• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatahadharisha mvua kubwa mikoa 11

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi vya mvua kubwa vinavyotarajiwa kuendelea katika maeneo ya mikoa 11 nchini.

TMA imetaja mikoa itakayoathirika na mvua hizo ni Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro, Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa na Njombe.

Taarifa iliyotolewa leo na mamlaka hiyo inabainisha kuwa kuanzia leo Machi 12 hadi 13 ,2018 kunatarajiwa vipindi vya mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24.

“Hali hii inatokana na kuendelea kuimarika kwa ukanda wa mvua, wakazi wa maeneo yaliyotajwa wanatakiwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa na tahadhari zinazotolewa, TMA inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejesho kila itakapobidi,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Share:

Rais Magufuli kuongoza mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC)

Baraza  la Taifa la Biashara (TNBC) limeandaa Mkutano wa 11 wa Baraza ambao utaongozwa na Rais John Magufuli wiki hii.

Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Raymond Mbilinyi, Amesema kuwa mkutano huo unaonyesha dhamira iliyonayo serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ya kuweka mazingira bora ya kufanya biashara na uwekezaji nchini.

“Mkutano huu wa Baraza ni muhimu sana sekta za umma na binafsi kwani unatoa fursa kwa pande mbili hizi kujadiliana namna bora ya kujenga mazingira ya biashara na kuvutia uwekezaji zaidi kwa manufaa ya Watanzania,” alisema Mbilinyi.

Alisema mkutano utafanyika tayari kukiwa na mafanikio makubwa chini ya awamu ya Tano ambapo viwanda zaidi 3,500 vikiwa vimeshaanzishwa katika kipindi kifupi tu cha uongozi wa Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza.

“Huu utakuwa ni mkutano wake wa pili kuuongoza kama Mwenyekiti wa Baraza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Awamu ya Tano. Mkutano wake wa kwanza umeleta mafanikio mengi katika sekta za umma na binafsi,” alisema na kuwa utafanyika Jumapili.

Mbilinyi alisema serikali ya awamu ya tano imesimamia mabadiliko mbalimbali yaliyolenga kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuhamasisha ujenzi wa uchumi wa kati na viwanda.
Share:

GEITA: Mwili wa marehemu watelekezwa nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa

Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Nyakabale wilayani Geita wametelekeza mwili wa marehemu nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa huu, Elias Ndarawa.

Ndarawa anatuhumiwa kutoshughulikia tukio la Zacharia Shaban kupigwa na polisi jamii hadi kufa.

Wananchi hao waliubeba mwili wa Zacharia na kuulaza kwenye kitanda cha mwenyekiti huyo.

Majaliwa Shaban ambaye ni ndugu wa marehemu Zacharia amesema leo Machi 12,2018 kwamba nduguye alipigwa Machi 5,2018 akiwa eneo la Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM) akiokota mabaki ya mawe ya dhahabu maarufu magwangala.

Amesema Zacharia alipelekwa polisi alikokaa kwa siku sita na aliporudi uraiani hali yake ilikuwa mbaya.

Majaliwa amesema nduguye alipelekwa hospitali alikofariki dunia Jumamosi Machi 10,2018 na hadi sasa hakuna kiongozi aliyefika kwenye msiba huo wala kutoa kauli yoyote.

Mkazi wa mtaa huo, Johnson John amesema hawapo tayari kuzika hadi Serikali itakapotoa kauli kuhusu hatima ya maisha yao kwa kuwa polisi jamii wamekuwa wakiwapiga na kuwajeruhi.

Jana, Machi 11,2018 wananchi walivamia eneo la kituo cha polisi jamii kilichopo mtaa wa Manga na kukichoma moto kwa madai kwamba wamempiga na kumuua Zacharia
CHANZO: MPEKUZI
Share:

DODOMA: Spika Job Ndugai apangua kamati za Bunge

Spika Job Ndugai amefanya uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu za Bunge.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Machi 12,2018 inasema Spika amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa Ibara ya 96 ya Katibu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa hiyo imesema ibara hiyo imeweka wazi kwamba, Kanuni za Kudumu za Bunge zinafafanua muundo wa shughuli za Kamati za Bunge.

“Kwa msingi huo Kanuni ya 118 ya Kanuni za kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 imeweka Kanuni za Kudumu za Bunge zenye muundo na majukumu mbalimbali kama yanavyofafanuliwa katika nyongeza ya nane. Uteuzi wa wabunge kwenye kamati mbalimbali unaonekana utaratibu katika Kanuni ya 116.”

“Kanuni ya 116(1) inaweka utaratibu kwamba, ujumbe kwenye Kamati za Kudumu za Bunge utadumu mpaka mwisho wa Mkutano wa Kumi wa Bunge ambao ni nusu ya kwanza ya maisha ya Bunge,” anasema Spika Ndugai.

Katika uteuzi huo, wajumbe mbalimbali wamerejea katika kamati zao, wengine wakibadilishwa huku baadhi ya wenyeviti waliokuwa wakiongoza baadhi ya kamati wameondolewa.

 “Kwa mamlaka niliyopewa na Kanuni ya 115(3) na kwa kuzingatia vigezo vilivyoanishwa katika Kanuni ya 116(5) nimefanya uteuzi mpya wa ujumbe katika Kamati za Kudumu za Bunge. Wajumbe wa kila kamati wanawajibika kuchagua mwenyekiti na makamu mwenyekiti kwa mujibu wa Kanuni ya 116(10) kuwa viongozi wao,” amesema.
Share:

DAR ES SALAAM: Maria Tsarungi kumburuza mahakamani mhariri wa gazeti la Tanzanite


Mjasiriamali/Mwanahabari na Mkurugenzi wa Compass Communications, Maria Sarungi amefungua kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Mhariri wa Gazeti la Tanzanite na Mwanasheria Cyprian Musiba kwa kumkashifu na kuchafua jina lake kupitia mkutano wake na Waandishi wa Habari uliyofanyika tarehe 25 Februari, 2018.

Barua hiyo iliyotolewa na Mwanasheria wa Maria Sarungi, Benedict Alex Ishabakaki imeeleza kuwa mteja wake alitajwa na gazeti la Tanzanite toleo Namba 50 lililotoka Februari 26, 2018 kuwa ni moja ya watu hatari kwenye usalama wa taifa.

Kwa upande mwingine, barua hiyo imeitaka Blog ya Dar24 kufuta habari hiyo na kuomba radhi hadharani kwa kitendo cha kuandika habari hiyo yenye lengo la kumfedhehesha mteja wao.

CHANZO: MUUNGWANA

Share:

MWANZA: Ekari tatu za bangi zateketezwa kwenye hifadhi


Zaidi ya ekari tatu za bangi zimeteketezwa kwenye msitu wa hifadhi ya Maisome iliyopo katika kisiwa cha Maisome Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza .

Kwa mujibu wa Katibu Tawala Wilaya ya Sengerema, Alan Mhina, bangi hiyo ilikuwa imelimwa kwenye sehemu ya msitu huo wenye ukubwa wa hekta 12,800, na kwamba, iliteketezwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya katika operesheni maalum ya kukomesha kilimo cha zao hilo haramu.

Kwa upande wake, Meneja Wakala wa Misitu Tanzania, TSF, Wilaya ya Sengerema, Bw. Urio Jeremiah, amesema, operesheni hiyo pia imelenga kukomesha shughuli nyingine za kibinadamu zinazotishia uhai wa hifadhi hiyo.

Share:

DAR ES SALAAM: Serikali yaanza mazungumzo na kampuni ya Bharti Airtel


 Kamati Maalum iliyoundwa na Rais Dkt. Magufuli na Kampuni ya Bharti Airtel yameanza rasmi leo tarehe 12 Machi, 2018 Jijini Dar es Salaam. 

kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na kurugenzi ikulu lengo ni kuweka mazingira safi ya mawasiliano kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bharti Airtel

Share:

MAREKANI: Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW umeanza leo


Mkutano wa 62 wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani, CSW umeanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Maudhui ya mkutano huo wa wiki mbili ni changamoto na fursa katika kufikia usawa wa jinsia na kuwezesha wanawake na wasichana waishio vijijini.

Akizungumza katika ufunguzi wa kamisheni hiyo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres amesema huu ni wakati muhimu kwa kuhakikisha madaraka na usawa unamfikia mwanamke na hususani wa Kijijjini ambaye amekuwa akisahaulika

Naye mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wanawake, UNWomen, Phumzile Mlambo-Ngucka amesema maudhui hayo yanazingatia ukweli kwamba kampeni nyingi za kumkwamua mwanamke na msichana zinaangazia zaidi wale waishio mijini.

“Kwa msing iwa kutokumuacha nyuma mtu yeyote ni kuhakikisha hakuna anayeachwa nje. Moja ya michango mikubwa zaidi ya kufanikisha ajenda 2030 ni kuondoa ukosefu wa usawa unaokabili wanawake na wasichana waishio vijijini, ” amesema Bi. Mlambo-Ngucka.

Wakati wa mkutano mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwemo vikwazo vinavyokabili wanawake wa vijijini na mwelekeo bora ili wajikwamue.

Zaidi ya washiirki 8000 watahudhuria wakiwakilisha mashirika zaidi ya 1200 ya kiraia. Halikadhalika viongozi wa serikali za nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na vijana.

Share:

DAR ES SALAAM: Wakili ashindwa kuonana na Abdul Nondo


Mwanasheria Jebra Kambole na Wakili wa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo amefunguka na kusema kuwa mpaka sasa ameshindwa kuonana wala kuongea na mteja wake huyo ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi.

Wakili huyo amesema kuwa amejaribu kufika ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili kujua hali ya mteja wake pamoja na kuweza kuongea naye lakini ameshindwa.

"Mpaka sasa sijafanikiwa kuzungumza wala kumuona kwa sababu mara ya mwisho wakati tunafanya mazunguzo na DCI ambaye ana mamlaka juu ya hilo kwa sababu Abdul Nondo alikuwa anashikiliwa ofisini kwake mpaka dakika ya mwisho, tulipokwenda ofisini kujaribu kumuona akasema sisi huyu mtu tunamshikilia kama kama mlalamikaji lakini siyo kama mtuhumiwa kwa hiyo nyinyi kama Mawakili hamtakiwi kumhoji ila tukiona kwamba huyu mtu ni mtuhumiwa basi tutawaita muweze kuongea naye na kusikiliza maelezo yake, sisi tulimweleza tunahitaji kumuona ili tuweze kujua afya yake ili tuweze kurejesha mrejesho kwa familia na Watanzia wengine kwa ujumla ambao wanahofia juu ya usalama wake akasema yupo salama" alisema Kombole

Aidha Wakili huyo aliendelea kudai kuwa mpaka sasa Abdul Nondo anashikiliwa kinyume na sheria kwa kuwa sheria ya makosa ya jinai haitoi ruhuusa kwa jeshi la polisi kumshikilia mlalamikaji.

"Anayeshikiliwa ni mtuhumiwa lakini mpaka siku ya leo hajaachiwa kama ni mtuhumiwa kweli kwa sababu mtu ambaye anakwenda kutoa taarifa polisi anaachiwa arudi nyumbani huwezi kushikiliwa huko polisi na kwa kuwa wao wanasema wanamshikilia ana haki ya kupata uwakilishi kwa sababu kwa mujibu wa sheria yetu ya mwenendo wa makosa ya jinai sura namba 20 ya sheria za Tanzania, kifungu cha tano kinasema kwa muda gani mtu atakuwa chini ya dola au polisi, mtu ambaye amewekwa chini tu akiwa hana uhuru wa kwenda anakotaka huyo ina maana yupo chini ya ulinzi kwa hiyo kama upo chini ya ulinzi una haki ya kupata wakili kuweza kuongea naye na kujua nini kinaendelea na hatma yake na kupata fursa ya kuongea na ndugu zake na familia lakini fursa hiyo kwa Nondo haijapatikana kwani saizidi ni zaidi ya masaa 10 yamepita akiwa ameshikiliwa na jeshi la polisi" alisema Kombole

Mbali na hilo Wakili huyo amesema kuwa mpaka sasa wao hawajui Abdul Nondo ameshikiliwa kwa sababu zipi na kusema kuwa kijana huyo ameshikiliwa kinyume na sheria, kinyume cha Katiba, kinyume cha haki za binadam na kinyume na utaratibu wetu kama taifa kiujumla.
CHANZO: EATV
Share:

BURUNDI: Pierre Nkurunzinza atangazwa kuwa kiongozi wa kudumu chama tawala cha CNDD/FDD Burundi

Chama tawala nchini Burundi CNDD/FDD kimemtangaza Rais Pierre Nkurunzinza kama kiongozi mkuu wa kudumu au kiongozi wa milele ndani ya chama hicho.

Uamzi huo umefikiwa baada ya vikao vya siku tatu vya mkutano mkuu wa chama hicho uliofanyika katika eneo la Buye anakozaliwa Bwana Nkurunziza Kaskazini mwa nchi hiyo.

Uamuzi huo pia unachukuliwa wakati Burundi inajiandaa kufanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Rais Nkurunzinza kuendelelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Taaarifa fupi ya chama cha CNDD/FDD imesema vikao hivyo vilinuwia kuimarisha chama tawala na taasisi zake.

Lakini pia chama hicho tawala kimechukua uamuzi wa kumuongezea hadhi na kumpa cheo cha juu Rais Nkurunziza na hivyo kumtangaza kuwa ni kiongozi mkuu wa kudumu ndani ya chama.

Kwenye hafla na makundi ya utamaduni ya chama tawala, katibu mkuu wa CNDD/FDD Bwana Evariste Ndayishimiye aliutangazia umati azimio hilo alolitaka kuwa ni muhimu mno katika uhai wa chama tawala.

Tangazo hili la chama tawala CNDD/FDD kumfanya Rais Nkurunzinza kama Kiongozi Mkuu wa Kudumu linajiri wakati Burundi inajiandaa kwa kura ya maoni kuhusu Marekebisho ya Katiba baadae mwezi Mei. Kati ya mambo mengi katiba hiyo ikipitishwa itamuwezesha Rais Nkurunzinza kuweza kuwania Urais mpaka mwaka wa 2034.

Wadadisi wengi wa siasa za Burundi wanaamini kuwa hatua hii ya chama tawala inanuwia kumalizia mapema mjadala wa mtetezi wa kiti cha Urais kwa niaba ya Chama hicho na kuonyesha mustakabali wa uongozi kabla hata uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2020.

Lakini pia uamzi huo unapeleka ujumbe kwa wafuasi wa CNDD/FDD na haswa viongozi wenye nia pengine ya kuwania nafasi hiyo na hivyo kujaribu kukiepusha chama tawala na mpasuko kama ilivyotokea mwaka wa 2015 katika mzozo kuhusu muhula wa sasa wa Rais Nkurunzinza.

Isitoshe kwa Wachanganuzi wa siasa za bado wanaiona hatua hii ya Rais Nkurunziza kutangazwa Kiongozi wa maisha kama dalili tosha ya jinsi kiongozi huyo alivyokidhibiti chama cha CNDD/FDD.

CHANZO: MUUNGWANA BLOG
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>