• VIPINDI VYA ELIMU HASA KILIMO

    Tuna vipindi mbalimbali vinavyohamasisha jamii katika kilimo cha Korosho, ufuta na Mhogo. tunaendelea na jamii inafurahia uwepo wa vipindi kwa sababu wanakutana na wataalamu moja kwa moja

  • SAUTI ZA WANAJAMII HUSIKIKA

    Sauti ni muhimu hasa unapohudumia jamii ya vijijini, wasikilizaji hupenda kusikia sauti zao kwakua watu wao wanawafahamu, hivyo huwa kivutio kwako na ni rahisi jamii kuamini kuwa mpo pamoja nao

  • MICHEZO MBALIMBALI

    Afya ni sehemu ya vipindi vyetu kwenye radio, hii husaidia kuwapa fursa watu wanaopenda michezo kuwa pamoja na kubadirishana mawazo, michezo hujenga urafiki na undugu baina mwa jamii

  • WATOTO KATIKA RADIO

    Hupenda kushiriki na hujiona sehemu ya radio kwa kuwa huishi katika jamii, kipindi cha watoto kimekuwa kikifuatiliwa na watu wazima kwasababu kuu moja tu, watoto waishio vijijini huwa hawapewi kipaumbele kama tulivyofanya Jamii fm

  • SIKIKA KATIKA RADIO

    Kipengere hiki hutoa fursa kwa wanajamii wanaotuzunguka kuongea moja kwa moja na kueleza hoja zao ambazo baadae hufuatiliwa kwa undani

Wafanyabiashara Mtwara walia na ongezeko la tozo

 

Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia kwa umakini mkutano wa ushirika wa Wafanyabiashara uliofanyika November 15, 2025 viwanja vya Mashujaa Manispaa ya Mtwara Mikindani (Picha na Musa Mtepa)

Wafanyabiashara wa Mtwara wamelalamikia ongezeko la tozo na ushuru linalodaiwa kupandisha bei za bidhaa, huku wakitaka serikali kupitia upya kanuni hizo. Manispaa imesisitiza kuwa tozo zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria na iko tayari kushughulikia malalamiko kupitia majadiliano

Na Musa Mtepa

Wafanyabiashara mjini Mtwara wamelalamikia ongezeko la ushuru unaoendelea kutungwa katika biashara zao, wakieleza kuwa hatua hiyo inaathiri bei za bidhaa na kuhatarisha uwezo wa mlaji wa mwisho kumudu bidhaa hizo.

Wakizungumza Novemba 15, 2025 katika mkutano wa Ushirika wa Wafanyabiashara (WABISOKO) uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa, Manispaa ya Mtwara Mikindani, wafanyabiashara hao wamesema mkutano huo umewezesha kutoa taarifa za maendeleo ya ushirika pamoja na changamoto zinazowakabili.

Akielezea hali ya tozo wanazokutana nazo wanapoingiza bidhaa ndani ya manispaa, Selemani Kadege amesema kuwa endapo serikali haitapitia upya ushuru unaotozwa, bidhaa zitaendelea kuwa ghali na hivyo kumuumiza mlaji wa mwisho.


Sauti ya Selemani Kadege, mfanyabiashara Soko Kuu Mtwara

Kwa upande wake, Asha Abilahi, mfanyabiashara wa Soko la Chuno, amesema kuwa wamekuwa wakitozwa ushuru katika vizuizi vya barabarani, ambapo baadhi ya watendaji hawatoi risiti, hali ambayo imekuwa kero kwao. Ameiomba serikali kufuatilia suala hilo kwa umakini zaidi.


Sauti ya 1 Asha Abilahi, mfanyabiashara Soko la Chuno

Aidha, Bi. Asha ameiomba serikali kuhakikisha wafanyabiashara wakubwa wa vyakula, minada na nguo wanapelekwa Soko la Chuno ili kulihuisha na kuongeza mzunguko wa biashara, badala ya wafanyabiashara kufanyika nje ya eneo la soko hilo.


Sauti ya 2 Asha Abilahi, mfanyabiashara Soko la Chuno

Akitoa ufafanuzi kuhusu tozo hizo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Rugembe Maiga amesema kuwa ushuru unaotozwa unatokana na sheria iliyopitishwa kwa kuzingatia taratibu. Ameongeza kuwa iwapo kuna malalamiko au changamoto, manispaa ipo tayari kukaa na wafanyabiashara kupitia maeneo yenye matatizo.

Amesisitiza kuwa kwa sasa sheria tayari imetungwa, hivyo wafanyabiashara wanapaswa kuendelea kulipa kodi, ada na ushuru kwa viwango vilivyowekwa mpaka pale maboresho yatakapofanyika na kupitishwa na mamlaka husika.

Sauti ya Rugembe Maiga Mwakilishi wa mkurugenzi Manispaa ya Mtwara Mikindani
Share:

Mtwara kutenga milioni 500 kuboresha Soko Kuu

 

Bw. Rugembe Maiga akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya Manspaa ya Mtwara Mikindani katika mkutano wa WABISOKO(picha na Musa Mtepa)

Manispaa ya Mtwara–Mikindani imetangaza mpango wa kutenga zaidi ya shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuboresha Soko Kuu la Mtwara, ikilenga kuboresha miundombinu na mazingira ya biashara huku wafanyabiashara wakiyakaribisha maboresho hayo na kuomba kupewa kipaumbele baada ya ujenzi kukamilika

Na Musa Mtepa

Zaidi ya shilingi milioni 500 zinatarajiwa kutengwa kwa ajili ya kuanza mchakato wa uboreshaji wa ujenzi wa Soko Kuu la Mtwara, hatua inayolenga kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika mazingira bora na yenye hadhi inayolingana na Manispaa ya Mtwara–Mikindani.

Akimwakilisha Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara–Mikindani kwenye mkutano wa Ushirika wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu (WABISOKO) uliofanyika Novemba 15, 2025 katika Viwanja vya Mashujaa, Bw. Rugembe Maiga amesema kuwa pamoja na jitihada nyingi zilizofanywa na serikali, bado wanatambua kuwa soko hilo ni chakavu na linahitaji maboresho ili liendane na hadhi ya manispaa.

Sauti ya Rugembe Maiga, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara–Mikindani

Aidha, Bw. Rugembe amesema kuwa mbali na mipango ya ujenzi mpya, tayari wameanza kushughulikia baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili wafanyabiashara ikiwemo uboreshaji wa huduma za choo, maeneo ya kufanyia biashara pamoja na mitaro ya kupitisha maji.

Sauti ya Rugembe Maiga, mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara–Mikindani

Wakizungumzia mpango huo, wafanyabiashara wa soko hilo, Selemani Kadege na Ramadhani Mtumba, wameishukuru serikali kwa hatua hizo za maboresho, huku wakitoa ombi la kupewa kipaumbele wafanyabiashara waliopo sasa mara baada ya ujenzi kukamilika.


Sauti ya Selemani Kadege na Ramadhani Mtumba – Wafanyabiashara
Share:

DC Mtwara awataka wajasiriamali kuwajibika kwa mikopo

 

DC Mwaipaya akizungumza na wajasiliamali na wafanyabiashara wa soko kuu mtwara wakati wa mkutano wa WABISOKO katika viwanja vya Mashujaa jana November 15,2025 (Picha na Musa Mtepa)

Mkuu wa Wilaya Abdala Mwaipaya amesisitiza uwajibikaji huo kwenye mkutano wa WABISOKO na kuwapongeza wafanyabiashara kwa kudumisha amani na kuwasilisha changamoto zao kwa utulivu. Makamu Mwenyekiti Rashidi Johana amewasilisha maendeleo na changamoto za ushirika.

Na Musa Mtepa

Wajasiriamali wametakiwa kutimiza wajibu wao katika kufanikisha upatikanaji na urejeshaji wa mikopo inayotolewa na serikali kupitia benki washirika, ili kuwezesha watu wengine kunufaika na huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa Novemba 15, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Abdala Mwaipaya, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Ushirika wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mtwara (WABISOKO) uliofanyika katika viwanja vya Mashujaa, Manispaa ya Mtwara–Mikindani.

Mwaipaya amesema kuwa serikali inatekeleza wajibu wake, lakini ni muhimu kwa wajasiriamali kama walengwa wa mikopo hiyo kuhakikisha wanatimiza masharti na vigezo vinavyohitajika ili kupata na kurejesha mikopo ipasavyo.

Sauti ya 1: Abdala Mwaipaya, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara

Aidha, DC Mwaipaya ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kwa kudumisha amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita. Pia amewapongeza viongozi wa jumuia hiyo kwa kuwa watulivu na kuwasilisha changamoto zao bila kuanzisha vurugu au fujo.

Sauti ya 2: Abdala Mwaipaya, Mkuu wa Wilaya ya Mtwara

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Ushirika wa Wafanyabiashara wa Soko Kuu Mtwara (WABISOKO), Bw. Rashidi Issa Johana, amesema kuwa dhamira kuu ya mkutano huo ni kuwapa wanachama taarifa ya maendeleo tangu viongozi wa sasa walipochukua madaraka, pamoja na changamoto na mafanikio yaliyopatikana.

Sauti ya Rashidi Issa Johana, Makamu Mwenyekiti WABISOKO
Wajasiliamali wakiwa kwenye mkutano wa WABISOKO (Picha na Musa Mtepa)
Share:

PPRA yatoa mafunzo kwa makundi maalumu Mtwara

 

Makundi maalumu washiriki wa mafunzo yaliyotolewa na PPRA November 12,2025 katika ukumbi wa Mikutano wa Benjamini Mkapa kilichokuwa chuo cha ualimu Mtwara wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo(Picha na Musa Mtepa)

PPRA imeendesha mafunzo kwa makundi maalumu mkoani Mtwara kuhusu taratibu za ununuzi wa umma, yakilenga kuongeza uelewa na ushiriki wao katika zabuni za serikali. Mafunzo hayo yamezinduliwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Bi. Bahati Geuzye, na yataendelea hadi Desemba katika halmashauri zote za mkoa

Na Musa Mtepa

Mtwara, Novemba 12, 2025Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imeendesha mafunzo maalumu kuhusu taratibu za manunuzi ya umma kwa makundi maalumu yakiwemo watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuongeza uelewa na ushiriki wao katika zabuni za serikali.

Akifungua mafunzo hayo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Bahati Geuzye, amesema mafunzo hayo ni fursa muhimu na ya kipekee kwa wadau kutoka makundi maalumu kujifunza kuhusu sheria, kanuni na taratibu za ununuzi wa umma.

Sauti ya 1 – Bi. Bahati Geuzye, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara
Katibu tawala mkoa wa Mtwara Bi Bahati Geuzye akikibidhi hati ya TRA kwa wajasiliamali wakati wa mafunzo ya PPRA (Picha Musa Mtepa)

Aidha, Bi. Geuzye amesema zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya serikali hutumika kwenye ununuzi wa umma, hivyo ni muhimu kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki na kunufaika na miradi ya maendeleo kupitia mfumo rasmi wa serikali.

Sauti ya 2 – Bi. Bahati Geuzye, Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara

Kwa upande wake, Afisa Ununuzi kutoka PPRA, Bw. Magnus Steven, amesema mafunzo hayo yalianza Novemba 10, 2025, na yataendelea hadi mwezi Desemba katika halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara.

Sauti ya 1 – Magnus Steven, Afisa PPRA
Afisa Ununuzi kutoka PPRA, Bw. Magnus Steven akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mafunzo hayo(Picha na Musa Mtepa)

Bw. Steven ameongeza kuwa lengo ni kujenga uelewa na kuimarisha uaminifu kati ya makundi maalumu na serikali, ili waweze kushiriki kikamilifu na kunufaika na zabuni mbalimbali.

Sauti ya 2 – Magnus Steven, Afisa PPRA

Washiriki wa mafunzo hayo wamesema wamepata uelewa mkubwa kuhusu namna zabuni za serikali zinavyotangazwa na nafasi ya watu wenye ulemavu katika mchakato huo, huku wakiahidi kuwa mabalozi wa kutoa elimu zaidi kwa jamii.

Sauti ya washiriki wa mafunzo
Share:

Wakulima waomba bei bora zaidi ya Korosho

 

Viongozi wa Bodi ya Korosho,TANECU na Serikali wakiwa katika uzinduzi wa rasmi wa mnada wa Korosho msimu wa 2025/2026 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Tandahimba (Picha na Musa Mtepa)

Wakulima wa korosho wilayani Tandahimba wamepokea kwa mitazamo tofauti bei ya zao hilo katika mnada wa kwanza wa msimu 2025/2026, ambapo kilo moja imenunuliwa kwa bei ya juu ya shilingi 3,520 na ya chini shilingi 2,550, huku wakitaka wanunuzi kuongeza bei ili kuendana na gharama za uzalishaji

Na Musa Mtepa

Wakulima wa zao la korosho wamepokea kwa mitazamo tofauti bei ya zao hilo kupitia mnada wa kwanza uliofanyika tarehe 8 Novemba 2025, wilayani Tandahimba, mkoani Mtwara. Katika mnada huo, bei ya juu kwa kilo moja ya korosho imeuzwa kwa shilingi 3,520 na kwa shilingi 2,550 kwa bei ya chini.

Mnada huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba, kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU), ambapo zaidi ya tani 26,000 za korosho zimeuzwa.

Wakulima wameishukuru serikali na vyama vya ushirika kwa kufanikisha mnada huo, huku wakitoa wito kwa wanunuzi kuongeza bei ya korosho ili iendane na gharama kubwa za uzalishaji wa zao hilo.

Sauti ya wakulima wa korosho wilayani Tandahimba
Wakulima wa zao Korosho wakifuatilia mwenendo wa soko la korosho katika mnada wa kwanza wa uzinduzi wa msimu wa korosho nchini uliofanyika wilayani Tandahimba(Picha na Musa Mtepa)

Bi. Tatu Mahupa mkulima wa korosho amefurahi kufanyika kwa mnada huo huku akiwataka wakulima kutumia vizuri fedha watakazopata kutokana na mauzo ya korosho, kwa kuweka bajeti nzuri ya matumizi na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima, ili ziweze kusaidia katika mahitaji muhimu ya familia ikiwemo elimu ya watoto.

Sauti ya Tatu Mahupa, mkulima wa korosho, Mchichira.

Akiongoza mauzo katika mnada huo, Mwenyekiti wa TANECU Ltd, Karim Chipola, amewapongeza wakulima kwa mwitikio wao mkubwa. Amesema kati ya tani 26,000 na kilo 254 zilizouzwa, Tandahimba imechangia tani 18,102 na Newala tani 8,152, zikiuzwa kwa bei ya juu ya shilingi 3,520 na bei ya chini shilingi 2,550 kwa kilo.

Sauti ya Karim Chipola, Mwenyekiti wa TANECU.
Mwenyekiti wa TANECU,Ltd akizungumza na wakulima waliojitokeza kwenye mnada huo(Picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Bw. Godfrey Marekano, amesema matarajio yao ni kuona idadi ya wanunuzi inaongezeka katika minada inayofuata ili kuongeza ushindani na hatimaye kuinua bei ya korosho kwa manufaa ya wakulima.

Sauti ya Godfrey Marekano, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Ndugu Frances Alfred, amesema mnada huo ni wa kwanza kitaifa kwa msimu wa 2025/2026, na ndio unaoashiria mwenendo wa soko la kimataifa la korosho kwa mwaka huu.

Sauti ya – Frances Alfred, Mkurugenzi Mkuu wa CBT
Share:

Makala: mabinti wa Mtwara wavunja ukimya

Bi Thea Swai akizungumza katika moja ya vikao vya wadau. Picha na Mwanahamisi Chikambu

“Wasichana wanajifunza kwamba sauti yao ina thamani, na kwamba wao pia wana nafasi muhimu katika jamii hasa mabinti wa Mtwara”

Na Mwanahamisi Chikambu

Katika dunia ya sasa inayokua kwa kasi kutokana na maendeleo ya teknolojia, bado mtoto wa kike wa Kiafrika anakabiliwa na vikwazo vingi vinavyomnyima nafasi ya kuonekana, kusikika, na kushiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu maisha yake.

Lakini mkoani Mtwara, hali inaanza kubadilika, Sauti za wasichana zinapata nguvu mpya kupitia mradi wa Binti Paza Sauti (Girls Speak Out) mpango unaolenga kuwajengea uwezo mabinti kujieleza, kushiriki katika maamuzi, na kuvunja ukimya kuhusu changamoto zinazowakabili kila siku kupitia michezo

Kupitia mradi huu, wasichana wanajifunza kwamba sauti yao ina thamani, na kwamba wao pia wananafasi muhimu katika jamii, Karibu katika makala haya, tujifunze kwa pamoja namna ambavyo mabinti wa Mtwara.

Bonyeza hapa kusikiliza

Share:

CBT yaruhusu usafirishaji wa korosho Saa 24

 

Gari lililobeba Korosho kutoka vya vya ushirika likishusha katika Ghala kuu tayari kwa ajili ya Mnada (Picha Kwa Msaada wa Mtandao)

Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imeruhusu usafirishaji wa korosho saa 24 kwa mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara ili kuharakisha uondoaji wa mizigo na kuongeza ufanisi wa Bandari ya Mtwara. Katika mnada wa kwanza, TANECU iliuza tani 26,000 kwa bei ya juu ya Sh. 3,520 kwa kilo

Na Musa Mtepa

Tandahimba-Mtwara, Novemba 8, 2025 Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imeruhusu magari yote yanayosafirisha korosho kutoka mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara kufanya usafirishaji wa korosho masaa 24, usiku na mchana.
Hata hivyo, mikoa mingine itaendelea kusafirisha korosho kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni kama kawaida.

Hatua hiyo inalenga kuharakisha uondoaji wa mizigo kwenye maghala makuu ili kutoa nafasi kwa korosho nyingine za wakulima kuingia ghalani kwa ajili ya minada inayofuata.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi rasmi wa msimu wa minada wilayani Tandahimba, Mkurugenzi Mkuu wa CBT, Ndugu Frances Alfred, amesema kuwa ruhusa hiyo inahusisha mikoa inayosafirisha korosho kupitia Bandari ya Mtwara au maghala makuu yaliyopo mjini Mtwara.

Sauti ya Frances Alfred – Mkurugenzi Mkuu wa CBT

Aidha, Ndugu Frances amesema kuwa sababu kubwa ya kutoa ruhusa hiyo ni kuhakikisha korosho zinatoka kwa haraka katika maghala makuu ili korosho nyingine za wakulima ziweze kuingizwa kwa ajili ya minada inayofuata.
Ameeleza kuwa hatua hiyo pia inalenga kuongeza mzunguko wa malori, kuboresha ufanisi wa Bandari ya Mtwara katika kurahisisha usafirishaji wa korosho nje ya nchi, pamoja na kuwavutia wanunuzi zaidi kushiriki katika minada mingine ijayo ya zao hilo.

Sauti ya Frances Alfred Mkurugenzi wa CBT
Mkurugenzi mkuu wa CBT ndugu Frances Alfred akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kufanyika kwa mnada wa Kwanza 2025/2026 uliofanyika wilayani Tandahimba ,mkoani Mtwara.(Picha na Musa Mtepa)

Novemba 8, 2025, mnada wa kwanza wa zao la korosho umefanyika katika wilaya ya Tandahimba, ambapo Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala (TANECU Ltd) kimefanikiwa kuuza korosho tani 26,000 na kilo 254.

Bei ya juu katika mnada huo ilikuwa shilingi 3,520 kwa kilo, huku bei ya chini ikiwa shilingi 2,550 kwa kilo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa TANECU, Ndugu Karim Chipola, katika jumla hiyo ya korosho zilizouzwa, Tandahimba imechangia tani 18,102, huku Newala ikichangia tani 8,152.

Share:

Wadau wanashiriki vipi kutatua changamoto za watu wenye ulemavu

 

Wadau wenye ulemavu wakiwa katika mafunzo. Picha na Mwnahamisi Chikambu

Tutahakikisha elimu jumuishi inatekelezwa kwa vitendo ili kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye ulemavu na kuboresha kiwango cha elimu mkoani Mtwara

Na Msafiri Kipila

Shirika lisilo la kiserikali Sport Development Aid (SDA) kwa kushirikiana na Jamii FM, linaendelea kuhimiza jamii kuwashirikisha na kuwatambua watu wenye ulemavu katika juhudi za kutatua changamoto zinazowakabili.

Kupitia programu zake, SDA imetoa mafunzo maalum kwa baadhi ya watendaji na walimu wanaofundisha wanafunzi wenye ulemavu, ili wawe mabalozi wa kutoa elimu na kuibua uelewa katika jamii. Lengo ni kuwasaidia wale wanaowaficha watu wenye ulemavu majumbani, jambo linalowanyima haki zao za msingi kama vile elimu.

Kasimu Samuel Shabani, mwalimu wa Shule ya Sekondari Chekeleni iliyoko Mtwara Vijijini, amesema kuwa yeye kama mwalimu atahakikisha elimu jumuishi inatekelezwa kwa vitendo ili kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye ulemavu na kuboresha kiwango cha elimu mkoani Mtwara.

Kwa upande wake, Jackline Mpunjo, Meneja Mradi wa SDA, amesema wameamua kuendesha mpango huo baada ya kubaini kuwa jamii nyingi bado hazijawatambua ipasavyo watu wenye ulemavu. Amesema ni muhimu kuwashirikisha kikamilifu ili waweze kutimiza malengo yao ya kila siku na kujenga jamii yenye usawa na fursa sawa kwa wote.

Bonyeza hapa kusikiliza Makala haya

Share:

Sikiliza jamii FM Radio

🎧 Jamii FM Live

IDADI YA WASOMAJI

HABARI ZA HIVI PUNDE

Blog Archive

WAENDESHA WEBSITE

Contact Form



1 ] )[0]; $title = $recent_post['post_title']; $excerpt = wp_trim_words( $recent_post['post_content'], 20 ); $image = get_the_post_thumbnail_url( $recent_post['ID'], 'full' ); ?>