• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Waziri Ummy Awashauri Wananchi Kwenda Vituo Vya Tiba Haraka Pindi Wanapogundua Dalili Za Ugonjwa Wa Dengue

WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.

Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA jana  jijini Dar es salaam.

“Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo Wizara inashauri kuwa wananchi wasiwe na hofu, bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba " alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo basi wananchi wanaaswa kuwa, wakipata homa wahakikishe kuwa wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au Dengue, au sababu nyingine, ili hatua stahiki zichukuliwe.

Waziri Ummy amesema kuwa ili kujikinga na ugonjwa huo ni lazima Kuangamiza mazalio ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo pamoja na Kujikinga na kuumwa na mbu kwa  kuvaa nguo ndefu muda wote hasa nyakati za mchana.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa Wizara itaendelea Kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa nchi nzima kwa kutumia mfumo uliopo wa ukusanyaji wa taarifa (IDSR), ambapo tunaendelea kupata taarifa za kila siku juu ya mwenendo wa ugonjwa huu na Kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari.

Mbali na hayo Waziri Ummy amesisitiza kuwa  hakuna vikwazo vyovyote vilivyowekwa kwa ajili ya wasafiri wanaoingia na wanaotoka nchini na  Wizara itaendelea kushirikiana na wadau na sekta mbalimbali katika kufuatilia na kudhibiti ugonjwa huo.

Homa ya Dengue ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vinavyoenezwa na mbu wa aina ya Aedes ambao ni weusi wenye madoa madoa meupe yenye kung’aa.
NA WAMJW-DAR ES SALAAM.
Share:

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Waziri Wa Ulinzi Wa Israel Ikulu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 22 Machi, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Ulinzi wa Israel Mhe. Avigdor Lieberman Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Noah Gal Gendler, viongozi wakuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Polisi.

Katika mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Lieberman kwa kuitembelea Tanzania na amemhakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira ya dhati ya kuukuza zaidi na kuuimarisha uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Israel.

Mhe. Rais Magufuli ametaka makubaliano ya ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika maeneo mbalimbali yakiwemo ulinzi na usalama, mafunzo na masuala ya kiuchumi yatiwe saini haraka ili utekelezaji uanze mara moja.

“Tanzania na Israel ni marafiki wa miaka mingi, nataka kuona urafiki wetu unakuwa zaidi, nawakaribisha wawekezaji kutoka Israel kuja kuwekeza katika kilimo, madini na gesi na pia kuwepo ndege za moja kwa moja kutoka Israel hadi Dar es Salaam na Kilimanjaro ili kukuza utalii” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemuomba Mhe. Lieberman kumfikishia ujumbe Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu wa kumualika kutembelea Tanzania na pia kuanzisha ofisi ya ubalozi hapa nchini badala ya kutumia ofisi za ubalozi zilizopo Nairobi nchini Kenya.

Kwa upande wake Mhe. Avigdor Lieberman amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumkaribisha na kufanya nae mazungumzo na pia amemhakikishia kuwa Israel imejipanga kuongeza uhusiano na ushirikiano wake na Tanzania katika maeneo yote ya makubaliano pamoja na kusaidia kilimo na usindikaji wa chakula.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
22 Machi, 2018
Share:

Viongozi Wakuu CHADEMA Waripoti tena Polisi

Viongozi wanne wa Chadema wamewasili Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu Dk  vicenti Mashinji.

Viongozi hao ambao  wamewasili Polisi kwa ajili ya kuitikia wito ni pamoja na manaibu katibu John Mnyika na Salum Mwalimu pamoja na Mwenyekiti wa Kanda ya Serengeti John Heche.

 Wakili wao Fredrick Khiwelo amesema wengine wako njiani akiwamo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Aikaeli Mbowe.

Awali Mbowe  ambaye pia ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai kwa Taifa Leo tarehe 22 Machi 2018, ametoa waraka wa kuitwa Polisi yeye na viongozi wenzake.

Katika waraka huo Mbowe amesema kwamba kuna taarifa pia ya  kumuunganisha  Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa (Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa) na Mjumbe wa Kamati Kuu katika shauri hili.

Updates: Mbowe, Mwalimu Wameachiwa Kwa Dhamana......, Heche na Mnyika washikiliwa, Mdee na Matiko wanasakwa..


Viongozi watatu  wa Chadema walioripoti Kituo Kikuu cha Polisi wakiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Vicent Mashinji wameachiwa kwa dhamana huku wawili wakitakiwa kubaki.

Viongozi walioachiwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar), Salum Mwalimu na Dk Mashinji.

Mwalimu amesema Naibu Katibu Mkuu (Bara), John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Serengeti, John Heche wamebaki polisi kwa maelezo kuwa wamekuwa wakikwepa taratibu za dhamana.

Heche na Mnyika hawakuripoti polisi Machi 16, 2018 huku chama hicho kikieleza kuwa moja ya sababu ya wabunge hao kutoripoti ni kutokana na kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge mjini Dodoma.

Dk Mashinji ameeleza kuwa viongozi wengine wa chama hicho waliotakiwa kuripoti polisi leo akiwemo mbunge wa Kawe, Halima Mdee wamepata dharura.

Hata hivyo,  Jeshi la Polisi limetoa amri kuwa Wabunge hao, Halima Mdee na Ester Matiko wakamatwe popote walipo na kufikishwa Polisi kwa mahojiano.
Share:

Fatma Karume Ajitosa Kumrithi Tundu Lissu Urais TLS

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.

Lissu, ambaye aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo.

Kwa mujibu wa sheria mpya, Lissu hataweza kugombea tena nafasi hiyo kwani kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa chama chochote  cha siasa, kuongoza chama hicho.

Katika kinyang’anyiro hicho, Fatma atachuana na Godwin Mwapongo, Godfrey Wasonga na Godwin Ngwilimi huku nafasi ya umakamu wa rais ikiwa na mgombea pekee, Rugemeleza Nshalla na Mweka Hazina akiwa Sadock Magai.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uteuzi wa chama hicho, Dk. Kibuta Ongwamuhana, uchaguzi wa rais utatanguliwa na viongozi wa kanda utakaofanyika kila mkoa kuanzia Machi 27, mwaka huu.

Wakizungumzia uchaguzi huo baadhi ya mawakili wamesema wanamtabiria Fatma ushindi wa kishindo kutokana na kuwa na kariba inayofanana na Lissu.

“Fatma atashinda kwa sababu anapenda mtu mwenye ‘tension’ na ni mtu mwenye kujiamini anaweza akaitetemesha serikali na wanasheria wanapenda hivyo,” amesema mawakili wa kujitegemea ambaye hakutaka jina lake litajwe.

Wakili mwingine alisema ingawa sheria hiyo inamkataza Lissu kugombea ambapo walipanga kumchagua tena mwaka huu lakini Fatma anaweza kuziba pengo la Lissu.
Share:

DAR ES SALAAM: TPDC YAKANUSHA TAAARIFA ZA KUFUNGWA KIWANDA CHA SARUJI CHA DANGOTE

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) mapema leo limewataka wananchi kupuuza taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kiwanda cha saruji cha Dangote mkoani Mtwara kimefungwa.
Taarifa kutoka kitengo cha mawasiliano cha shirika hilo imesema taarifa hiyo inayoendelea kusambazwa ni ya mwaka 2016 hivyo imeshapitwa na wakati kwani kiwanda hicho kinaendelea na zoezi la usimikaji wa mitambo yake ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia na kazi hiyo inatarajiqa kumalizika mwezi ujao april mwaka huu.
Aidha,taarifa hiyo imesema Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini(TPDC) tayari lilishatimiza makubaliano yote ikiwemo mauzo ya gesi asilia pamoja na ujenzi wa mitambo ya kusafirishia gesi asilia hadi kwenye mitambo ya kuzalisha umeme ya kiwanda hicho tangu mwaka jana 2017.
Kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo mkoani Mtwara mwaka 2016 kimewahi kuripotiwa kuingia mgogoro na TPDC kwa Kile kilichoelezwa kushindwa kukubaliana na shirika hilo juu ya mauzo ya gesi asilia na kupigwa marufuku kwa kiwanda hicho kutoingiza makaa ya mawe kutoka Afrika Kusini na kutakiwa kutumia ya Liganga ambayo kilidai yapo chini ya kiwango na bei ghali.
Share:

Matumizi Mabaya Ya Umeme, Chanzo Cha Moto Katika Mabweni.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeeleza kuwa uchunguzi wa matukio ya moto katika mabweni ya shule mbalimbali, umebaini kuwa ni kutokana na matumizi mabaya ya umeme yanayofanywa na wanafunzi kwa kujiunganishia nyaya za umeme wenyewe bila kuwa na weledi.
Na Swahili Times.
Share:

Muhimbili Yakabidhiwa Msaada Wa Vifaa Tiba.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeikabidhiwa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 25, kutoka kwa Shirika la Australia Tanzania Society
Mkurugenzi wa Shirika hilo, James Chialo amekabidhi msaada huo jana Jumanne Machi 20, kwa Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji MNH, Dk. Julieth Magandi.
Baada ya kupokea msada huo, amesema unajumuisha vitanda vya wagonjwa, mashuka, ‘stand’ za kusimamishia dripu na viti maalum vya wagonjwa vifaa ambavyo vimekuja wakati mwafaka ambapo Muhimbili inaendelea kuboresha huduma zake.
“Tunashirikiana nao kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ikiwamo kutuunganisha na madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia na hivi karibuni ndani ya mwaka huu tutaanzisha kozi ya ‘plastic surgery’ katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas),” amesema.
Aidha, Mkurugenzi wa Shirika hilo, James Chialo ameyashauri mashirika mengine kuwa na moyo wa kujitolea kwa jamii.
“Kutoa ni moyo, sisi tupo tayari kuendelea kujitolea kusaidia jamii, hivi tunavyoongea madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia wapo mkoani Mwanza ambapo watafanya upasuaji kwa watoto waliozaliwa na tatizo la mdomo sungura,” amesema.
Share:

RAIS MAGUFULI AWAHURUMIA WAFANYABIASHARA WENYE MADENI SUGU, ATOA AGIZO KWA WAZIRI FEDHA, TRA

Rais John Magufuli amewataka wafanyabiashara wenye madeni sugu ya kodi kufanya mazungumzo na Wizara ya Fedha pamoja na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ili waweze kupata punguzo la madeni wanayodaiwa.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo katika Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dkt. Magufuli amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango kuwangalia wafanyabiashara hao kwa jicho la kibinadamu na kwamba asipotumia njia hiyo wafanyabishara hao wanaweza kufilisika iwapo watalipisha ffedha zote wanazodaiwa.
“Mnaodaiwa kwa miaka ya nyuma nendeni mkazungumze na wizara ya fedha, najua kuna kipengele kinaweza kuwapunguzia, wapo watu wanadaiwa zaidi ya bilioni 400, waziri wa fedha muwe na human ground la sivyo mtawafilisi wafanyabiashara, mkiwafilisi mtakusanya wapi kodi, Nawaachia wizara ya fedha na TRA muliangalie hili” amesema na kuongeza.
Katika hatua nyinge, Rais Magufuli ameiagiza TRA kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kodi ili kuwavutia wafanyabiashara, huku akiwataka wafanyabiashara hao kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Nilizungumza na watendaji wa TRA na wizara ya fedha, TRA niliwambia tunategemea wafanyabisahara ikitokea umewavuruga utakusanya wapi kodi, inatakiwa ujenge mazingira ya kuwavutia wafanyabiashara.”
Share:

DAR ES SALAAM.Serikali Yatenga Shilingi Bilioni 5 Kwa Ajili Ya Kununua Mashine Nyingine Ya Kupima Vipimo Vya TB

SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini jana jijini Dar es salaam.

“Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka  vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure.

Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka.

Waziri Ummy alisema kuwa takribani  watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016.

Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali za  ,Kairuki, Agakhan,  Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .

Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara.

NA WAMJW
Share:

KIGOMA: Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba apata Ajali Kigoma

Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.
 
Kamanda  Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.

Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.

Kamanda Otieno aliongeza kwwa kutoa tahadhari kufuatia  Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.

Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>