• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

TMA yatoa angalizo la mvua kubwa

Dar es Salaam. Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo ya kunyesha kwa mvua kubwa katika baadhi ya maeneo nchini kuanzia leo Alhamisi na kesho Ijumaa.
Taarifa ya TMA imebainisha mikoa itakayokubwa na mvua hizo ni Pwani ya Kusini ambayo ni Lindi na Mtwara, Nyanda za Juu Kusini Magharibi ambayo ni Mbeya, Iringa, Songwe na Rukwa, Dar es Salaam na Pwani.
“Upepo wa Pwani, unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini; kwa kasi ya Km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini,” imeeleza taarifa hiyo na kuongeza;
“Hali ya Bahari, inatarajiwa kuwa mawimbi madogo hadi makubwa kiasi na matazamio kwa siku ya Ijumaa Januari 5,2018, kuongezeka kwa mvua katika mwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za Juu Kusini Magharibi.”
Hata hivyo, tayari mvua hizo zimekwisha kuanza na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani mvua ilinyesha jana Jumatano usiku katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo.
Chanzo: mwananchi


WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
                             MAMLAKA  YA HALI YA HEWA
S.L.P.3056, DAR-ES-SALAAM
Fax: 2460735.email:met@meteo.go.tz
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO
TAREHE:03/01/2018.

[Mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe na Songwe]:
[Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi na Mtwara]:
[Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara]:
Hali ya Mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya Maeneo na vipindi vifupi vya jua.
[Mikoa ya Mwanza, Mara, Geita, Shinyanga, Kagera na Simiyu]: [Mikoa ya Ruvuma, Kigoma, Tabora na Katavi]:
[Mikoa ya Singida na Dodoma]:
Hali ya Mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika Maeneo machache na vipindi vya jua.

[Mikoa ya Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba]: 
[Mkoa wa Morogoro]:





Hali ya Mawingu, Mvua na ngurumo katika Maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.


ANGALIZO
VIPINDI VIFUPI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA DAR ES SALAAM, PWANI, ARUSHA, KILIMANJARO, MANYARA, LINDI, IRINGA, MBEYA, SONGWE, NJOMBE NA MTWARA.

VIWANGO VYA JOTO, MAWIO NA MACHWEO YA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

MJI
Kiwango cha juu cha joto

Kiwango cha chini cha joto
Mawio (Saa)

Machweo (Saa)

ARUSHA
29°C
18°C
12:30
12:44
D'SALAAM
31°C
26°C
12:11
12:41
DODOMA
29°C
21°C
12:27
12:53
KIGOMA           
29°C
19°C
12:53
01:15
MBEYA
25°C
16°C
12:31
01:07
IRINGA
24°C
19°C
12:24
12:56
NJOMBE
19°C
11°C
12:24
12:56
MWANZA
28°C
19°C
12:45
12:57
TABORA
28°C
19°C
12:41
01:03
TANGA
29°C
20°C
12:16
12:38
ZANZIBAR
30°C
26°C
12:11
12:41

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvumakutoka Kaskazini;kwa kasi ya Km 30 kwa saakwaPwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa Mawimbi MadogohadiMakubwa kiasi.

Matazamio kwa siku ya Ijumaa:05/01/2018: Kuongezeka kwa mvua katikaMwambao wa Pwani na maeneo ya Nyanda za juu Kusini Magharibi.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 03/01/2018.


NA: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.
Share:

Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 03 Januari, 2018 ameagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT)

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, tarehe 03 Januari, 2018 ameagana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) anayemaliza muda wake Prof. Benno Ndulu Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo yao, Prof. Ndulu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kumuamini na kufanya nae kazi tangu alipoingia madarakani na amebainisha kuwa anafurahi kumaliza kipindi chake huku uchumi wa nchi ukiwa mzuri.
Prof. Ndulu amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa miongozo muhimu iliyosaidia kuimarisha uchumi ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei ambao mwezi Novemba 2017 ulifikia asilimia 4.4 na kuongezeka kwa akiba ya fedha za kigeni kutoka Dola za Marekani Bilioni 1.8 hadi kufikia Dola za Marekani Bilioni 6 hivi sasa, hali ambayo imeimarisha uwezo wa Serikali kujiendesha na kugharamia miradi mikubwa ya maendeleo.
“Nimekuja kumuaga Mhe. Rais na kumshukuru, nafurahi kuwa naondoka wakati hali ya uchumi ikiwa nzuri, Taifa linakopesheka na kuna mazingira mazuri zaidi ya uchumi kuendelea kukua, nampongeza sana Mhe. Rais kwa kusimamia mambo mbalimbali muhimu ya kuimarisha na kukuza uchumi katika kipindi chote nilichofanya nae kazi” amesema Prof. Ndulu.
Mhe. Rais Magufuli pia amezungumza na Gavana Mteule Prof. Florens Luoga na baada ya mazungumzo hayo, Prof. Luoga amemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa uteuzi huo na kumhakikishia kuwa ataisimamia BOT ili iendelee kuwa chombo imara cha kusimamia uchumi wa nchi, kuisimamia fedha ya Tanzania na kuhakikisha nchi inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kama vile ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na mradi wa umeme katika maporomoko ya maji ya mto Rufiji (Stiegler’s Gorge).
Prof. Luoga ameungana na Prof. Ndulu kueleza kuwa taarifa zinazotolewa na BOT kuhusu ukuaji wa uchumi zinaandaliwa kitaalamu na kwa kushirikisha vyombo mbalimbali vikiwemo Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na ameonya dhidi ya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipotosha ukweli kuhusu takwimu za uchumi zinazotolewa na BOT.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Prof. Ndulu kwa utumishi wake wa miaka 10 na kazi nzuri aliyoifanya kusimamia uchumi ambapo katika kipindi hicho kasi ya ukuaji wa uchumi imeongezeka kutoka wastani wa asilimia 5 hadi kufikia asilimia 7, ameimarisha usimamizi wa benki na maduka ya kubadilishia fedha, amesimamia ongezeko la akiba ya fedha za kigeni inayoiwezesha nchi kumudu kuagiza bidhaa na huduma kwa miezi 6 na kuanza kwa utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa reli, umeme, ununuzi wa ndege na mingine.
“Nakushukuru sana Prof. Ndulu, umefanya kazi nzuri ya kusimamia uchumi wa Taifa letu, ndio maana leo unamaliza muda wako lakini tayari Benki ya Dunia na kamisheni ya dunia inayoshughulikia teknolojia na maendeleo shirikishi wanakuhitaji ufanye nao kazi, na mimi nimeidhinisha uende ukatuwakilishe” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Mhe. Rais Magufuli amempongeza Gavana Mteule Prof. Luoga kwa kupokea uteuzi wake na amemtaka kufanya kazi ya kusimamia uchumi wa Taifa kwa ufanisi mkubwa zaidi ili nchi ipige hatua za maendeleo kwa kasi zaidi.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amesema mwezi ujao Serikali itatoa Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya kulipa madeni ya ndani yatakayokuwa yamehakikiwa yakiwemo ya wazabuni mbalimbali waliotoa huduma katika taasisi za Serikali, madai ya walimu na madai ya wakandarasi.
“Nasisitiza madeni tutakayolipa ni ya ndani, na tutalipa madeni ambayo yamehakikiwa, kwa hiyo maandalizi ya kutoa fedha hizo yaanze mara moja na ni matarajio yangu fedha hizi zitasaidia kuchochea ukuaji wa uchumi wetu” amesema Mhe. Rais Magufuli.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Januari, 2018 
Share:

Utafiti : MATUMIZI YA Wi-Fi ,SIMU ZA MKONONI YATAJWA KUHARIBU MIMBA KWA 48%

Kukua kwa sayansi na teknolojia kumeleta WiFi inayowaruhusu watu wengi kutumia intaneti kutoka kwenye chanzo kimoja bila kuhitaji kuunganishwa na nyaya.


WiFi ni teknolojia ya mtandao inayotumia mawimbi ya redio kutoa huduma za intaneti yenye kasi kubwa. WiFi na simu za mkononi huongeza hatari ya ujauzito kuharibika mimba kwa asilimia 48, utafiti unaonyesha.


Miali ya usumaku ni mlolongo wa mawimbi ya nishati yanayosafiri kwa kasi ya mwanga inayotokana na mzunguko wa umeme wa usumaku mfano mawimbi ya redio (radio frequency), mionzi mikali ya jua (ultraviolet) au miali isiyoonekana (infrared).


Hapo zamani, watafiti wamewahi kugundua kuwa miali ya usumaku inayotolewa na minara ya simu na nyaya za umeme mkubwa husababisha msongo kwenye mwili unaoharibu chembe za urithi (jeni) tatizo linaloweza kusababisha kuharibika kwa mimba kwa wajawazito.


Miali ya usumaku ambayo kila mmoja wetu humpata kwa viwango tofauti, zamani ilihusishwa na ugonjwa wa saratani na Shirika la Afya Duniani lilipendekeza utafiti zaidi ufanyike kuona athari zake kwa wajawazito.


Watafiti wa kituo cha utafiti Kaiser kilichopo Oakland, Marekani waliwachunguza wajawazito 913 wenye mimba za umri tofauti na kugundua baadhi Wajawazito walikuwa washaharibikiwa angalau mara moja kwa vipindi vilivyopita.


Wajawazito wote walipimwa viwango vya mionzi kila siku na kifaa kijulikanacho kama Emdex Lite Meter. Watafiti walifuatilia matokeo ya kila mjamzito.

Utafiti

Watafiti waligundua wajawazito waliokuwa kwenye miali ya hali ya juu waliongeza hatari ya mimba kuharibika kwa asilimia 48 kuliko wale waliokuwa kwenye viwango vya chini.


Wajawazito waliokuwa kwenye viwango vikubwa vya miali, asilimia 24.2 waliharibikiwa mimba ikilinganishwa na asilimia 10.4 ya wale waliokuwa kwenye miali ya viwango vidogo.


Watafiti wanadai hatari hutokea bila kujali mwanamke aliwahi kuharibikiwa mimba au la. Kiongozi wa utafiti huo, Dk De-Kun Li alisema: “Utafiti huu unatoa ushahidi kwa watu kwamba miali ya usumaku huathiri afya ya binadamu kibaiolojia.”

Sababu nyingine

Nchi zilizoendelea kwenye masuala ya tiba kama Marekani wajawazito huharibika mimba kati ya asilimia 15 na 20. Nchi zinazoendelea kama Tanzania hakuna takwimu rasmi za mimba kuharibika ingawa tatizo linaweza kuwa kubwa kuliko nchi zilizoendelea.


Kitaalamu tunasema mimba imeharibika yenyewe ikiwa chini ya wiki 20 sawa na miezi mitano. Mara nyingi mimba huharibika miezi mitatu ya mwanzo ingawa mimba yaweza haribika miezi mitatu ya pili.


Mimba ikiharibika miezi mitatu ya mwanzo mara nyingi hutokana na kusababishwa na mtoto mtarajiwa. Inakadiriwa mimba nne zinazoharibika hutokea miezi mitatu ya mwanzo.


Wataalamu wanadai mimba ikiharibika miezi mitatu ya pili (kati ya wiki ya 14 na 26) basi inaweza kuwa imesababishwa na tatizo la kiafya alilonalo mjamzito. Vile vile mimba kuharibika baada ya wiki ya 26 huwa ni kwa sababu ya mfuko wa maji kupasuka kabla ya wakati kutokana na maambukizi kumzunguka mtoto. Na mara chache hutokea njia (shingo ya kizazi) inapofunguka kabla ya wakati.


Sababu za kuharibika mimba miezi mitatu ya mwanzo zinatia ndani matatizo ya kromosomu (nyuzi nyuzi katika kiini seli cha kila kiumbe ambazo hubeba viiniurithi yaani jeni), matatizo ya plasenta au kondo la nyuma.


Plasenta hupitisha lishe kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kuondosha taka za kimetaboli za mtoto. Plasenta huanza kufanya kazi kuanzia mwezi wa tatu wa ujauzito.


Vitu vinavyoongeza hatari ya kuharibika mimba ni pamoja na umri. Mmoja kati ya wanawake 10 wa chini ya miaka 30 huharibikiwa mimba Kwa wanawake wenye miaka 35 hadi 39 wanawake wawili kati ya 10 huharibikiwa mimba na kwa wanawake walio na miaka zaidi ya 45, zaidi ya nusu ya mimba zote huharibika.


Vitu vingine vinavyoongeza hatari ni pamoja na unene, uvutaji sigara wakati wa ujauzito, matumizi mabaya ya dawa mfano Ibuprofen au Misoprostol, kunywa kafeini zaidi ya miligramu 200 kwa siku, unywaji wa vileo uliokithiri zaidi ya viwango viwili vya vileo kwa wiki.


Kiwango kimoja cha kileo ni sawa na bia (lager) moja, mililita 25 za pombe kali (spirits) glasi ya mililita 125 ya divai au mvinyo ni sawa na kiwango kimoja na nusu. Sababu za kuharibika mimba miezi mitatu ya pili hujumuisha matatizo ya kiafya ya muda mrefu mfano kisukari, kupanda sana kwa shinikizo la damu, ugonjwa wa figo na magonjwa ya tezishingo (thyroid). Maambukizi ya magonjwa kama vile surua, Ukimwi, kaswende, kisonono na malaria pia husababisha mimba kuharibika.


Nyingine zinazochangia mimba kuharibika ni kula chakula chenye sumu au vyakula visivyoiva vizuri mfano nyama na mayai mabichi. Sababu nyingine ni kizazi kuwa na umbo lisilo la kawaida, kulegea kwa shingo ya kizazi na ovari kuwa kubwa kuliko kawaida hali inayosababisha mabadiliko ya homoni.


Kupunguza athari za WiFi, simu


Kuweka simu mbali na tumbo pia kutohifadhi simu kwenye mifuko ya nguo zao husaidia kupunguza athari kufika tumboni na kusababisha madhara kwa mtoto.


Inashauriwa uzime WiFi ikiwa huitumii hasa wakati umelala. Kuweka simu kwenye hali ya ndege (airplane mode) ikiwa huitumii. Kutumia waya wa sauti (speakerphone) wakati ukiongea, vilevile inashauriwa kutozungumza kwa muda mrefu.


Hivyo ni vyema kuwa mchaguzi bora wa maneno. Kutotumia vifaa vinavyotoa miali ya usumaku mfano kifaa chochote kinachotumia umeme unapokuwa kwenye gari kwa maana viwango vya miali vinakuwa juu tayari.

Fikra potofu

Kuongeza hatari ya mimba kuharibika hakuhusiani na hali ya kihisia ya mjamzito mfano kuwa na msongo au huzuni, kuwa na mshtuko kutokana na jambo fulani, kunyanyua vitu vizito, kufanya mazoezi mzazito ya viungo ingawa inapendekezwa kuwasiliana na daktari ili akupangie aina ya mazoezi ya kufanya kulingana na hali yako.


Nyingine ni kufanya kazi wakati wa ujauzito mfano kukaa au kusimama muda mrefu, kufanya ngono kipindi cha ujauzito, kusafiri kwa anga (ndege) na kula vyakula vyenye viungo vingi.


Napenda kuwatia moyo walioharibikiwa mimba kutoogopa kutafuta mimba tena baada ya mimba ya mwanzo kuharibika.

Na Dk Joachim Mabula, Mwananchi

NINI MAONI YAKO
Share:

RAIS AWASILISHA FOMU ZAKE ZENYE ORODHA YA MALI ZAKE TUME YA MAADILI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Desemba, 2017 amewasilisha fomu yake ya tamko kuhusu rasilimali na madeni katika ofisi ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma iliyopo Mtaa wa Ohio, Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuwasilisha fomu hiyo Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kazi inazofanya na amemtaka Kamishna wa Maadili Jaji Mstaafu Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yeyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake ifikapo tarehe 31 Desemba, 2017.
“Mhe. Jaji Nsekela ikifika tarehe 31 Desemba, ambayo ni siku ya mwisho kwa Mujibu wa Sheria, weka mstari na usipokee fomu zingine, halafu tuone sheria itafanyaje, nakutakia kazi njema” amesisistiza Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela amemshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutekeleza matakwa ya kisheria yanayomlazimu kujaza fomu hizo na amesisitiza kuwa ujazaji wa fomu hizo kwa viongozi wa umma sio ombi.
“Viongozi hawaombwi kujaza fomu hizi, kuna baadhi wanadhani labda kutuletea hilo tamko ni fadhila, hapana, sheria ya nchi inahitaji hivyo na kuna sababu zake za msingi” amesema Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela.
Aidha, Mhe. Jaji Mstaafu Nsekela amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kuwasilisha taarifa ya akaunti yake ya benki sambamba na tamko hilo, na amekiri kuwa ameonesha mfano wa kuigwa na viongozi wengine.
Tamko la viongozi wa umma kuhusu rasilimali na madeni linatolewa kwa mujibu wa kifungu cha 9 na cha 11 cha sheria ya maadili ya viongozi wa umma namba 13 ya mwaka 1995.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017
Share:

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU

Simu : +255-22-2114512, 2116898
Tovuti : www.ikulu.go.tz
Faksi : 255-22-2113425
OFISI YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 28 Desemba, 2017 amekutana kwa mara ya kwanza na kamati maalum aliyoiunda kwa lengo la kuhakiki mali za chama hicho, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kamati hiyo aliitangaza tarehe 20 Desemba, 2017 Mkoani Dodoma na inaongozwa na Dkt. Bashir Ally.
Katika Mazungumzo hayo Mhe. Rais Magufuli amewataka wajumbe wa kamati hiyo kufuatilia na kuhakiki mali zote za chama, kumhoji mtu yeyote ambaye atahitajika kutoa taarifa juu mali za chama na kubaini thamani ya mali, mahali zilipo, makusanyo ya mapato na wanaozishikilia ama kutumia mali hizo.
Mhe. Rais Magufuli pia ametoa wito kwa wanachama wa CCM na wananchi wengine kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zote zinazohusu mali za chama kwa kamati hiyo, na watakaoitwa kuhojiwa waitikie wito huo.
“Nataka mali za chama zikinufaishe chama, nataka mkamhoji mtu yeyote, awe kiongozi, awe mwanachama, awe mfanyabiashara, mtu yeyote. Mkazihakiki mali zote ili chama kipate haki yake” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Akizungumza kwa niaba ya kamati hiyo, Dkt. Bashiru Ally amesema kamati imeanza kazi rasmi na ametoa wito kwa wanachama, wananchi na wote wanaozitumia mali za chama kutoa ushirikiano watakapoitwa kuhojiwa.
“Tumezungumza na Mwenyekiti kwa karibu saa mbili, katueleza matarajio yake, sababu za kuunda tume hii, kazi zake na faida zake kwa chama na kwa nchi, kwa hiyo ametukabidhi vitendea kazi na taarifa mbalimbali na ametueleza kazi yetu ni kuhakiki mali zote za chama kwa kushirikiana na wanachama na wale wanaoshirikiana na chama kuzitumia hizo mali kama vile wapangaji, wasimamizi, nakadhalika” amesema Dkt. Bashiru Ally.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Desemba, 2017
Share:

WAZIRI MWIGULU AWATAKA WANANCHI MTWARA KUJIANDIKISHA KITAMBULISHO CHA TAIFA


Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dr Mwigulu Nchemba amewataka kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Mtwara kushirikiana wote kwa pamoja katika zoezi la uandikishaji wa kitambulisho cha uraia ili pasiwepo na ambao si Raia wa Tanzania kuandikishwa kama Raia.

Waziri Dr Nchemba amewataka Watanzania hasa maeneo ya mipakani kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho vya uraia na kuwafichua wale ambao si Raia wa Tanzania ambao wamejitokeza sasa kuandikishwa ili pasiwepo baadae kesi za wasio watanzania kuandikishwa.

"Wananchi jitokezeni mtimize jukumu lenu la kujiandikisha hamnunui kitambulisho ni kutoa taarifa sahihi na zikikidhi mtapewa vitambulisho" Waziri Nchemba

Naye mkuu wa mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa amesema kuwa zoezi la uandikishaji wa  kitambulisho cha taifa unaendelea vizuri changamoto kubwa wanayokutana nayo ni mwitikio mdogo wa wananchi kujiandikisha huku wengi wakisingizia wanafatilia fedha zao za korosho walizouza.
Share:

WAZIRI MKUU AKAGUA UJENZI WA ZAHANATI MIBURE

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Nachingwea, kwa ajili ya mapumziko ya mwisho wa mwaka ambapo aliamua kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake wilayani Ruangwa, mkoani Lindi, Desemba 28, 2017. (Picha Zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Mibure, Mzee Menrad Kilian, baada ya kukagua ujenzi wa zahanati kijijini hapo, wilayani Ruangwa mkoani Lindi, Desemba 28, 2017. 
 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mibure, wakati alipoenda kukagua ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho Desemba 28, 2017. Waziri Mkuu yupo jimboni kwake kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka
Mkurugenzi Mtendaji wa KALIF Construction, Ally Mohamed Libaba akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) wakati wakijaribu kuvuta maji kutoka kwenye pampu ya mradi wa maji wa kijiji cha Namakuku, Desemba 28, 2017. Wa kwanza kulia ni msimamizi wa mradi huo, Bw. Fadhil Ally Libaba. 

*Aagiza zahanati ikiisha ipelekewe kifaa cha kutunzia watoto njiti

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameanza ziara fupi ya siku tatu, kukagua miradi ya maendeleo jimboni kwake katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye mapumziko ya mwisho wa mwaka, amekagua miradi ya maji, ujenzi wa zahanati na kuzungumza na wananchi kaika vijiji vya Mibure, Namakuku, Chienjere, Namahema A na Namahema B.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Mibure jana mchana (Alhamisi, Desemba 28, 2017) mara baada ya kukagua zahanati ya kijiji hicho, Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na ujenzi unavyoendelea na akamwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa ahakikishe zahanati hiyo ikikamilika inapata kifaa cha kuwatunzia watoto njiti kwa sababu kijiji hicho kiko mbali na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa.

“Nilileta makontena yenye vifaa vya hospitali, na humo ndani mlikuwa na vifaa vya kuwatunza watoto njiti (watoto wanaozaliwa kabla ya muda kutimia). Hakikisha hawa wanapata kifaa hicho kwa sababu hawana gari la kubeba wagonjwa, na pia wako mbali na hospitali ya wilaya na pia kituo cha afya cha jirani kiko mbali pia,” alisisitiza.

Akizingumzia kuhusu upatikanaji wa umeme kijiji hapo, Waziri Mkuu alisema: “Mibure ipo kwenye mipango ya kupata umeme ambao unatoka Nagurukuru, -Nghimbwa-Chienjere-Namakuku-Mibure.”

Aliwataka vijana wa kata hiyo, wachangamkie fursa kwa muanda mitaji ya kuwa na gereji za kuchomelea vyuma, saluni na viwanda vidogo vya usindikaji.

Mapema, akisoma taarifa ya ujenzi wa zahanati ya Mibure mbele ya Waziri Mkuu, Mwenyeiti wa kijiji hicho, Bw. Samwel Chilemba alisema mradi huo umekwishagharimu sh. milioni 52, ambapo kazi zilizokamiliak ni jengo la zahanati, kichomea taka na choo chenye matundu matatu.

Alisema wanakabiliwa na changamoto ya kupanda holela kwa gharama za vifaa vya ujenzi, kupokea michango kidogo kutoka kwa wananchi, ukosefu wa nyumba ya mganga na wauguzi na kiasi cha fedha cha sh. milioni 8.26 za kununulia samani.

Bw. Chilemba alisema kukamilika kwa ujenzi wa zahanati hiyo kutasaidia wakazi wa vijiji jirani vya Njawale, Namakuku, na vijiji jirani vya wilaya ya Nachingwea ambavyo vinapakana na wilaya ya Ruangwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, DESEMBA 28, 2017
Share:

WANANCHI WA MKOA WA MTWARA NA MIKOA JIRANI WAMEHASWA KUTUMIA FURSA YAKIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA COMORO ILI KUIMARISHA UCHUMI

Na Gregory Millanzi

Chama cha Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA)wamesaini hati ya makubaliano ya kibiashara na ushirikiano  kati ya Tanzania na Comoro kupitia Chama cha Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo nchini humo(UCCIA).

Hafla ya makubaliano hayo yamefanyika mkoa hapa kwa ujumbe wenye wawakilishi saba wa vyama vya wafanyabiashara viwanda na kilimo kutoka Comoro na visiwa vyake vidogo vya Ngazija, Hanjuani .

Mwenyekiti wa  chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah(kushoto) akiwa na Rais wa Chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo nchini Comoro (UCCIA) Ahmed Ali Bazi (kulia)

Mwenyekiti wa  chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara (TCCIA) Swallah Said Swallah amesema ni fursa kwa wafanyabiashra wa Mtwara kuuza bidhaa zao nchini Comoro kwani kiwango cha mauzo ya Tanzania kwa sasa ni asilimia 0.53 kiasi ambacho ni kidogo sana kulingana na ukaribu wetu, na lengo ni kufikia asilimia 5 ifikapo mwaka 2020.

Swallah ameweka wazi mikakati ya chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo Mkoa wa Mtwara kuhusu kuimarisha huduma za kibiashara baina ya Comoro na Tanzania na kuwaasa wananchi kuitumia Meli mpya ambayo itaanza safari zake Januari 2018.

Naye Rais wa Chama cha wafanyabiashara viwanda na kilimo nchini Comoro (UCCIA) Ahmed Ali Bazi amesema wameamua kuja kusaini makubaliano Mkoani Mtwara kwasababu ni karibu sana na nchi yao na kuna bidhaa nyingi ambazo wao wanazihitaji kama ambavyo wameanza kupata cement lakini bado wanahitaji zaidi vyakulana  na bidhaa zingine.

Mfanyabiashara kutoka Mtwara Fadhiri Bashir ambae wamenunua meli kwa kushirikiana na mfanyabiashara kutoka Comoro ili kuimarisha biashara, kwani Meli ya awali ambayo inaendelea kufanya kazi ni ndogo ukilinganisha na huhitaji wa bidhaa kutoka Mtwara kwenda visiwa vya Comoro na Meli hiyo itatatua tatizo la uhaba wa usafirishaji, na itaanza kufanya kazi mwezi wa kwanza January   2018 na itafanya safari kwenda msumbiji, Tanzania na Comoro.

Biashara baina ya nchi hizi mbili kupitia Bandari ya Mtwara ulianza rasmi mwezi August mwaka huu na uzinduzi huo ulifanywa na aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi Halima Dendego na pia Balozi wa Comoro nchini Tanzania.
Share:

OMOG BYE BYE SIMBA



Aliekuwa kocha Mkuu wa timu ya Simba SC Joseph Omog


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

_____________
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.

Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.

Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.

Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu.

Mwisho

klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.

IMETOLEWA NA....

Haji S MANARA
Mkuu wa Habari Simba Sc

SIMBA NGUVU MOJA
Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>