NAIBU WAZIRI MADINI ATUA MKOANI SONGWE KWA ZIARA YA KIKAZI
Maeneo mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika kata ya Saza, Wilayani Songwe ambapo atazungumza pia na wafanyakazi wa mgodi huo.
Sambamba na hayo pia Naibu Waziri wa Madini atazungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano ulioandaliwa Mara baada ya kutembelea maeneo ya uchimbaji.
Mara baada ya kuwasili katika Mkoa wa Songwe Mhe Biteko amesifu juhudi za mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo kutokana na uwajibikaji mkubwa katika kuwasemea wananchi wa jimbo hilo hususani katika kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta ya Madini.
Alisema kuwa mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea wananchi wake katika katika kuchochea shughuli za maendeleo ili kuongeza ufanisi wa maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.
Aidha, Mhe Biteko alimuhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Songwe kuwa Wizara ya Madini Kupitia sheria mpya ya madini kutakua na Tume ya Madini ambayo kimuundo itakua na Afisa madini wa Mkoa wa Songwe ambapo utapelekea kuwa na Ofisi hiyo ya Madini.
Mhe Biteko aliutaka uongozi wa Wilayani na Mkoa wa Songwe kuongeza zaidi ushirikiano na Chama Cha Mapinduzi kwani ndicho Chama chenye dhamana ya kuisimamia na kuikosoa serikali pindi inapoenda mrama.
Alisema kuwa baadhi ya watumishi wanapaswa kutambua kuwa wanatekeleza wajibu wa matakwa ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2015-2020 hivyo haijalishi kuwa wanaipenda ama wanaichukia wanatakiwa kutekeleza ilani pasina kuogofya.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo alisisitiza kuwa ujio wa Naibu Waziri wa Madini utakuwa chachu ya mwanzo mzuri wa maendeleo ya wananchi kupitia sekta hiyo.
Awali akisoma taarifa ya Mkoa wa Songwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe Samwel Jeremiah ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songwe alizitaja changamoto zinazoukabili Mkoa huo katika sekta ya madini kuwa ni pamoja na kukosekana Ofisi ya Madini ya Mkoa.
Changamoto zingine ni pamoja na ukosefu wa Vifaa pamoja na elimu ndogo juu ya sheria zinazosimamia shughuli za uchimbaji Madini, pamoja na wachimbaji wengi kutokuwa waaminifu katika ulipaji wa maduhuli ya serikali yatokanayo na shughuli za uchimbaji wa Madini.
Naibu Waziri wa Madini atakuwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe kwa siku mbili kuanzia leo 22 Februari 2018 na kufika ukomo hapo kesho 23 Februari 2018 ambapo ataelekea mkoa wa Rukwa.
RAIS JPM AWASILI UGANDA, AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MUSEVENI
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amewasili nchini Uganda ambapo atahudhuria mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 23 Februari, 2018 Mjini Kampala. Baada ya kuwasili amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.
|
DCC LUSHOTO YASITISHA MPANGO WA UJENZI WA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI
Mwenyekiti wa Kikao hicho ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Lushoto January Lugangika alisema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya
kuwepo sintofahamu kati ya Madiwani wa halmashauri hiyo na viongozi wengine juu
ya suala hilo. .
Hivi karibuni kumekuwepo na mvutano mkubwa kati ya
viongozi hao juu ya wapi pajengwe majango ya makao makuu ya Halmashauri hiyo. Baadhi ya
viongozi wanadai utaratibu wa fedha za manunuzi haukufuatwa katika
kufikia maamuzi ya kujenga jengo la Halmashauri katika eneo la Kwehangala na
kuacha majengo yaliyokwisha jengwa Bumbuli kwa gharama ya Sh. Milioni 700.
Kutokana na mvutano huo, Mkuu huyo wa Wilaya
amesema kikao kiliafiki kisitishe zoezi hilo mpaka maelewano
yatakapopatikana. ” Wajumbe wameshauri suala la kuhamisha makao makuu lisitishwe
hadi hapo utakapopatikana utangamano, kwani tayari imeonekana kuna mgogoro ambao
umeleta utengano kwa viongozi” Alisema Lugangika . Mbunge wa
jimbo hilo, January Makamba alikiri kuwepo kwa mvutano huo ambao alisema hauna
tija katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Bumbuli.
Makamba alisema ni vyema kama viongozi
wakazungumzia suala la maendeleo mfano;maji,barabara,umeme,nyumba za watumishi
badala ya kila siku kuzungumzia wapi kujengwe jengo la halmashauri. Alishauri
kuwa wananchi washirikishwe katika suala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu
ya kutosha juu ya hoja ya kuhamisha halmashauri kwa kuwa ndio wenye chombo chao
badala ya viongozi kuamua wao pekee.
“Suala hilo nakubaliana na maoni wa kikao cha DCC
tulisitishe kwani kwa sasa hatuna shida na majengo ya halmashauri kwa sababu
majengo tunayo ambayo hatulipii kodi ya pango. Sasa hivi tuzungumzie maendeleo
kwani wananchi mwaka 2020 hawatatudai majengo ya halmashauri bali watatudai
maendeleo juu ya huduma muhimu za jamii alisema Makamba. Hivi karibuni
baadhi ya Madiwani wa Halmashauri hiyo walipiga kura ya kupitisha azimio
la kujenga jengo hilo la halmashauri huku Madiwani nane wakigoma kupiga
kura kwa madai kuwa hawawezi kupiga kura wakati kuna ukiukwaji wa kanuni na
utaratibu ktk kitengo cha manunuzi.
Madiwani hao nane ambao waligoma kupiga kura
kupitisha azimio hilo mnamo January 18 mwaka huu walimuomba Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kuingilia kati mgogoro na kuzuia walichokiita
ukiukwaji wa utaratibu wa manunuzi pamoja na maelekezo mbalimbali ya
viongozi juu ya mpango huo.
Pia walimuomba aingilie kati na kuchukua hatua
dhidi ya ubadhirifu wa fedha za umma na ukiukwaji wa utaratibu wa
uendeshaji wa halmashauri na kudharau kwa makusudi maelekezo yaliyotolewa na
viongozi mbalimbali wa serikali kuu.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Amir Shehiza
alisema kuwa baraza ni chombo chenye maamuzi sahihi hivyo alikitaka Kikao
hicho cha DCC kuacha kuingilia Kazi za baraza.
MAJALIWA AKUTANA NA WADAU WA PAMBA JIJINI MWANZA

Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba akizungumza katika mkutano wa wadau wa zao la pamba ulioitishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Februari 21, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 21, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 21, 2018. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na kushoto ni Waziri wa Fedha na Uchumi, Dkt. Philip Mpango

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa zao la pamba kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza, Februari 21, 2018

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda (TCCIA) mkoa wa Mwanza, Christopher Mwita Gachuma wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza kuongoza kikao cha wadau wa zao la pamba alichokiitisha, Februari 21, 2018.Watatu kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula na kushoto ni Mbinge wa Sumve, Richard Ndassa.
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
MASAUNI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI KUJADILI UPUNGUZAJI WA AJALI

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.

Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu (kulia meza kuu), akizungumza wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.

Mjumbe kutoka Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Geoffrey Silanda, akichangia hoja wakati wa wakati wa kikao cha kujadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Wengine ni Mwakilishi kutoka Wizara ya Elimu, Hidaya Mohamed na Mwakilishi kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA), Elimboto Mtatulu (kushoto).

Wajumbe wa kikao kinachojadili mikakati ya kupunguza tatizo la ajali za barabarani kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakishiriki kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
WAKAZI WA MAGURUWE WAISHUKURU SERIKALI YA AWAMU YA TANO
Wakazi wa kijiji cha Maguruwe wilayani #Mvomero Mkoani
Morogoro wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwathamini
na kuweza kufika kwenye kijiji hicho mteule wa Rais ambaye ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, #TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo, kwa kuwa hakuna kiongozi wa ngazi ya Uwaziri ambaye amewahi kufika
kwenye eneo hilo.
Kutokana na Waziri Jafo kuwa Waziri wa kwanza kufika
kwenye kijiji hicho wazee wa kimila wa kijiji hicho walimsimika na
kumpa heshima maalum ya waluguru.
Wakizungumza huku wakiwa wamejawa na furaha, Wananchi
hao wamesema kijiji chao ambacho kipo juu kabisa ya safu za
milima ya Ulugulu hakuna kiongozi yeyote wa ngazi ya uwaziri aliyewahi kufika maeneo hayo kwa kuwa barabara
zake hazipitiki kirahisi.
Wamesema wamefurahishwa na kiongozi huyo kwa kuweza kuwafikia
walipo hali ambayo imewafanya kujisikia furaha.
Katika ziara hiyo ya kikazi, Waziri Jafo amefanikiwa
kuzindua vyumba vitatu vya madarasa vilivyojengwa na Taasisi ya CDTF.
Hata hivyo, kutokana na changamoto kubwa
ya barabara katika eneo hilo, Waziri Jafo alimuagiza meneja wa TARURA wilaya ya Mvomero kufanya
tathmini ya barabara hiyo ili serikali ione jinsi ya kuifanyia kazi hapo baadae ili wananchi hao waweze kuondokana na
adha hiyo.
WAZIRI MWIGULU:GEREZA JIPYA CHATO KUPUNGUZA MSONGAMANO MAGEREZANI NA GHARAMA ZA USAFIRISHAJI WA WAHARIFU
Akizungumza
katika hafla fupi ya kuzindua wa Gereza
hilo , Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt.Mwigulu Nchemba alisema katika Wilaya ya Chato kumekuwa na changamoto ya kutokuwa na Gereza na kulazimika kupeleka waarifu katika Gereza la Biharamulo hivyo gereza hilo litapunguza gharama za usafirishaji wa waharifu ambao wa walikuwa wakipelekwa magereza ya mbali ili kuhifadhiwa.
hilo , Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt.Mwigulu Nchemba alisema katika Wilaya ya Chato kumekuwa na changamoto ya kutokuwa na Gereza na kulazimika kupeleka waarifu katika Gereza la Biharamulo hivyo gereza hilo litapunguza gharama za usafirishaji wa waharifu ambao wa walikuwa wakipelekwa magereza ya mbali ili kuhifadhiwa.
“
Ujenzi wa Gereza hili utasaidia kuendeshwa kwa mashitaka kwa kufuata ratiba kwa
kuwa wakati mwingine ratiba zinaingiliana lakini pia changamoto za magari,
mafuta na umbali zilikuwa kikwazo kikubwa katika uendeshaji wa mashitaka hivyo kusababisha
watu wenye matatizo mbalimbali kuendelea kushikiliwa katika magereza kwa muda
mrefu huku akikosa haki zake hata kama hana hatia”Alisema Mwigulu.
Aidha,
Dkt Mwigulu nchemba ametoa rai kwa maafisa na askari wa gereza kuhakikisha wanatunza
majengo na miundombinu ya gereza hilo na kufanya kazi kwa uadilifu ili maadili
yaliyowekwa katika magerezani yanazingatiwa .
”
licha ya kazi nzuri inayofanywa na viongozi walio wengii zipo taarifa kwenye
baadhi ya magereza watumishi hawazingatii maadili ya kazi kwa kuwa wengine
wamekuwa wakiwapa waalifu simu bila kujua wanafanya mawasiliano na watu wa
namna gani vitendo hivi vina hatarisha usalama wa gereza na askari
pia”Alisisitiza Mwigulu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel amelitaka jeshi la magereza kupitia gereza la Wilaya ya Chato ambalo limejengwa kijiji cha Nyangomango kutumia maeneo yaliyopo na watakayopewa na Mkoa kuzalisha mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Mkoa na taifa.Ameongeza kuwa jeshi la magereza limejijengea heshima kubwa nchini kwa kuzalisha vifaa bora kama vile samani za nyumbani na ofisini, viatu hivyo jeshi linaweza kuleta mapinduzi ya kimkakati ya kiuchumi.
Robert Gabriel amelitaka jeshi la magereza kupitia gereza la Wilaya ya Chato ambalo limejengwa kijiji cha Nyangomango kutumia maeneo yaliyopo na watakayopewa na Mkoa kuzalisha mazao mbalimbali ya kilimo na mifugo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Mkoa na taifa.Ameongeza kuwa jeshi la magereza limejijengea heshima kubwa nchini kwa kuzalisha vifaa bora kama vile samani za nyumbani na ofisini, viatu hivyo jeshi linaweza kuleta mapinduzi ya kimkakati ya kiuchumi.
Naye
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera Nehemia Nkondo ameeleza katika taarifa kuwa
ujenzi wa Gereza la Chato ulianza mwaka 2011 katika kijiji cha Nyangomango kwa
kupata hekari 50 kutoka kwa wananchi ambapo serikali ilitoa zaidi ya Shilingi
bilioni 1.5 mpaka sasa mradi umetumia kiasi cha shilingi milioni 613.6 sawa na
asilimia 40%. kiasi cha Shilingi milioni 903.6 zinaendelea kutumika ambapo kuna
ujenzi wa mabweni 4 ya wafungwa yenye uwezo wa kuhifadhi wafungwa 50 kila moja,
uvutaji wa maji na ujenzi wa mabweni 2 ya wanawake.Kazi zinazoendelea ni ujenzi
wa jengo la utawala, nyumba za watumishi.
BENKI ZAWAHAKIKISHIA WAFANYABIASHARA MIKOPO
Pia
viongozi wa benki hizo wamesema wako tayari kusaidia katika uwekezaji wa
miundombinu ya aina yeyote ama eneo litakalohitaji mkopo wa fedha ili
kufanikisha mchakato wa ununuzi wa pamba katika msimu huu ikiwa ni pamoja na
kusaidia ujenzi wa maghala.
Hayo
yamesemwa leo (Jumatano, Februari 21, 2018) na viongozi wa benki mbalimbali
nchini katika mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa uliowahusisha
wafanyabiashara wote wa pamba , Wakuu wa Mikoa ,Viongozi wa Halmashauri na
wadau wote.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti viongozi wa benki za NMB, CRDB, TIB, EXIM, AZANIA,
Mkombozi, Bank of Africa, Equity na Eco waliwahakikishia wafanyabiasha hao
mbele ya Waziri Mkuu kwamba wana fedha za kutosha na wako tayari kuwapa mikopo
ili wakanunue pamba mara msimu utakapoanza.
Akizungumza
katika mkutano huo, Waziri Mkuu amewataka wanunuzi wa zao hilo kuandikisha
katika ofisi ya Mkurugenzi wa Bodi ya Pamba kiasi cha pamba wanachohitaji
kununua pamoja na maeneo ambayo wanatamani kwenda kununua.
Waziri Mkuu amesema suala hilo litaiwezesha bodi kufahamu idadi ya
wafanyabiashara watakaonunua pamba pamoja na kiasi wanachohitaji na eneo
husika. “Serikali itaendelea kusimamia zao hilo kikamilifu.”
Amesema kwa sasa wanauhakika kuwa pamba yote itanunuliwa kwa sababu benki
zimewathibitishia kwamba ziko tayari kuwakopesha wafanyabiasha, hivyo wadau
wote watambue kuwa Serikali itashirikiana nao hadi katika hatua za mwisho za
ununuzi.
Waziri Mkuu aliwahakikishia wafanyabiashara hao kwamba maombi waliyoyatoa
kuhusu uboreshaji wa mauzo ya zao hilo yatayafanyiwa kazi na Serikali
itaendelea kusimamia zao hilo ili ununuzi wake uwe rahisi.
Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba amesema
wamejipanga kikamilifu katika kudhibiti ubora wa pamba, ambapo amewataka
viongozi wa maghala wasipokee pamba chafu.
Pia amewataka wakulima wa pamba wasithubutu kuchanganya na maji, mawe au
mchanga kwa sababu wataharibu soko. Serikali itapambana na watu wote
wakaothubutu kuharibu zao hilo kwa kcuhukua hatua kali za kisheria kwani huo ni
uhujumu uchumi.
Aliendelea kusema kuwa uamuzi wa Serikali kusimamia ongezeko la
uzalishaji wa zao la pamba unakwenda sambamba na mazao mengine makuu ya
biashara ambayo ni korosho, chai, tumbaku, kahawa na mahindi kwa upande wa chakula.
Dkt. Tizeba amesema inatazamiwa kuwa ifikapo 2021 mchango wa mazao katika
pato la Taifa unakadiriwa kufikia sh. trilioni 13.6, ambapo yataliwezesha Taifa
kuvuka mstari wa kiwango cha umasikini.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amesema kuwa zao la pamba
lina mchango mkubwa katika kukuza uchumi, hivyo watahakikisha zao hilo
linaendelea kukua.
Dkt. Mpango amezitaka benki zichukue tahadhari kwa mikopo chechefu
hivyo wajiridhishe kama wakopaji wote wanatumia mikopo hiyo kwa mujibu wa
makusudio.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.
Waziri Mkuu: Watanzania jiepusheni na Dawa Za Kulevya
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wakiwemo wakazi wa mkoa wa Mwanza kuachana na biashara ya dawa za kulevya.
Pia Waziri Mkuu amegiza vijana nchini waelimishwe madhara mbalimbali yanayosababishwa na matumizi ya dawa za kulevya ili wajiepushe nazo.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumanne, Februari 20, 2018) alipozindua kliniki ya methadone kwa ajili ya waathirika wa dawa za kulevya.
Alizindua kliniki hiyo iliyopo kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza ya Sekou Toure akiwa katika siku ya sita ya ziara yake ya kikazi mkoani Mwanza.
“Serikali imejizatiti katika vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya, hivyo nawataka wananchi wasijishughulishe nayo. waache kutumia, kusambaza na kuuza.”
Pia aliwaomba wananchi washirikiane na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na dawa hizo.
Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers Siyanga aliishukuru Serikali kwa kutambua madhara ya dawa za kulevya na kuchukua hatua.
Bw. Siyanga alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa waathirika wa dawa za kulevya kwenda katika kliniki za methadone ili wapatiwe matibabu yatakayowafanya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Naye, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw. John Mongella alisema kuwa, mkoa huo ni miongoni mwa waathirika wakubwa wa biashara ya dawa za kulevya. Aidha, aliongeza kuwa bado kuna watu wanaoendeea kujishughulisha na biashara hiyo na kwamba Mkoa unaendelea kupambana nao.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndungulile alisema dawa za kulevya zinasababisha madhara makubwa katika sekta ya afya kwa kuwa yanachangia kusambaa kwa magonjwa mbalimbali yakiwemo ukimwi na kifua kikuu.
Pia alisema kwa sasa dawa za methadone zinazotolewa kwa waathirika wa dawa za kulevya wanazipata kutoka kwa wahisani mbalimbali. Hata hivyo, Serikali imepanga kuingiza suala hilo katika bajeti ijayo ili ianze kuagiza yenyewe.
Baadhi ya vijana waliokuwa wanatumia dawa za kulevya mkoani Mwanza akiwemo, Nyamizi Sospeter na Abdul Abdallah, waliishukuru Serikali kwa kuanzisha vituo vya methadone.
Nyamizi alitumia dawa za kulevya kwa muda wa miaka saba na muda wote huo alikuwa akiisumbua familia yake kutokana na matukio mbalimbali ya kihalifu aliyokuwa akiyafanya ili apate fedha za kununulia dawa hizo.
Naye Abdul Abdallah alisema alitumia dawa za kulevya aina ya heroine kwa takribani miaka 20 na muda wote huo alikuwa anakaba watu ili apate fedha za kununulia dawa hizo.
“Naishukuru Serikali kwa kuanzisha kliniki ya methadone na sasa nimeacha mimi pamoja na mke wangu. Najiona binadamu maana nilikuwa mwizi, mchafu kwani nilikuwa nakaa mwezi bila kuoga na hata kutengwa na jamii.”
Kwa pamoja waathirika hao wa dawa za kulevya waliiomba Serikali kuwasaidia kwa kuwapa elimu ya ujasiriamali ili waweze kupata ujuzi utakaowawezesha kufanya kazi na kupata kipato kitakachowasaidia kuendesha maisha yao.
Awali, Waziri Mkuu alizindua muongozo wa uendeshaji wa nyumba za waathirika wa dawa za kulevya (Soba Houses) ambao unalenga kuwawezesha wamiliki wa nyumba hizo kuziendesha vizuri na kuwasaidia ipasavyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO, FEBRUARI 21, 2018.
Dodoma: 18 wapoteza maisha #Kipindupindu
Watu 18 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mkoani Dodoma ndani ya miezi minne huku zaidi ya watu 470 wakiugua ndani ya muda huo.
Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Dk. James Kiologwe, alisema jana kuwa ugonjwa huo tangu uingie Dodoma Oktoba, mwaka jana, hadi sasa umesababisha vifo hivyo na idadi hiyo ya wagonjwa.
Alisema wagonjwa wengi wanatoka katika wilaya za Mpwapwa na Chamwino na miongoni mwa sababu za kuenea kwa ugonjwa huo ni unywaji wa maji ya kwenye madimbwi ambayo si safi na salama.
Mganga mkuu huyo alisema ugonjwa huo ulianza Oktoba, mwaka jana, katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma lakini zaidi katika wilaya hizo mbili.
“Kuna wakati ulipungua, lakini umerudi tena na umekuja sana kwa kasi mwezi huu wa pili,” alisema.
Aidha, Dk. Kiologwe alisema hadi juzi kulikuwa na wagonjwa wapya 26 na 22 kati yao waliruhusiwa kurudi nyumbani na wanatoka Mpwapwa na Chamwino.
Kuhusu hatua zilizochukuliwa, Dk. Kiologwe alisema jitihada zinaendelea kukabiliana na ugonjwa huo kwa kugawa ‘Water Guard’ vidogo 250,000 kwa ajili ya kusafisha maji na kuweka katika vyanzo vya maji.
Aliwataka wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanachemsha maji ya kunywa na kuzingatia kanuni zote za usafi, ili kuepukana na ugonjwa huo.










