Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabililiyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando hadi February 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).Kilichoendelea Leo Mahakamani Katika Kesi ya Tido Mhando
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi ya uhujumu uchumi ya kusababisha hasara ya Shilingi Milioni 887 inayomkabililiyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Tido Mhando hadi February 28,2018 kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali (Ph).
Mwendesha Mashtaka wa (TAKUKURU), Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mfawidhi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kumsomea Tido maelezo ya awali.
Hata hivyo, Wakili wa Tido, Ramadhan Maleta ameieleza Mahakama kuwa amechelewa kumuandaa mteja wake kutokana na kuchelewa kupewa maelezo ya (Ph), hivyo anaomba ahirisho.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi February 28,2018 kwa ajili ya Tido kusomewa (Ph).
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Tido anakabiliwa na makosa matano ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka.
Inadaiwa alilitenda kosa hilo June 16,2008 akiwa Dubai kama mtumishi wa TBC alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mikataba ya uendeshaji wa vipindi kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BVI) bila kutangaza zabuni na kuisababishia channel hiyo kunufaika.
Inadaiwa kati ya June 16 na November 16,2008 akiwa Falme za Kiarabu, kama muajiriwa wa TBC kwa cheo cha Mkurugenzi Mkuu kwa mamlaka yake alilisababishia shirika la TBC hasara ya Sh.Mil 887.
Oparesheni Za Kuzuia Uhalifu Zatakiwa Kuzingatia Sheria
Viongozi wanaohusika na Oparesheni za kuzuia uhalifu wameshauriwa kufuata na kuzingatia sheria inayoongoza namna ya ukusanyaji wa ushahidi ili kuepuka kuharibu ushahidi kabla haujawasilishwa Mahakamani na kupelekea kesi nyingi kuharibika kwa kukosa ushahidi au Mahakama kushindwa kutoa hukumu zinazoendana na kosa husika.
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Uyui alipomtembelea Mkuu wa wilaya hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake inayoendelea Mahakama Kuu kanda ya Tabora.
Akitolea mfano wa Oparesheni za uteketezaji wa dawa za kulevya yakiwemo mashamba ya bangi, Jaji Mkuu amesema ushahidi kuteketezwa bila ya kufuata utaratibu huathiri mienendo ya kesi Mahakamani.
Akizungumzia suala la Maadili ndani ya Mahakama, Jaji Mkuu amewaomba Wakuu wa mikoa pamoja na Wakuu wa wilaya ambao anawatambua kama walezi wa Mahakama kushirikiana kwa karibu zaidi na Mahakama ili kuhakikisha wanawahudumia wananchi ipasavyo katika suala zima la utoaji wa Haki.
Kuhusu kusogeza huduma za kimahakama karibu Zaidi na wananchi, Jaji Mkuu amesema Mahakama kwa kushirikiana na Benki ya Dunia inao Mpango wa kuanzisha Mahakama zinazotembea (Mobile Courts) ili kuwafikia wananchi walio mbali na huduma za kimahakama hasa katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora
Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora na Kaimu Mkuu wa wilaya ya Uyui, Queen Mlozi alimweleza Jaji Mkuu kuwa kwa namna wilaya ya Uyui ilivyokaa kijiografia, wananchi hulazimika kufuata huduma za kimahakama umbali wa Zaidi ya kilometa 150 katoka Loya kwenda Kigwa mkoani Tabora.
Awali akiwa wilaya ya Urambo, Jaji Mkuu alipata wasaa wa kuzungumza na Mkuu wa wilaya hiyo, Angelina Kwingwa ambaye alimshukuru Jaji Mkuu kwa mkakati wa Mahakama wa kukarabati na kujenga majengo ya mahakama maeneo mbalimbali nchini ambayo yatasaidia kupunguza mashauri mahakamani.
“Tumepata faraja kusikia suala la kuongezeka kwa majengo ambayo yatasaidia kupunguza mlundikano wa kesi Mahakamani na upatikanaji wa haki kwa wakati”, alisema.
Jaji Mkuu anaendelea na ziara Mahakama kuu kanda ya Tabora inayojumuisha mikoa ya Tabora na Kigoma. Leo alitembelea na kukagua shughuli za Mahakama katika Mahakama ya Mwanzo Ilolangulu, Mahakama ya wilaya ya Urambo na Mahakama ya Mwanzo Upuge-Uyui zilizopo mkoani Tabora.
Hakuna Kuchukua Maeneo Bila Kulipa Fidia –Naibu Waziri wa Ardhi Angelina Mabula
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Mkazi Angelina Mabula amesema ni marufuku halmashauri kuchukua maeneo ya wananchi bila ya kuwalipa fidia.
Mhe. Mabula amesema hayo Wilayani Butiama mkoa Mara wakati wa ziara yake yenye nia ya kutatua migogoro ya ardhi pamoja na kukagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya ardhi.
Amesema wakati wa mchakato wa kuchukua maeneo ya mwananchi ni vyema wahusika wakashirikishwa kuanzia hatua ya awali sambambana na kuelimishwa juu ya zoezi hilo ili kuepuka migogoro inayoweza kutokea.
‘’Cha msingi ni kuanza kuzungumza na mwananchi kabla ya kuchukua eneo lake na kumueleza eneo ambalo ataachiwa na halmashauri zihakikishe mwananchi huyo anapimiwa pamoja na kupatiwa hati yake’’ alisema Mabula
Aidha, mhe. Mabula amesema eneo litakalochukuliwa na halmashauri viwanja vyake kuuzwa fedha itakayopatikana halmashauri ihakikishe inatumika katika kutengeneza miundo mbinu na huduma nyingine za jamii na kusisitiza kuwa kwa kufanya hivyo migogoro haiwezi kutokea.
Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ameziagiza halmashauri kuhakikisha zinapanga miji kulingana na ‘master plan’ ili kuwa miji bora iliyopangika
Zitto Kabwe Kaachiwa kwa Dhamana
Mbunge Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana leo asubuhi baada ya kushikiliwa katika kituo kikuu cha Polisi mkoani humo tangu jana usiku.
Kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo alikuwa kwenye ziara ya chama chake mkoani humo.
Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya milioni 50 na amedhaminiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula.
Ametakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Zitto Kabwe na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wamesema wataendelea na ziara ya kutembelea kata zinazoongozwa na chama hicho
Zitto Kabwe ameachiwa kwa dhamana ya maneno yenye thamani ya milioni 50 na amedhaminiwa na Wakili wake, ndugu Emmanuel Lazarus Mvula.
Ametakiwa kuripoti Polisi Kituo Kikuu cha Polisi cha Mkoa wa Morogoro Jumatatu, Machi 12, 2018.
Baada ya kuachiwa kwa dhamana, Zitto Kabwe na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho wamesema wataendelea na ziara ya kutembelea kata zinazoongozwa na chama hicho
Waziri Mkuu Akutana Na Rais Wa FIFA
SERIKALI ya Tanzania inalipongeza Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa jitihada na hatua mbalimbali zinazochukuliwa na shirikisho hilo katika mapambano dhidi ya rushwa.Kauli hiyo imetolewa jana (Alhamisi, Februari 22, 2018) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika kikao chake na Rais wa FIFA Bw. Gianni Infantino kilichofanyika jijini Dae es Salaam.
“Serikali tunaunga mkono mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo pamoja na matumizi mabaya ya fedha na ya madaraka yanayofanywa na FIFA”.
Waziri Mkuu amesema wanaunga mkono mapambano hayo ili Taifa liweze kupata mafanikio makubwa katika mpira wa miguu ikiwa ni pamoja na kupata viongozi wenye maono ya mbali katika kuendeleza mchezo huo.
Amesema FIFA ambayo ni kitovu cha mapambano dhidi ya rushwa kwenye michezo , hivyo Tanzania inaiunga mkono kwa kuhakikisha sekta ya michezo inatumia vizuri fedha zilizopo kwa ajili ya kuendeleza michezo.
Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inasimamia matumizi sahihi ya madaraka katika sekta ya michezo nchini ili kuleta maendeleo kwenye mpira wa miguu.
Serikali inaipongeza FIFA kwa jitihada za dhati za kuendeleza mpira wa miguu duniani kwa kuwa mipango mbalimbali ya kuendeleza mpira wa miguu kwa vijana wadogo wa kike na wa kiume nchini.
“Tunatambua msukumo wa FIFA wa kuendelea mpira wa miguu duniani ikiwa ni pamoja na kuboresha viwanja vya michezo pamoja na maendeleo yote wanayoyafanya katika sekta hiyo.
Pia ameishukuru FIFA kwa kuipa Tanzania heshima ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 yatakayofanyika mwakani jijini Dar es Salaam na kwamba Serikali itayasimamia vizuri na inajiandaa kwa kushinda.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemshukuru Rais wa FIFA Bw. Infantino kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli kwa kuendesha mkutano mkubwa wa viongozi wa mpira wa miguu duniani Tanzania. Mkutano huo ulihusisha Marais na Makatibu Wakuu wa nchi 21.
Pia alimpongeza Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Bw. Ahmad Ahmad kwa jitihada zake za anazozifanya katika kuendeleza mpira barani Afrika na kwamba Serikali ya Tanzania inamuunga mkono.
Rais wa FIFA Bw. Infantino ambaye ameahidi kuisaidia Tanzania kwa kuboresha miundombinu ya viwanja vya michezo aliwasili nchini leo alfajiri akiongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Bw. Ahmad Ahmad kwa ajili ya mkutano wa FIFA uliofanyika nchini Tanzania February 22, 2018.
Bw. Infantino amewasili kwa mara ya kwanza Tanzania toka awe Rais wa FIFA na alipokelewa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dtk. Harrison Mwakyembe na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Leodger Tenga na Rais wa TFF Bw. Wallace Karia.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, FEBRUARI 22, 2018
Msajili wa Vyama vya Siasa Aiweka Kitanzini CHADEMA
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amekiandikia barua Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akitaka kijieleza kwa nini asikichukulie hatua kwa kufanya maandamano Februari 16, 2018.
Chadema waliandamana Februari 16 mwaka huu wakishinikiza kupewa viapo vya mawakala wao kabla ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kinondoni.


MAKAMU WA RAIS AWAHIMIZA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU
Mhe.Makamu
wa Rais ameyasema hayo wakati akizungumza na Wananchi wa Wilaya ya Maswa
Mkoani Simiyu kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Nguzo Nane
wakati wa ziara yake mkoani humo.
Amesema
Serikali imeamua kutoa elimu bila malipo na kuwapunguzia wazazi mzigo wa
kulipia gharama za karo na michango mbalimbali ya uendeshaji wa shule lakini
suala la kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu wananchi wanapaswa kuunga
kuchangia ili kuunga mkono juhudi hizo.
“
Tunapeleka fedha katika shule zote za Msingi na Sekondari ili wanafunzi waweze
kusoma vizuri lakini kwenye suala la ujenzi wa matundu ya vyoo, madarasa, maabara
pamoja na kwamba Serikali ina wajibu wa kufanya hayo na ninyi wananchi mnao
wajibu wa kusaidia kufanya hayo” alisema Mhe. Makamu wa Rais.
Wakati
huo huo Mhe.Makamu wa Rais ameipongeza Wilaya ya Maswa kwa kuongeza ufaulu
kutoka asilimia 45 hadi asilimia 75 kwa mwaka 2017 na akakemea vikali tabia ya
wanaume wanaoua ndoto za watoto wa kike kwa kuwapa mimba , ambapo amesema jicho
la Serikali liko kwa watoto wa kike na itawachukulia hatua kali wote
watakaobainika kufanya hivyo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt.Seif Shekalaghe amesema watoto wa kike
28 wameripotiwa kuwa na mimba katika kipindi cha mwezi Desemba 2017 hadi sasa
na Serikali ya Wilaya kupitia Operesheni tokomeza Mimba imefanikiwa kuwakamata
watuhumiwa 15 na kati ya hao wawili wamehukumiwa miaka 30 jela kila mmoja.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu
Waziri wa Madini , Mhe.Stanslaus Nyogo amewashukuru viongozi wa Wilaya kuleta
mafanikio katika elimu ikiwa ni pamoja na ongezeko la ufaulu.
Katika
hatua nyingine Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia
Suluhu Hassan mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Upasuaji Hospitali ya
Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING
THEATER” amewataka Watumishi wa Afya kufanya kazi kwa bidii
Aidha,
amesema Serikali itahakikisha inaboresha huduma za afya ikiwa ni pamoja na
ujenzi wa vituo vya Afya katika kila kata na kuboresha huduma za Afya ya Mama
na Mtoto ili kupunguza Vifo vya mama na mtoto.
Naye
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Josephat Kandege amesema Serikali
imekusudia kujenga vituo vya Afya 286 kufikia mwisho mwa mwaka
2017/2018 lengo likiwa ni kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa
kupunguza mrundikano wa wagonjwa katika Hospitali za Wilaya.
Mbunge
wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe.Mashimba Ndaki amesema pamoja na kuendelea
kuboresha sekta ya Afya kwa kujenga miundombinu, ni vema Serikali ikaajiri
watumishi wa Idara ya Afya kukabiliana na upungufu uliopo.
Mhe.Makamu
wa Rais amemaliza Ziara yake Wilayani Maswa ambapo amefungua Jengo la Upasuaji
la Upasuaji Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA
SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” na kuzungumza na wananchi katika Uwanja wa
Nguzo Nane.
NAIBU WAZIRI DK. NDUGULILE AFANYA ZIARA WILAYA YA SHINYANGA KUKAGUA HUDUMA ZA AFYA
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amepiga marufuku
dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye maduka ya watu binafsi kwani serikali
haitaki kuingia kwenye matatizo ya uhaba wa dawa kwenye sehemu zake za kutolewa
huduma ya afya.
Dk. Ndugulile
amepiga marufuku dawa za serikali kuonekana zikiuzwa kwenye maduka ya watu
binafsi wakati wa ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Shinyanga,
Februari 21,2018 akikagua shughuli za huduma za afya zinavyotolewa kwa
wananchi pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kujiunga na Bima ya afya ya jamii CHF
iliyoboreshwa.
Dk. Ndugulile alisema katika bajeti
ya mwaka wa fedha (2017-18) serikali kwenye bajeti ya wizara hiyo ya afya
imetenga jumla ya shilingi bilioni 270, tofauti na mwaka wa fedha (2015-16)
ambapo zilikuwa milioni 30 hivyo hawatarajii kusikia sehemu za kutolewa huduma
zake za kiafya kuwa zina upungufu wa dawa.
Akiwa katika hospitali ya Rufaa
ya mkoa wa Shinyanga na Kituo cha Afya cha Kambarage manispaa ya Shinyanga na
kukagua bohari za dawa, Dk. Ndugulile alitoa tahadhari kwa wauguzi kuwa ni
marufuku dawa hizo za serikali kukutwa zinauzwa kwenye maduka ya watu binafsi
na ikibainika watachukuliwa hatua kali.
“Serikali ya awamu hii ya tano
imedhamiria kuboresha huduma za afya hapa nchini, na ndio maana hata bajeti
yake imetolewa ni ya fedha nyingi hivyo sisi kama wizara husika hatutarajii kuwepo
kwa upungufu wa dawa kwenye sehemu za huduma za afya”,alieleza.
Pia aliwataka wananchi kujiunga
na Bima ya afya ya jamii CHF iliyoboreshwa, ili kuwa na uhakika wa kupata
matibabu hasa pale watakapougua na kukutwa hawana pesa ambapo wataweza kutibiwa
kwa shilingi hiyo 10,000/= ili kuokoa maisha yao.
Naye kiongozi wa Mradi wa
Maendeleo ya Tuimarishe Afya (HPSS) kutoka makao makuu Dodoma Profesa Manoris
Meshack, alisema mradi huo wa Bima ya afya ya jamii CHF ulianza mwaka 2011
mkoani Dodoma, na baada ya kufanya vizuri mwaka 2015 ukaongezwa katika mikoa miwili
ya Shinyanga na Morogoro.
Alitaja takwimu za kaya katika
mikoa hiyo mitatu zilizojiunga na CHF iliyoboreshwa hadi sasa kuwa ni 318,334
sawa na asilimia 26 kati ya kaya 1,220,413, na hadi kufikia Disemba 2017
kupitia uandikishaji wa wanachma wamekusanya shilingi bilioni 7,027,605,547.
ambapo shilingi bilioni 2,435,194,000 ni malipo ya tele tele.
Nao baadhi ya wazee kati ya
kumi wasiojiweza ambao walikatiwa Bima hiyo ya Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa
na Naibu Waziri huyo wakati wa ziara hiyo,Mohamed Mkumbola na Regina Kulwa
waliipongeza serikali kwa kujali makundi hayo maalumu, na kuomba wazee wote
wakatiwe Bima hiyo pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi wajiunge.
SERIKALI YAAGIZA VIWANDA NCHINI KUTUMIA BARCODES ZA GS1
Ametoa
agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 22, 2018) wakati akifungua Mkutano wa Sita
wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa simbomilia (barcodes). Hadi sasa GS1 ina
wanachama 2000.
“Natoa
wito kwa wenye viwanda kutumia GS1 Tanzania kutangaza na kuuza bidhaa zenye
ubora katika maduka ya kimataifa, ambapo pia bidhaa zao zitachangia katika
ulipaji wa kodi kwa usahihi”.
Amesema
matumizi ya alama hiyo, iwe ndio chanzo cha kulipeleka Taifa kwenye kampeni ya
kuhamasisha jamii kununua bidhaa zilizotengenezwa nchini. Hadi sasa
Waziri
Mkuu amesema kama kila bidhaa itakuwa na utambuzi wa Taifa kiambishi “620”,
wataweza kuwa na takwimu sahihi za wazalishaji ambao wanatambulika.
Pia
Waziri Mkuu amesema utambuzi wa bidhaa zinazozalishwa nchini ukifanyika kwa
kutumia GS1 kila duka litalipa kodi kwa kila bidhaa inayouzwa.
Hata
hivyo Waziri Mkuu amesema barcodes ni muhimu kwa sababu zinawawezesha
wajasiriamali kuuza bidhaa zao katika maduka rasmi ya nje na ndani ya Tanzania.
Amesema
miaka ya nyuma kabla ya kuanzishwa kwa GS1 Tanzania, wazalishaji wa bidhaa za
Tanzania walilazimika kwenda nje ya nchi yetu
kutafuta barcodes ili waweze kuuza bidhaa zao.
Waziri
Mkuu amesema hali hiyo iliifanya Tanzania kuwa wategemezi na kuchangia
kuzalisha ajira kwa ajili ya nchi nyingine kwa kununua barcodes zao.
“Tangu kuanzishwa kwa chombo chetu, tumejinasua kutoka katika utegemezi huo.
Pia
Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na mipango iliyowekwa na GS1 Tanzania ya
kuhakikisha kwamba mazao ya kilimo yanapatiwa barcodes na
kuwaelimisha wananchi kuhusu alama hizo.
Mkutano
huo umehudhuriwa na Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhandisi
Stella Manyanya, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara SMZ, Balozi Amina Salum
Ally, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof.
Elisante Ole Gabriel.
Wengine
ni Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Dkt. Gidion Mazara, Wakuu wa Taasisi na
Wadau wa GS1 kutoka Tanzania Bara na Visiwani (TBS, BRELA, TANTRADE, ZNCIAAL,
COSTECH na Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania Bi. Fatuma Kange.
MAKAMU WA RAIS: ELIMU YA JUU NI NGUZO MUHIMU KATIKA KUFIKIA TANZANIA YA VIWANDA
Makamu wa Rais wa amesema hayo ,wakati wa akifungua kongamano la elimu ya juu na Tanzania ya viwanda lililofanyika mjini Bariadi, lililokuwa limeandaliwa na Chuo kikuu huria Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
Amesema kutokana na umuhimu huo Serikali imeamua kuwekeza katika Elimu na Dira ya Maendeleo ya Mwaka 2025 imeweka elimu kuwa kipaumbele cha juu kwa kuwa ndiyo kitovu cha kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika jamii.
“Ninyi ni mashahidi kuwa Serikali imeweka mkazo kwenye elimu, tumeanza na shule za msingi, sekondari lakini pia tumeongeza bajeti kubwa kwenye mikopo ya Elimu ya Juu na tutakwenda polepole mpaka tuhakikishe Watanzania wanapata elimu ya kutosha ili kuendana na uchumi wa Viwanda” alisema.
Ameongeza kuwa lengo kuu la ni Serikali kuongeza kipato cha wananchi kupitia viwanda ambavyo vitaongeza thamani ya mazao yanayozalishwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Aidha, amewataka washiriki wa Kongamano hilo kuja na majibu ya ni kwa namna gani wahitimu wa Vyuo Vikuu walivyojipanga katika suala la uzalishaji viwandani na kubainisha ikiwa fani, stadi na mafunzo waliyosomea yatakidhi mahitaji ya viwanda vinavyotakiwa kujengwa hapa nchini.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Prof.Elifas Bisanda amesema nchi zote zilizoendelea katika Sekta ya Viwanda zina msukumo mkubwa na udahili mkubwa wa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, hivyo upo umuhimu wa kujadili Mchango wa Elimu ya Juu katika Tanzania ya Viwanda.
Aidha, Prof.Bisanda ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Simiyu kutumia fursa ya uwepo wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa ajili ya kujiendeleza katika masomo ya elimu ya juu.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataka waajiri wote mkoani humo kuwaruhusu watumishi kwenda kusoma kwa ajili ya kuwaandaa watumishi hao kuwa na maarifa ya kutosha.
“ Tuna shida kwenye ofisi zetu tena wakati mwingine ni roho mbaya tu, mtumishi anaomba kwenda kusoma Mkurugenzi anamkatalia, tukitaka nchi yetu iende mbele turuhusu watu wasome, miaka ijayo tunataka mkoa wetu ushindane hatuwezi kushindana kama hatutawekeza kwenye maarifa” alisisitiza Mtaka.
Wasomi waliowasilisha mada mbalimbali katika Kongamo hilo la Elimu ya Juu na Tanzania ya Viwanda ni pamoja na Prof. Rwekaza Mukandala, Prof.Elifas Bisanda , Prof.Uswege Minga, Dkt. Adolf Rutayuga, Dkt. George Mgode, Balozi Nicholas Kuhanga na Mhe.Anthony Diallo.
Kongamano hili lililokuwa na Mada kuu isemayo: “Mustakabali wa Elimu ya Juu kuelekea Tanzania ya Viwanda” limehudhuriwa na wanafunzi wa shule za sekondari, walimu, Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka Mwanza pamoja na viongozi wa Serikali.










