 Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ametangaza leo kwamba kuanzia tarehe 1 Machi 2018 kuwa utaanza ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kwamba kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ametangaza leo kwamba kuanzia tarehe 1 Machi 2018 kuwa utaanza ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kwamba kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu.Ukaguzi Magari Binafsi Kuanza tarehe 1 Machi 2018
 Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ametangaza leo kwamba kuanzia tarehe 1 Machi 2018 kuwa utaanza ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kwamba kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ametangaza leo kwamba kuanzia tarehe 1 Machi 2018 kuwa utaanza ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kwamba kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu.
Akizungumza jana na wanahabari, Mh. Masauni alisema kwamba Wamiliki wa magari madogo wanatakiwa kupeleka magari yao katika vituo vya polisi ili yafanyiwe Ukaguzi kama yanastahili kuendelea kuwepo barabarani.
Aidha Mh. Masauni amewaonya maaskari kuhusu zoezi hilo kwa kuwaambia kwamba "Askari yoyote atakayetumia nafasi yake kutoa stika ya gari bila kulifanyia ukaguzi na ilihali halina vigezo vya kupewa stika nataka niwaambie kuwa huu si wakati wake, zama zimebadilika".
Pamoja na hayo Mh. Masauni aliongeza kwamba "Nataka madereva  wa pikipiki ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja".
Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Fortunatus Musilimu alisema katika Ukaguzi wa magari madogo utakaoanza mwezi ujao, mtu atakaekiuka na kukataa kupeleka gari lake kufanyiwa ukaguzi atakamatwa na sheria itachukua mkondo wake.
UGANDA: Makubaliano waliyoyafikia wakuu wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki
 Mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umemalizika jioni  tarehe 23 Februari, 2018 katika hoteli ya Munyonyo mjini Kampala nchini Uganda.
Mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umemalizika jioni  tarehe 23 Februari, 2018 katika hoteli ya Munyonyo mjini Kampala nchini Uganda.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amehudhuria mkutano huo pamoja na Marais wengine Mhe. Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda, Mhe. Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya, Mhe. Salva Kiir Mayardit wa Sudani Kusini na Rais wa Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza amewakilishwa na Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Gaston Sindimwo na Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame amewakilishwa na Waziri wa Miundombinu Mhe. James Musoni.
Mkutano huo umeongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Yoweri Kaguta Museveni na kwa pamoja Waheshimiwa Marais wamemteua Mhe. Jaji Charles Ayako Nyachae kuwa Jaji wa Mahakama ya Awali ya Afrika Mashariki na Mhe. Jaji Faustin Ntezilyayo kuwa Naibu Jaji Mkuu wa Mahakama ya Afrika Mashariki kuanzia tarehe 01 Julai, 2018.
Pia wameamua Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa na Naibu Makatibu Wakuu wawili badala ya mapendekezo ya kuwa na Naibu Makatibu Wakuu watano.
Aidha, wakuu wa nchi wamezindua mkakati wa tano wa maendeleo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaoanzia 2016/17 hadi 2020/21, wameamua kuendelea na majadiliano kuhusu mkataba wa ubia wa kibiashara kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya (EPA) na wamepokea ripoti ya maendeleo ya majadiliano ya kutafuta amani ya mgogoro wa Burundi kutoka kwa Mratibu wa mazungumzo hayo Mhe. Rais Mstaafu Benjamin Willian Mkapa.
Halikadhalika wakuu wa nchi wamewahimiza wahusika wote katika mgogoro wa Burundi kushirikiana na Mratibu na Msuluhishi wa mgogoro huo ili kufanikisha mazungumzo hayo.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kampala
23 Februari, 2018
Waziri Mkuu: Mabalozi Tafuteni Wawekezaji Wa Sekta Ya Utalii (Dar es Salaam)
Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hayo wakaimarishe diplomasia kwa lengo la kuzifanya nchi hizo ziendelee kushirikiana na Tanzania katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Febriari 24, 2018) wakati akizungumza na Balozi Dkt. Wilbrod Slaa anayewakilisha Tanzania nchini Sweden na Balozi Muhidin Ally Mboweto anayewakilisha Tazania nchini Nigeria, katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu amesema Tanzania ina vivutio vingi vya utalii kama uwepo wa fukwe za bahari kuanzia Tanga hadi Mtwara, maziwa na mito, mbuga za wanyama hivyo ni vema wakajielekeza katika kuvutia wawawekezaji kwenye sekta hiyo ili Taifa lipate watalii wengi.
Amesema mbali na kutangaza sekta ya utalii, pia watafute wawekezaji kwa ajili ya kuwekeza kwenye sekta ya madini, viwanda na kutafuta masoko ili wafanyabiashara na wakulima wa Tanzania waweze kuuza bidhaa zao nje ya nchi.
“Tumejiimarisha katika mazao ya chakula na biashara, hivyo tunatakiwa kuwa na uhakika wa masoko kwenye kilimo ili mkulima anapozalisha pamba, tumbaku, kahawa, chai, korosho, dengu pamoja na mazao mengine tuwe na mahali pa kuuza, kwa hiyo washawishini wafanyabiashara kuja kununua.”
Pia Waziri Mkuu amewataka mabalozi hao wakawatambue na kuwaunganisha Watanzania waishio kwenye nchi wanazoiwakilisha ili nao washiriki kwenye ujenzi wa uchumi wa viwanda na wawasisitize wafuate sheria za nchi wanazoishi na wakumbuke nyumbani.
Waziri Mkuu amewasisitiza mabalozi hao kwenda kupunguza gharama za uendeshaji wa Balozi kwa kuzuia matumizi katika mambo yasiyo ya lazima. “Pia maslahi ya nchi lazima mkayasimamie huko muendako hasa katika masuala ya kiuchumi”
Kwa upande wao mabalozi hao  wamesema watahakikisha wanayafanyia kazi maelekezo yote waliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi wanazoziwakilisha.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, FEBRUARI 24, 2018.
MWANZA: MHE. RAIS MAGUFULI AZUIA BOMOA BOMOA UWANJA WA NDEGE
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo
Februari 24, 2018 baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wafanyakazi wa
Uwanja huo ambao walimweleza Kuwa uwepo wa Kaya hizo unakwamisha Ujenzi wa
uwanja Huo.
“Hawa watu ndiyo walionipa kura, pamoja
na hivyo msiwaondoe hadi pale mtakapokamilisha kuwalipa madai yao,” amesema
Rais Magufuli.
Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli
aliagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 2,000
wanaodaiwa kuvamia eneo la uwanja huo, kituo cha polisi na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ).
Siku hiyo wakati akizungumza na wananchi
wakati wa uzinduzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo la Furahisha
jijini Mwanza, Rais Magufuli aliagiza ubomoaji huo usitishwe hadi atakapotolea
uamuzi suala hilo.
Leo mjini Mwanza, Meneja wa uwanja huo,
Ester Mandale alimweleza Rais Magufuli kuwa wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo ya ukosefu wa jengo la wasafiri, Uwanja kukosa uzio pamoja
na ndege kuzuiwa kubeba samaki.
Amesema baada ya ndege kuzuiwa
kusafirisha samaki kwenda nchi za nje, wanalazimika kusafirisha kwa kutumia
magari wakati wenzao wa Kenya wanatumia ndege, hivyo kuikosesha Serikali
mapato.
Akizungumzia changamoto hiyo, Rais
Magufuli amemwagiza meneja huyo kufanya tathmini inayohitajika Katika Ujenzi wa
Jengo la Usafiri Pamoja na Uzio kisha Aiwasilishe Serikalini Kwa ajili Ya
kuanza ujenzi Huo.
Rais Ameondoka jijini Mwanza na
anaelekea Chato kwa ajili ya mapumziko.
DAR ES SALAAM: DIWANI KATA YA KIBONDE MAJI AISHUKURU OFISI YA MKUU WA MKOA
Mhe. Mtinika ameyasema hayo leo  Jumamosi Februari 24, 2018 alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa uzinduzi wa utambulisho wa kikundi cha waendesha bodaboda kata ya Mbagala Kibonde Maji jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mtinika ameyasema hayo mbele ya mkuu wa wilaya ya Temeke, ndugu Felix Lyaniva, ambapo amesema wao kama viongozi walichokifanya ni kuwaunganisha vijana kufanya kazi kwa pamoja na kushiriki katika kulinda usalama wa eneo hilo.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mtinika amelipongeza jeshi la polisi katika maeneo hayo kwa kufanya kazi zake kwa weledi, huku akiwalaumu baadhi ya mgambo ambao wamekuwa wakikamata raia kinyume na taratibu.
Aidha Mhe. Mtinika amesema wataendelea kushirikiana na taasisi na mashirika mbalimbali katika kusimamia ulinzi na usalama wa eneo hilo, huku akisema kuna vijana wa kujitolea ambao watakuwepo kwenye ofisi za kata kwaajili ya kutoa msaada wa huduma za kisheria
ARUSHA: ZITTO KABWE AZUNGUMZIA MASUALA MBALIMBALI YANAYOENDELEA NCHINI, AKEMEA UKIUKWAJI WA DEMOKRASIA
Katika mkutano huo Zitto
ameambatana na viongozi wengine akiwemo mwenyekiti wa chama hicho mkoani
Arusha,na  Mwenyekiti, Kamati ya Sera na Utafiti  wa chama hicho
ndugu  Emmanuel Lazarus Mvula.
Mhe. Zitto amezungumzia
kuhusu uminywaji wa demokrasia nchini, matukio ya mauaji ya raia na wanasiasa,
pamoja na kukosekana kwa uwiano wa huduma za kijamii na rasilimali kati ya
maeneo ya mijini na vijijini.
Akizungumzia suala la
demokrasia nchini, Mhe. Zitto amesema kumekuwa na tishio kubwa la uminywaji wa
demokrasia nchini ikiwa ni pamoja na uhuru wa vyama vya siasa kufanya mikutano
yake, jambo ambalo ni kinyume kabisa na katiba ya nchi.
“Nchi yetu ni ya demokrasia ya vyama
vingi, ni wajibu wa kila mtanzania kulinda demokrasia hii, Kwakuwa kuna dalili
zote za kurudishwa kwenye mfumo wa chama kimoja, ni wajibu wa watanzania kujitokeza
kupinga mambo haya” amesema
Zitto
Akizungumzia matukio ya mauji
ambayo yamekuwa ya kiendelea hapa nchini dhidi ya wanasiasa, na wananchi wa
kawaida, Mhe. Zitto amesema chama chake kina laani vikali matukio hayo, huku
akiitaka serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika.
“chama chetu kinalaani vitendo vya
mauaji nchini kwa nguvu zote” amesema Zitto.
Akiongelea kuhusu uwiano wa
upatikanaji wa huduma za kijamii nchini, Zitto ameseam hakuna uwiano wa
rasilimali kati ya mjini na vijijini, akitolea mfano wilayani Kibaha kuwa shule
za maeneo ya mjini zina walimu wa kutosha huku zile zilizopo maeneo ya vijijini
zikikosa walimu wa kutosha.
Zitto amehitimisha mkutano
huo kwa kupendekeza kuundwa tume huru itakayochunguza masuala ya mauji ya
kisiasa nchini na yale ya wananchi wa kawaida, pia kuchunguza vitisho vya
mauaji vinavyotolewa dhidi ya wanasiasa.
Zitto pia amependekeza
kuhitishwa kwa mkutano wa kitaifa wa kujadiliana masuala ya kisiasa nchini
ikiwa ni pamoja na mstakabali wa vyama vya siasa nchini, na kama serikali
haihitaji mfumo wa vyama vingi basi walete pendekezo la kuwa na chama kimoja.
TAHARUKI DODOMA! RISASI ZAPIGWA KUKAMATA WAHALIFU
Hayo yamebainishwa Jana Ijumaa Februari
23, 2018 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi
Gilles Muroto, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma.
Kamanda Muroto alisema jeshi hilo
linawashikilia watu wanne waliokamatwa wakiwa kwenye harakati ya kuuziana
vipande tisa vya meno ya tembo yenye uzito wa kilo 2.450 na thamani ya shilingi
milioni 67.5, baada ya kukutwa wakiwa karibu na maeneo ya benki ya NMB wilayani
Kondoa.
Kamanda Muruto amesema mara baada ya
watuhumiwa kuona wamezingirwa na polisi walijaribu kutoroka kwa kuwatishia
askari kwa visu, lakini askari walilazimika kufyatua risasi sita hewani na
kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wote.
Aidha kamanda Muroto aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na: Juma Gindae (50), mkulima na mkazi wa
Kwamatoro wilaya ya Chemba mkoani Dodoma na Patrick Mwaluko (49), mkulima mkazi
wa Kidoka wilaya ya Chemba,  Daudi Masinga (22), dereva wa bodaboda na
mkazi wa Kidoka,  na Khalifa Saluti (21), dereva bodaboda ambaye pia ni
mkazi wa Chemba.
MELI 19 ZA UVUVI ZATIWA KITANZINI NCHINI TANZANIA
 Meli zipatazo 19 zimetozwa faini ya jumla ya shilingi bilioni 19
kutokana na  kubainika kufanya uvuvi haramu na uchafuzi wa mazingira
katika ukanda wa uchumi wa bahari kuu.
Meli zipatazo 19 zimetozwa faini ya jumla ya shilingi bilioni 19
kutokana na  kubainika kufanya uvuvi haramu na uchafuzi wa mazingira
katika ukanda wa uchumi wa bahari kuu.
Hayo yamesemwa na waziri wa
mifugo na uvuvi, Luhaga Mpina siku ya jana Ijumaa Februari 23, 2018 jijini Dar
es Salaam ambapo alisema  kuwa uamuzi huo umefuatia meli hizo kukiuka
Sheria ya uvuvi wa bahari kuu kwa kutoripoti katika bandari za Dar es Salaam,
Zanzibar, Mtwara au Tanga kwa ajili ya ukaguzi kabla ya kuondoka katika bahari
kuu ya Tanzania.
Mpina amesema mbali na
kutakiwa kulipa faini hizo, serikali pia imeiagiza Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari
Kuu (DSFA) kuwaandikia notisi wamiliki wa meli hizo kutaarifu maamuzi hayo na
kuijulisha kamisheni ya kusimamia samaki aina ya Jodari Bahari ya Hindi (IOTC)
hatua zilizochukuliwa na serikali kwa meli hizo.
“Kwa kitendo hiki cha kukiuka masharti
haya ya leseni zao maana yake wameshiriki uvuvi haramu, wamechafua mazingira” alisema Waziri Mpina.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA), Hosea Mbilinyi
alizitaja meli hizo zilizopigwa faini ambapo kila moja itapaswa kulipa faini ya
shilingi bilioni moja kuwa ni pamoja na: Tai Hong no.2,  Tai Hong no. 8,
Tai Xiang no.5, Tai Xiang no.5, Tai Xiang no. 8, Tai Xiang no. 9, Tai
 Xiang no. 10, Tai Xiang no.7, Tai  Xiang no 6, Tai Hong no .7.
Mbilinyi ameongeza kwa kuzitaja meli zingine kuwa ni pamoja na:
Xian Shiji no. 81, Xin Shiji no. 82, Xin Shiji no. 83, Xin Shiji no. 86, Xin
Shiji no. 76, na Jian Shen no. 1.
Katika hatua nyingine Mpina
alisema eneo la bahari kuu lenye ukubwa wa kilomita za mraba 223,000 limekuwa
likinufaisha mataifa mengine na kwamba msimamo wa serikali kwa sasa ni
kuhakikisha rasilimali zilizomo ndani ya eneo hilo zinachangia katika ukuaji wa
pato la taifa.
WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI
Hayo yalisemwa na naibu
waziri nishati Mhe. Subira Mgalu kwa niaba ya waziri wa nishati katika hotuba
yake ya kufunga kongamano la wadau kuhusu fursa za mradi wa bomba la mafuta
ghafi la Afrika Mashariki lililofanyika Jana Februari 23, 2018.
Katika kongamano hilo
lililoandaliwa na baraza la uwekezaji la taifa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu na
Wizara ya Nishati ambalo lilifunguliwa na Waziri wa Nchi Sera, Bunge, Uratibu,
Ajira, Kazi na Vijana, Mhe. Jenister Mhagama (Mb).
Mada mbalimbali
ziliwasilishwa ikiwa ni pamoja na: taarifa fupi ya mradi,fursa zilizopo kwenye
mradi huu wa bomba la mafuta ghafi, sheria ya mafuta ya mwaka 2015 juu ya
vifungu vinavyohusiana na ushiriki wa watanzania, fursa zilizopo katika sekta
ya bima zinazopatikana na mradi huu, na umuhimu wa viwango na ithibati
zinazohitajika katika mradi huo.
Mada hizo zilitolewa na
Wizara ya Nishati, TOTAL, EWURA, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima TIRA, na TBS.
Katika kongamano hilo, Mhe.
naibu waziri aliwataka washiriki kutumia taarifa walizozipata kupitia mkutano
huo katika kujipanga zaidi na kuhimili ushindani wakati wa kutangaza kazi
mbalimbali kipindi cha ujenzi wa mradi huo na uendeshaji wake, na kutumia fursa
ya mazingira mazuri yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria.
Aidha Mhe. Mgalu amesema
serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli ina
nia ya dhati kabisa ya kuweka mazingira wezeshi  katika miradi mikubwa hii
ili kuwawezesha Watanzania kufaidika na mradi huu wa bomba la mafuta ghafi.
Serikali za Tanzania na
Uganda zilisaini makubaliano ya Kutekeleza Mradi huu kupitia Tanzania 1 Machi
2016 na bomba hili litapita kwenye mikoa nane Kagera ,Geita , Shinyanga, Tabora
,Singida ,Dodoma ,Manyara na Tanga pamoja na Wilaya 24 na Kata 134.
Bomba hili litakuwa na urefu
wa jumla ya Kilometa 1443 kutoka Hoima Uganda hadi eneo la Chongoleani mkoani
Tanga kati ya hizo kilometa 1147 zitakuwa upande wa Tanzania  .
Mhe naibu waziri amewapongeza
waandaji na wadhamini wa kongamano hilo na kuwashukuru washiriki zaidi ya mia
nne waliohudhuria na kuahidi wizara ya nishati itaendelea kuandaa mikutano
mbali mbali  ya wadau kwa ajili ya kupeana taarifa  za fursa na
kupanga mikakati ya namna ya ushiriki madhubuti wa watanzania katika nyanja
mbalimbali ikiwemo ajira za kitaalam na ajira za kawaida , huduma za kibima na
kibenki, huduma za vyakula , sekta ya ujenzi na usafirishaji, nakadhalika.











