• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

DODOMA: Makamu wa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO wafanya mazungumzo kuhusu viwanda

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) Bw. Li Yong.

Katika mkutano huo ambao ulikuwa na lengo ya kujadiliana masuala mbalimbali ya uendelezaji Viwanda nchini Tanzania.

Mkurugenzi huyo amemjulisha Makamu wa Rais kuwa Tanzania ni nchi ya nne kuitembelea tangia ateuliwe .

Aidha katika mazungumzo hayo Mkurugenzi wa UNIDO amesema anajua Tanzania ajenda yao kuu ni uanzishwaji wa Viwanda na alimhakikishia Makamu wa Rais kwamba UNIDO itajitahidi kusaidia ajenda hiyo.

“Kuna umuhimu wa kuzingatia sekta binafsi na viwanda vidogo na vya kati wakati wa uanzishwaji viwanda ili vijana na wanawake wapate ajira,” alisema Mkurungenzi Mkuu wa UNIDO.

Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Yong amesema pia suala la uanzishwaji na Uendelezaji wa Viwanda  ni lazima lizingatie masuala ya upatikanaji wa nishati na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha Mkurugenzi huyo alisifia mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea ndani ya Serikali ya awamu ya tano na kusema UNIDO suala muhimu ni Utekelezaji.

Pia aliupongeza uongozi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania na mashirikiano mazuri na Serikali.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alimhakikishia Mkurungenzi huyo wa UNIDO ushirikiano wa hali ya juu kutoka Serikalini na alimuomba kuipa Tanzania kipaumbele  katika programu yake muhimu itakayochochea maendeleo ya Viwanda ya “Programmes For Country Partnership-PCP”.

Mwisho Kiongozi huyo aliishukuru Tanzania kwa mapokezi mazuri na programu nzuri walizompangia.

Viongozi wengine walioshiriki kwenye mazungumzo hayo ni Waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Philip Mgango pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Augustine Mahiga ambapo pia Waziri wa Viwanda , Biashara na Uwekezaji alitia saini pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNIDO Bw. Li Yong 

Tamko la Kusudio la kuanzisha (Declaration of Intention) Mpango wa UNIDO unaojulikana kama “Programmes For Country Partnership-PCP”  ambapo Makamu wa Rais alishuhudia kusainiwa kwa Tamko hilo,kusainiwa kwa tamko hilo kutarahisisha mchakato wa  wa kukamilika kwa uwasilishwaji wa ombi la Tanzania kuomba iingizwe katika Mpango Maalumu wa UNIDO  ambao ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya Viwanda.

CHANZO: MPEKUZI
Share:

DAR ES SALAAM: Mvua yaleta maafa kwa Jeshi la Polisi


Mvua zilizoambatana na upepo mkali zilizonyesha usiku wa jana zimeacha athari kubwa  kwa Jeshi la Polisi kwa kuharibikiwa na jengo lao la ofisi pamoja na kujeruhiwa askari mmoja.

Akizungumza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni,  ACP Muliro Jumanne Muliro amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema ofisi ndogo iliyopo ndani ya jengo la serikali ya Mtaa wa Goba limeharibika kufuatia kuangukiwa na nguzo ya mnara wa simu kuangukia.

"Askari mmoja amejeruhiwa katika ajali hiyo ila alifanikiwa kukimbizwa katika hospitali  ya Taifa Muhimbili kwa matibabu", amesema Kamanda Muliro.

Mbali na tukio hilo, mvua zilizonyesha usiku wa jana (Machi 07, 2018) zimeweza kuwaathiri pia baadhi ya jamii kwa kuezua paa za nyumba zao na kusababisha kukosa makazi.


Share:

CHATO: Rais Magufuli kuzindua tawi la benki Chato Kesho

Rais John Magufuli kesho Machi 9, 2018 anatarajiwa kuzindua tawi la benki ya CRDB katika jengo jipya lililopo eneo la mlimani mjini Chato mkoani Geita.

Taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa Wilaya ya Chato Shaban Ntarambe, inaeleza kuwa hafla ya uzinduzi wa tawi hilo itaanza saa mbili asubuhi katika eneo lilipo jengo jipya la benki hiyo.

Ntarambe amewataka wananchi wa Chato na maeneo ya jirani kujitokeza kumsikiliza rais na kushuhudia uzinduzi huo ambao unaendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa wananchi.

Baadhi ya wananchi wa mjini Chato wamepongeza juhudi zinazofanywa na wadau wa maendeleo kusogeza huduma karibu na wananchi na kusema Chato ya sasa sio kama ya zamani na kwamba, uwepo wa miundombinu hiyo inafungua maendeleo.

CHANZO: MPEKUZI
Share:

DODOMA: Makamu wa Rais atoa neno siku ya Wanawake duniani

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu amesema ana kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.

Makamu wa Rais amesema kuwa serikali ina sera kuendeleza wanawake,huku akisema kuwa sheria ya ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi.

"Leo katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, Mimi kama mwanamke na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nina kila sababu ya kuzungumza japo kwa kifupi jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na zinazoendelea kuchukuliwa na serikali katika kuimarisha usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini.

"Serikali inayo Sera ya kuendeleza Wanawake, Sheria za ardhi za mwaka 1999 ambazo husimamia haki za wanawake katika kumiliki ardhi.

"Sera ya elimu bure inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano imetoa fursa kwa watoto wengi wa kike kuandikishwa shuleni.

"Kuboreshwa kwa huduma za kijamii kama vile kujengwa zahanati na vituo vya afya na usambazaji wa maji vimempunguzia mwanamke usumbufu na hivyo kumpa muda wa kutosha kufanya shughuli za maendeleo.

"Usambazaji umeme vijijini kwa kiasi kikubwa umesaidia wanawake wengi kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujiingizia kipato.

"Uwezeshaji wa Wanawake kwa kuwapatia asilimia 5 ya mapato ya halmashauri na asilimia 30 ya zabuni za halmashauri kumewawezesha wanawake wengi kufanya biashara na hatimaye kuwa na uhakika wa kipato .

"Serikali kuendelea kuhimiza taasisi za kifedha kutoa mikopo yenye riba nafuu ili kuwawezesha wanawake wengi kunufaika na mikopo hiyo.

"Kurasimisha vikoba pamoja na kuwashawishi wanawake wengi zaidi kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuweza kunufaika na mafao na mikopo itolewayo na taasisi hizo.

"Kauli Mbiu:Kuelekea Uchumi wa Viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake Vijijini."
Share:

IRINGA: Walichokisema Polisi baada ya kupatikana kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) aliyekuwa ametekwa

Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limeeleza kuwa limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama Mwenyekiti wa  Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Omari Nondo alikuwa ametekwa au la ili liweze kuwachukulia hatua za kisheria wote waliohusika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire akiongea na waandishi wa habari ameeleza kuwa bado uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea ili waweze kubaini kama ni kweli ametekwa na kuwakamata wahusika kwa ajili ya kuwachukulia hatua zaidi za kisheria.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa alimefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama alikuwa ametekwa, na kama kweli alikuwa ametekwa tunaahidi kwamba sisi jeshi la polisi tukiwapata watuhumiwa sheria itachukua mkondo wake,” amesema Kamanda Bwire.

Kamanda Bwire ameongeza kuwa pamoja na kufanya uchunguzi, jeshi hilo linapeleleza zaidi ili kujiridhisha kama taarifa iliyotolewa ni ya uongo kwa nia ovu ya kuhamasisha wanafunzi nchini kuleta uvunjifu wa amani, na wakibaini hilo watamchukulia hatua kali za kisheria.

“Aidha tunaendelea kuchunguza kama ametoa tarifa za uongo kwa nia ovu, kwa lengo la kutaka kuhamasisha wanafunzi wenzake ili kuleta uvunjifu wa amani nchini. tutamshughulikia kama wahalifu wengine,” alisema.

Hata hivyo, Kamanda bwire amesema kuwa Abdul anaonekana kuwa na afya njema na hana majeraha yoyote kuashiria kuwa alipigwa au kuteswa.

“Kwa sasa anaonekana hali yake ni nzuri, hana majeraha yoyote, hajapigwa ni mzima wa afya njema. hivyo basi Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kupitia maeneo yote aliyopitia ili tuweze kujua nini kilichomsibu,” alisema Kamanda.

Vile vile aliwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa polisi wakati wa uchunguzi dhidi ya tukio hilo ili waweze kubaini kilichotokea na wahusika waweze kufikishwa mahakamani.

Abdul Nondo (24) ambaye ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo na mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka wa tatu kitivo cha Siasa na Utawala, alisemekeana kupotea katika mazingira ya kutatanisha siku ya Jumanne majira ya kati ya saa 5 na 6 usiku jijini Dar es Salaam na kupatikana jana Jumatano akiwa Mkoani Iringa.
Share:

DAR ES SALAAM: Rais Magufuli atoa neno kifo cha Dkt. Kabourou

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Dkt. Walid Amani Kaburu na kusisitiza kuwa amepokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa.

Dkt. Magufuli ametoa salamu hizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga baada ya kupokea taarifa za kifo cha Dkt. Kabourou aliyekuwa anatibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbuili Jijini Dar es Salaam kilichotokea usiku wa kuamkia leo Machi  07, 2018.
"Kwa masikitiko nimepokea taarifa ya kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma Dkt. Walid Amani Kabourou kilichotokea usiku wa kuamkia leo. Dkt. Walid Amani Kabourou atakumbukwa kwa mchango wake alipokuwa kiongozi katika nyadhifa mbalimbali ndani ya CCM, na alipokuwa Mbunge wa Kigoma Mjini na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki. Natoa pole kwa familia yake, wana CCM wote, wananchi wa Kigoma, ndugu jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu",amesema Rais Dkt. Magufuli.
Pamoja na salamu hizo Dkt. Magufuli ameiombea familia ya marehemu na wote walioguswa na msiba huu kuwa na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi.
NA ISMAEL MOHAMED - EATV
Share:

DAR ES SALAAM: Huyu ndio paka anayeharibu mimba

Daktari wa wanyama nchini Tanzania, Dkt. Obed Kiariro amedai kuna uwezekano mkubwa wa Paka anayefugwa majumbani hupelekea kuharibu ujauzito kwa binadamu endapo mnyama huyo hatopewa matunzo mazuri yanayostahili kwa wakati.

Dkt. Kiariro ameeleza hayo kupitia kipindi cha Supamix kinachorushwa na East Afrika Radio baada ya kuwepo matatizo mengi wanayoyapata jamii ya kike (wanawake) hasa hasa pale wanapokuwa wamebahatika kushika ujauzito na kwa bahati mbaya hutokea kuharibika bila ya kujua sababu za msingi kilichopelekea kupoteza ujauzito wake.
"Kuna ugonjwa tunaita 'toxoplasmosis' kitaalamu ugonjwa huu unatoka kwa Paka ambao unapelekea kutoka kwa mimba 'abortion', kama Paka hawatibiwi vizuri wala kuwepo na matunzo ya aina yeyote basi wanakuwa na ugonjwa huo na matokeo yake wanaambukia wanadamu. Unaweza ukawa na paka nyumbani unamtunza vizuri lakini huwezi kumzuia kwa namna yeyote ile kutokutana na paka wengine wanaozurura mtaani maana wakikutana tu wanaambukizana ugonjwa huo", amesema Dkt. Kiariro.
Mtazame hapa chini Dkt. Kiariro akielezea vizuri namna ya paka anayesababisha kuharibika kwa ujauzito (mimba).
NA ISMAEL MOHAMED - EATV
Share:

DODOMA: Watumishi wa umma walioondolewa kazini kimakosa kurejeshwa

Share:

LHRC wafafanua hoja za NEC dhidi ya tamko la asasi za Kiraia

TAARIFA KWA UMMA
UFAFANUZI WA HOJA ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) DHIDI YA TAMKO LA ASASI ZA KIRAIA


Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimepokea barua Kumb. Na. BA.71/75/01/124 ya tarehe 22 February 2018 kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Ndugu Kailima Ramadhani na kupitia kwa umakini mkubwa hoja za Tume Ya Uchaguzi dhidi ya tamko lililotolewa na umoja wa Asasi Za Kiraia, chini ya Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI, Februari 21, 2018 kuzungumzia hali ya usalama wa raia, haki za binadamu na utawala wa sheria hapa nchini.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kama moja ya asasi zinazounda umoja wa AZAKI hizo kimelazimika kujibu hoja hizo kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika tamko lake lililotolewa Ijumaa Februari 23, 2018 imekituhumu moja kwa moja Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kupitia kwa aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi, Bw. Paul Mikongoti, kwa kutoa tamko lenye tuhuma za kupotosha baadhi ya mambo kupitia tamko hilo la umoja wa AZAKI.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kutanguliza pongezi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kupitia hoja pamoja na mapendekezo yaliyotolewa na asasi za kiraia nchini na hata kutoa kasoro za uwasilishaji wa baadhi ya hoja hizo. 

Hata hivyo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kuikumbusha Tume kwamba, tamko husika halikutolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu bali tamko hilo lilitolewa na Umoja wa AZAKI chini ya Jukwaa la Wakurugenzi wa AZAKI.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilishiriki kwenye tamko hilo kama mwanachama wa AZAKI kwa kutambua wazi kuwa lengo la tamko hilo ni kuimarisha hali ya haki za binadamu na demokrasia nchini na si vinginevyo. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kuitoa wasiwasi Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa hakuna maslahi tofauti wala upotoshaji wa makusudi katika utoaji wa tamko hili.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinakiri kufahamu kwa kina sheria na kanuni zinazoratibu chaguzi na kinatambua kwamba lengo la AZAKI haikuwa kubeza wala kuvunja kanuni hizo bali kutoa mapendekezo kwa ajili ya maboresho ya chaguzi na hatimaye kuimarisha demokrasia nchini Tanzania.

Hata hivyo, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimesikitishwa na kitendo cha Tume ya Taifa ya Uchaguzi kumshambulia moja kwa moja Bw. Paul Mikongoti licha ya ukweli kwamba, Bw. Paul Mikongoti alikiwakilisha Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kama mwanachama wa umoja huo wa AZAKI. 

Kituo kinapenda kuifahamisha Tume kuwa tamko hili la AZAKI lilisomwa na wakurugenzi tofauti maeneo tofauti nchi nzima na hivyo haikuwa busara kwa Tume kumshambulia moja kwa moja Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wala Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa ubinafsi wake.

Ingawa Tume ya Taifa ya Uchaguzi haikuwa sahihi kukituhumu Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Bw. Paul Mikongoti, bado Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeonelea ni busara kufafanua hoja zilizotolewa na umoja wa AZAKI kama ifuatavyo:

1. Kuhusu kituo cha televisheni cha ITV kuadhibiwa na kutakiwa kuomba radhi kwa kurusha habari za kuibwa kwa sanduku la kura

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinapenda kuijuza Tume ya Uchaguzi kuwa kilikubaliana na hoja hii iliyotolewa na umoja wa AZAKI kwa kuzingatia misingi ya uhuru wa vyombo vya habari kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya Katiba Tanzania inayotoa haki kwa kila Mtanzania pamoja na vyombo vya habari kutafuta na kupokea habari mahali popote pale bila kujali mipaka ya nchi.
 
Hata hivyo baada ya kupitia hoja hii kama ilivyofafanuliwa na Tume ya Uchaguzi, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaishauri Tume kuboresha kanuni za usimamizi wa uchaguzi ili kutokuweka mipaka kwa vyombo vya habari kwa kuzingatia kwamba vyombo vya habari vinatoa taarifa kwa maslahi ya umma.

2. Kuhusu mashirika mbalimbali kunyimwa kibali cha uangalizi wa uchaguzi

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilikubaliana na hoja hii kwa kuzingatia malalamiko yaliyotokana na AZAKI ya PACUSO ambao walikiri kupata majibu kutoka Tume kuwa tayari nafasi zimejaa.
Hata hivyo baada ya kupitia hoja hii ya Tume, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaishauri Tume ya Uchaguzi kuboresha utaratibu wa maandalizi kuelekea uchaguzi ili kutoa nafasi kwa asasi zenye lengo la kufanya uangalizi kufurahia haki hiyo bila kuhisi uwepo wa kuzuiliwa. Moja ya maboresho hayo ni kuweka muda wa kutosha wa kutuma maombi na kuweka nguvu katika kufikisha taarifa kwa mashirika na wadau wengine. Kufuatia ukweli kwamba Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ndio asasi pekee iliyopata kibali kutazama uchaguzi huu, hili lilipelekea butwaa kwa umoja wa AZAKI kwa kulinganisha na chaguzi zilizopita.

3. Tume kuweka utaratibu mpya unaowataka watazamaji kuwasilisha taarifa hizo ili zikaguliwe, kuangalia yaliyomo na kuridhiwa na Tume ikiipendeza.

Katika hoja hii, Kituo kinaungana na AZAKI kuhoji umuhimu wa utaratibu ulioanzishwa na Tume mwaka 2015 wa AZAKI kusubiri hadi Ripoti ya awali ya uangalizi iwasilishwe kwa Tume, na Tume kukiri kupokea ripoti hiyo ndipo AZAKI zinazoangalia uchaguzi kuweza kutoa kwa umma taarifa za uangalizi. AZAKI zimeonelea kwamba utaratibu huu unafifisha misingi ya uhuru wa asasi za kiraia katika uangalizi wa uchaguzi.

Utaratibu huu pia umelalamikiwa kwa kuzingatia kuwa Tume haijaweka muda maalumu ambao itatumia kabla ya kukiri kupokea ripoti ya uchaguzi.
 
Utaratibu huu umelalamikiwa na AZAKI kuwa kwa upande mwingine unaondoa dhana ya AZAKI kuwa vyombo huru vya uangalizi wa uchaguzi.

Mwisho Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaishauri Tume ya Uchaguzi kuzishirikisha asasi za kiraia na wadau wengine muhimu katika maboresho ya sheria, kanuni na taratibu zinazoratibu utendaji wa Tume na usimamizi wa chaguzi kwa lengo la kuboresha na kuimarisha demokrasia nchini Tanzania. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaisihi Tume ya Uchaguzi bila kujali madhaifu katika uwasilishaji, kufanyia kazi changamoto zinazoibuliwa na wadau kwa lengo la kujenga Jamii yenye Haki na Usawa.

Imetolewa na;

Naemy Sillayo (Wakili)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji

Share:

DAR ES SALAAM: Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) adaiwa kutoweka Katika mazingira Ya Kutatanisha

Taarifa zilizoenea mchana huu zinadai kuwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo, ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajulikani alipo tangu jana saa sita usiku.

Marafiki za Nondo wamedai alituma ujumbe kwa viongozi wenzake wa TSNP kuwa yuko katika hatari na baada ya kutuma ujumbe huo simu yake ilikuwa ikipokelewa lakini hakuwa akiongea chochote, na baada ya muda alianza kujiondoa kwenye magroup ya WhatsApp.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa viongozi wa TSNP kuhusu Nondo inasema hajulikani alipo wakiwemo wazazi wake.   

Viongozi wa TSNP wamefika Kituo cha Polisi kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM) na  kutoa taarifa za kupotea kwake.

February 18, 2018, Nondo alijitokeza na kuikosoa mienendo ya Jeshi la Polisi na Waziri wa Mambo ya Ndani, na mara ya mwisho kuongea na wanahabari, alishinikiza Waziri  Mwigulu Nchemba ajiuzulu. 

Akizungumza na wanahabari jana March 6 2018, Nondo aliwataka TAHLISO waache kuwa wasemaji wa wizara na serikali na kuwataka wakumbuke majukumu yao mazito ya kusemea wanafunzi wa vyuo vikuu kwa sababu wanalipishwa ada vyuo vikuu.

“TAHLISO ambayo kila chuo kikuu nchini kinatoa ada isiyopungua shillingi laki tano kwa mwaka ili TAHLISO iweze kutetea maslahi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini, imeacha kutimiza wajibu wake wa msingi na badala yake imegeuka kuwa taasisi yenye kusema kwa niaba ya serikali pamoja na kushambulia taasisi ambazo zinatetea maslahi ya wanafunzi nchini ikiwemo TSNP.

“Akwiline alikuwa ni mwanafunzi pia, TSNP ni mtandao wa kutetea wanafunzi, tunayo hayo mamlaka kusemea, kukemea, kushauri na hata kutoa mapendekezo yetu juu ya tukio lolote linaloashiria upotevu wa haki kwa wanafunzi.  TAHLISO wanatoa wapi ujasiri, mamlaka ya kutuzuia TSNP tusitimize wajibu wetu?” alisema Nondo.
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>