WATOTO WOTE WAPEWE ELIMU SAWA
Wananchi wa Mkoa wa Mtwara na
wilaya zake wametakiwa kuachana na mawazo mgando ya kuwabagua watoto kijinsia
katika suala la utoaji wa elimu ili kuwajengea misingi bora watoto wao.
Hayo yamesemwa na Afisa elimu,
vifaa na takwimu wa Wilaya ya Mtwara vijijini Bw. Kitonka Manase na kuwahasa
wazazi kutowanyima haki ya msingi ya kupata elimu watoto wa kike kwa sababu za
kimila na desturi.
Aidha Bw.Manase amewaomba
Wasichana waliofanikiwa katika elimu kuwasaidia wasichana ambao bado wapo kwenye
adha hii na jamii kwa ujumla kwa kuwapa elimu ili waeze kubadilika kifikra,na
kuongeza kuwa sheria haibagui jinsia,dili ,wala kabila.
Na kwa upande wake Lenfrida Mwagama Mwanafunzi wa chuo cha kilimo mkoani
Mtwara,amewashauri wasichana ambao wamepata nafasi ya kupata elimu waitumie
vizuri ili iwasaidie kujiajiri wenyewe katika maisha yao na si kuajiriwa.
Hata hivyo nchini Tanzania takwimu zinaonyesha tatizo la ubaguzi wa
kijinsia katika utoaji wa elimu kwenye miaka ya hivi karibuni kutokana na
jitahada zinazofanywa na serikali pamoja
na taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo elimu zinazoendelea kutolewa kwa
wananchi,ikiwa kwa Mwaka 2012 takwimu zinaonyesha uwiano sawa kati ya wasichana
na wavulana katika elimu ya msingi,katika elimu ya sekondari ya kawaida uwiano
ni 0.6% na sekondari ya juu ni 0.5%,hali inayoashiria kupungua kwa uwiano huo
ukilinganisha na mwaka 2017 ambapo
uandikishaji katika elimu msingi wavulana
milioni 4,629,027 sawa na 49.7% wasichana milioni 4,688,383 sawa 50.3%
katika jumla ya wanafunzi milioni 9,317,410 na kwa upande wa sekondari jumla ya
wanafunzi 199,019 wameandikishwa ikiwa wavulana 947,486 sawa 49.6% na wasichana 961,531 sawa 50.4%.
SDA YAWANOA WATOTO WA KIKE
Na Ramla Massali
Shirika lisilo la kiserikali ya Sports Development Aid ambalo limejikita katika michezo na kutoa Elimu kwa watoto wa kike, wameendelee kuwaelimisha watoto wa kike hasa wale waliopo sekondari katika kata ya mayanga.
lengo kuu ni mtoto wa kike kutambua haki zake na kuza sauti pale anapohitaji msaada. sikiliza upate kujua kile kilichijiri
Shirika lisilo la kiserikali ya Sports Development Aid ambalo limejikita katika michezo na kutoa Elimu kwa watoto wa kike, wameendelee kuwaelimisha watoto wa kike hasa wale waliopo sekondari katika kata ya mayanga.
lengo kuu ni mtoto wa kike kutambua haki zake na kuza sauti pale anapohitaji msaada. sikiliza upate kujua kile kilichijiri
Amuua Mkewe, aenda polisi na kuwaambia “Nimemmaliza nendeni mumchukue
Na Mwandishi Wetu, Kenya.
Anthony Karanja mwenye umri wa miaka 25 anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kumuua mkewe kwa kumkata na shoka na kumchoma visu kufuatia ugomvi uliozuka baada ya kupokea ujumbe wa mapenzi kwenye simu yake (ya Karanja).
Kwa mujibu wa Polisi wa eneo la Trans Nzoia nchini Kenya, Karanja alipokea ujumbe huo kwenye simu yake ambao mkewe aliouna na kuanzisha ugomvi kutokana na wivu wa mapenzi, lakini alijibiwa kwa kushambuliwa kwa visu na kumkata na shoka.

Polisi wameeleza kuwa mtuhumiwa ambaye alijisalimisha mwenyewe polisi baada ya kutekeleza mauaji hayo alieleza kuwa alimchoma mkewe Esther Wangui kisu kwenye paja, kwenye miguu na kifuani.
Imeelezwa kuwa baada ya kutekeleza mauaji hayo Jumapili iliyopita, alijaribu kujiua bila mafanikio na ndipo alipofika katika kituo cha polisi akipiga kelele, “Nimemmaliza endeni mumchukue.”
Majirani wameeleza kuwa walisikia ugomvi kati ya wawili hao majira ya saa moja na nusu asubuhi. Wameeleza kuwa baada ya kutekeleza mauaji, mtuhumiwa alikunywa sumu ili ajiue lakini hakufanikiwa ndipo alipoamua kujinyonga kwa kamba lakini pia hakufanikiwa.
“Mtuhumiwa aliwapeleka maafisa wetu nyumbani kwake na akawapa funguo kuwawezesha kuuchukua mwili wa marehemu,” Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Jackson Mwenga anakaririwa.
Mwenga alisema kuwa wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa na wameanza kufanya upelelezi.
FAMILIA YA BABU SEYA YAPATA PIGO

Ikiwa ni siku chache zimepita mara baada ya msanii mkongwe Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya na mwanae Papii Kocha kuachiwa huru kutokana na kupewa msamaha wa rais Magufuli katika sherehe za maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania yaliyofanyika Desemba 9, mwaka huu mjini Dodoma familia hiyo imepata pigo baada ya mdogo wa Babu Seya aitwaye Crizo Chimbukizi kufariki dunia.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia hiyo, King Kikii, Crizo alifariki dunia jana kutokana na mshtuko wa moyo baada ya kupewa taarifa ya kuachiliwa huru kwa wawili hao na kwamba taratibu za mazishi zinafanywa.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa mkoa wa Katanga Kongo nyumbani kwa familia ya Nguza.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli alitoa msamaha kwa mwanamuziki maarufu Nguza Viking maarufu kama Babu Seya na mwanaye Jonson Nguza maarufu kama Papii Kocha wasanii waliokuwa wanatumikia kifungo cha maisha jela.
MSAADA WA KISHERIA
Na Mwandishi wetu
Naibu katibu mkuu wa wizara na sheria Amon Mpanju
ameongoza wadau mbalimbali wanaojihusisha na masula ya utoaji wa msaada wa
kisheria katika maadhimisho ya wiki ya wasaidizi wa sheria nchini, katika kanda
ya kusini
ameongoza wadau mbalimbali wanaojihusisha na masula ya utoaji wa msaada wa
kisheria katika maadhimisho ya wiki ya wasaidizi wa sheria nchini, katika kanda
ya kusini
SHERIA ZA BARABARANI ZATEKELEZWA
Madereva nchini wamepongezwa kwa kuanza kubadilika na kutii sheria bila shuruti katika kukabiliana na ajali za barabarani na hivyo kupungua kwa ajali pamoja na vifo vitokanavyo na ajali kwa uendeshaji usiozingatia sheria za barabarani.
Kamanda wa Kikosi cha Barabarani Tanzania Fotunatus Mselemu –Kamishana Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) amezungumzo pindi akifungua mkutano wa siku mbili wa kupokea maoni ya sheria kuhusu ajali za barabarani unaojumlisha mashirika yasiyo ya Kiserikali
Kamanda Mselemu amesema tatizo la ajali barabarani bado ni kubwa kwani watu wengi wanafariki na kujeruhiwa kutokana na ajali barabarani”sisi sote ni wahanga wa usalama barabarani hivyo hatuna budi wadau wote kushirikiana katika kukabiliana na suala hili na kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia ili usalama wa barabarani uimarike na kuboreka zaidi”Alisema.
Alisema hivi sasa watu wengi wameanza kubadilika hususan madereva wengi ambapo kuna wakati inabidi jeshi la polisi kutumia nguvu nyingi ili kuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika na nguvu hizi zimetumika kwa nia nzuri ili watanzania kuwa salama wanapotumia vyombo vya moto
Akitolea mfano kwa hali ya usalama barabarani kwa siku ya jana (juzi) nchi nzima kulikua na ajali nne ambazo zimesababisha vifi viwili na majeruhi nne,hivyo ni hatua nzuri na
Hata hivyo aliwataka wadau hao kuhakikisha wanatoa maoni mazuri ambayo yatasaidia kupata sheria ambayo haitamkandamiza mwananchi na ambayo itakua salanma na kupunguza ajali za barabarani nchini na kuwa na sheria inayotekeklezeka kwa kupunguza ajali kwa asilimia 50 kama
“Serikali ya awamu ya tano inapenda kulinda maisha ya watanzania,serikali inatengeneza uchumi wa kati na viwanda kwa kuboresha miundombinu ikiwemo barabasha hivyo jukumu letu kushirikiana na serikali kuilinda miundombinu yote inayotengenezwa”
Aidha,Kamanda Mselemu aliwataka wananchi waondoe dhana kwamba ajali zinatokana na nmapenzi ya Mungu “hii siyo kweli ila matatizo yote ya ajali ni sisi wenyewe tunasababisha kutokana na mwendo kasi na kutotii sheria za barabarani.
Alitaja takwimu za ajali barabarani kwa Tanzania kwa mwezi Julai hadi Septemba mwaka 2016 2 ilikua 639,vifo 923 na majeruhi 2,469 na kwa mwaka 2017 kuanzia Julai hadi Septemba ajali za barabarani zilikuwa 1,376,vifo 655 pamoja na majeruhi 1,469.
Naye Mwakilishi toka shirika la Afya Dunia Mery Kessy alisema zaidi ya asilimia 90 za ajali zinazotokea katika nchi zinazoendelea ingawa ni asilimia 10 tu nchi hizo zinamiliki vyombo vya moto na hiyo ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo miundombinu,mazingira pamoja na tabia.
Alisema wahanga wakubwa wanaopata ajali na vifo ni vijana kati ya miaka miaka 15 mpaka 29 kwani umri huu wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kusababisha ajali na hivyo ajali hizo kuchukua zaidi ya asilimia 3 za pato la Taifa kwani serikali inaingia gharama kubwa kutibu majeruhi katika sekta ya afya.
CHANZO: MJENGWA
KUANGUKA KWA TAKATAKA BARABARANI KUELEKEA DAMPO KUU LA MTWARA
Na Msafiri
kipira
Wananchi wanaoishi
jirani na dampo la mangamba wamelalamika kutokana na hali ya dampo, pia
udondokaji wa takataka barabarani kutokana na uendeshaji wa mwendo na
kusababisha udondokaji wa takataka barabarni kitendo kinachosababisha kuonekana
wananchi ndio watupaji wa takataka.
Kauli ya mkazi mmoja anaefahamika kwa jina
la shungi mkazi wa mangamba amewaomba wafanyakazi wa magari yanayobeba takataka
kufunika vizuri pindi wanapobeba takataka ili kuepuka kudondoka kwa takataka
barabarani. Sikiliza ripoti hii inahusu mazingira na kero hii katika barabara
kuu inayoelekea dampo kuu la mkoa wa mtwara.
Je Diwani wa kata hii analizungumziaje jambo hili?
ATHARI ZA UKATAJI WA MITI - MTWARA
Na Karimu
Faida
Kwa mujibu
wa tafiti ya sera ya taifa ya misitu ya mwaka 1998, theruthi mbili ya misitu
iko hatarini kuvamiwa huku Tanzania ikiathirika kwa matumizi ya mkaa. Kijiji
cha Moma ni sehemu ya maeneo yaliyoathirika kutokana na matumizi mabovu ya
ardhi.
Wananchi wengi
hasa maeneo ya vijijini huvamia na kukata miti hovyo, pamoja na kuwepo kwa hali
hiyo kumesababisha kuhama kwa wanyama pamoja na upotevu wa Mvu. Fuatilia makala
haya kujua nini jitihada zinazofanyika ili kuhakikisha misitu inahifadhiwa.
IFAHAMU JAMII FM
Utangulizi
Jamii FM Radio, ilianza matangazo yake rasmi mwezi Septemba mwaka
2016. Madhumuni ya Radio hii ni kupasha Habari na kutoa fursa ya Mawasiliano
kwa Jamii, hasa Jamii ya vijijini. Vipindi vyake vinaandaliwa kwa namna
inayogusa na kulenga maisha ya jamii ya vijijini, ikiwa ni pamoja na watu wenye
mahitaji maalum kama Walemavu na watu wasiojiweza.
Radio Jamii FM hutangaza habari
zinazoelimisha na kuwa Jukwaa la kubadilishana habari za maendeleo ya jamii,
hivyo kutengeneza fursa huru kwa jamii kupaaza sauti. Ushirikishwaji jamii
unasisitizwa katika kuandaa vipindi. Hivyo,Radio Jamii hutoa fursa kwa wasio na
sauti katika Jamii kupaza sauti.
Introduction
JAMII FM is a Community Radio that was launched in September 2016 for
the purpose of giving community members particularly from rural areas access to
information and means of communication. The programmes are basically focused on
issues that directly or indirectly reflects community livelihood including
people with special needs. Through Jamii FM Radio, educational and
developmental information is disseminated and exchanged; important local issues
are aired; a free market place of ideas and opinions is opened up and people
are given the opportunity to express themselves. Broad participation by
community members is always encouraged in Program production. JAMII FM RADIO
gives voice to the voiceless.
Jamii fm On-Air
Dira
Kuona kwamba kupitia Radio
Jamii FM, Jamii ya Mikoa ya Mtwara na Lindi hasa inayoishi vijijini, inapata habari
na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika shughuli zinazohusu maendeleo yao.
Vision
The
VISION of Jamii FM is to see the community of Lindi and Mtwara Regions
particularly from rural areas have access to information and increased capacity
to play a meaningful role for their own development through media..
Production control room Production room
Dhima
Kuwezesha Jamii kutumia Vyombo
vya habari katika kukuza mawasiliano shirikishi ili kujiletea maendeleo
endelevu
Dhima
Kuwezesha Jamii kutumia Vyombo
vya habari katika kukuza mawasiliano shirikishi ili kujiletea maendeleo
endelevu
Eneo
Kituo cha Radio Jamii kipo Kitongoji cha Naliendele, kilichopo
umbali wa kilometa 9 kutoka Mtwara Mjini katika barabara inayoelekea Newala.
Kituo hiki kipo mkabala na Kituo cha Utafiti wa Mazao ya Kilimo, Naliendele,
Mtwara
Location
JAMII FM Radio Station is located at Naliendele area 9km
from Mtwara Town along Mtwara-Newala road. The station is opposite to Naliendele
Agriculture Research Institute.
News Room
Eneo la Huduma
Radio Jamii inamiliki Mnara
wenye urefu wa Mita 60 unaowezesha Kituo kurusha matangazo na kufikia idadi
kubwa ya wakazi wa eneo hili kuanzia Manispaa ya Mtwara na kusambaa hadi
kufikia Nanyamba, Tandahimba, Newala, Masasi, Nachingwea, Lindi na baadhi ya
maeneo yanayoambaa kwenye mpaka wetu na Nchi jirani ya Msumbuji
Coverage:
JAMII
FM RADIO owns its 60 meters transmission tower that enables to reach the huge
population from both Mtwara and Lindi regions, from Mtwara Municipal up to Nanyamba,
Tandahimba, Newala, Nachingwea, Lindi and some parts along the boarder with
neighbouring country-Mozambique.
Adminstration
Ratiba ya Vipindi
0600 – 1000hrs – Dira ya
Asubuhi
1000 – 1300hrs – Kapu la Jamii
1300 – 1300hrs – Habari kwa
ufupi
1300 – 1600hrs – Mchakamchaka
1600 – 1610hrs – Habari (News
Bulletin)
1610 – 1800hrs – Sauti ya
Jamii
1800 – 1900hrs – Radio France
International (RFI)
1900 – 1910hrs – Habari (News
Bulletin)
1910 – 2000hrs – Dimba la
Michezo (Sports)
2000 – 2100hrs – Makala Maalum
2100 – 2200hrs – Usiku Mwema
2200 – 0000hrs – Love Boat
0000 – 0600hrs – Music Mix
Programme Schedule
0600 – 1000hrs – Dira ya
Asubuhi
1000 – 1300hrs – Kapu la Jamii
1300 – 1300hrs – Habari kwa
ufupi
1300 – 1600hrs – Mchakamchaka
1600 – 1610hrs – Habari (News
Bulletin)
1610 – 1800hrs – Sauti ya
Jamii
1800 – 1900hrs – Radio France
International (RFI)
1900 – 1910hrs – Habari (News
Bulletin)
1910 – 2000hrs – Dimba la
Michezo (Sports)
2000 – 2100hrs – Makala Maalum
2100 – 2200hrs – Usiku Mwema
2200 – 0000hrs – Love Boat
0000 – 0600hrs – Music Mix
















