• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

SERIKALI YATAKIWA KUBORESHA MABARAZA YA ARDHI YA KATA



Serikali imetakiwa kuimarisha utendaji wa Mabaraza ya Ardhi ya Kata ili kuboresha ufanisi wa mabaraza hayo katika kuwafikia wananchi.
Wito huo umetolewa leo Februari 13 jijini Dar es Salaam na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) kupitia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake, Felista Mauya wakati akitoa tamko la kituo hicho kuhusu usimamishwaji wa mabaraza hayo.
Mauya amesema usimamishwaji wa mabaraza hayo ni kinyume na sheria,kutokana kwamba serikali ilitakiwa kuboresha utendaji kazi wake badala ya uamuzi huo, ambapo amekiri kwamba mabaraza ya ardhi kata yana mapungufu katika utendaji kazi wake.
Katika hatua nyingine, Mauya amesema LHRC inaitaka serikali kufuata taratibu za kisheria katika utatuzi wa kero za wananchi sambamba na kuboresha vyombo vya utoaji haki kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Aidha, amewataka wananchi kujifunza na kufuata mifumo sahihi ya utoaji haki kwa kutambua kwamba mahakama ndio muhimili wenye mamlaka juu ya utoaji haki kwa mujibu wa katiba. 

CHANZO: dewjiblog
Share:

MAAFISA HABARI WATAKIWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO KWA KUZINGATIA WELEDI WA KAZI


Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Raphael Joseph Nyanda amewataka Maafisa habari na TEHAMA nchini kutekeleza majukumu yao kwakuzingatia Weledi, maarifa na ubunifu kwakuwa wao ni Mawakala wa mabadiliko.
Akifungua kikao cha siku nne mkoani humo kilicho andaliwa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwakushirikiana na Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya umma PS3, na kushirikisha maafisa habari na TEHAMA kutoka mikoa ya Mara na Arusha, amewatahadharisha  maafisa hao kuwa endapo watazembea kutekeleza wajibu wao wa msingi kwa weledi basi watu wengine watapotosha umma.
“Kila mmoja miongoni mwenu anayo dhamana yakutangaza mambo mazuri yanayofanywa na serikali, lakini mkikaa kimya ninyi kama sauti za taasisi zenu watu wasio wema watapotisha maudhui hayo na mwisho wa siku kuchafua taswira ya serikali” amesisitiza Nyanda.
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano serikalini, Rebbeca Kwandu, akizungumza kabla yakumkaribisha Mgeni rasmi, amewataka maafisa hao kubadilika katika utendaji wao mara baada ya mafunzo ya mfumo huo juu ya uendeshaji wa tovuti.
“Mwanzoni tulipoanzisha tovuti hizi, hatukuwa na muongozo ambao ni dira ya uendeshaji lakini mara baada ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kuandaa muongozo huu kwakushirikiana na wadau wetu PS3 ni imani yangu tutabadilika,”amesema Kwandu na kuongeza kuwa uwepo wa tovuti bila ya uwepo wa habari haina maana.
Akizungumza kwa niaba ya Mradi wa PS3 Mkurugenzi anayeshughulia utawala bora na Ushirikishwa wa wananchi Dkt. Peter Kilima, amekiri kuwa Maafisa habari na Maafisa TEHAMA ndio roho ya taasisi, hivyo ushirikishwa hasa kwenye vikao vya maamuzi itakuwa ni fursa kwao kuchuja na kuujuza umma mambo mazuri ya nchi.
Awali akitoa Salaam za Idara ya habari maelezo, Mkurugenzi Msaidizi wa habari na picha Thadeus Rhodney, amesema kuwa ili kutangaza mambo mazuri yanayofanywa na  serikali lazima maafisa habari wawe na zana (tools) za utendaji kazi na zana yenyewe katika mustakabali wa sasa kwa ngazi za Mikoa na mamlaka za Serikali za Mitaa ni Tovuti.
“Wafadhali PS 3 wametuwezesha kuwa na mfumo wa Government Website Fremwork (GWF) tumieni hizi tovuti kama tools ya kuujuza umma,” alisema Rhodney.
Ofisi Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na  Mradi wa Uimarishaji mifumo ya umma chini ya mradi wa  PS3 wanaendesha Mafunzo ya nanna bora ya uendeshaji wa tovuti za serikali ambapo Maafisa habari pamoja na Maafisa TEHAMA wapatao 418 nchini kote watapatiwa mafunzo.
Na Atley Kuni
Share:

UNESCO KUADHIMISHASIKU YA RADIO DUNIANI

Shirika la UNESCO kwa kushirikiana na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania (TADIO) wataaungana na Dunia nzima kuadhimisha Siku ya Redio Duniani.  Maadhimisho hayo yatafanyika Dodoma mnamo Tarehe 13/ Februari mwaka 2018 na yatajumuisha waandishi wa habari  wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani na Wadau wengine wa habari.
Kauli Mbiu ya Redio Jamii mwaka 2018 ni Redio na Michezo huku msisitizo mkubwa ukielekezwa kwenye utandawazi katika suala la kutoa kipaumbele cha kutangaza michezo,  usawa wa kijinsia katika michezo na kutangaza michezo pamoja na kuhuisha amani kupitia michezo.
Maadhimisho hayo yatajumuisha maada juu ya kauli mbinu na miiko ya uandishi wa habari mtandaoni,   Kanuni za Mtandaoni za mwaka 2017 pamoja na kuchagizwa na mdahalo juu ya michezo.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Dkt. Harrison Mwakyembe.
Mnamo January 14, 2013, Umoja wa Mataifa uliidhinisha rasmi Tamko la UNESCO  katika Mkutano wake Mkuu wa 67 juu ya Siku ya Redio Duniani.
Azimio hilo lilipitishwa katika kikao cha 36 cha UNESCO na kutamka kuwa February 13 itakuwa siku ya Umoja wa Mataifa ya Redio.
Mpaka sasa, Redio imeendelea kuwa chombo cha uhakika  huku kikibadilika kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kutoa mbinu  mpya kwa jamii kuwasiliana na kushiriki.
Redio ina nafasi kubwa ya kuzileta jamii pamoja na kuhuisha majadiliano ya kuleta mabadiliko chanya.  Kwa kusikiliza halaiki, na kujibu mahitaji yao, radio inatoa wigo wa Maoni na sauti zinazohitajika kutatua changamoto katika nyakati hizi.
Radio ni, na inaendelea kuwa njia yenye nguvu katika nchi zilizo Nyingi za bara la Afrika.  Si tu redio inatumika kubadilishana  Taarifa katika jamii bali pia ni nafuu na inafikika.
Maadhimisho haya yametanguliwa na mafunzo ya siku saba kwa waandishi wa habari wa redio jamii juu ya uhariri, kuandaa vipindi na kufanya ufuatiliaji wa masuala mtambuka katika jamii.
Mafunzo hayo yamejumuisha waandishi 49 kutoka vyombo vya habari vya kijamii kutoka redio 24 zinazofadhiliwa na UNESCO ikiwa ni asilimia 77.4 ya mikoa yote katika  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Washiriki wa mafunzo hayo wanajumuisha Waandishi na Maripota pamoja na maafisa tathmini  ambao awali walipata mafunzo ya tathmini na ufuatiliaji kutoka UNESCO.
Shirika la UNESCO kwa msaada kutoka Shirika la SDC wanasaidia utekelezaji wa mradi unaolenga kuzijengea uwezo redio jamii katika nyanja za ushiriki katika michakato ya kidemokrasia na maendeleo.
Mradi huo unalenga kukuza na kujenga uwezo wa redio jamii takribani 25 nchiini Tanzania kwa kukuza nafasi yao kama watoa huduma za jamii,  kupanua wigo wa kijiografia katika masuala ya habari mtambuka katika maeneo yao na  kuboresha uwezo wao katika kazi
Share:

Rais Mwinyi atengua Rasmi kauli yake



Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi amekiri kufuta kauli yake iliyodumu kwa takribani miaka 30 kuwa Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu na haitakaa ifanye vizuri kwenye michezo.

Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya awali kati ya Simba SC dhidi ya Gendarmerie ya Djibouti, baada ya mchezo alisema kiwango cha mpira nchini kwasasa kimekua hivyo anafuta kauli yake.

''Mchezo umekuwa mzuri na sasa nafuta lile neno (Tanzania ni kichwa cha Mwendawazimu anayejifunza kunyoa atunyoe sisi) lakini sasa sisi ndio vinyozi'', alisema.

Katika mchezo wa jana Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 hivyo kujiweka vizuri kwenye mchezo wake wa marudiano huko Djibouti. Yanga pia ilishinda dhidi ya St. Louis ya Shelisheli.

Yanga inayocheza klabu bingwa Africa itasafiri kwenda Shelisheli kwaajili ya mchezo wake wa marudiano Februari 20 huku Simba inayoshiriki Kombe la Shirikisho nayo itasafiri kuelekea Djibouti kwaajili ya mchezo wa Februari 20 au 21.

Share:

RC Mnyeti: Siwezi kutoa msaada kwa diwani wa CHADEMA , Labda Ahamie CCM Ndo Ntamsikiliza



Mkuu wa Mkoa wa Manyara,  Alexander Mnyeti amewataka madiwani wa vyama vya upinzani kujiunga na CCM ili waweze kushirikiana naye kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama tawala.

Amesema yupo tayari kupokea simu ya diwani wa CCM hata akipigiwa usiku wa manane, ili kumpa msaada lakini si diwani kutoka vyama  vya upinzani.

Akizungumza jana Februari 11, 2018 katika mkutano wa hadhara kata ya Haydom wilayani Mbulu, Mnyeti amesema ni vyema madiwani wa Chadema wakajiunga na CCM.

Amesema diwani wa Chadema ni ngumu kufanikisha maendeleo ya wananchi kwa madai kuwa, hakuna ambaye atamsikiliza akiwasilisha hoja zake katika vikao vya halmashauri husika.

"Hata hapa Haydom najua ni ngome ya Chadema hata mwenyekiti wa kijiji namuona ana damu ya CCM, sasa ondokeni huko mje huku tutekeleze ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kuleta maendeleo," amesema Mnyeti.

Awali, mkazi wa kata ya Hayderer,  John Tluway aliuliza swali kwa mkuu huyo wa mkoa akitaka kujua sababu za mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Chelestino Mofuga kutofika kwenye kata hiyo inayoongozwa na Chadema.

Akijibu swali hilo, Mnyeti amempongeza Mofuga kwa kutokufika kwenye kata hiyo inayoongozwa na Chadema kwa maelezo kuwa diwani wa kata hiyo anapaswa kujiunga na CCM ili kufanikisha maendeleo.

"Mkuu wa wilaya ninakupongeza kwa wewe kutofika kwenye kata hiyo kwani ningepata taarifa umefika mara ya kwanza, mara ya pili na mara ya tatu ningekuwa na mashaka na wewe lakini hongera sana kwa kutokwenda," amesema Mnyeti.

Pia, amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kutekeleza na kufanikisha kwa vitendo ilani ya CCM hata kama hawana kadi ya chama hicho kwani ndicho ambacho kipo madarakani.

"Mtekeleze hayo kwa nia safi, hiyo ni sawa na imani kwani hata kanisani huwezi kusikia padri akimsifu Muhammad na pia kule msikitini imamu huwa hamsifu Yesu," amesema Mnyeti.

Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Mbulu, Nasaeli Sulle alimhakikishia Mnyeti kuwa wananchi wa Haydom wamejitambua kuwa walifanya makosa na kuchagua Chadema ila sasa wapo tayari kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM.


SOURCE: MPEKUZI
Share:

WAANDISHI WA HABARI NCHINI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI.

Waandishi wa Habari wa Redio za kijamii Nchini, Wameashwa kuzingatia Maadili pindi wawapo katika Majukumu yao ya kazi. Wito huo umetolewa na BI ROSE HAJI MWALIM amabye ni Mkufunzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Waandishi hao zaidi ya 50 kutoka Redio mbalimbali za Kijamii yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO, ambapo wamepiga kambi katika Ukumbi wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoani Dodoma kwa siku nane mfululizo.

Akizungumza na Washiriki hao Bi Rose amesema Redio ni chombo muhimu cha kupashana Habari na hivyo Waandishi wa Habari wanatakiwa kusimamia Misingi ya Taaluma yao ili kuepuka Madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na kukosa umakini na kupuuza kwa Misingi hiyo muhimu.
Ameongeza kuwa Redia inasikilizwa na watu wengi kwa wakati mmoja na bila kujali Mapungufu yao kama vile Walemavu wa Macho, Wasiojua Kusoma, Watoto wadogo na hata Wazee hivyo amewataka washiriki hao kuandaa  Habari zenye kuleta Maslahi na kupunguza Mihemko kwa Jamii.

Kwa upande wao Washiriki hao wamefurahishwa na Mafunzo hayo ambayo yatawaongezea Uwezo katika kukamilisha Majukumu yao na wameahidi kuzingatia na kuyafanyia kazi yale yote wanayoendelea kujifunza kwa kipindi cha Siku hizo Nane .
Wameahidi kuwa Mabalozi wazuri pindi wataporudi katika Vituo vyao vya kazi kwa kuwashirikisha na Waandishi wengine ambao hawakuwepo kwenye Mafunzo hayo.

Mafunzo kama haya yamekuwa yakileta mabadiliko makubwa ya kiutendaji kutokana na kufundisha Masuala Muhimu na Nyeti yanayohusu Tasnia hii muhimu ya Habari Tanzania Hasa ukizingatia Redio za Kijamii ndio muhimili wa Maendeleo ya Wanajamii hasa wa Vijijini.

Pamoja na kufundisha mambo ya kuzingatia Maadili, Mengine ni pamoja na Kuwashirikisha Wanawake katika kuandaa na kutangaza Vipindi vya Michezo, Kuzipa kipaumbele Habari za Eneo husika, Waandishi wa Habari Wanawake kujiepusha na Rushwa ya Ngono, Kuzingatia Utofauti wa Kijinsi pamoja na kutumia Vyanzo Sahihi vya Habari.
Mafunzo hayo yanategemea kumalizika siku ya 13-02-2018 ambayo ni Siku ya Redio Duniani.

Karim Faida.

Share:

Dodoma: wanawake waamka na ujasiliamali

Image may contain: 1 person, sitting and food


Wanawake wa Mkoani Dodoma wameamua kuachana na mambo ya kumtegemea mwanaume kwa kila kitu ndani ya nyumba na badala yake kujikita zaidi kwenye biashara ndogondogo ili kukamilisha dhana ya kusaidiana kwenye familia.

Mama Hellen, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara wa mbogamboja kwenye soko kuu la Mkoani hapa maarufu kama soko la Majengo amesema, hapo awali haikuwa rahisi sana Mwanamke kufanya biashara katika maeneo ya sokoni na ingawa walikuwepo ila walikuwa wachache tofauti na siku za hivi karibuni.

Hata hivyo ametoa wito kwa Wanawake wenzake Nchini kuachana na biashara haram kama vile kuuza miili yao au kugeuka ombaomba hali ya kuwa wana uwezo wa kufanya kazi ndogondogo na kujiingizia kipato.

Kwa kufanya hivyo itasaidia kurudisha heshima ya Mwanamke katika maisha yetu ya kila siku.

Karim Faida.
Share:

Waziri Mkuu Majaliwa ahamasisha ulimaji wa mazao ya biashara …. Pamba na Korosho vimo



#Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ameyasema hayo  jana Bungeni Mjini #Dodoma wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Sumve Mhe. Richard Ndassa juu ya namna Serikali ilivyojipanga na utafutaji wa masoko ya Pamba kutokana na mwitikio mkubwa wa kulima zao hilo mwaka huu.
 .
“Miongoni mwa mikakati ya kuendeleza mazao hayo ni pamoja na kulima kisasa na kutafuta masoko ndani na nje ya nchi,” alisema Waziri Mkuu.
 .
Amesema, mwezi huu anatarajia kukutana na watumiaji wa zao la Pamba hapa nchini ili kuweka mfumo endelevu wa ununuzi wa zao hilo. Aidha, Wizara ya Kilimo inafanya kazi ya kutafuta masoko nje ya nchi.
 .
Pia, Mhe. Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa #Liwale Mhe. Zuberi Kuchauka juu ugawaji wa pembejeo za korosho kwa mwaka huu alisema, Serikali ilitoa pembejeo ya Salfa bure mwaka jana kwa wakulima wa korosho ili kufanya hamasa kwa zao hilo baada ya wakulima kutelekeza zao hilo kutokana na kukosa pembejeo hiyo.
 .
“Baada ya ugawaji wa pembejeo hiyo ya Salfa zao hilo limevunwa kwa kiwango cha juu kwa mwaka jana, hivyo kutokana na fedha walizozipata wakulima wa zao hilo watatatikiwa kuchangia gharama za Salfa kwa mwaka huu,” alisema Mhe. Majaliwa.
 .
Wakati huo huo, Mhe. #Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Urambo Mhe. Margaret Sitta juu ya migogoro ya mipaka ya mapori na misitu, alisema Serikali imeiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikisha wanavijiji na viongozi wa kijiji wakati wa uwekaji wa mipaka hiyo.
 .
Hata hivyo alisema ikiwa kijiji kitaonekana kiko ndani ya mipaka ya msitu au pori, tathmini itafanyike na baadae watapewa #elimu ya kutoingia ndani ya mipaka ya misitu na mapori ya Serikali Kuu
Share:

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA (TEA) YAKABIDHI MRADI WA UKARABATI WA SULE YA WASICHANA- KONDOA.



Kaimu Mkurugenzi wa Mmlaka ya Elimu Tanzania Graceana Shirima amesema ni matumaini yao kuwa fedha hizo zitatumika kwa ufanisi mkubwa na makusudio waliyoyaweka na matokeo yake yaonekane kwani kiasi kilichotolewa ni kikubwa.
Wakati akikabidhi #fedha hizo katika hafla iliyofanyika kwenye ukubi wa shule hiyo, Bi. Graceana amesema lengo la ukarabati huo ni kuhakikisha kuwa shule inakuwa na mazingira mazuri kwa ajili ya kupata elimu iliyokusudiwa na kuongeza ufaulu kwani miundombinu ya maabara, maktaba na madarasa vyote vitakarabatiwa na kuwa na mwonekano mzuri kwa mwanafunzi kusoma.

 “Tuna imani uongozi wa Halmashauri ya Mji na Bodi ya #Shule hawatatuangusha katika usimamizi na watatumia fedha hizi kwa umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha taratibu zote za manunuzi zinazingatiwa na hatutasita kumchukulia hatua mtu yoyote atakayekwenda kinyume na taratibu za manunuzi sababu mradi huu force akaunti ambayo inatumia jamii zaidi” Alisema Bi Graceana

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Hamza Mafita ametoa shukrani kwa serikali kwa kuwaletea fedha zote za mradi kwani fedha hizo zitabakia kwa wananchi wa Kondoa kwani mafundi watanunua vifaa vyote Kondoa na mafundi ni wenyeji wa Kondoa na kuwataka mafundi kumaliza mradi huo kwa wakati na haoni sababu ya kuchelewa ikiwa fedha zote zipo.
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji #Kondoa Khalifa Kondo akipokea mradi huo alisema kuwa anashukuru kupata mradi huo sababu ingekuwa ni jukumu la Halmashauri kukarabati kwa kutumia mapato ya ndani na kuahidi kuzisimamia fedha hizo kwa kushirikiana na wataalam wa Halmashauri na Bodi ya shule ili kuhakikisha lengo la mradi linakamilika.

Mamlaka ya #Elimu Tanzania imetoa kiasi zaidi ya bilioni kumi kwa ajili ya ukarabati wa shule kongwe Tanzania ikiwemo Shule ya Wasichana Kondoa ambapo imepewa shilingi bilioni moja kwa ajili ya ukarabati wa #majengo ya shule hiyo
Share:

ODINGA ASEMA ATAANZA KUFANYA KAZI RASMI KAMA RAIS WA WATU

Image result for raila odinga

Kiongozi mkuu wa Muungano wa NASA Raila Odinga amesema ataanza kufanya kazi kama rais wa watu na hatishwi na lolote. #Odinga amesema hayo katika hafla mazishi ya bzbz yake na mkurungenzi wa mawasiliano wa chama cha ODM Philip Etale yaliyofanyika katika eneo la Embusakami jimbo la Vihiga. Aidha Raila ameishutumu serikali ya Jubilee kwa kuingilia majukumu ya idara ya Mahakama na kupuuza maagizo ya mahakama.
Vile vile amelaumu serikali ya jubilee kwa kutumia idara ya polisi kuwahangaisha viongozi wa upinzani
#Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Amos Wako ambaye alitetea Raila Odinga dhidi ya kushtakiwa na kosa la uhaini kufutia kuapishwa kwake.
Hata hivyo, kiongozi wa chama cha ANC Musalia Mudavadi hakuhudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika ngome yake ya kisiasa, suala ambalo liliwatia hofu wafuasi wengi wa muungano wa NASA huku wengi wao wakihofia ushirikiano miongoni mwa vigogo wa muungano huo.
Ikumbukwe kwamba Muasilia Mudavadi, Kalonzo Musyoka na Moses Wetangula vile vile hawakudhuria hafla ya kuapishwa kwa Raila Odinga, jambo ambalo lilipokelewa na hisia tofauti miongoni mwa wafausi wa #NASA huku wengine wakidai kwamba, vinara hao watatu ni walisaliti wa bwana Odinga. Hata hivyo, Raila aliwahakikishia wafuasi wa NASA kwamba muungano huo uko imara na utaendelea kushirikiana kwa vyovyote vile.
Katika siku za hivi karibuni, kwenye mahojiano na shirika la utangazi la kimataifa la BBC Odinga alidokeza kwamba anataka uchaguzi uandaliwe upya kufikia mwezi wa Agosti mwakani, ikiwa ni siku chache tu baada ya serikali ya Jubilee kutangaza msako mkali dhidi ya viongozi wa upinzani, hasa wale waliohusika katika kuandaa hafla ya kuapishwa kwake Raila.
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>