• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Wilayani Kwimba - Serikali Yawasimamisha Kazi Maafisa Utumishi Kwa Kutowajibika





Share:

Rais Magufuli ampandisha cheo na kumteua Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Februari, 2018 amempandisha cheo na kumteua Bw. Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw. Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo tarehe 10 Februari, 2018.

Kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Februari, 2018
Share:

DODOMA: Majaliwa awashauri CHADEMA kuhusu kuporwa ushindi

DODOMA

Waziri Mkuu wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amefunguka na kuwapa ushauri Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu tetesi za kuporwa ushindi wa Kata kadhaa ambazo wao wanaona walishinda na kuwataka kukata rufaa.

Kassim Majaliwa amesema hayo leo Februari 8, 2018 akiwa anajibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa wabunge mbalimbali, ambapo Mbunge wa viti maalum CHADEMA Devotha Minja alitaka kufahamu kama ni sera ya Serikali ya awamu ya tano kupora ushindi kwa watu ambao wameshinda kihalali.
Devotha Minja alihoji suala hilo na kudai kuwa katika baadho ya Kata zikiwepo Kata ya Sofi Malinyi CHADEMA ilipata kura 1,908 wakati CCM ilipata kura 1,878, Kata ya Siuyi Singida CHADEMA ilipata kura 1,358 huku CCM ikipata kura 1,304 lakini katika Kata hizo CCM ilitangazwa kushindi dhidi ya CHADEMA, ndipo hapa Waziri Mkuu aliposema kuwa anaamini Tume ya Uchaguzi haiwezi kutangaza matokeo ndivyo sivyo.
"Sitarajii kama Tume ya Uchaguzi (NEC) inafanya kazi ya kutangaza walioshindwa na kuwaacha walioshinda na masuala haya ya tume serikali imeweka utaratibu na tumeunda chombo kinachoshughulikia chaguzi zote nchini Tume ya Uchaguzi (NEC) lakini chombo kingine ni ile kwenye Mamlaka ya Serikali za mitaa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na vyombo hivyo lakini tunazo sheria zinazosimamia simamia uchaguzi na zote hizi zinasimamiwa na Tume" alisema Majaliwa 
Majaliwa aliendelea kutoa ufafanuzi kuwa kwa mujibu wa Sheria hizo zinatoa nafasi kukutana na vyama mbalimbali ambavyo havijaridhika juu na matokeo ya uchaguzi hivyo alitumia nafasi hiyo kuwashauri CHADEMA kufanya hivyo ili kutafuta haki yao kama wanaona kuna haki imeporwa.
"Ipo Sheria inatoa miezi mitatu ya kukata rufaa juu ya hizo namba ulizosisoma mimi sina uhakika nazo, sasa Mhe Mbunge kama una uhakika na takwimu ulizosisoma kwamba hao wenye namba nyingi ndiyo walishinda lakini ametangazwa mwingine bado unayo fursa ya kukata rufaa kwa mujibu ya Sheria ya uchaguzi, kwa hiyo nikushauri kufuata chombo chetu na kwa kuwa sheria zipo na wewe una fursa ya kufuata sheria ile ili kupata haki yako ya msingi" 
chanzo: eatv 
Share:

BANGLADESH : Waziri Mkuu Mstaafu ahukumiwa miaka mitano


BANGLADESH

Polisi nchini Bangladesh wamekabiliana na maelfu ya waandamanaji wanaopinga kufungwa jela miaka mitano kwa kiongozi wa upinzani nchini humo Khaleda Zia kwa tuhuma za rushwa.

Bi Khaleda ambaye ni Waziri Mkuu wa zamani amekana tuhuma za kutumia vibaya fedha za misaada ya kimataifa zilizotolewa kwa ajili ya kusaidia vituo vya watoto yatima nchini humo.
Kufuatia hukumu hiyo kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 72, hawezi kugombea katika uchaguzi wa Bunge utakaofanyika baada ye mwaka huu .
Hiyo ni moja ya mlolongo wa kesi zinazomkabili Bi. Khaleda ambaye ni mpinzani wa muda mrefu wa Waziri Mkuu wa sasa Sheikh Hasina .
Kiongozi huyo anatuhumiwa kutumia vibaya Dola 252,000 zilizotolewa kwa ajili ya watoto yatima .
Bi Khaleda alikuwa Waziri Mkuu wa Kwanza mwanamke mwaka 1991 akiongoza chama cha Bangladesh Nationalist Party, BNP.
chanzo: eatv page
Share:

MASASI : KAMATI YAUNDWA KUFUATILIA MALIPO YA WAKULIMA WA KOROSHO

MASASI

MKuu wa Mkoa wa Mtwara MHE GELASIUS BYAKANWA ameunda kamati maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kina kuhusu madai ya wakulima wa zao la korosho wilayani Masasi kufuatia wakulima wengi kulalamika kutolipwa malipo yao.
 Image may contain: 4 people, people sitting and indoor
Agizo hilo amelitoa Leo ( Feb 6 ) kwenye kikao kilichojumuisha viongozi wa Vyama vya ushirika ( AMCOS ) , wakulima na viongozi wa mabenki Lengo ikiwa ni kujua matatizo ya wakulima ili yatafutiwe ufumbuzi na hatimaye wakulima wapate haki yao.

BYAKANWA ameipa siku 14 kamati hiyo ambayo itaongozwa na MKuu wa wilaya ya MASASI kufanya uchunguzi huo na tarehe 22 mwezi huu kikao cha kuwasilisha taarifa ya uchunguzi huo kitafanyika.

Aidha ameagiza akaunti ya Katibu Wa Chama Cha Msingi Mmbaka isitoe fedha mpaka uchunguzi utakapo kamilika kutokana na katibu huyo kutolipa wakulima fedha tasilimu wakati utaratibu ulielekeza kila mkulima alipwe fedha zake kupitia akaunti na si vinginevyo.


UTEKELEZAJI WA AGIZO 

Kufuatia taarifa ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara  MHE. GELASIUS BYAKANWA  la kuunda kamati maalumu ya kufanya uchunguzi juu ya tatizo la baadhi ya wakulima wa zao la korosho Wilayani Masasi kutolipwa fedha zao, mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi MHE. JUMA SATMAH amewata watendaji wa Kata wa Halmashauri hiyo kutoa ushirikiano kwa kamati ya uchunguzi ili kuhakikisha takwimu sahihi za kila mkulima zinapatikana.

Image may contain: 4 people, people sitting


Hayo ameyasema jana Katika mkutano wa Baraza la Madiwani kwa ajili ya kupokea taarifa za utekelezaji za Kata robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo ameeleza kuwa Watendaji wa Kata wana wajibu wa kufahamu idadi ya wakulima ambao hawajalipwa maana ni sehemu ya majukumu yao.

ikumbukwe kuwa wakulima wamekuwa na tatizo la kutopata malipo yao kutokana na kuhamia kwenye mfumo wa malipo kwa njia ya bank ambapo wakulima wachache wamepata changamoto ya kutumia huduma za kibenki.


Share:

WAANDISHI WASISITIZWA USAWA WA KIJINSIA KATIKA KAZI ZAO

DODOMA  

Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na utamaduni –UNESCO- BI ROSE HAJI MWALIMU amewataka Waandishi wa habari nchini kuweka usawa wa kijinsia wanapofanya kazi zao.

Waandishi wa Habari wakiendelea na mfunzo katika ukumbi wa TBA -DODOMA

Yamesemwa hayo katika mafunzo yanayoendelea katika ukumbi wa Wakala wa Majengo Mkoani DODOMA  ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kufanya kazi zao kwa ufasaha na  kwa  uweledi.

Mkufunzi huyo amesema iwapo Waandishi wa Habari watashindwa basi watakuwa hawajatenda haki katika Jamii, kwani wengi wao wamekuwa wakifanya kazi bila kuzingatia usawa kijinsia ambapo mara nyingi wanaume ndiyo wamekuwa wakipewa kipaumbele kuliko wanawake .

Mafunzo hayo yanayaoendelea Mjini DODOMA yanatarajiwa kumalizika tarehe 12/2/2018 ambapo yatahitimishwa na maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yatakayofanyika katika ukumbi wa NASHEERA HOTEL mjini DODOMA
Share:

TAHADHARI KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA


DAR ES SALAAM

 Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania -TMA- imetoa tahadhari ya vipindi vifupi vya mvua kubwa vinatarajiwa kuwepo katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya  Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombena Ruvuma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Vipindi vifupi vya upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili vinatarajiwa katika maeneo ya mikoa ya Tanga. Dar es salaam, Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.


Mwananchi wa maeneo husika mnaombwa kuchukua Tahadhari
Share:

WAANDISHI WANAWAKE WAKEMEWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA YA NGONO


DODOMA

Waandishi wa habari wanawake nchini  wametakiwa kutumia uwezo wao kitaaluma wanapotekeleza majukumu yao badala ya kutegemea upendeleo kutoka kwa waajiri wao.

Baadhi ya wanawake wamekuwa wakijiingiza katika masuala ya mapenzi kwa mategemeo ya kupandishwa vyeo au kupata upendeleo badala ya kutumia uwezo walio nao kitaaluma jambo ambao linawashushia hadhi na heshima mahali pa kazi.
Waandishi wa habari kutoka Redio za Jamii Tanzania wakiendelea na mafunzo
Hayo yamesemwa na  Mkufunzi wa Redio za Kijamii nchini kutoka Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni – UNESCO - Bi ROSE MWALIMU katika semina inayoendelea katika Ukumbi wa Wakala wa Majengo  mjini DODOMA ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za kijamii kutoka vituo 24 vya redio za kijamii nchini kuhusu uandaaji wa habari na vipidi bora.

Akiwasilisha mada inayohusu maadili ya vyombo vya habari kwa washiriki wa semina hiyo Bi ROSE amesema  wazazi na walezi wamewasomesha watoto wao ili kuwapa uwezo na kuwajenga kitaaluma kwa lengo la kulitumikia taifa kiuadilifu pamoja na kujipatia kipato cha kujikimu na maisha.

Amesema badala yake waandishi wengi wanawake wamekuwa wakishindwa kutumia elimu waliyoipata katika utendaji wao wa kazi na wamekuwa wakidanyanyika kwa kufanya mapenzi na waajiri wao kwa lengo la kujinufaisha kwa kipato na upendeleo mbadala.

Image result for mwakyembe
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe anatarajia kuhudhuria maadhimisho ya siku ya redio duniani

Wakichangia mada hiyo baadhi ya washiriki wa semina wamesema wanawake wengi hushindwa kufanya kazi zao kiuadilifu kutokana na tamaa  za maisha na kipato kidogo wanachopewa na waajiri na wakati mwigine kukosekana kabisa.
Mafunzo hayo ya siku nane yatahitimishwa tarehe 13/2/2018 ambapo maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yataadhimishwa mjini DODOMA na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. HARRISON MWAKYEMBE anatarajia kuhudhuria hafla hiyo.



Share:

Rais Dk. John Pombe Magufuri azindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 06 Februari, 2018 amezindua Kituo cha Mafunzo Maalum ya Kijeshi (Comprehensive Training Center – CTC) kilichopo Mapinga katika Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani.
Kituo hicho kimejengwa kwa msaada kutoka Jeshi la Ukombozi la Watu wa China kwa gharama ya Shilingi Bilioni 67.87 na kitatumika kutoa mafunzo ya kijeshi ya kisasa yatakayowawezesha askari kukabiliana na vitisho vya kisasa vya kiusalama.
Kabla ya kuzindua kituo hicho Mhe. Rais Magufuli na Balozi wa China hapa nchini Mhe.  Wang Ke wameshuhudia makabidhiano ya kituo hicho kutoka Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China lililowakilishwa na Naibu Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Utawala ya Kamisheni Kuu ya Jeshi hilo Jenerali Yang Jian kwenda kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lililowakilishwa na Meja Jenerali Yakub Hassan Mohamed.
Mhe. Rais Magufuli pia ameshuhudia mazoezi ya kijeshi yaliyofanywa katika kituo hicho yakiwemo shambulizi la kutokea baharini (amphibian landing), makomandoo kukabiliana na magaidi na kupiga shabaha kwa kutumia miundombinu ya kisasa.
Akizungumza na Maafisa, Askari na wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio la makabidhiano ya kituo hicho Mhe. Rais Magufuli amelishukuru Jeshi la Ukombozi la Watu wa China na Serikali ya China kwa kutoa msaada wa kujengwa kwa kituo hicho na amesema Serikali ya Awamu ya Tano inathamini na kutambua mchango wa China katika Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania.
Mhe. Rais Magufuli amesema China imeendelea kudhihirisha urafiki na udugu wake na Tanzania kwani licha ya kujenga kituo hicho pia imetoa msaada wa kujenga kituo cha mafunzo ya kijeshi ya anga cha Ngerengere Mkoani Morogoro na miradi mingine ya maendeleo ya jamii na hivyo amemuomba Balozi wa China hapa nchini Mhe. Wang Ke kufikisha shukrani zake kwa Rais wa China Mhe. Xi Jinping.
Mhe. Wang Ke na Jen. Yang Jian wamesema China imejenga kituo hicho cha mafunzo maalum ya kijeshi ambacho ni alama nyingine ya uhusiano na ushirikiano wa kirafiki na kidugu kati yake na Tanzania na wameipongeza JWTZ kwa kupata kituo ambacho wanaamini kitatumika kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania na nchi nyingine za Afrika.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Jenerali Venance Salvatory Mabeyo amesema miundo ya kituo hicho inakifanya kuwa kituo cha kimataifa kilicho bora zaidi Afrika Mashariki na Kati kitakachoweza kutoa mafunzo ya kisasa kwa askari wengi na amemuomba Mhe. Rais Magufuli kusaidia ujenzi wa daraja la mto Mpigi litakalokiunganisha na barabara ya kwenda Dar es Salaam.
Pamoja na kukubali ombi hilo Mhe. Rais Magufuli pia amekubali maombi ya Jen. Mabeyo ya kupeleka maji, umeme na barabara katika eneo ambalo China imekubali kutoa msaada wa kujenga makao makuu ya JWTZ Mkoani Dodoma na ameahidi kuziagiza wizara husika kutekeleza maombi hayo haraka.
Tukio la kukabidhiwa kwa kituo cha mafunzo maalum ya kijeshi limehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Mapinga waliosimamisha msafara wake na kumuomba awasaidie kulipwa fidia kufuatia maeneo yao kuchukuliwa kwa ajili ya miradi ukiwemo mradi wa ujenzi wa kituo hicho cha mafunzo cha jeshi na kuvunjiwa nyumba zao katika eneo la Makurunge.
Katika majibu yake Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali haiwezi kurudia kuwalipa watu ambao tayari walishalipwa fidia na hawezi kuwatetea watu ambao wamevunja sheria kwa kuvamia maeneo yasiyokuwa yao.
Mhe. Rais Magufuli pia amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya kutekeleza  mradi wa bandari na eneo la uwekezaji la Bagamoyo na amewataka watu wote waliolipwa fidia wakati hawakuwa na maeneo warejeshe fedha za Serikali, waliolipwa fidia kuondoka katika maeneo yaliyolipiwa, na kwa wale ambao hawajalipwa fidia waendelee kutumia maeneo yao kwa shughuli zao mbalimbali.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Februari, 2018
Share:

SIMANZI NA MAJONZI VYATAWALA MAZISHI YA MARIA SANDALI, WILAYANI MASASI.

NA Gregory Millanzi.

Ikiwa leo ni Jumapili ya  tatu tangu tuuanze mwaka huu 2018, Simanzi na vilio vimetawala katika familia ya mzee Sandali, kufuatia kifo cha binti yake Maria Sandali, ambaye amefariki dunia alfajiri ya Januari 20 mwaka huu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ambako alikua akitibiwa tatizo la Saratani ya Mifupa.

Hali ilikuwa ya huzuni  katika makaburi ya familia ya Mzee Sandali, katika kijiji cha Chikundi, halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, umati wa watu umekusanyika katika safari ya mwisho ya kuumpumzisha mwili wa binti Maria Sandali.


Marehemu Maria Sandali, wakati wa uhai wake akiwa nyumbani kwao kijiji cha Chikundi, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara


Wazazi wa Marehemu walikuwa na wakati mgumu sana kuamini kuwa hawatamuona tena Binti yao mpendwa Maria Sandal, Mama mzazi wa Mariam bi  Benardetha Raymond na Baba yake Mzee Saidi Sandali, wameungana na wananchi pamoja na wanafamilia wengine kuumsindikiza binti yao katika pumziko la milele, pia wametoa pongezi kwa taasisi zote zilizojitolea kwa ajili ya matibabu ya mtoto wao wakiwemo wizara ya Afya,hospitali ya Muhimbili(MOI) na Ocean Road.

Msiba huu umegusa hisia za watu wengi kutoka maeneo mbalimbali wilayani Masasi, pamoja na viongozi wa serikali wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Masasi Selemani Mzee aliyeambatana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya Masasi Changwa Mkwazu, walihudhuria mazishi hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Masasi Selemani Mzee(mwenye kaunda suti ya bluu)  aliyeambatana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Changwa Mkwazu(mwenye mtandio wa njano) wakiwa kwenye makaburi ya Familia wakimsindikiza Marehemu Maria Sandal kwenye nyumba yake ya milele.


Awali, afisa mtendaji wa kata ya Chikundi, Joseph Mtungulia, akaeleza wasifu wa marehemu kuwa baada ya kupatiwa matibabu katika hospitali ya Ndanda Masasi, waliandikiwa rufaa ya nkwenda kutibiwa Muhimbili na ndipo Wizara ya Afya walichukua jukumu la kusimamia matibabu ya Maria Sandali, mpaka mahuti yanamkuta tarehe 20 mwezi huu katika Hospitali ya Ocean Road Dar  Es Salaam.


Maria Sandali ambaye alikua ni mwanafunzi katika shule ya sekondari ya King David Manispaa ya Mtwara Mikindani  alikuwa anasumbuliwa na uvimbe kwenye bega kwa muda mrefu na baada ya kufanyiwa vipimo wiki iliyopita akajulikana kuwa anatatizo la saratani ambayo ilikuwa imeshakuwa sugu, 

Maria amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 17, Mungu ailaze roho ya Marehemu Maria, mahali pema peponi  aaamen.

…………………………………………mwisho………………………………………
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>