Mkuu wa Mkoa wa MTWARA, Gelasius Byakanwa ameagiza kukamatwa kwa
meneja wa Benki ya NMB, tawi la Masasi na kuwekwa chini ya ulinzi ili ufanyike
uchunguzi wa sababu za baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao zaidi ya Sh3
bilioni.Wakulima wa Korosho kutolipwa Fedha zao: Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aagiza kukamatwa kwa meneja wa NMB, tawi la Masasi na Viongozi wa AMCOS.
Mkuu wa Mkoa wa MTWARA, Gelasius Byakanwa ameagiza kukamatwa kwa
meneja wa Benki ya NMB, tawi la Masasi na kuwekwa chini ya ulinzi ili ufanyike
uchunguzi wa sababu za baadhi ya wakulima kutolipwa fedha zao zaidi ya Sh3
bilioni.
Agizo hilo limetolewa jana Ijumaa Februari 23, 2018 baada ya
meneja huyo kushindwa kuhamisha fedha za wakulima kutoka benki hiyo kwenda
CRDB, huku akikopesha chama msingi kiasi cha Sh300 milioni bila chama kuomba
ikiwa ni pamoja na muamala wa Sh45 milioni kulipwa mara 11 kwa siku moja.
Wengine walioagizwa kukamatwa ni pamoja na baadhi ya viongozi wa
Amcos ambao waliwalipa wakulima mara mbili na kusabisha baadhi yao kudai malipo
yao, wakiwemo waliopokea fedha hizo mara mbili.
Hatua hiyo imekuja baada ya Byakanwa kuagiza kuundwa kwa tume
ili kuchunguza madai ya baadhi ya wakulima kutolipwa fedha za msimu wa mwaka
2016/17 na 2017/18.
Akisoma taarifa ya tume, Mwenyekiti wake, Remidius Bantulaki
ameeleza sababu iliyochangia kucheleweshwa kwa malipo ni pamoja na NMB
kuchelewa kutoa taarifa za vyama ambavyo miamala yake haijakamilika yenye
thamani ya Sh400 milioni na mpaka tume inaandaa taarifa zilikuwa hazijarudishwa
kwenye vyama vya ushirka.
“Mfano Chama cha Msingi Namalenga waliomba taarifa Desemba 6, 2017,
lakini wamekuja kupatiwa yenye thamani ya Sh 12.4 milioni Februari 17, 2018,” alisema.
“Jambo lingine benki hiyo inachelewa kuhamisha fedha kwenda benki
nyingine ili kulipa wakulima wanaotumia benki tofauti na wao,” amesema.
“Novemba 17, 2017 Chama cha Chimana kiliandika hundi ya Sh 45.5
milioni kwenda CRDB mpaka tarehe 12, hiyo fedha ilikuwa haipo kwenye akaunti ya
chama wala kufika kwenye akaunti ya CRDB na wakulima walikuwa bado wanadai.”
Hata hivyo, ameeleza wamegundua baadhi ya vyama vya
ushirika vimewalipa wakulima mara mbili na hivyo kuwalazimu ambao hawajalipwa
kusubiri mpaka waliolipwa mara mbili kurudisha fedha.
“Kwenye Chama cha Nanjota Amcos mnada wa saba uliokuwa na kiasi
cha Sh31.4 milioni uliokuwa na jumla ya wakulima 12, kuna wakulima wamelipwa
mara mbili kwa hiyo wengine wanasubiri wao watakaporudisha fedha ndipo
walipwe,”amesema.
Amesema tume hiyo imegundua benki ya NMB kutoa fedha kwenye
akaunti ya chama mara mbili kinyume na taratibu.
“Chama cha Chimane Amcos iliyoandika hundi ya Sh45.5 milioni yenye
namba 00040, Novemba 17 ilitolewa kwenye akaunti ya chama Novemba 18 2017,
lakini kiasi hicho hicho kikatolewa tena Novemba 30, 2017 na kufanya fedha
iliyotolewa kwa wiki moja kuwa Sh91.1 milioni na hiyo fedha haikufika kwenye
akaunti ya CRDB wala kurudi kwenye akaunti ya chama.”
Baada ya taarifa hiyo, Byakanwa amekubaliana na mapendekezo yote
ya tume na kutoa maagizo ya kukamatwa kwa watuhumiwa.
SIMON GROUP YACHANGIA MILIONI 25 UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU SIMIYU
Akikabidhi
hundi hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Simon Group, Ndg. Leonard Kitwala amesema
Kampuni hiyo imetoa fedha hizo ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika
maendeleo ya Sekta ya Elimu na kwa kuwa Simiyu ni mahali alipozaliwa Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo Ndg. Simon Kisena ameona ni vema asaidie maendeleo ya
elimu nyumbani kwao.
Aidha,
Kitwala amesema kama kampuni wameamua kuunga mkono ujenzi wa miundombinu ya
Elimu Simiyu kwa kuwa wamependezwa na juhudi za Viongozi wa Mkoa wa Simiyu,
wakiongozwa na mkuu wa Mkoa huo, Mhe.Anthony Mtaka katika kuwaletea maendeleo
wananchi katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu.
Akipokea
hundi ya shilingi milioni 25 kwa niaba ya Viongozi na wanafunzi wa Mkoa
wa Simiyu, Mkuu wa Mkoa huo Mhe.Anthony Mtaka amesema anaishukuru Kampuni ya
Saimon Group ambayo inaendesha mradi wa Usafrishaji wa Mabasi Dar es
Salaam(UDA) kwa kuamua kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani humo.
“Nawashukuru
sana SAIMON GROUP kwa kuamua kusaidia ujenzi wa miundombinu ya elimu Simiyu,
shilingi milioni 25 ni fedha nyingi sana kwenye kufanikisha ujenzi wa
mundombinu ya elimu hasa kwa mkoa kama wa kwetu ambao shughuli nyingi za
ujenzi tunatumia “Force Account” , tunatumia nguvu za wananchi na Serikali ina
nafasi yake katika ujenzi wa miradi hiyo” alisema.
“Zaidi
sana namshukuru Mkurugenzi wa SIMON GROUP ndugu Robert Kisena ambaye ni
mzaliwa wa Mkoa huu kwa kuona arudishe sehemu ya faida ya biashara
zake nyumbani, kwa niaba ya viongozi wenzangu ninamkikishia kwamba mchango huu
utaenda kwenye matokeo yanayoonekana, hata wakati wa uzinduzi wa madarasa
yatakayojengwa tutaipa nafasi Kampuni ya SIMON GROUP kuja kuona alama
waliyoweka katika mkoa wetu” alisisitiza Mtaka.
Naye
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Mhe.Robert Lweyo amesema mchango
huo wa SIMON GROUP umekuja katika muda muafaka ambao mkoa huo una uhitaji
mkubwa wa vyumba vya madarasa hivyo alimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Ndg.
Robert Kisena na kuahidi pia kuwa fedha hizo zitafanya kazi iliyokusudiwa.
SERIKALI KUIFUTIA LESENI MGODI WA UCHIMBAJI MADINI WA EL HILAL
Kauli
hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila wakati
wa ziara yake ya kikazi ya kukagua migodi
ya
uzalishaji almas ya kampuni za Wiliamson Diamond na El Hilal
zilizopo
eneo la Mwadui mkoani Shinyanga,Februari 21, 2018.
Prof.
Msanjila alisema mgodi wa El Hilal unamiliki leseni kubwa ya uchimbaji wa madini ya almas,iliyotolewa mwaka 2010 na unadaiwa
ada ya mwaka ( annual rent) Dola za Kimarekani 1,447,360 sawa na shilingi
bilioni 3.1 ambazo hazijalipwa kwa kipindi cha miaka 6, kuanzia 2012/13 hadi
2017/18.
Vilevile
aliweka wazi kuwa kampuni hiyo pia inadaiwa zaidi ya kiasi cha shilingi milioni
294.2 ikiwa ni mrabaha pamoja na adhabu yake iliyotokana na mauzo ya ndani ya
almasi yaliyofanyika
kwa kipindi cha miaka
tatu kuanzia 2011 hadi 2013.
“Haiwezekani
kampuni ikawa inafanya biashara ndani ya kipindi
chote
hicho halafu hailipi mapato ya Serikali, Sheria ya madini ya mwaka 2010
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 iko wazi inaelekeza hatua za kuchukua kwa
vitendo kama hivyo, sasa tumewapa muda na sheriaitachukua mkondo wake”, alisema Msanjila.
Aidha
aliitaka kampuni hiyo kufanya shughuli zake kwa kuziangatia Sheria na Kanuni za
uchimbaji madini, na pia katika
kutoa ajira kwa wafanyakazi wake na kwamba sheria na kanuni za madini zinapaswa
kufuatwa hata kama ni mwekezaji mzawa.
Sambamba
na hilo,Msanjila ilizitaka kampuni za uchimbaji zinazoendeshwa na wawekezaji wa
nje kuwa na akaunti
za fedha hapa nchini tofauti
na ilivyo sasa ambapo kampuni nyingi akaunti zake zipo nje ya Tanzania.
Msanjila
pia aliwataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini kufanya kazi kwa
kuzingatia weledi, juhudi na maarifa na bila kumpendelea mtu yeyote wakati
wakitekeleza majukumu yao.
Vilevile
aliwataka kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali katika
madini yanayopatikana kwenye maeneo yao, akitolea mfano wa Madini ya Ujenzi kuwa
yamesahaulika kabisa katika makusanyo.
Aliendelea
kuwakumbusha Makamishna hao kuendelea kutoa
elimu
sahihi kwa wachimbaji na wadau wote wa madini katika maeneo yao juu ya
marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka
2017 pamoja na kanuni zake.
RC Wangabo Asisitiza Kutumia Bidhaa Za Viwanda Vya Ndani Kujihakikishia Soko
Ameyasema
hayo baada ya kutembelea Kiwanda cha Unga Energy Sembe na Kiwanda cha maji Dew
Drop vinachomilikiwa na Azizi Mohamed Sudi, Mbasira Fodd Industries na Kiwanda
cha maziwa OTC Kizwite kinachomilikiwa na kikundi cha wafugaji vyote
vikipatikana katika Manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa vinavyozalisha bidhaa
zinazouzwa ndani ya Mkoa, nje ya Mkoa na kuvuka mipaka ya nchi.
Amesema
kuwa Kazi ya Serikali kutoa mazingira bora na wezeshi ili wawekezaji wawe na
fursa nzuri za kuwekeza na kuongeza kuwa serikali haitakubali kuona viwanda
vikifa kwa mambo ambayo yapo ndani ya uwezo wa serikali na kuwahakikishia
wamiliki wa viwanda hao kuwa serikali haiwezi kuendelea kuhamasisha viwanda
bila ya kutatua changamoto mbalimbali zinazokumba viwanda vilivyopo.
“Tujivunie
viwanda vyetu vya hapa, hasa vile vinavyozalishwa na wazawa wenyewe ambavyo
vinatoa ajira kwa wananchi wa Mkoa huu, changamoto zipo kama masuala ya
kimazingira, malighafi na umeme, kama serikali tutayachukua ili kuhakikisha
wawekezaji wanafanya kazi katika mazingira bora kabisa, kazi ya serikali kuweka
mazingira wezeshi ili wenzetu waweke viwanda ili tuweze kufikia uchumi wa kati
wa Viwanda kufikia 2025,” Alisema.
Na
kushauri kuwa viwanda hivyo havinabudi kujitangaza katika vyombo mbalimbali vya
habari na mitandao ili kuweza kupata masoko ya uhakika.
Kwa
upande wake Mmiliki wa Kiwanda cha Unga Energy Sembe na Dew Drop, Aziz Mohamed
Sudi amesema kuwa kiwanda cha sembe kimesimama uzalishaji wake tangu Mei, 2017
baada ya kukosa soko la ndani ya nchi na kutegemewa kuanza tena mwaka 2018
baada ya kupata maombi kutoka nchi ya Kongo.
“Wawekezaji
katika mikoa ya pembezoni tumekuwa mbali na masoko makubwa, gharama za
uzalishaji, umeme na kupeleka bidhaa hizo kwenye masoko makubwa zimekuwa kubwa
pamoja na pamoja na utititiri wa kodi, hivyo tunaiomba serikali iruhusu kuuza
bidhaa za kiloimo zilizoongezwa thamani na tunakubalina na hatua za kudhibiti
chakula kwa kuuza nafaka,” Azizi Alisema.
WATANZANIA CHANGAMKIENI FURSA ZA AJIRA NA UTAFITI WA LUGHA YA KISWAHILI KATIKA SOKO LA AFRIKA MASHARIKI
Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa
Bodi mpya ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) pamoja na uzinduzi wa kanzi
data ya wataalamu wa Kiswahili jana Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mwakyembe amesema kuwa leo hii kiswahili
kimetandawaa na kuenea kote duniani huku kikipewa kipaumbele katika nyanja
mbalimbali ikiwemo hapa nchini na hata nchi za nje, kwani nchi mbalimbali
zimekua zikionyesha mahitaji ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili hivyo kuwataka
watanzania kuwa sehemu ya mahitaji hayo.
Aidha Mhe. Mwakyembe ameiambia Bodi mpya ya
BAKITA kuwa Wizara inaitarajia bodi hiyo kuwa muhimili wa BAKITA na chachu ya
kuirejeshea nchi ukombozi na ukuzaji wa lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Tanzania
kwa kufanya kazi kisayansi zaidi kuliko kutumia nguvu na rasilimali nyingi bila
tija.
“Leo tunazindua rasmi bodi ya BAKITA, naamini
kuwa mko tayari kufanya kazi hii kwa juhudi, uteuzi wenu umezingatia sana
masharti na weledi kwa mujibu wa sheria ya BAKITA kwani hakuna hata mmoja
wenu aliyeteuliwa kwa kubahatisha” amesema Mhe. Mwakyembe.
Akizungumzia kuhusu kanzi data ya wataalamu wa
lugha ya Kiswahili nchini Waziri Mwakyembe amesema kuwa kanzi data hiyo
itasaidia kuwapata na kuwajua wataalamu wa Kiswahili tulionao nchini kwa ajili
ya mahitaji ya ndani na nje ya nchi lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watanzania
wenye sifa sahihi wanapata nafasi za kazi na kueneza lugha ya Kiswahili
duniani hivyo ni wajibu wa Baraza la Kiswahili la Taifa kuboresha kanzi data
hiyo ili ikidhi mahitaji ya soko la ajira la wataalamu wa lugha ya Kiswahili.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi amesema kuwa wazo la kuwa na kanzi data ya
wataalamu wa lugha ya Kiswahili ni jambo kubwa sana na kwa kuwa kanzi data
itatumia njia ya Tehama wananchi watahudumiwa kwa haraka kwa wepesi na
kwa usahihi.
TANZIA: Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara Hassan Simba Afariki Dunia
![]() |
| Hassan Simba enzi za uhai wake |
Ndugu wanahabari, napenda kuwafahamisha kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mtwara (MTPC) Bw.Hassan Simba amefariki Dunia Mchana wa leo Jumamosi katika Hospitali ya Temeke Jijini Dar es salaam, alipokuwa amelazwa kwa ajili ya Matibabu.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho jumapili February 25, 2018 Saa 7 Mchana Wilayani Kilwa mkoa wa Lindi.
Bryson Mshana
Katibu-MTPC
Katibu-MTPC
Kwa niaba ya Uongozi na wafanyakazi wetu wa Jamii Fm Radio, Tunatoa Salam za rambi rambi kwa wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wote wa Tasnia ya Habari mkoani mtwara na Tanzania kwa ujumla kwa Kuondokewa na Ndugu Hassan Simba Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Mtwara.
Jamii fm radio inatoa pole kwa wale wote waliguswa na msiba huu kwa namna moja ama nyingine.
Mbele yako nyuma yetu, Jina la Bwana lihimidiwe.
Francis Cheka apokelewa Kimila na wazee wa Kimakonde

Francis Cheka aliyezaliwa na Francis Boniface Cheka mnamo Aprili 15, 1982 ni mshambuliaji wa taasisi ya Tanzania na sasa ni Champion ya Dunia ya Boxing Federation (WBF) Super Middleweight Champion.
Leo amepokelewa Kimila na wazee wa jadi/Kimakonde Mtwara Old Boma na kuwekwa wakfu kabla ya pambano
Lake la kuutetea Mkanda wake wa #UBO uzito wa kati na Bondia Bondia Bingwa wa
Taifa la Phillipine.
Bingwa huyo anayetokea kwenye Kambi ya Manny Pacquiao chini ya kocha
maarufu Duniani Dante Almarios . watachuanza vikalikatika Uwanja wa #Nangwanda Sijaona Mkoani #Mtwara, usiku wa pasaka tarehe 01 mwezi 04 mwaka 2018.
#Cheka ahaaidi kumsulubu Mfilipino huyo lleo mbele ya waandiahi wa habari mara baada ya kusimikwa na kupewa #baraka za #kimila


MTANDAO WA WANAWAKE NA KATIBA, WAHARIRI WAJADILI USAWA WA KIJINSIA KATIKA SIASA
Akiwasilisha mada kwa wahariri na wanahabari waandamizi katika
mkutano huo, mtoa mada na mjumbe wa WFT, Dk. Dinah Richard Mmbaga aliwataka
wanahabari kuangalia mfumo mzima wa siasa za vyama vingi na nini
kinachoitenganisha siasa ya Tanzania na nchi nyingine bila kujali tofauti za
itikadi za vyama kwenye masuala yanayohusu utu wa mwanamke, ushiriki wa
mwanamke kuchangia fikra za siasa na uongozi.
Aliwataka kuchambua na kuangalia mambo yapi yatakayounganisha
wanasiasa wote katika kutetea masuala ya kitaifa ikiwa ni pamoja na utu na haki
za mwanamke na pia mfumo wa uongozi utakaowezesha vyama vya siasa kuimarisha
demokrasia shirikishi yenye mrengo wa jinsia ndani ya vyama.
Pia kuchambua mfumo wa uongozi unaowezesha vyama kutatua migogoro
ndani ya vyama vyao bila kutumia vitisho, na hususani vinavyoashiria
kumsababisha mwanamke wa Tanzania asipende kushiriki katika shughuili za siasa
au anaposhiriki ajisikie yuko salama.
Kwa upande wake Mjumbe wa Wanawake na Katiba/uchaguzi na uongozi,
Bi. Laeticia Mukurasi akizungumza katika majadiliano hayo, alisema malengo ni
kujadili kwa pamoja umuhimu wa kuzingatia misingi ya usawa wa jinsia katika
masuala ya siasa na uongozi nchini nchini.
Kujenga makubaliano ya pamoja jinsi waandishi wa habari
watakavyochechemua umuhimu wa kuzingatia misingi ya jinsia kwenye masuala ya
siasa na uongozi katika majukumu yao, na kujengeana uwezo wa masuala ya usawa
wa jinsia na uongozi kwa ujumla.
NAIBU WAZIRI WA MADINI AKERWA NA USIRI WA MAPATO YA MWEKEZAJI
Mhe Biteko ameonyesha masikitiko makubwa wakati akizungumza na uongozi wa mgodi huo mara baada ya uongozi wa mgodi huo kushindwa kumpatia taarifa ya mapato na matumizi wakati akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani humo kukagua shughuli za uchimbaji Madini.
Kumbukumbu hizo zimekosekana kufuatia viongozi wa ngazi ya juu ya mgodi kutokuwepo kwenye kikao hicho pamoja na kukiri kupokea taarifa ya ujio wake kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.
Alisema kuwa viongozi hao kukosekana pamoja na kuwa na taarifa ya muda mrefu juu ya ziara hiyo ni utovu mkubwa na nidhamu kwa serikali ya awamu tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema kuwa pamoja na kutokuwepo kwao lakini taarifa zilitakiwa kuwepo ofisini kwani ni kosa kisheria kukosekana kwa taarifa za mgodi ilihali sheria ya Madini ya mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017 inaeleza vyema kuwa mmiliki wa leseni ya Madini anatakiwa kutunza kumbukumbu za mapato na matumizi kwa miaka mitano.
“Endapo atashindwa kufanya hivyo serikali itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kifungo cha mwaka mmoja jela ama faini ya shilingi Milioni 50 mpaka milioni 150,” alisema Naibu Waziri huyo
Mhe Biteko akizungumza huku akionyesha kukerwa na baadhi ya viongozi ambao walikuwepo katika eneo la ofisi ya mgodi huo huku wakishindwa kuhudhuria katika kikao hicho cha kazi alisisitiza kuwa muwekezaji wa mgodi huo anapaswa kuzingatia na kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi.
Sambamba na hayo pia Mhe Biteko aliutaka uongozi wa mgodi huo kutoa taarifa sahihi za uwepo wa mashapu katika mgodi waliyokuwa wakichimba au kama mashapu katika mgodi huo yameisha wafuate taratibu za kisheria za ufungaji wa mgodi ikiwemo kuyarudisha mazingira katika halo take ya kawaida.
Na Mathias Canal, Mbeya
DKT. NDUGULILE ACHANGIA MIL. 6.5 UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA MAKAZI YA WAZEE
Akiongoza harambee hiyo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amesisitiza wananchi kujitolea kwa hali na mali katika kufanikisha ujenzi wa nyumba hiyo ambao itasaidia kuwaweka karibu watumishi wa makazi yao katika kuwezesha upatikanaji wa huduma stahiki kwa wazee ikiwemo miundombinu bora, matibabu, chakula, malezi, na haki nyingine wanazostahili.
Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wanawajibu wa kuwashirikisha wananchi kuchangia katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
“Niwaombe wananchi wa Kiilima tuwasaidie kile kidogo cha kwako kiwe fedha au nguvu zako tusaidie ujenzi huu wa nyumba hii ya watumishi ikamilike,” alisema Dkt. Ndugulile.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amewashukuru wadau kwa michango yao na kuwapongeza wananchi kwa kujitolea nguvu zao na kusisitiza matumizi mazuri ya fedha hizo kwa ajili ya kufanikisha juhudi za kukamilisha jengo la nyumba za watumishi wa makazi ya wazee.
Kwa upande wake Kaimu Mfawidhi wa Makazi hayo Bi. Gladness Luiza ameishukuru Serikali na wadau kwa kuwa wasikivu na kuonesha dhamira ya dhati ya kutatua changamoto inayowakabili na kuahidi kuendelea kuwahudumia wazee kwa moyo wa unyenyekevu katika siku zote za maisha yao.
Washiriki wa Harambee hiyo pia waliahidi kuchangia shilingi Millioni 12, mifuko ya saruji 350, mabati 52, magodoro 20, viti vya miguu mitatu 6, masanduku ya huduma ya kwanza 10, na vifaa vingine muhimu vya kuwahudumiwa wazee vilivyoahidiwa kutolewa na Bohari ya Madawa(MSD). Aidha, wadau waliahidi kuendelea kuchangia ujenzi wa kituo hicho ili kuboresha miundombinu na ustawi wa wazee ambao wamechangia kwa kiasiki kubwa maendeleo ya Taifa.











