa
maji ya uhakika hapa Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya Nchi,” alisisitiza
Mhandisi Kamwelwe.
Aliongeza
kuwa moja ya mikakati ya Wizara yake kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji
Taka Dodoma (DUWASA) ni kuongeza visima virefu katika eneo la Mtumba
ambapo visima vingine tayari vimechimbwa tangu mwaka jana ili kukidhi mahitaji
ya maji katika Mji huo ambayo ni takribani lita milioni mbili na laki
sita.
Mhandisi
Kamwelwe amesema mradi huo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi kisichozidi
miezi mitatu tangu sasa. Kazi
ya uchimbaji wa visima vingine katika eneo la Mtumba nje kidogo ya Mji wa
Dodoma inatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia leo, ikitekelezwa na Wakala wa
Uchimbaji Visima na Mabwawa (DDCA).
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema anaridhishwa
na hatua zinazochukuliwa na Wizara hiyo kupitia DUWASA katika kuhakikisha kuwa
mji wa Dodoma unakuwa na maji ya uhakika yatakayochochea ujenzi wa uchumi wa
viwanda na uwekezaji kwa ujumla.
Mradi
wa Kufikisha maji katika mji wa Serikali ni moja ya Maagizo ya Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa hivi karibuni kwa
Wizara hiyo, pamoja na Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa miundo mbinu ya umeme
inawekwa katika eneo hilo.
CHANZO: Frank Mvungi- Maelezo, Dodoma
HALMASHAURI YA LONGIDO YAPEWA GARI LA CHANJO
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemkabidhi mbunge wa jimbo la Longido, Dkt. Stephen Kiruswa gari aina Tunland
Double cabin kwa ajili ya kuboresha huduma za chanjo na afya katika jimbo hilo.
Amemkabidhi gari hilo leo (Jumatano, Februari 14, 2018) mbele ya Mkurugenzi
wa Halmashauri ya wilaya ya hiyo, Bw. Jumaa Mhina na Mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Longido, Bw. Sabore ole Moloimet.
Waziri Mkuu amesema amekabidhi gari hilo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi
aliyoitoa alipofanya ziara wilayani Longidi, Agosti, 2017. Gari la kutolea
huduma za chanjo lilikuwa ni miongoni mwa changamoto zilizokuwa zinaikabili
wilaya hiyo.
Kwa upande wake, Dkt. Kiruswa alitumia fursa hiyo kumshukuru
Waziri Mkuu kwa niaba ya wananchi wa Halmashauri ya wilaya ya Longido. “Gari
hili ni zuri sana na linahimili mazingira ya wilaya ya Longido.”
“Naishukuru sana Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuboresha huduma
mbalimbali wilayani Longido zikiwemo za afya na maji licha ya jimbo hilo kukaa
muda mrefu bila ya kuwa na mbunge.”
Amesema atahakikisha gari hilo linatunzwa na linatumika kwa ajili ya
matumizi yaliyokusudiwa ambayo ni huduma za chanjo na afya pamoja na huduma za
mama na mtoto.
MAPENZI BILA KUPIMA AFYA YADAIWA KUWA CHANZO KIKUBWA CHA MAAMBUKIZI YA VVU
Dk. Musagasa akizungumza wakati wa mafunzo hayo. Aliwataka watu wanaoishi na maambukizi ya VVU kuzingatia matumizi sahihi ya dawa zinazofubaza makali ya VVU pamoja na kuzingatia lishe bora.
Imeelezwa kuwa watu wengi
wanaendelea kupata maambukizi ya Virusi vya #Ukimwi (VVU) kutokana na kuanza
mahusiano ya kimapenzi bila kutambua afya zao hali inayosababisha waanze kuishi
kama mume na mke bila kujua hali zao za kiafya.
Hayo yamesemwa leo
Februari 14,2018 na wahudumu wa jamii wanaosaidia kazi katika vituo vya tiba na
matunzo kwa watu wanaoishi na Maambukizi ya VVU vilivyopo katika halmashauri 7
za wilaya mkoani Mwanza yanayofanyika katika ukumbi wa hotel ya Midland jijini
Mwanza.
Wahudumu hao wapo
katika #mafunzo ya msaada na huduma za kisaikolojia yanayotolewa na Shirika la
Ariel Glaser Pediatric #AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) kwa ufadhili wa Watu
wa Marekani kupitia Centres for Disease Control (CDC).
Wahudumu walisema
kitendo cha kuanza mahusiano ya kimapenzi na kuoana bila kutambua afya ni
miongoni mwa tabia hatarishi zinazochangia kwa kiasi kikubwa kuambukizana VVU.
Mmoja wa washiriki hao
Chausiku Sitta kutoka halmashauri ya wilaya ya Kwimba alieleza kuwa vijana
wanapata maambukizi ya VVU kutokana na kukosa elimu sahihi juu ya VVU na Ukimwi
na wengi wao kutawaliwa na tamaa ya ngono isiyo salama na kudhani kuwa kila mtu
anayeonekana kuwa na umbo zuri basi hana maambukizi ya VVU.
“Vijana wanakurupuka tu,tena
wakiona mwanaume ana mvuto ama mwanamke ana makalio makubwa wao wanaita
‘wowowo’ wanachanganyikiwa kabisa,ndugu zangu huwezi kumtambua mtu mwenye
maambukizi ya VVU kwa kumwangalia kwa macho mpaka apimwe”,aliongeza Chausiku.
Naye Musa Ordas kutoka
halmashauri ya wilaya ya Buchosa aliitaka jamii kutoendekeza waganga wa jadi
kwani baadhi yao wanawadanganya watu wanaoishi na VVU kuwa wamerogwa kwa
kuwalaghai kuwa wametupiwa majini mahaba.
Kwa upande wake,
Mwezeshaji katika mafunzo hayo, Dk. Joseph Musagasa aliwataka wanaume kuacha
tabia ya kutumia majibu ya wake zao wanapopima VVU kwani majibu yanatofautiana
na hutokea wakati mwingine mmoja kati yao kuwa na maambukizi na mwingine
kutokuwa nayo.
Dk. Musagasa
aliwashauri akina mama #kupima #afya zao kabla ya kubeba ujauzito,na kujifungulia
katika vituo vya afya ili kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa
mtoto.
“Siyo watoto wote wanaozaliwa
na mama mwenye maambukizi ya VVU wana VVU,hivyo mama unapotaka kubeba mimba
pima kwanza afya yako,ukibainika una maambukizi utashauriwa na wataalamu wa
afya namna ya kufanya ili usimwambukize mtoto wako”,alieleza Dk. Musagasa.
SERIKALI YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA AFYA KWA WANANCHI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akimjulia hali moja ya mama aliyekuwa akiuguliwa na mtoto wake, akifanya hivyo baada ya kuzindua jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda
SERIKALI
yaendelea kuongeza vituo vya Afya nchini ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali
za kuboresha Huduma za afya nchini jambo litakalo saidia kupunguza msongamano
wa wagonjwa katika Hospitali za Wilaya na Mkoa kwa kuwa huduma zote zitakuwa
zimeishia kwenye ngazi ya Kata.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim
Majaliwa wakati wa ufunguzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika Hospitali
ya Amana, mapema leo jijini Dar es salaam.
“Kumekuwa
na ongezeko kubwa la vituo vya Afya nchini kutoka vituo vya Afya 6321 kwa mwaka
2010 hadi vituo vya Afya 7680 kwa mwaka 2016, na kazi ya nyongeza inaendelea,
kwaiyo tunaamini vituo hivi vitaweza kupunguza msongamano katika
hospitali za Wilaya, pamoja na Hospitali za Mkoa”, alisema Mhe. Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa.
Mhe.
Waziri Mkuu alisema kwamba Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli ametenga kiasi cha Zaidi ya Bilioni 100 ikiwa ni fedha za
kuboresha Vituo vya Afya nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi
katika maeneo yote nchini.
“Tumeanza
kuboresha Vituo vya Afya kwa kujenga Wodi yakinamama wanaojifungua, thieta,
wodi za magonjwa yakawaida, maabara, tunaongeza na nyumba za watumishi, ili
kila kituo cha Afya kiwe na miundombinu hiyo ili utoaji huduma uwe rahisi”
alisema Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Mhe.
Waziri Mkuu aliendele kusema kwamba Serikali imetumia Zaidi ya Bilioni 161
katika kuendelea kuboresha Huduma za Mama na Mtoto kwa lengo la kuokoa Maisha
ya mama na mtoto jambo ambalo ni moja kati ya changamoto kubwa nchini.
Aidha
Mhe. Waziri Mkuu alisema kwamba Serikali imeendelea kuboresha Huduma za Afya
kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni 129 kwaajili ya vifaa vya kuwezesha
kundesha shughuli za upasuaji katika kila kituo cha Afya ambacho kinaboreshwa.
Wakati
akitoa taarifa ya Afya ya Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Poul Makonda alisema
kwamba wakina mama 126,164 walipata nafasi ya kujifungua katika vituo vya Afya,
huku wakinamama 202 ambao ni sawa na Asilimia 0.5 walilazimika kujifungua kwa
wakunga, na Asilimia 1.5 zaidi ya akinamama 1976 walijifungua njiani wakielekea
kupata huduma, idadi inayoonekana kuwa kubwa sana katika Mkoa wa Dar Es salaam.
Idadi
ya 2016 inaonesha Zaidi ya akina mama 85 walikuwa wanapoteza Maisha kati ya
kina mama 100,000 waliokuwa wanajifungua lakini kwa sasa tangu maboresho
yafanyike ni akina mama 57 kati ya akina mama 100,000 wanaojifungua ndio
hupoteza Maisha, huku mikakati thabiti yakupunguza vifo hivyo ikiendelea
kuwekwa.
Mhe.
Makonda aliendelea kusema kwamba zaidi ya watoto ambao wanafanikiwa kuwa hai na
kuwa salamakatika kujifungua ni Zaidi ya watoto 126,712, na watoto 131 huzaliwa
wakiwa tayari wameshakufa, idadi hii ikilinganishwa .
Pia
Mhe. Makonda alimshukuru AMSONS GROUP ambayo imetoa mchango mkubwa katika
ujenzi wa Jengo hilo la Mama na Mtoto lililopo katika Hospitali ya Amana huku
akiwataka Wadau wengine kuiga mfano huo katika dhana ya kusukuma gurudumu la
maendeleo katika jamii zetu.
Nae
Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine
Ndugulile alisema kuwa Serikali ya awamu ya tano tangu iingie madarakani
imeongeza Bajeti ya Dawa kutoka Bilioni 30 mpaka sasa ni Bilioni 270 likiwa ni
ongezeko la Zaidi ya mara 9, huku Wastani wa upatikanaji wa dawa ukiwa Zaidi ya
asilimia 80.
“Serikali
wakati inaingia madarakani Bajeti ya dawa ilikuwa ni Bilioni 30, mwaka
unaofuata ikafikia Bilioni 200, na hivi tunavyoongea Bajeti ya Dawa ni Bilioni
270, likiwa ni ongezeko la mara 9, kama msaidizi wako nasimama kifua mbele
WAZIRI KALEMANI AMWASHIA MOTO MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME VIJIJI
| Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akitoa maagizo ya utekelezaji wa usambazaji wa umeme kwenye maeneo ya vijiji na Kata za Iparamasa pamoja Kalembela wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mojo kati ya ziara zake za kukagua utekelezaji wa usambazaji wa umeme wa REA awamu ya tatu. |
| Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani akiwatunza wanakwaya wa kwaya ya kijiji cha iparamasa. |
| Meza kuu ikiongozwa na viongozi mbali mbali akiwemo Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chato,Dk Medard Kalemani. |
| Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji akielezea namna ambavyo wananchi wameendelea kupata changamoto kutokana na kukosa umeme kwa muda mrefu. |
Waziri
wa Nishati,Dkt Medard Kalemani amemwagiza mkandarasi
shirika la White City Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea
awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.
shirika la White City Internationala mbaye anasambaza umeme wa rea
awamu ya tatu kwenye Vijini na kata za Iparamasa na Kalembela kuhakikisha anafanya kazi hiyo kwa haraka zaidi ili kuwasaidia wananchi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha uhitaji wa nishati ya umeme.
Hayo
aliyasema wakati alipokuwa kwenye ziara ya Kukagua na
kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa
kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.
kuangalia utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini Wilayani Chato ambapo Diwani wa kata ya Iparamasa Amos Jiji ,amemweleza Waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa Jimbo hilo matatizo ambayo yameendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa umeme kwenye kata yake na kwamba kwa sasa kuna nguzo ambazo zimekaa
kwa muda wa miezi mitatu bila ya kusambazwa kwa wananchi ambao wanashida na huduma hiyo.
Mmoja
kati ya wananchi wa kata hiyo ,Bw Peter Mabula ameelezea
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara
zao.
kukosekana kwa umeme ni chanzo kikubwa ambacho kinakwamisha utendaji kazi hususani kwa upande wa biashara kutokana na wengi wao kutegemea nishati hiyo ili waweze kuendesha biashara
zao.
Aidha
kutokana na maombi hayo kutoka kwa Diwani pamoja na wananchi Mbunge wa Jimbo la
Chato na waziri wa nishati Dk Kalemani alitoa maagizo kwa Mkandarasi
kuhakikisha nguzo ambazo zimelala ndani ya miezi mitatu zisimame na kufikia
siku ya alhamisi vijiji hivyo na kata hizo ziwe zimepata umeme.
“Nimesikia
kuwa nguzo zimelala tu chini ndani ya miezi mitatu na kwamba mkandarasi alivyosikia
nakuja ndio ameanza kazi sasa namwagiza kuwa ahakikishe alhamisi wiki ijayo awe
amewasha umeme kwenye kata ya iparamasa na vijiji vyote na mimi siondoki hapa
nitahakikisha namsimamia”Alisisitiza Kalemani.
Mradi
wa usambazaji wa umeme vijijini Mkoani Geita,unatekelezwa na mkandarasi
wa Shirika la White City International ambapo unatarajia kufanyika ndani
ya miezi 16 kwenye jumla vijiji 220 vilivyopo mkoani
humo na jumla ya fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kutekeleza mradi huo
ni Sh Bilioni 78.56.
Naibu Waziri aagiza Muhandisi akamatwe
Naibu waziri wa maji Mhe Jumaa Aweso
ameagiza mhandisi wa manispaa ya Temeke Damas Shirima kukamatwa na kuhojiwa na
polisi kwa kosa la kutoa maelezo yasiyo ridhisha juu ya utekelezaji wa mradi wa
maji wa mwasongo uliopo Kigamboni Dar es salaam.
Akizungumza katika majumuisho ya siku yake ya pili ya ziara yake
jijini Dar es salaam Mhe Aweso amesema kuwa serikali haiwezi kunyamaza kimya
pale inapooneka miradi ya maji inahujumiwa waziwazi na kwamba watahakikisha
wale wote ambao wanagundulika kuhujumu miradi ya maji hatua za kisheria
zitachukuliwa dhidi yao.
Awali mbunge wa jimbo la Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa
Afya Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa jimbo lake bado linachangamoto ya
upatikanaji wa maji kwa baadhi ya maeneo ambapo amehaidi kulisimamia suala hilo
ili wananchi waondokane na kero hiyo.
chanzo: eatv
Waziri Jafo aweka mgomo

Waziri wa Nchi, Ofisi ya rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za mitaa, Tamisemi, Seleman Jafo, amegoma kuzindua mradi wa
maji katika kijiji cha Itiso wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma kutokana na
baadhi ya wananchi kuharibu kwa makusudi miundombinu hiyo
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho, Waziri Jafo, amesema
awali mkandarasi wa mradi huo alisuasua na halmashauri ya chamwino na kuamua
kumbadilisha mhandisi wa maji ili kuweza kukamilika kwa haraka na kiwango bora.
Amesema wananchi wa kijiji hicho wamekuwa hawana Ushirikiano na
viongozi wao na wale wa mradi hadi kusababisha kuharibu miundombinu ya maji, na
kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya chamwino kusimamia na wale watakaoharibu
miundombinu washughulikiwe.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Chamwino, Athumani
Masasi, amesema serikali ya awamu ya tano imetoa kiasi kikubwa kwa ajili ya
mradi wa maji lakini wananchi wamekuwa mstari wa mbele kuharibu miundombinu
hiyo.










