Muhimbili Yakabidhiwa Msaada Wa Vifaa Tiba.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeikabidhiwa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 25, kutoka kwa Shirika la Australia Tanzania Society
Mkurugenzi wa Shirika hilo, James Chialo amekabidhi msaada huo jana Jumanne Machi 20, kwa Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji MNH, Dk. Julieth Magandi.
Baada ya kupokea msada huo, amesema unajumuisha vitanda vya wagonjwa, mashuka, ‘stand’ za kusimamishia dripu na viti maalum vya wagonjwa vifaa ambavyo vimekuja wakati mwafaka ambapo Muhimbili inaendelea kuboresha huduma zake.
“Tunashirikiana nao kwa zaidi ya miaka mitatu sasa ikiwamo kutuunganisha na madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia na hivi karibuni ndani ya mwaka huu tutaanzisha kozi ya ‘plastic surgery’ katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas),” amesema.
Aidha, Mkurugenzi wa Shirika hilo, James Chialo ameyashauri mashirika mengine kuwa na moyo wa kujitolea kwa jamii.
“Kutoa ni moyo, sisi tupo tayari kuendelea kujitolea kusaidia jamii, hivi tunavyoongea madaktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia wapo mkoani Mwanza ambapo watafanya upasuaji kwa watoto waliozaliwa na tatizo la mdomo sungura,” amesema.
RAIS MAGUFULI AWAHURUMIA WAFANYABIASHARA WENYE MADENI SUGU, ATOA AGIZO KWA WAZIRI FEDHA, TRA
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo katika Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara, uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dkt. Magufuli amemtaka Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango kuwangalia wafanyabiashara hao kwa jicho la kibinadamu na kwamba asipotumia njia hiyo wafanyabishara hao wanaweza kufilisika iwapo watalipisha ffedha zote wanazodaiwa.
“Mnaodaiwa kwa miaka ya nyuma nendeni mkazungumze na wizara ya fedha, najua kuna kipengele kinaweza kuwapunguzia, wapo watu wanadaiwa zaidi ya bilioni 400, waziri wa fedha muwe na human ground la sivyo mtawafilisi wafanyabiashara, mkiwafilisi mtakusanya wapi kodi, Nawaachia wizara ya fedha na TRA muliangalie hili” amesema na kuongeza.
Katika hatua nyinge, Rais Magufuli ameiagiza TRA kuweka mazingira rafiki ya ulipaji kodi ili kuwavutia wafanyabiashara, huku akiwataka wafanyabiashara hao kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
“Nilizungumza na watendaji wa TRA na wizara ya fedha, TRA niliwambia tunategemea wafanyabisahara ikitokea umewavuruga utakusanya wapi kodi, inatakiwa ujenge mazingira ya kuwavutia wafanyabiashara.”
DAR ES SALAAM.Serikali Yatenga Shilingi Bilioni 5 Kwa Ajili Ya Kununua Mashine Nyingine Ya Kupima Vipimo Vya TB
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya imetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kununua mashine za kupima vipimo vya ugonjwa wa kifua kikuu katika zahanati na vituo vya afya nchini.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa uzinduzi wa dawa za kutibu ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa watoto kuanzia umri wa miaka 14 kushuka chini jana jijini Dar es salaam.
“Serikali imadhamiria kupambana na ugonjwa wa Kifua Kikuu hivyo tumetenga shilingi bilioni 5 kwa ajili ya kuongeza mashine nyingine za kufanya uchunguzi kwa haraka vya ugonjwa wa Kifua Kikuu zinazoitwa Genexpert ” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy alisema kuwa marufuku kwa watoa huduma kutoa matibabu ya Kifua Kikuu kwa gharama yoyote kwani huduma hiyo ni bure.
Aidha, Waziri Ummy alisema kuwa ni marufuku kwa waganga wa kienyeji kuwashikilia wagonjwa wa Kifua kikuu na badala yake wawaruhusu waende hospitali kwa ajili ya msaada wa haraka.
Waziri Ummy alisema kuwa takribani watu laki moja na 60 wana maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu kwa makadirio ya mwaka 2016.
Sambamba na uzinduzi wa dawa hizo Waziri Ummy amegawa mashine nyingne za Genexpert kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wa makohozi ili kugundua kuna maambukizi au hapana kwa hospitali za ,Kairuki, Agakhan, Regency , TMJ na Indumandal ambazo kila mashine moja inagharimu shilingi milioni 34 .
Aidha Waziri Ummy ametoa rai kwa wazazi na walezi wa watoto kwenda hospitali mara wanapoona dalili moja wapo ya TB ikiwemo kuumwa mara kwa mara kwa muda wa wiki mbili, kukosa furaha, mtoto kulia mara kwa mara, kupungua uzito , kuchelewa kukua na kikohozi cha mara kwa mara.
NA WAMJW
KIGOMA: Mkurugenzi wa TBC, Dkt. Ayub Rioba apata Ajali Kigoma
Watu wawili wamefariki Dunia wilayani Kasulu mkoani Kigoma kufuatia ajali ya gari la Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC Dkt. Ayub Rioba, lililokuwa likitokea wilayani Kibondo kwenda Kigoma Mjini.Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma, Kamishna Msaidizi Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababisha gari kuacha njia na kuwagonga waenda kwa miguu watatu.
Kamanda Otieno aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni watembea kwa miguu wawili, waliofahamika kwa majina ya Teresia Mpoma (55) mkulima na Mkazi wa Nyakitonto, Yuster Masharubu (55) mkazi wa Nyakitonto na Majeruhi mmoja aliefahamika kwa jina la Diana Shedrack (10) mwanafunzi shule ya Msingi Nyakitonto, ambae hali yake ilielezwa kuwa mbaya huku akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Kasulu.
Amesmea Gari la Mkurugenzi Mkuu wa TBC lililopata ajali lenye namba za usajili STK 8769 lilikuwa na abiria wawili akiwemo mkurugenzi mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba na Mkuu wa kanda ya magharibi TBC Mhandisi Zebron Mafuru ambao wote wametoka salama na hali zao ni nzuri.
Kamanda Otieno aliongeza kwwa kutoa tahadhari kufuatia Chanzo cha ajali hiyo kuwa ni utelezi unaotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo,hivyo amewaomba madereva kuendesha magari kwa umakini kutokana na ubovu wa barabara hiyo na kuzingatia sheria za barabarani.
Dkt. Rioba yuko katika ziara ya kukagua vituo vipya vya matangazo vilivyojengwa katika maeneo ya mipakani.
DAR ES SALAAM: Rais Magufuli Katengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)
Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Blandina Nyoni na kuivunja bodi hiyo. katika taarifa hiyo iliyotolewa leo ikulu jijini dar es salaam haijaeleza sababu za kuvunja Bodi hiyo na kutengua nafasi ya Mkurugenzi huyo. Uteuzi wa Mwenyekiti na bodi nyingine utafanyika baadaye.
DAR ES SALAAM: Mei Mosi Kitaifa Kufanyika Jijini Arusha....Mgeni Rasmi Anatarajiwa Kuwa Rais Magufuli
Chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (Tuico), kimeanza maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei mosi), yanayotarajiwa kufanyika kitaifa mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Tuico taifa, Paulo Sangeze, alisema, mgeni rasmi katika maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli.
Akizungumza katika semina ya kuelimisha na kubadilishana uzoefu, iliyowashirikisha viongozi wa matawi mbalimbali ya Tuico mwishoni mwa wiki, iliyofanyika jijini hapa, Mwenyekiti wa Tuico taifa, Sangeze, alisema Shirikisho la Vyama vya Huru vya Wafanyakazi nchini (Tucta), limekiteua chama chao kuwa mratibu wa shughuli zote za Mei mosi kwa mwaka huu.
Alisema baada ya kupewa fursa hiyo wanafanya vikao vya maandalizi na tayari wamepanga maadhimisho hayo kwa mwaka huu, yatafanyika mkoani Arusha katika Uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid.
Katibu wa Tuico, Boniface Nkakatisi, alisema maandalizi hayo yanaenda na mialiko ya wageni watakaohudhuria ikiwamo wafanyakazi mbalimbali nchini, wanachama wa Tuico, mabalozi kutoka nchi mbalimbali duniani.
DAR ES SALAAM: RC Makonda atoa taarifa kuhusu tukio la kushambuliwa kwa afisa ubalozi wa Syria
Kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar Es Salaam nimeshtushwa na taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Afisa Ubalozi wa Syria ameshambuliwa na kuporwa kiasi kikubwa cha fedha leo mchana Jijini Dar Es Salaam. Taarifa hiyo imeenda mbali zaidi na kusema kwamba Dar Es Salaam sio salama na kueleza watu wawe makini zaidi.
Nawaomba sana wananchi wa Dar es Salaam muendelee kuwa watulivu na mkielewa kwamba Mkoa wenu ni salama salama sana. Vyombo vya usalama vinalifanyia kazi tukio hili na taarifa za awali nilizopokea zinaonyesha tukio hili linaweza kuwa limepangwa na watu wa ndani. Tunafuatilia zaidi kujua kwa nini Afisa huyo hakuomba ulinzi wa polisi akiwa amebeba kiasi hicho kikubwa cha fedha na pia kwa nini dereva wake amekimbia.
Kwa hali ilivyo mpaka sasa kuna uwezekano ikawa ni tukio la kupangwa na watu wa ndani. Hatutaruhusu watu wachache wachafue taswira ya Mkoa wetu.
Uchunguzi ukifikia sehemu nzuri taarifa rasmi itatolewa na vyombo vyetu vya usalama. Ulinzi na usalama wa wananchi wetu ni muhimu sana.
Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa Dar Es Salaam
IRINGA: Hatimaye Abdul Nondo amefikishwa Mahakamani
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amesafirishwa usiku wa kuamkia leo Machi 21, 2018 kupelekwa mkoani Iringa.
Taarifa zilizotolewa na wakili wake, Jebra Kambole leo Jumatano Machi 21, 2018 zinaeleza kuwa sasa Nondo yupo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.
Nondo anadaiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018 na siku inayofuata akaonekana mjini Mafinga, wilayani Mufindi, Iringa ambako alishikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo na baadaye kurejeshwa Dar es Salaam.
Tangu akamatwe Nondo hajawahi kuzungumza na wakili wake wala mtu yeyote wa karibu yake jambo ambalo limekuwa likipingwa na watetezi wa haki za binadamu.
Jana, Jebra alisema kuwa wamefungua kesi kwa ajili ya kuiomba mahakama mambo matatu, kwanza kumpa dhamana Nondo, pili kutoa amri ya kuwapa mawakili haki ya kuonana na Nondo na kingine ni kuitaka mahakama itamke mwanafunzi huyo wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) ameshikiliwa kinyume cha sheria.
MTWARA: Madiwani watatu wamuunga Mkono Rais Magufuli kwa kuhama chama
Madiwani Watatu wa
kata za Nalingu Shaibu Mtavanga
(CUF), Muungano HASSAN HASSAN LIKUTU (CHADEMA) na nanguruwe ERISHA WALLA (CUF,
) kutoka halmashauri ya mtwara vijijini Mkoani MTWARA, wamejiuzulu nyadhifa zao
na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM) .
Madiwani hao kwa
pamoja wameamua kujiunga na chama cha mapinduzi (ccm) ili kuunga mkono juhudi
za Rais John Pombe Magufuri.
Wakiongea wa Nyakati
tofauti wamethibitisha kuwa wameamua wenyewe bila kushurutishwa wala kurubuniwa
na mtu yeyote.
Katibu mwenezi wa wilaya Mtwara vijijini SELEMANI SANKWA amethibitisha kuwapokea
madiwani hao mbele ya waandishi wa habari hapo jana.













