• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Vifaranga 5,000 kutoka Kenya vyateketezwa

Picha kwa hisani ya mtandao(haihusiani na tukio)


Vifaranga 5,000 na trei za mayai 416 kutoka nchi jirani ya Kenya ambavyo vilikamatwa vikiingizwa nchini kinyume na sheria vimeteketezwa moto kwa kuzingatia haki za wanyama.
Vifaranga hao walikamatwa katika eneo la mpakani mwa Kenya na Tanzania Namanga ambapo baada ya kukamatwa vifaranga wa kuku wa mayai 5000 wenye thamani ya Tsh 11,500,000 na Trei 416 zenye mayai, yenye thamani ya 3,120,000/ kwa pamoja viliteketezwa kwa moto kwa kuzingatia haki za wanyama (Animal welfare) ambapo kabla ya kuteketezwa mifugo hiyo ililazwa kwa kutumia dawa aina ya Farmaldehyde na kuhakikisha wamekufa kabla ya kuchomwa.

Mayai hayo pamoja na vifaranga vimekamatwa vikiingizwa nchini kinyume na sheria, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la chakula (FAO) ya mwezi Desemba ilitoa taadhari kuwa nchi ya Tanzania pamoja na nchi jirani Kenya na Uganda na nchi nyingine za Afrika ziko hatarini kuambukizwa mafua makali ya ndege


Share:

KAMATI YA NIDHAMU YA TFF YAMFUNGIA JUMA NYOSO MECHI TANO



Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imemfungia Mchezaji wa Timu ya Kagera Sugar, Juma Nyoso kutocheza mechi tano baada ya kumtia hatiani kwa kutaka kumpiga shabiki, kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ambapo timu yake ilicheza na Simba.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Nidhamu ya TFF imempiga faini ya Shilingi milioni moja Juma Nyoso.
Vilevile, Kamati hiyo imemfungia Mchezaji wa Transit Camp, Mohamed Ussi kutocheza mechi tatu kutokana na utovu wa nidhamu kwa kutaka kumpiga  mwamuzi wa mchezo. 
Ussi alifanya kosa hilo katika mechi namba 48 ya kundi C Ligi Draja la Kwanza Tanzania Bara.Kamati ya Nidhamu pia imempiga faini ya shilingi laki tatu Ussi


Share:

KENYA: Mwanasheria mkuu ajiuzulu




Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai amejiuzulu nafasi hiyo aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka sita. Na tayari Rais Uhuru Kenyatta amemteua Jaji Paul Kihara Kariuki kushika wadhifa huo.

Kwa upande wake, Rais Uhuru Kenyatta amemshukuru Profesa Githu kwa namna alivyolitumikia Taifa kwa weledi katika nafasi yake ya mwanasheria mkuu wa Serikali.

Profesa Muigai ametangaza leo kujiuzulu wadhifa huo alioteuliwa Agosti 27, 2011.

"Nimepokea kwa masikitiko uamuzi wa mwanasheria mkuu Githu Muigai. Namshukuru kwa huduma yake katika kipindi cha miaka sita na nusu. Nimemteua Jaji Paul Kiharara Kariuki,” Rais Uhuru Kenyatta amechapisha katika mtandao wake wa Twitter.

Profesa Muigai atakumbukwa kwa namna alivyokuwa mstari wa mbele kuwatetea watuhumiwa dhidi ya uhalifu wa binadamu uliotokana na vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007 na kuendelea hadi 2008.

Vurugu hizo zilifunguliwa kesi kwenye Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) iliyopo The Hague nchini Uholanzi na aliyekuwa mwendesha mashtaka mkuu, Luis Moreno-Ocampo.

Orodha ya watuhumiwa hao iliyofahamika kama ‘Ocampo six’ ni Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto wakati huo alikuwa waziri wa Elimu, mawaziri wengine wa zamani Henry Kosgey, Francis Kirimi Muthaura, aliyekuwa mkuu wa polisi Mohammed Hussein Ali na mwandishi wa habari Joshua Arap Sang.

Pia, Profesa Muigai aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari vya Kenya akimtaka Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Fatou Bensouda kuliheshimu Taifa la Kenya kwa kuonyesha weledi wakati wa kuendesha kesi iliyomkabili Rais Uhuru na wenzake, kwamba Kenya siyo Taifa lililoshindwa kutekeleza wajibu wake.

Hata hivyo, Profesa Muigai mwaka 2016 alipata changamoto baada ya muungano wa makanisa ya Kipentekoste kumtaka kujiuzulu kwa madai ya kushindwa kuishauri Serikali kuhusu masuala ya kidini.

Muungano wa makanisa hayo ulitoa hoja hiyo kufuatia kusajiliwa kwa kikundi cha watu waliokuwa wakidai hawamuamini Mungu, kwa madai anakwenda kinyume na katiba inayotambua uwapo wa Mungu.
Share:

ACT WAZALENDO NA UJUMBE WA BARAZA LA MAASKOFU


Chama cha ACT-Wazalendo, kimesema ujumbe wa Kwaresma mwaka 2018 uliotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kuhusu masuala  ya kisiasa, kichumi na kijamii unaonyesha jinsi demokrasia inavyominywa nchini.
TEC imetoa ujumbe huo Februari, 2018 ulioandikwa na maaskofu wote 35 wa baraza hilo, wakiongozwa na Rais wake, Mhashamu Tarcisius Ngalalekumtwa upo katika kitabu cha kurasa 20 ikiwa ni maandalizi ya ibada ya siku 40, kipindi ambacho ni cha mfungo wa kukumbuka siku 40 za Kristo kufunga na kwenda jangwani.
Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu amesema, “Tunawapongeza  sana viongozi wetu wa dini kwa kujitokeza waziwazi kuonyesha ugandamizaji wa haki unaoendelea nchini.”

“TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 umalizike.” Katika ujumbe huo,  TEC wamezungumzia hali ya kisiasa na kusema uamuzi wa Serikali kuzuia, maandamano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ni kwenda kinyume cha Katiba ya nchi.
Shaibu ameitaka Srikali kuondoa zuio batili la vyama vya siasa kutofanya mikutano ya hadhara ya kuzungumza na wananchi.
 Mbali na hilo, Shaibu ameiomba Serikali itoe taarifa ya uchunguzi kupotea kwa mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory  Gwanda aliyefikisha siku 84 tangu kupotea kwake sanjari na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kibondo, Simon  Kanguye.

Share:

Waziri Lukuvi Apiga Marufuku Wathamini Wanaofanya Uthamini Nje Ya Serikali



Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi leo amezindua rasmi bodi ya wathamini ambayo imeundwa kwa mujibu wa sheria ya uthamini na usajili wa wathamini ya mwaka 2016 ambayo imeanza  kutumika rasmi Januari mwaka huu.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo Waziri Lukuvi amesema kwa mujibu wa sheria wajumbe wa bodi ni lazima kutoka katika taasisi mbalimbali ikiwemo Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, ofisi ya Rais TAMISEMI, vyuo vikuu, vyama vya kitaluma vya wathamini, ofisi ya mwanasheria mkuu, taasisi ya mabenki, na bodi ya wakaguzi na wahasibu(NBAA) na kuongeza kuwa kwa muundo huo bodi inahitaji mpana mkubwa wa uwakilishi ili kutekeleza majukumu yake kwa urahisi.
 
Pia amesema kuwa serikali iliona umuhimu wa kuwa na chombo madhubuti kwa ajili ya kusimamia taaluma ya uthamini baada ya kuonekana kuwa kumekuwa na ongezeko la udanganyifu katika kazi ya uthamini hasa kwenye miradi ya serikali na ya mikopo katika mabenki baada ya Kazi hiyo ya uthamini kuwa chini ya Baraza la wapima ardhi na wathamini (NCPS).
 
Aidha ameweka wazi kwamba tasnia ya uthamini ni ya muhimu sana kwa ustawi wa uchumi kwa ujumla kwani Kazi za wathamini zunahusiana na ukadiriaji wa Mali kwa malengo mbalimbali ikiwemo kuweka rehani za mikopo kwenye mabenki, kodi za ardhi na majengo, mahesabu ya makampuni binafsi na taasisi za serikali hivyo kama Kazi hiyo haitafanywa kwa umakimi na uadilifu inaweza kuchangia kuanguka kwa uchumi na hata watu kupoteza mali sambamba na kusababisha migogoro ya ardhi.
 
Pia amebainisha masuala ambayo yanatakiwa kufanyiwa Kazi kwa haraka ili kufuta dosari zilizopo na kusema kuwa ni kudhibiti kazi ya uthamini kufanywa na watu wasiosajiliwa na bodi na wale wasio ma taaluma ya uthamini, kudhibiti udanganyifu wa thamani kwa ajili ya uthamini kwa ajili ya fidia, kodi na mikopo ya benki, kutoa na kusimamia mafunzo ya Mara kwa Mara kwa wathamini pamoja na kuandaa viwango na miongozo ya uthamini.
 
Pia Waziri ametoa onyo kwa wathamini wanaotumia udanganyifu pindi wanapofanya tathimini pamoja na wale wanaofanya kazi ya uthamini nje ya kazi au miradi ya serikali na kuwaomba wathamini wote kujisajili kwenye bodi ya wathamini ili watambulike na kupata usajili unaotambulika.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya usajili wa wathamini Dkt.Cletus E.Ndjovu amesema kuwa bodi ya wathamini ni muhimu sana katika suala la maendeleo na kuahidi kwamba watafanya kazi kwa weledi na kwa kufuata sheria ya bodi ya uthamini bila kumwonea mtu aibu ili kuleta heshima katika taaluma ya uthamini.

CHANZO: 
Florah Raphael.
MPEKUZI HURU
Share:

Waziri Mkuu Azindua Mpango Mkakati Wa Afya Moja



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mpango Mkakati wa Afya Moja na Dawati la Kuratibu Afya Moja nchini ni muhimu katika kuhakikisha Tanzania inaendelea kuwa mahala safi na salama kwa kuishi na kufanya kazi za kimaendeleo.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Februari 13, 2018) wakati akizindua mpango mkakati huo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, ambapo amesema dhana ya Afya Moja inafaa kutumika zaidi katika nchi zinazoendelea.

Waziri Mkuu amesema mbali na mpango kufaa kutumika katika nchi zinazoendelea pia hata kwa nchi zinazokaribia maeneo ya wanyama pori kama Tanzania kutokana na kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa rasilimali.

Amesema kwa upande wa nchi za Afrika hali ni hatarishi zaidi kwa kuwa Bara hilo, lina sehemu nyingi zinazokaribia mapori makubwa ya wanyama kama Bonde la Mto Kongo, ambalo mazingira yake yamekuwa ni kitovu cha magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola, Homa ya Bonde la Ufa (RVF), Marburg na mengineyo.

Waziri Mkuu amesema kwa kutambua hilo, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) na wadau wengine wa Maendeleo, imeendelea kutekeleza agenda ya Afya Moja nchini tangu mwaka 2013 ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza mjini Arusha na  Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohamed Gharib Bilal.

“Utekelezaji wa Mpango huu unakwenda sambamba na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (2015-2020) ya kujenga Taifa lenye watu wenye afya bora itakayowawezesha kuzalisha mali na kutoa huduma mbalimbali ambayo ni muhimu sana katika kufikia azma ya Serikali ya kujenga Uchumi wa Viwanda.”

Awali, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema uzinduzi wa mkakati huo ni ngao tosha kwa nchi katika kuzuia na kudhibiti magonjwa.

Alisema pamoja na kutekeleza kanuni za Kitaifa, Kikanda na Kimataifa ambazo zinahitaji ushirikiano  wa sekta mbalilmbali kwa kutumia dhana ya afya moja, mpango mkakati huo unaleta msukumo katika Ofisi ya Waziri Mkuu  kuendelea kushirikiana na Taasisi mbalimbali kudhibiti magonjwa.

Bibi Jenista alisema uratibu wa afya moja unakwenda sambamba na matakwa ya Shirika la Afya Duniani (WHO), Shirika linaloshughulika na Afya ya Wanyama (IOE) na Shirika la Kimataifa la Chakula la Kilimo (FAO) ambayo yanashirikiana katika kudhibiti magonjwa yanayoambukiza na usugu wa dawa.
Share:

Benki ya Dunia Yakana Kuishinikliza Serikali kusimamisha zoezi la bomoa bomoa Dar



Benki ya Dunia (WB) ofisi ya Tanzania imekanusha madai ya kwamba iliishinikiza Serikali kusimamisha zoezi la bomoa bomoa ya makazi ya watu kwenye hifadhi ya barabara ya Morogoro.

Madai hayo ambayo yaliripotiwa na chombo kimoja cha habari, kabla ya kusambaa kwenye mitandao ya jamii yalibainisha kwamba WB walishinikiza kusimamishwa kwa bomoabomoa kwa kuwa ndio wafadhili wa mradi wa barabara hiyo.

Ilidaiwa na vyombo hivyo kuwa WB ilitishia kusimamisha utoaji wa fedha kwa ajili ya upanuzi wa barabara hiyo, ambayo itakuwa na miundombinu ya barabara ya mwendokasi (BRT) pamoja na barabara kuu kuelekea Morogoro, mpaka hapo fidia itakapolipwa.

Akitolea ufafanuzi madai hayo leo Februari 13, 2018  msemaji wa ofisi ya WB Tanzania,  Loy Nabeta amesema ofisi yake haijatoa taarifa yoyote ya kuitaka Wakala wa Barabara (Tanroads) kisitisha bomoa bomoa hiyo.

“Tunaelewa kwamba gazeti lilifanya mahojiano na baadhi ya wamiliki wa nyumba. Benki ya dunia inathamini sera na utaratibu unaotakiwa kufuatwa kutekeleza mradi wowote ule inaoufadhili,” amesema msemaji huyo.

“Hizi ni nyaraka za kisheria ambazo tulisaini na Serikali kwa kila mradi tunaoufadhili na huwa tunahakikisha kwamba utekelezaji wake unafuata utaratibu.”

 Msemaji huyo aMEsema wamepokea malalamiko mengi mwaka jana kutoka kwa wamiliki wa nyumba zilizojengwa pembezoni mwa barabara ya Morogoro ambao walipewa notisi ya kubomoa na Tanroads.

“Tuliwawasilisha malalamiko serikalini. Desemba 22, 2017, tulipata barua toka kwa katibu mkuu wizara ya ujenzi, mawasiliano na uchukuzi kwamba watasimamisha ubomoaji wa nyumbakwenye kipande cha kuanzia Ubungo hadi Kimara,” amesema kwenye taarifa hiyo.

Amesema bomoa bomoa hiyo ambayo ilitekelezwa kuanzia Kimara hadi Kiluvya, ni mwendelezo wa utekelezaji wa upanuzi wa barabara ya Morogoro, haihusiani na mradi wowote unaofadhiliwa na WB.

Bomoa bomoa hiyo inahusisha nyumba na mejengo 1,300 ambavyo vinadaiwa kujengwa kwenye hifadhi ya barabara  ambayo ni meta 121.5 toka katikati ya barabara ya sasa. Hata hivyo, nyumba 1,000 zimekwisha bomolewa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, upanuzi wa barabara ya Morogoro (kutoka Kimara hadi Kiluvya) unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa.

CHANZO: MPEKUZI HURU
Share:

LHRC Yamvaa Makonda kuingilia mahakama



Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimesikitishwa na kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kusimamisha shughuli za mabaraza ya kata na kuingilia utendaji kazi wa mahakama.

Kimesema kuwakusanya wananchi kusikiliza kero zao za ardhi maana yake ni kutatua kero hizo bila sheria.

Akizungumza leo Februari 13, 2018 wakati akitoa tamko dhidi ya ukiukwaji wa utawala wa sheria, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Felista Mauya amesema watendaji wa Serikali wanapaswa kuheshimu utaratibu wa utendaji kazi, kuacha kuingilia majukumu ya taasisi na mihimili mingine.

Huku akinukuu alichokisema Makonda Februari 10, 2018 jijini Dar es Salaam, Mauya amesema, “ Makonda alisema ‘mahakama haitaki kuguswa kwa kisingizio cha mhimili mwingine, wamechukua nafasi ya Mungu na mimi ni mteule wa Mungu lazima niwaseme’. Huku ni kushambulia utendaji wa mahakama kinyume cha Katiba aliyoapa kuilinda.”

Februari 10, 2018 Makonda alipokea ripoti kutoka kwa wanasheria waliosikiliza kero za wananchi kwa uratibu wa ofisi yake.

Katika mkutano huo, mkuu huyo wa mkoa aliwaita jukwaa kuu wakuu wa idara ya ardhi na nyinginezo kutoka manispaa zote tano za Dar es Salaam na kuwahoji kuhusu idadi ya migogoro na changamoto katika maeneo yao ya kazi.

Katika maelezo yake ya leo, Mauya amesema ibara ya 107A ya Katiba inasema mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki Tanzania itakuwa mahakama.

“Wakati huohuo Ibara ya 107B inasisitiza uhuru wa mahakama katika utekelezaji wa majukumu yake. Kwa hiyo kwa mujibu wa ibara hii mihimili mingine ya dola na watendaji wake hawapaswi kwa namna yoyote ile kuingilia utendaji wa mahakama,” amesema Mauya.

Amebainisha kuwa kituo hicho kinawakumbusha viongozi wa Serikali na wanasiasa kuwa hawana mamlaka kisheria kuingilia utendaji kazi wa chombo hicho wala kuelekeza utendaji, badala yake wanapaswa kuheshimu na kufuata taratibu katika upatikanaji wa haki.

“Tumebaini mkutano wa mkuu huyo wa mkoa na wananchi wa jiji lake kulikuwa na mapungufu kadhaa ambayo yamekuwa yakifanywa na sio tu na Makonda, bali pia na baadhi ya viongozi wengine wa Serikali,” amesema.

 Amesema sheria ya utatuzi ya migogoro ya ardhi inamtaja waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuwa na mamlaka juu ya mabaraza ya ardhi ya kata.

“Kifungu cha 10(1) cha sheria ya utatuzi wa migogoro ya ardhi namba 216 ya mwaka 2002 kinayatambua mabaraza ya kata kama mahakama ya utatuzi wa migogoro ya ardhi kwa ngazi ya kata, hivyo kwa mujibu wa sheria hizi wakuu wa mikoa hawana mamlaka ya kusimamisha, kuendesha wala kuelekeza utendaji,” ameongeza Mauya.

Kwa upande wake, Mkurugezi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga amesema lengo la tamko hilo ni kutaka umma ufahamu kuwa kitendo cha wakuu wa mikoa kuingilia mahakama si sahihi.

Amesema pia wametoa tamko hilo ili wananchi waelimike na kutambua kuwa ili kufikia haki kuna utaratibu umewekwa kisheria.

“Kwanza wajue ni utaratibu upi uliopo kisheria kwani kuna mahakama kitengo cha ardhi, mabaraza ya kata lakini tukisema tuwakusanye kila mmoja aeleze shida yake tutakuwa tunatatua kero bila sheria,” amesema.

CHANZO: MPEKUZI HURU


Share:

DODOMA: Naibu waziri awatahadharisha waandishi kutojihusisha na siasa


Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutojihusisha na maswala ya kisiasa katika utendaji wao wa kazi ili kuandika habari za ukweli na usahihi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Waziri ya Habari, Tamaduni, sanaa Na Michezo JULIANA SHONZA katika maadhimisho ya siku ya Redio duniani ambayo kitaifa yamefanyikia Mjini DODOMA.
Naibu waziri amesema waandishi wa habari wanajukumu la kufikisha habari kwa jamii ili kulinda amani na upendo kwa kujali utu wa mtu.
Amesema vyombo habari vina nafasi kubwa katika jamii na kama vikitumika kwa mrengo sahihi itasaidia kuiunganisha jamii na serikali.

Maadhimisho ya siku ya redio duniani kitaifa yamefanyika Mjini DODOMA  ikiwa ni kwa mara ya pili kufanyika mkoani humu. Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa ni ‘Redio na Michezo’ ambapo Naibu waziri wa Habari, Utamadunii sanaa na Michezo Mh JULIANA SONZA amehudhuria kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Dr. HARRISON MWAKYEMBE.





Share:

NAIBU WAZIRI WA MAJI KUONGOZA KIKAO CHA DHARURA KUTATUA KERO YA MAJI DAR

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso anatarajiwa kuongoza kikao baina ya uongozi wa Manispaa ya Ilala, DAWASA na DAWASCO ili kutafuta njia ya kupata fedha za kukamilisha mradi wa maji wa Kimbiji ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa maji kwenye maeneo kadhaa ya jiji ikiwemo wilaya hiyo.
Naibu Waziri aliyasema hayo Februari 12, 2018 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Bonyokwa huko Kinyerezi Wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, baada ya kuambiwa kuwa awamu ya kwanza ya uchimbaji visima virefu 20, umekamilika na unakusudia kuondoa kabisa tatizo la upatikanaji maji kwenye maeneo ambayo hayana mtandao wa maji.
“Mamlaka ya DAWASA ndio iliyopewa jukumu kusimamia awamu ya kwanza ya uchimbaji visima virefu vilivyo kwenye takriban mita 405 hadi 600 na viko 20 kilichobaki ni awamu ya uendelezaji wa visima (kuweka mtandao wa usambazaji maji ili maji yaweze kuwafikia wananchi wa jiji la Dar es Salaam likiwemo eneo hili.” alisema Aweso.
Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam, (DAWASA) Bi. Modester Mushi. Bi. Mushi alifafanua kuwa sababu ya kutenga mradi huo kwa awamu ni kutokana na gharama na upatikanaji wa fedha lakini akabainisha kuwa Mamlaka iko kwenye hatua nzuri kwa ajili ya kutekeleza awamu ya pili ambapo nyaraka ziko kwa Mwnaasheria Mkuu kwa ajili ya mapitio na kupitia Wizara wanategemea kuanza mradi huo kwa wakati katika mwaka wa fedha ujao, alisema.
Baada ya maelezo hayo ndipo Naibu Waziri ambaye alifuatana na Mbunge wa jimbo la Segerea Mhe. Bonna Kalua, aliagiza mkutano wa dharuara ufanyike Jumanne baina yake, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, DAWASA na DAWASCO ili kutafutia ufumbuzi mkwamo huo kwani wananchi wanataka maji na si vinginevyo.
Na Khalfan Said, K-Vis Blog
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Jumaa Aweso, (aliyesimama), akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa majumuisho ya ziara yake aliyoifanya kuangalia hali ya upatikanaji wa maji kwenye wilaya ya Ilala hususan jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam Februari 12, 2018.
 Mhe. Aweso, akisikiliza kwa makini kero za wananchi kuhusu maji.
 Baadhi ya wananchi wa jimbo la Segerea waliohudhuria mkutano huo uliofanyika Bonyokwa Februari 12, 2018.
 Mbunge wa jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, Mhe. Bonna Kaliua, akizunguzma na wananchi wa Bonyokwa kwenye mkutano huo.
 Mbunge wa jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam, Mhe. Bonna Kaliua, akizunguzma na wananchi wa Bonyokwa kwenye mkutano huo.
 Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka, Dar es Salaam, (DAWASA), Bi. Modester Mushi, akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maji jijini Dar es Salaam ikiwemo jimbo la Segerea.
 Mwakilishi kutoka DAWASCO, akizungumza kwenye hadhara hiyo.
 Meneja Uhusiano wa Jamii wa DAWASA, Bi. Neli Msuya, na wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia hotuba.
Mhe. Aweso na Mhe. Bonna Kalua, wakijadiliana jambo mwishoni mwa mkutano huo
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>