• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Tamko La Waziri Wa Afya Ummy Mwalimu Kuelekea Maadhimisho Ya Siku Ya Kifua Kikuu Duniani Machi 24 – Leo Mjini Dodoma

Na WAMJW-Dodoma.
# Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.

# Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua Kikuu kila mwaka Duniani na Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini ya miaka 15.

# Tafiti nyingi zinaonesha kuwa karibia theluthi moja ya Watanzania tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu na wanaishi na vimelea mwilini mwao.

# Kauli mbiu ya mwaka huu inasema *” Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB.”*

#Nchini Tanzania kila mwaka jumla ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.

# Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele.

# Napenda kuwakumbusha TB inatibika na kupona kabisa, dawa zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini katika vituo vya Umma na Binafsi.

# Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kikuu nchini ikiwemo kuimarisha uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu katika Vituo vya Afya.

# Serikali na wadau mbalimbali tunaendelea na utekelezaji wa kampeni za uhamasishaji na upimaji wa Wananchi katika maeneo ya migodi, makazi duni kwenye miji mikubwa, magereza na shule za bweni.

# Pia Serikali imezindua dawa mpya za TB za watoto ili kuhakikisha zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani ( WHO), dawa hizo mpya ni za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na  tayari zimeshawasili nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na Halmashauri zote nchini.

# Nawaagiza waganga wafawidhi wote wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya  kuanza masomo.

#Ni marufuku kwa Madaktari  kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima wanafunzi husika. Kufanya hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa  kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.

# Serikali inatambua umuhimu wa ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.

#Mpaka sasa takribani watoa huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.

Share:

Anna Makinda ataka viongozi wanawake kupewa elimu

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Tanzania mstaafu, Mama Anna Makinda ametoa elimu wa uongozi wa Kijinsia kwa madiwani wanawake wa Mkoa wa Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na TGNP Mtandao ikiwa na lengo la kuwajengea uwezo madiwani hao.

Akizungumza katika warsha hiyo, Bi. Makinda alisema suala la kuwajengea uwezo wanawake linapaswa kuanza mapema mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi ili kupata muda zaidi wa viongozi hao kupata elimu stahiki, kwani mara nyingi elimu hiyo hucheleweshwa kutolewa.

“…Kimsingi muda huu tumechelewa mikakati ya kuanza kumuwezesha kiongozi mwanamke hupaswa kuanza mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi hii itatusaidia hata kujipanga mapema uongozini…,” alisema Mama Makinda akizungumza na madiwani hao.

Aliwataka wanawake wote viongozi kuwa pamoja hasa wanapopigania masuala ya wanawake ili kwani umoja mara zote ni nguvu na utengano ni udhaifu. Changamoto za wanawake hazitofautiani kiitikadi za chama, rangi wala imani hivyo kuna kila sababu ya kuungana pale wanapogombea ajenda za wanawake.

Pamoja na hayo aliwataka madiwani wanawake kujipanga kimikakati na kutokubali kuondolewa katika nafasi za uongozi kizembe, kwani uwezo wa kuwatumikia wananchi wanao tena wa kiwango kikubwa kama watajipanga vizuri.

“…Hivi unakubalije mtu aliye nje kuja kukutoa katika nafasi yako kirahisi rahisi ilhali wewe upo karibu na wananchi, usikubali tuwaoneshe kwa vitendo tulioingia tusitoke kirahisi bila kupenda labda tupande ngazi lakini sio kushuka,” alisisitiza Mama Makinda.

Aidha aliwaomba kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano na viongozi wa kiume kwani idadi yao ni kubwa hivyo ushawishi pekee ndio unaweza kuongezea nguvu ajenda zao. 

Alibainisha idadi ya madiwani na wabunge wa kiume ni kubwa ukilinganisha na wao hivyo njia pekee ya wao kufanikiwa ni kujenga urafiki, ukaribu na ushawishi kwa agenda anuai zinazobebwa na wanawake.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge Wanawake Tanzania (TWPG), Bi. Suzan Lyimo akizungumza na madiwani hao aliwaomba kuwa kitu kimoja haswa wanapopigania masuala ya msingi kumuwezesha mwanamke.

Alisema kama wanawake hawatakuwa kitu kimoja hawawezi kufanikiwa katika agenda zao. Hata hivyo aliongeza kuwa usawa wa kijinsia unapaswa kuanzia ndani ya vyama vya siasa kwani ndipo mipango mingi ya chama upangwa kwa utekelezaji zaidi.
Share:

DODOMA: Polisi Wamtia Mbaroni aliyejifanya JWTZ na Usalama wa Taifa

Jeshi la polisi Mkoani Dodoma linawashikilia watuhumiwa 14 wa makosa mbalimbali ya kiuhalifu wakiwemo matapeli waliojifanya kuwa ni maofisa ununuzi kutoka Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na maofisa usalama wa Taifa.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema watuhumiwa hao walikamtwa kwenye mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakifanya vitendo vya uhalifu baada ya kumtapeli mfanyabishara mmoja kiasi cha sh. Million 8.

Waliokamatwa katika tukio hilo ni Shaaban Kwiyela (58) Mkazi wa Kijiji cha Igunga Mkoani Tabora, ambaye alifukuzwa kazi kwa  utovu wa nidhamu tangu mwaka 1995 akiwa kikosi cha 36KJ Msangani Kibaha Mkoani Pwani akiwa na cheo cha sajenti lakini amekamatwa akiwa na mavazi ya cheo cha Kaptein.

Wengine ni Emmanuel Michael (45) mkazi wa Iringa, Juma Pesambili (33) Mkazi wa Sai Mbeya na Emmanuel Mwagonela (50) Mkazi wa Mtaa wa Ghana mkoani Mbeya.

Share:

DODOMA: Serikali kuwatumia waganga wa kienyeji Kuwasaka Wagonjwa wa TB

Katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) nchini, serikali imesema kuwa itawatumia waganga wa kienyeji katika kuwagundua wagonjwa hao ili waweze kufikishwa kwenye vituo vya afya na kupata tiba sahihi.

Kauli hiyo imetolewa jana (Machi 23, 2018) mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yanayofanyika leo (Machi 24, 2018).

Waziri Mwalimu alisema kuwa waganga wa kienyeji ni wadau muhimu katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa wagonjwa wengi hukimbilia kwao kwa kudhani kuwa wamerogwa.

Aidha, Ummy amesema kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO inakadiriwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua kifua kikuu kila mwaka duniani huku milioni moja kati yao wakiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 15 na hapa nchini kila mwaka jumla ya watu 60,000 wanaambukizwa ugonjwa huo wakati mwaka 2016 watu 65,908 waliogundulika kuugua na kuanza matibabu.
Share:

DODOMA: Mbarawa "Serikali itaendelea kuiwezesha TMA"

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amesema Serikali itaendelea kuiwezesha Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) kuwa na vifaa na mitambo ya kisasa ya hali ya hewa ili kuwezesha huduma bora za utabiri kutolewa kwa wakati na usahihi kwa manufaa ya taifa.

Profesa Mbarawa amesema hayo jana mjini Dodoma  wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine duniani kuadhimisha Siku ya Hali ya hewa, na kusisitiza kuwa kwa sasa TMA imeongeza imani kwa wananchi kwani imekuwa ikitoa utabiri wa kuaminika kwa  sababu ya kuwa  vifaa vingi na vya kisasa vya utoaji taarifa.

“Nipende kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwezesha TMA na kuhakikisha kuwa inatoa utabiri ambao ni sahihi na wa uhakika kwani kuwepo kwa utabiri sahihi kutawezesha vyombo husika kuchukua hatua mapema kabla ya madhara makubwa kutokea” alisema Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa amewataka wananchi kutunza mazingira kwa kuacha kulima kwenye vyanzo vya maji na kuepuka kuchafua maeneo ya bahari ili kuepusha athari zinazoepukika zikiwemo uharibifu wa miundombinu ya  uchukuzi.

 “Niwaombe wananchi wote watunze mazingira kwani kumekuwa na uharibifu mkubwa wa miundombinu kutokana na shughuli zinazofanywa na binadamu katika maeneo mbalimbali yasiyotakiwa kulimwa au kujengwa, alisisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi ameishukuru Serikali kwa jitihada inazozifanya kuwekeza kwenye miundombinu ya hali ya hewa kwa kutoa fedha kununua vifaa mbalimbali ambavyo vimewezesha mamlaka hiyo kutoa utabiri uliosahihi kwa zaidi ya asilimia 70.

Dkt Kijazi ameongeza kuwa kwa sasa taarifa za hali ya hewa hasa kwenye usafiri wa anga zimeimarika ambapo hutolewa kila baada ya nusu saa na kuwawezesha watumiaji wa usafiri huo kupata taarifa kabla ya kuanza safari zao.

“Kwa sasa utabiri wa usafiri wa anga ni wa  uhakika mpaka asilimia 90 na hutolewa kila baada ya nusu saa na marubani hupata taarifa hizo kwa wakati kabla ya kuanza safari zao, alisema Dkt. Kijazi.

Siku ya Hali ya Hewa duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 23 Machi ambapo mwaka huu yanaongozwa na kauli mbinu isemayo“JIWEKE TAYARI NA ZINGATIA TAARIFA ZA HALI YA HEWA”.
Share:

DAR ES SALAAM: Majaji watatu kusikiliza kesi ya ACT Wazalendo dhidhi ya Jeshi la Polisi

Mahakama  kuu ya Dar es salaam Aprili 5, 2018 itaanza kusikiliza kesi ya madai ya chama cha ACT Wazalendo dhidi ya jeshi la polisi

Tarifa iiliyotolewa jana  na Afisa Habari wa ACT Wazalendo, Abdallah Khamisi  ilisema kuwa kesi hiyo itasikilizwa chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba.

"Machi 18 tulizungumza na umma juu ya hali mbaya ya nchi Kiuchumi, na tukaeleza hatua ambazo kama chama tutachukua katika kutatua masuala kadhaa ya kinchi. 

"Kwenye eneo la DEMOKRASIA tulieleza kuwa tumefungua Kesi ya Madai Na. 8/2018 Mahakama Kuu hapa Dar Es Salaam, kulishtaki Jeshi la Polisi, kutokana na Jeshi hilo kuingilia, visivyo halali shughuli za ziara yetu ya kuhamasisha maendeleo katika Kata tunazoziongoza.

"Leo Mahakama imeipangia tarehe kesi husika, itasikilizwa kwa mara ya kwanza, Aprili 5, 2018 chini ya Majaji watatu, Jaji Ferdinand Wambari, Jaji Sameja na Jaji Rose Teemba."- Ilisema taarifa hiyo
Share:

Waziri Ummy Awashauri Wananchi Kwenda Vituo Vya Tiba Haraka Pindi Wanapogundua Dalili Za Ugonjwa Wa Dengue

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.

Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA jana  jijini Dar es salaam.

“Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo Wizara inashauri kuwa wananchi wasiwe na hofu, bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba " alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo basi wananchi wanaaswa kuwa, wakipata homa wahakikishe kuwa wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au Dengue, au sababu nyingine, ili hatua stahiki zichukuliwe.

Waziri Ummy amesema kuwa ili kujikinga na ugonjwa huo ni lazima Kuangamiza mazalio ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo pamoja na Kujikinga na kuumwa na mbu kwa  kuvaa nguo ndefu muda wote hasa nyakati za mchana.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wizara itaendelea Kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa nchi nzima kwa kutumia mfumo uliopo wa ukusanyaji wa taarifa (IDSR), ambapo tunaendelea kupata taarifa za kila siku juu ya mwenendo wa ugonjwa huu na Kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesisitiza kuwa  hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili ya wasafiri wanaoingia na wanaotoka nchini na  Wizara itaendelea kushirikiana na wadau na sekta mbalimbali katika kufuatilia na kudhibiti ugonjwa huo.

Homa ya Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu wa aina ya Aedes ambao ni weusi wenye madoa madoa meupe yenye kung’aa.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
Share:

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Waziri Wa Ulinzi Wa Israel Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Machi, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Lieberman Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Noah Gal Gendler, viongozi wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Lieberman kwa kuitembelea Tanzania na amemhakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira ya dhati ya kuukuza zaidi na kuuimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Israel.

Mhe. Rais Magufuli ametaka makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika maeneo mbalimbali yakiwemo ulinzi na usalama, mafunzo na masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili utekelezaji uanze mara moja.

“Tanzania na Israel ni marafiki wa miaka mingi, nataka kuona urafiki wetu unakuwa zaidi, nawakaribisha wawekezaji kutoka Israel kuja kuwekeza katika kilimo, madini na gesi na pia kuwepo ndege za moja kwa moja kutoka Israel hadi Dar es Salaam na Kilimanjaro ili kukuza utalii” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuomba Mhe. Lieberman kumfikishia ujumbe Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu wa kumualika kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi hapa nchini badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.

Kwa upande wake Mhe. Avigdor Lieberman amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumkaribisha na kufanya nae mazungumzo na pia amemhakikishia kuwa Israel imejipanga kuongeza uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania katika maeneo yote ya makubaliano pamoja na kusaidia kilimo na usindikaji wa chakula.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
22 Machi, 2018
Share:

Viongozi Wakuu CHADEMA Waripoti tena Polisi

Viongozi wanne wa Chadema wamewasili Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu Dk  vicenti Mashinji.

Viongozi hao ambao  wamewasili Polisi kwa ajili ya kuitikia wito ni pamoja na manaibu katibu John Mnyika na Salum Mwalimu pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti John Heche.

 Wakili wao Fredrick Khiwelo amesema wengine wako njiani akiwamo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe.

Awali Mbowe  ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai kwa Taifa Leo tarehe 22 Machi 2018, ametoa waraka wa kuitwa Polisi yeye na viongozi wenzake.

Katika waraka huo Mbowe amesema kwamba kuna taarifa pia ya  kumuunganisha  Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili.

Updates: Mbowe, Mwalimu Wameachiwa Kwa Dhamana......, Heche na Mnyika washikiliwa, Mdee na Matiko wanasakwa..


Viongozi watatu  wa Chadema walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wameachiwa kwa dhamana huku wawili wakitakiwa kubaki.

Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji.

Mwalimu amesema Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wamebaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.

Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.

Dk Mashinji ameeleza kuwa viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo akiwemo mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamepata dharura.

Hata hivyo,  Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
Share:

Fatma Karume Ajitosa Kumrithi Tundu Lissu Urais TLS

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.

Lissu, ambaye aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo.

Kwa mujibu wa sheria mpya, Lissu hataweza kugombea tena nafasi hiyo kwani kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote  cha siasa, kuongoza chama hicho.

Katika kinyang’anyiro hicho, Fatma atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi huku nafasi ya umakamu wa rais ikiwa na mgombea pekee, Rugemeleza Nshalla na Mweka Hazina akiwa Sadock Magai.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dk. Kibuta Ongwamuhana, uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.

Wakizungumzia uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma ushindi wa kishindo kutokana na kuwa na kariba inayofanana na Lissu.

“Fatma atashinda kwa sababu anapenda mtu mwenye ‘tension’ na ni mtu mwenye kujiamini anaweza akaitetemesha serikali na wanasheria wanapenda hivyo,” amesema mawakili wa kujitegemea ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Wakili mwingine alisema ingawa sheria hiyo inamkataza Lissu kugombea ambapo walipanga kumchagua tena mwaka huu lakini Fatma anaweza kuziba pengo la Lissu.
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>